Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, December 1, 2013

MASHINDANO YA TANZANIA BOXING AWARDS YAZINDULIWA KWA WANAMASUMBWI KUZIPIGA MWENGE





Bondia John Christian kushoto akipambana na Gervas Rogasiano wakati wa uzinduzi wa tunzo za Tanzania Boxing Awards  iliyofanyika katika kituo cha mabasi ya mwenge Dar es salaam Christian  alishinda kwa pointi mpambano huo, wananchi watatakiwa kupiga kula kwa mabondia waliochaguliwa kugombea tunzo hizo kilele chake kitakuwa desemba 28 ambapo washindi watatangazwa  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya viongozi na waau wa mchezo wa masumbwi wakifatilia mashinano hayo ya ngumi kwa ajili ya kuhamasisha tuzo za Boxing AWARD zitakazofikia kirere Desemba 28 mwaka huu wa 2013
Mabondia wa uzito wa juu Kulwa Makenzi kushoto akipambana na Haruna Swanga wakati wa mashindano ya wazi ya kutangaza tuzo za Tanzania Boxing Awards ambazo kilele chake kitakuwa Desemba 28 Swanga alishinda kwa pointi mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Hamad Furahisha kushoto akimsukumiza konde la kulia George Costantino wakati wa uzindunzi  wa Tuzo za Tanzania Boxing Awards iliyofanyika katika kituo cha mabasi mwende Dar es salaam Furahisha alishinda kwa point mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com



Matangazo ya kuamasisha tuzo za ngumi

mmoja ya wadau wa mchezo wa masumbwi akibandika tanzazo la kuhamasisha masumbwi

Bondia Haruna Swanga akipiga picha kwenye bango

Bondia John Christian kushoto akipambana na Gervas Rogasiano wakati wa uzinduzi wa tunzo za Tanzania Boxing Awards  iliyofanyika katika kituo cha mabasi ya mwenge Dar es salaam Christian  alishinda kwa pointi mpambano huo  wananchi watatakiwa kupiga kula kwa mabondia waliochaguliwa kugombea tunzo hizo kilele chake kitakuwa desemba 28 ambapo washindi watatangazwa  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia John Christian kushoto akitupa ngumi ya kulia wakati wa mpambano wake  na Gervas Rogasiano wakati wa uzinduzi wa tunzo za Tanzania Boxing Awards  iliyofanyika katika kituo cha mabasi ya mwenge Dar es salaam Christian  alishinda kwa pointi mpambano huo  wananchi watatakiwa kupiga kula kwa mabondia waliochaguliwa kugombea tunzo hizo kilele chake kitakuwa desemba 28 ambapo washindi watatangazwa  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

JOY KALEMERA NDIYE MSHINDI WA MISS TANZANIA USA PAGEANT





 Mlimbwende Joy Kalemera akipungia mashabiki baada ya kushinda mashindano ya Miss Tanzania USA Pageant yaliyofanyika usiku wa Jumamosi Novemba 30, 2013 kwenye ukumbi wa Hollywood Ballroom uliopo Silver Spring , Maryland na Mhe. Balozi Liberata Mulamula ndiye aliyekua mgeni rasmi. Joy Kalemera alipohojiwa na Vijimambo alikua na haya ya kusema.
 Mshindi wa Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalamera akipewa maua na aliyekua Miss District of Columbia baada ya kutangazwa mshindi kwenye Miss Tanzania USA Pageant ambapo mashindano haya ya kumtafuta Miss Tanzania USA Pageant ndiyo ya kwanza kufanyika kwenye ardhi ya Marekani. 
 Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera akiwa mwenye furaha baada ya kutangazwa mshinidi wa Miss Tanzania USA Pageant.
 Balozi wa Tnzania nchini Marekani na Mexico akimvisha taji Joy Kalemera baada ya kutangazwa mshindi wa Miss Tanzania Pageant
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa mwenye furaha baada ya shindano hili kufana sana na kuandika historia iliyobeba ukurasa mpya wa kutangaza Tanzania kwenye mashindano haya ya Miss Afrika USA Pageant ambayo Tanzania ilikua na mshiriki wa kwanza mwaka huu ambae ushiriki wake haukupitia ngazi hii.
Joy Kalemera akipongezwa na washiriki wenzake waliokua nae kwenye kinyang'anyiro hiki kilichoanzia miezi miwili iliyopita.
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa kwanza katika historia ya Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera kulia ni Mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Tanzania USA Pageant Ma Winny Casey.
 Joy Kalemera katika picha ya pamoja na majaji pamoja na mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA Pageant, Lady Kate (kulia)
 Kutoka kushoto ni Faith Kashaa kutoka Alabama ambaye ndiye mshindi wa tatu, Doreen Rumaya kutoka Pennsylvania mshindi wa pili, Joy Kalemera kutoka New Jersey Miss Tanzania USA Pageant, Julia Nyerere mshindi wa Tano na Namala Elias mshindi wa nne wakiwa kwenye picha ya pamoja
 Miss Tanzania USA Pageant katika picha ya pamoja na washiriki wenzake.

CHEGE, TEMBA NA BI CHEKA WAWA VIVUTIO VIKUBWA LEO KATIKA UWANJA WA TAIFA WAKATI WA ZIARA YA KOMBE LA DUNIA





Mh Temba na Chege wakikamua vilivyo katika Steji ya Coca Cola Fifa trouphy tour iliyotua jijini Dar jana usiku na leo kuwa katika uwanja wa Taifa kwaajilii ya wakazi wa Jiji la Dar na Vitongoji vyake kuweza kupata fursa ya kupiga nalo picha.
 Chege, Temba na Wanaume TMK wakirusha mapanga shaa shaaa katika shoo ya Kombe la Dunia katika Uwanja wa Taifa leo
 Baadhi ya Mashabiki na wakazi wa jiji la Dar wakiendelea kufuatilia Shoo kutoka Kwa Chege na Temba
 Chege na Temba wakitoa burudani...
 Mashabiki wakifuatilia
 Bi Cheka naye ndani ya steji akitoa burudani 
Huku Temba huku Bi cheka Stejini wakiwarusha Mashabiki katika ziara ya Kombe la Dunia katika Uwanja wa taifa ambapo wakazi wa Jiji la Dar na Vitongoji vyake waliweza kupata fursa ya kupiga nalo picha leo katika uwanja wa Taifa

DKT.BILAL AENDESHA ZOEZI LA HARAMBEE YA KUCHANGIA MADAWATI MFUKO WA MAENDELEO YA ELIMU JIMBO LA NKENGE





 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi chaeti, Mkurugeniz wa Kagera Sugar, Bw. Hamadi Yahaya, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake wa kuchangia maendeleo ya Elimu ya Jimbo la Nkenge mkoa wa Kagera,wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshana na (kushoto kwa Makamu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali (mst) Fabian Masawe. Jumla ya Shilingi milioni 114, pesa taslimu milioni 65.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, jana usiku. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumta Mshana na (kushoto kwa Makamu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanal Fabian Masawe. 
 - Sehemu ya wageni waalikwa kutoka mkoa wa Kagera waliohudhuria harambee hiyo
 Baadhi ya wageni waalikwa kutoka mkoa wa Kagera waliohudhuria harambee hiyo
 Meza Kuu wakijumuika kuimba wimbo maalumu wa mkoa wa Kagera wa kuhamasisha maendeleo ya mkoa huo, hususan katika suala la elimu na kuchangia madawati.
Msanii Saida Karoli na kundi lake wakiburudisha wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Picha na OMR.

WAZIRI MKUU PINDA MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI CBE LEO





Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Cheti cha ubora Baraka Magure ambaye aliibuka kuwa mwanafunzi aliyefanya vizuri katika wahitimu wa Shahada katika mahafali ya Chuo cha Biashara yaliyofanyika kwenye viwanja vya Klabu ya Sigara iliyopo Chang'ombe jijini Dar es salaam Novemba 30, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zwadi Revocatus Mavuno ambaye alifanya vizuri kwa wanafunzi wa ngazi ya Stashahada katika mahafali ya Chuo cha Biashara yaliyofanyika kwenye viwanja vya Klabu ya Sigara iliyopo Chang'ombe jijini Dar es salaam Novemba 30, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

EAC Heads Sign the Monetary Union Protocal today in Kampala





 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete together with his East African Heads Of States  Counterparts shortly after they signed the Protocol on the Establishment of the East African Monetary Union at Speke’s Bay Resort Munyonyo in Kampala this afternoon.Others from Left Presidents Pierre Nkurunzinza of Burundi, Yoweri Kaguta Museveni of Uganda, The new EAC chairman Uhuru Kenyatta of Kenya, and Paul Kagame of Rwanda.
Viongozi wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) leo kwa pamoja wametia saini itifaki ya Umoja wa Fedha. Kupata taarifa rasmi ya pamoja

EMMANUEL MSUYA ATWAA MILIONI 50 ZA EPQ BONGO STAR SEARCH 2013









Washiriki walioingia Tatu Bora kutoka kushoto ni Elizabeth Mwakijambile, Emmanuel Msuya na Mellisa John.



 
Walter Chilambo ambaye ndiye mshindi wa shindano la EBSS 2012 akitumbuiza stejini

Wednesday, November 27, 2013

SELCOM,VODA COM NA OIL COM WAUNGANA KURAHISISHA UNUNUZI WA MAFUTA KWA NJIA YA MPESA



Meneja wa huduma za Selcom,Bi,Everline Simpilu kushoto akitoa lisiti kwa mteja  wa mafuta wa kituo cha Oil Com Bw,Peter Ibrahimu wakati wa uzinduzi wa ununuaji wa mafuta kwa njia ya mtandao wengine wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Oil Com Bw,Mohamed Said Nahdi Ofisa wa Selcom Tumaini Mgori na Meneja husiano wa nje wa kampuni ya Vodacom Salumu Mwalimu huduma za kununua mafuta kwa njia ya mtandao zitakuwa zikitolewa na kampuni ya vodacom kupitia Mpesa ambapo uzinduzi huo ulifanyika Dar es salaam jana Kampuni ya Selcom ndio wawezeshaji na mashine zao  za POS ndio zitakazokuwa zikitumika picha na Mpiga picha  wetu

Meneja wa huduma za Selcom,Bi,Everline Simpilu kushoto akimpatia lisiti kwa mteja  wa mafuta wa kituo cha Oilcom Bw,Peter Ibrahimu wakati wa uzinduzi wa ununuaji wa mafuta kwa njia ya mtandao wengine wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Oilcom Bw,Mohamed Said Nahdi Ofisa wa Selcom Tumaini Mgori na Meneja husiano wa nje wa kampuni ya Vodacom Salumu Mwalimu huduma za kununua mafuta kwa njia ya mtandao zitakuwa zikitolewa na kampuni ya voda com kupitia Mpesa na mashine pekee za Selcom POS  uzinduzi huo ulifanyika Dar es salaam jana picha na Mpiga picha  wetu

Meneja wa huduma za Selcom,Bi,Everline Simpilu kushoto  akimweleza mwendesha bajaji Bw,Peter Ibrahimu  jinsi Selcom wanavyotoa huduma ya kununua mafuta kwa njia ya mtandao kwa kushirikiana na ,Vodacom Mpesa katika huduma ya lipa bidhaa pamoja na Oil Com

Meneja wa huduma za Selcom,Bi,Everline Simpilu kushoto Group IT meneja  wa Oil Com, Abubakari Mwita,Mkurugenzi wa Oil Com Bw,Mohamed Said Nahdi, Meneja husiano wa nje wa kampuni ya Vodacom Salumu Mwalimu.Ofisa wa Selcom Tumaini Mgori wakipata maelezo jinsi mashine ya Selcom inavyofanya kazi ya kununua mafuta kwa njia ya mtandao wakiungana na Oilcom na Vodacom  kupitia huduma ya lipa bidhaa  wakati wa uzinduzi uliyofanyika Dar es salaam jana picha na Mpiga picha  wetu
Ofisa wa Selcom Tumaini Mgori akiongea na wahandishi wa habari wakati wa huzinduzi wa huduma hiyo