Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, June 7, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA KIWANDA CHA COCACOLA MWANZA KATIKA MAADHIMISHO YA KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa ubora wa Mazingira na Usalama Kazini, Peter Simon, kuhusu jinsi wanavyo tunza mazingira kwa kutotupa maji machafu ambayo hutengenezwa na kuwa masafi  na kutumika upya kwa baadhi ya shughuli za kiwandani hapo kama kumwagia bustani, kuoshea magari na n.k,  wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana Juni 5, 2014. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Mwanza na wa Kiwada cha Cocacola, wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Cocacola Mwanza, Christopher Gachuma, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kuzungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho, wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wafanyakazi wa Kiwanda cha Cocacola, (hawapo pichani) wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda hicho wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akizungumza nao.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa ubora wa Mazingira na Usalama Kazini, Peter Simon, kuhusu jinsi wanavyo tunza mazingira kwa kutotupa maji machafu ambayo hutengenezwa na kuwa masafi  na kutumika upya kwa baadhi ya shughuli za kiwandani hapo kama kumwagia bustani, kuoshea magari na n.k,  wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa ubora wa Mazingira na Usalama Kazini, Peter Simon, kuhusu jinsi wanavyo tunza mazingira kwa kutotupa maji machafu ambayo hutengenezwa na kuwa masafi  na kutumika upya kwa baadhi ya shughuli za kiwandani hapo kama kumwagia bustani, kuoshea magari na n.k,  wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa ubora wa Mazingira na Usalama Kazini, Peter Simon, kuhusu jinsi wanavyo tunza mazingira kwa kutotupa maji machafu ambayo hutengenezwa na kuwa masafi  na kutumika upya kwa baadhi ya shughuli za kiwandani hapo kama kumwagia bustani, kuoshea magari na n.k,  wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa ubora wa Mazingira na Usalama Kazini, Peter Simon, kuhusu jinsi wanavyo tunza mazingira kwa kutotupa maji machafu ambayo hutengenezwa na kuwa masafi  na kutumika upya kwa baadhi ya shughuli za kiwandani hapo kama kumwagia bustani, kuoshea magari na n.k,  wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana.
 Makamu akionyeshwa maji masafi ambayo tayari yameshapita katika hatua kadhaa yakiwa machafu hadi kuweza kutumika upya.
 Maji safiiii,
 Picha ya pamoja....

Thursday, June 5, 2014

SIKU ZA HATARI ZA KUSHIKA MIMBA NI ZIPI?




HABARI za leo wasomaji wangu? Kabla ya kuanza mada hii ya leo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mungu kwani ameniwezesha kufika siku hii.Mada leo inahusu siku za hatari ambazo mwanamke  akifanya ngono bila kinga basi anakuwa katika hatari ya kushika mimba.

Nimeamua kutoa mada hii baada ya kugundua kuwa ongezeko la matukio ya utoaji mimba na kutupa watoto  na hata kuwa na watoto wa mitaani yanasababishwa  zaidi na mimba ambazo hazikutarajiwa.
Mimba nyingine zinaingia kwa sababu mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga asipate.

Ni muhimu sana kwa mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, mizunguko hiyo iko katika makundi makuu matatu ambayo: Mzunguko mfupi wa siku 25 kurudi nyuma, mzunguko wa kawaida wa siku 28 na mzunguko mrefu wa siku30-35.
Wanawake wengi mzunguko wao  huwa  ni wa kawaida yaani siku 28 hawa ndiyo leo nitawaongelea zaidi.
Ili kutambua mzunguko wako ni wa siku ngapi unatakiwa kuhesabu kuanzia siku ya kwanza kuona damu ya hedhi hadi siku ya kwanza ya kuona damu ya hedhi ya mwezi unaofuata. Kwa mfano ukiona damu ya hedhi tarehe 15 Oktoba  basi hiyo ndiyo siku yako ya kwanza.
Kwa mtu mwenye mzunguko huo wa siku 28 siku zake za hatari za kuweza kushika mimba ni siku ya kumi na nne 14, hivyo kuanzia siku ya 12 hadi siku ya 16 kama atafanya ngono bila kinga anaweza kushika mimba.
Najua mtu anaweza akajiuliza kama siku ya hatari ni ya 14 sasa kwa nini akifanya ngono siku ya 12 anaweza akapata mimba?Hii ni kwa sababu mbegu za kiume zina uwezo wa kudumu kwa masaa 24 hadi

48 baada ya kujamiiana hivyo kama mwanamke atafanya ngono tarehe 12 na yai likatoka tarehe14 bado litakuta zile mbegu zikiwa hai hivyo zitarutubishwa.Chanzo GPL

Mchungaji Daniel Mwasumbi aachiwa huru


MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe   


Mtoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi Elizabeth Mwasumbi akilia kwa furaha mara baada ya baba yake kuachiwa huru





Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, imebatilisha hukumu  ya kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 aliyokuwa akiitumikia Mchungaji wa Kanisa la EAGT la Iwambi Jijini Mbeya,  Daniel Mwasumbi(57) aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya ubakaji na kumpa mimba mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Itende Neema Beni(19) jijini hapa.
Mchungaji Mwasumbi alihukumiwa kifungo hicho, Januari 2 mwaka huu na mahakama ya Wilaya ya Mbeya na Hakimu Gilbert Ndeuruo na Serikali kuwakilishwa na wakili Achiles Mulisa, ambapo Mahakama ilimtia hatiani Mchungaji katika makosa kinyume cha sheria kifungu cha 130(2)e na 131(1) sura ya 16 ya sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Awali Mchungaji Mwasumbi alikuwa akitetewa na Wakili wa kujitegemea Victor Mkumbe ambapo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari 2008 hadi 2011 ambapo alimpa ujauzito na kumzalisha mwanafunzi huyo watoto wawili wa kiume kwa nyakati tofauti hivyo kumkatisha masomo kinyume cha sheria.
Katika Rufaa hiyo Mchungaji  Mwasumbi alikuwa akitetewa na Wakili wakujitegemea Benjamin Mwakagamba kutoka Dar es Salaam wakati Serikali iliwakilishwa na Wakili Prosister Paul.
Akisoma hukumu ya rufaa hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Atuganile Ngwala,  alisema kuwa sababu zilizowasilishwa kwenye mahakama  hiyo na Wakili wa upande wa utetezi zilidhihirisha kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa kisheria kwenye hukumu hiyo.
Jaji Ngwala ambaye alitumia takribani saa 1:15 kusoma huku hiyo alisema katika utoaji wa hukumu hiyo haukuzingatia vipengele muhimu vya kisheria viilivyotumika na mahakama ya wilaya kumtia hatiani Mchungaji Mwasumbi.
“katika rufaa hii ni kweli kuna mambo mengi ambayo yanaonekana kukiukwa katika utoaji wa hukumu, kama zilizovyoweza kuanishwa na wakili wa utetezi hivyo na mimi nakubaliana na wakili Mwakagamba (wakili wa utetezi) kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa kisheria kwenye hukumu hiyo” alisema
Aliongeza kwamba kama ilivyoelezwa na wakili Mwakagamba,  muda wa lilitopotekea tukio hilo na liliporitiwa kwenye vyombo vya usalama unaonekana kuchelewa na kukinzana,  lakini pia ushahidi ulitolewa mahakamani hapo na Mhanga  ulionekana kujichanganya hivyo haujaonesha mrufani kutenda kosa hilo’.
Awali Jaji Ngwala alimwita mchungaji Mwasumbi kuwa ni mende, na ni mtu hatari sana katika jamii kwa kosa kama hilo na hafai kuwa katika jamii jambo lililowafanya watu waliokuwa wakifuatilia mwenendo wa hukumu hiyo kuanza kuinamisha vichwa chini akiwemo Katibu wa Kanisa la Uinjisti Bwana Mwakasole.
Lakini  baadaye, Jaji Ngwala alionesha hisia zake kwamba kutokana na kujichanganya kwa ushihidi hususani wa shahidi namba moja ambaye ni binti aliyefanyiwa kitendo hicho hivyo kumtoa hivyo na haonekani kama ana kosa.
Alisema ‘Nasema hivi mtu huyu alikuwa ni mende na ni hatari sana katika jamii asiyefaa kwa namna yoyote ile na anastahili adhabu kali laiti kama ingethibitika hivyo, lakini hapa ushahidi umeshindwa kuthibitisha hili hivyo ana haki ya kuachiwa huru’.
Hata hivyo, Jaji Ngwala alisema kuwa kwa upande wa Jamhuri ambao ulikuwa ukiongozwa na wakili wa Serikali, Prosister Paul una haki zote za kukata rufaa na kesi kuanza upya endapo utaona haujaridhika na hukumu hiyo.
Wakili aliyekuwa akimtetea Mchungaji Mwasumbi alisema kuwa katika rufaa ya mteja wake aliwasilisha sababu saba za kupinga hukumu hiyo ambapo alidai kuwa  hakimu wakati wa kutoa hukumu hiyo alikosea kisheria na haki muda wa kuripotiwa kwa shauri hilo kwa vyombo vya usalama na lilipotokea ulikinzana na kwamba aliegemea kwa ushahidi wa Mhanga tu.
Sababu zingine alidai kuwa hakimu aliegemea katika ushahidi  au vidhibiti ambavyo awali alivikata mwenyewe, pia alidai kuwa hakimu hakuangalia uhalisia kosa lenyewe na badala yake alionekana kutoa maoni yake binafsi.
Lakini sababu nyingine wakili Mwakagamba alisema kuwa hakimu huyo, aliegemea ushahidi ambao ulijichanganya, wendesha mashtaka  walishindwa kuwapeleka mahakamani hapo  mashahidi wa msingi katika kesi hiyo, hakimu aliegemea upande wa vyeti vya watoto wawil waliodaiwa ni wa Mchungaji Mwasumbi ambapo vyeti vilidurufiwa (photocopy) na si vyeti halisi na  mwisho hakimu huyo alitoa hukumu ambayo haikufuata mtiririko uliosahihi wa mashahidi husika.
Akizungumza na Mbeyayetu blog, mtoto wa Mchungaji Mwasumbi,  Elizabeth Mwasumbi alisema anamshukuru Mola kwa kumwezesha Jaji Ngwala kwa kutenda haki katika rufaa ya baba yake.
Alisema; ’Mimi na wenzangu tulikuwa na wakati mgumu sana pindi baba yetu akiwa ndani, kwani mimi niliathirika sana kiafya na kiuchumi nilishindwa kufanya shughuli yoyote kutokana na mawazo lakini namshukumuru Mola kwa kutenda haki’.
Hata hivyo nje ya Mahakama ndugu na jamaa waliofurika kusikiliza hatma ya Rufaa hiyo waliokuwa na hamu ya kumlaki kwa furaha Mchungaji Mwasimbi ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili kushindwa kutokana na Maafisa wa Magereza kumpeleka Gerza la Ruanda kukamilisha taratibu za Magereza

Na Ezekiel Kamanga 
Mbeya yetu

HIVI NDIVYO MSAFARA ULIVYOKUWA WAKATI WA KUUPELEKA MWILI WA MAREHEMU GEORGE TYSON UWANJA WA NDEGE KWAAJILI YA KUUSAFIRISHA NCHINI KENYA




 Msafara wa Magari ukiongozwa na Askari wa Usalama Barabarani atumiaye Pikipiki Ukikatiza eneo la Daraja la Salenda ukielekea Uwanja wa Ndege wa Mwl Julius Nyerere Kuupeleka Mwili wa Marehemu George Tyson kwaajili ya Kuusafirisha Nchini Kenya Kwa Mazishi.
 Msafara Ukikatiza barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuelekea uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere
 Ukikatiza katika Barabara ya Nyerere eneo la Gerezani kuelekea Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere
 Msafara ukiingia Uwanja wa Ndege Wa Mwl Nyerere sehemu ya Mizigo kwaajili ya Kuupeleka Mwili wa Marehemu George Tyson tayari kwa kuusafirisha Kuelekea Nchini Kenya.
 Baadhi ya Wadau walioambatana na Msafara uliopeleka Mwili wa Marehemu George Tyson Uwanja wa Ndege kwaajili ya Kusafirishwa Nchini Kenya wakibadilishana mawazo wakati wakisubiria taratibu za kuupokea Mwili huo eneo la Mizigo kukamilika.Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

WASHINDI WA FUA NA OMO UPAE KWENDA DUBAI WAPATIKANA MBEYA





Meneja uhusiano wa Unilever Tanzania Limited, Nicholaus John (kushoto) akimkabidhi mshindi wa saba wa promosheni ya 'Fua Upae kwenda Dubai' Mwasiti Bilali mfano wa tiketi ya kwenda Dubai mara baada ya kuibuka mshindi katika droo iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki kwa wakazi wa jijini la Mbeya wanaotumia sabuni ya Omo.Hafla fupi ya makabhiano ilifanyika Beaco Hotel Mbeya jana. Katikati ni Balozi wa Omo Tanzania, Mariam Migomba.


Meneja Mauzo Unilever Tanzania wa eneo la Mbeya Rajab Kondo (kushoto) akimkabidhi mshindi wa promosheni ya 'Fua Upae', Marcko  j. Fihavango hundi fedha taslimu sh. 600,000 baada ya kununua sabuni ya Omo. Katikati ni Balozi wa Omo Tanzania, Mariamu Migomba.Hafla fupi ya makabidhiano ilifanyika Beaco Hotel  jijini Mbeya  jana.

Meneja Mauzo Unilever Tanzania wa eneo la Mbeya Rajab Kondo (kushoto) akimkabidhi mshindi wa promosheni ya 'Fua Upae', Marcko  j. Fihavango fedha taslimu sh. 600,000 baada ya kununua sabuni ya Omo. Katikati ni Balozi wa Omo Tanzania, Mariamu Migomba.Hafla fupi ya makabidhiano ilifanyika Beaco Hotel  jijini Mbeya  jana.



Meneja uhusiano wa kampuni ya unilever Tanzania  Nicholaus John ametoa wito kwa wananchi na wateja wote wa mkoa wa Mbeya  kuichangamkia fursa hiyo ya kipekee na kuongeza kuwa zoezi hilo na promosheni hiyo ni la ukweli hivyo hawanabudi kuipokea kwa moyo wote kwani bado zawadi nyingi zitaendelea kutolewa kwa washindi huku kampuni hiyo ikijipanga zaidi kwa siku za baadaye kuja na promosheni nyingine tofauti tofauti zenye lengo la kurejesha shukurani kwa wateja.

Balozi wa Omo Tanzania, Mariamu akiongea na waandishi wa habari ambao hawapo pichani

Tuesday, June 3, 2014

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' HAPATA LESENI YA NGUMI


 Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini T.P.B.O Yassin Abdalla 'Ostadhi' kushoto akimkabidhi leseni ya ngumi bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ambayo anaweza kutumiha Dunia nzima kwa ajili ya kutambulika kitaifa na kimataifa ambayo inaweka rekodi mbalimbali za bondia pindi anapocheza mchezo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini T.P.B.O Yassin Abdalla 'Ostadhi' kushoto akimkabidhi leseni ya ngumi pamoja na kitambulisho na nyaraka mbalimbali za bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya shughuli zake lesini hiyo inayotumika kitaifa na kimataifa kwa ajili ya kuhifadhia kumbukumbu mbalimbali za michezo aliyo shiliki hafla ya makabidhiano hayo zimefanyika katika ofisi ya ngumi za kulipwa nchini jana  Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
 Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto  akiwa na nyaraka mbalimbali alizo kabidhiwa na Rais wa TPBO Yassini Abdallah
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto  akiwa na nyaraka mbalimbali alizo kabidhiwa
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amekabidhiwa leseni kwa ajili ya ngumi pamoja na kitambulisho na nyaraka mbalimbali za kumtambua kitaifa na kimataifa 
akizungumza wakati wa utoaji wa leseni kwa bondia huyo Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini Yassini Abdalla 'Ostadhi' amesema leseni ni jambo la muhimu sana kuwa nayo bondia kitu ambacho kila bondia anatakiwa kuwa nayo ambapo ndio hinaweka kumbukumbu yako ya mapambano yako yote uliocheza ndani na nje ya nchi kitaifa na kimataifa 
hivyo ni kitu muhimu sana leo hii natoa leseni kwa bondia Class kwa kuwa natambua kazi yake na uwezo wake akiwa katika uringo ambapo itamsaidia kwa ajili ya kazi yake kumbuka hii ni ajira hapa kajiajiri mwenyewe' mtaji wa masikini nui nguvu zake mwenyewe'
nae bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' alishukulu kwa kusema leseni itamuongezea chachu ya kupigana vizuri zaidi awapo uringoni kwani ngumi ndio mchezo anao upenda na ndio anaucheza hivyo atafanya jitiada ili aweze kufika mbali kupitia mchezo wa ngumi
bondia huyo anaenolewa na jopo la makocha kutoka kambi ya Ilala likiongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta'  Kondo Nassoro, Sako Mtulya na Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye ana msimamia katika mapambano yake mbalimbali na kumpatia ushauri  wa jinsi gani ya kupigana na watu anaokabiliana nao awapo uringoni

MAJANGA DEREVA NA UTINGO WAJIIBIA MALI WALIZOKUWA WAKISAFIRISHA KWENDA KONGO ZIKIWA NA THAMANI YA TSH MILIONI 100 ,WACHOMA LORI LILILOKUWA NA MZIGO HUO



Kamanda  wa polisi  mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi kushoto akisalimiana na mwakilishi wa kampuni ya Dandu ambao lori lao limeteketezwa kwa moto 
Kamanda  wa  polisi mkoa wa Iringa akionyesha mitumba  iliyohifadhiwa katika nyumba  moja Nyololo baada ya kufaulishwa na dereva na utingo wake kisha lori kuchoma moto 
Hii ndio  mitumba  iliyohifadhiwa mali ya wizi 
Mitumba  hiyo ikionekana kwa nje baada ya kujaa ndani ya nyumba hiyo kupita kiasi 
Safari ya kwenda  kubaini mali ya wizi iliyofanywa na kamanda wa polisi Iringa 
RPC Iringa Ramadhan Mungi akiangalia  mitumba  iliyohifadhiwa porini baada ya  kuporwa 
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akitoka  kushuhudia mabelo ya mitumba yaliyofichwa  porini kijiji cha Maguhani Mufindi 
kamanda wa  polisi Iringa Ramadhan Mungi akimwonyesha mmiliki wa nyumba iliyohifadhi  mali  hizo za wizi kulia na dereva wa gari hilo mbele lenye namba  T 185 CJM ambalo  ndilo lilikuwa likisomba mali  hizo za wizi kutoka katika  lori lililochomwa moto 
Watuhumiwa wa  wizi wa mali  zilizokuwa  zikisafirishwa na lori la kampuni ya Dandu 
Hili ndilo lori  lililokuwa na mali  hizo  chini kukiwa na ubichi wa mafuta  ya taa yaliyomwagwa ili  kulilipua lori hilo bila mafanikio 
Mwonekano wa lori hilo kwa ndani baada ya mali zote  kuhamishwa kwa  lengo la kuziiba 
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akionyesha  lori hilo mali ya kampuni ya Dandu ambalo limechomwa moto na dereva na utingo wake baada ya  kufaulisha mali zote kwa lengo la kuiba 
JESHI la  polisi  mkoa  wa Iringa kupitia dhana ya polisi  jamii na ulinzi shirikishi  limefanikiwa  kukamata  mali za wizi zilizokuwa  zikisafirishwa kwenda nchi ya DRC Kongo zikiwa na thamani ya  Tsh milioni 100 pamoja na lori  lenye thamani  ya Tsh milioni 100 ambalo liliteketezwa kwa  moto kabla ya dereva na utingo wa  lori hilo  kulichoma moto kama njia ya kupoteza ushahidi.

Imedaiwa  kuwa  watu  zaidi ya 6  wanashikiliwa na  jeshi  hilo la polisi akiwemo  dereva  na utingo  wake ambao wanadaiwa  kuhusika na tukio  la wizi  huo.

Kamanda  wa  polisi mkoa  wa  Iringa Ramadhan Mungi  alisema  kuwa  tukio hilo  lilitokea juzi May 31 ambapo  askari  wa  doria  wilaya ya Mufindi  wakiwa katika shughuli   hiyo ya doria  walifanikiwa  kuliona  lori hilo  likiwa  limeegeshwa kando ya  barabara ya Iringa –Mbeya  eneo la Kinegembasi wilaya ya Mufindi  huku likiwa  limeteketea kwa moto katika kibini yake.

Alisema kuwa  watu hao waliteketeza lori lenye namba za usajili  T527 DPQ likiwa na tela lenye namba  T 974  EFE  aina ya  scania mali ya kampuni ya Dandu ambalo  walilikuta  likiungua   huku silizi  zake zikiwa  zimefunguliwa na  baada  ya uchungu wa awali  walibaini  kuwa lori hilo  lilikuwa limebeba mitumba na viatu  na baada ya msako  ndipo  walipofanikiwa  kukuta mitumba  hiyo  ikiwa imefichwa katika  nyumba moja kuukuu mali ya mama  Gray Mpinga  mwenyeji wa Maguhani Mufindi.

POLISI FEKI WAKAMATWA MKOANI IRINGA






Kamanda wa  polisi mkoa wa Iringa,Ramadhan Mungi akiwaonyesha maaskari  feki ambao  walikuwa wakifanya utapeli katika mikoa ya Iringa na Morogoro ,kulia ni Bazil Nyakunga ambae ni mwalimu akiwa na sare za polisi na katikati ni bossi wake Godlack Mbehale.
Askari polisi Mkoani Iringa (kushoto) akiwa na maaskari  feki katika ofisi ya kamanda wa polisi  leo 


Na Francis Godwin,Iringa

MATAPELI washindwa  kubaki njia  kuu sasa waanza  michepuko  mipya ni baada ya jeshi la  polisi mkoa  wa Iringa kumkamata  mwalimu aliyejifanya askari akiwa na fullu kombati za jeshi la polisi na  bossi wake aliyevalia kiraia ambae pia ni  feki  na ni  mmiliki wa studio eneo la Kihesa mjini hapa.

Upo usemi  usemao  kuwa usiombe  likukute usilo litegemea kukukuta katika maisha yako na ukipenda kudanganya uwe tayari kudanganywa  ,hakuna asiyepata  kusikia ama kusoma habari kuhusu utapeli  unaoendelea hapa nchini kwa  watu wa kada mbali mbali na mazingira  yanaonyesha matapeli hawa  siku  zote ni watu  wanaopenda wengine yawakute na sio  wao na hata kupenda kudanganya na sio kudanganywa kama ambavyo mwalimu huyo Bazil Nyakunga (20) ambae anatuhumiwa  kutapeli  wazazi wengi Iringa na Morogoro ambao  wanataka  watoto wao kwenda kusomea uaskari .

Mwalimu Nyakunga  akiwa na bossi  wake  feki Godlack Mbehale (21) walijikuta matatani kwa  kukutwa na wasilotegemea  kulipata  baada ya  jeshi la  polisi kuweka mtego kufuatia wananchi wengi kufika  polisi  kulalamikia utapeli huo wa  ajira  kwa vijana  wao katika  jeshi la  polisi.

Ramadhan Mungi ni kamanda  wa  polisi  wa mkoa  wa Iringa alilitonya gazeti  hili kuwa jeshi  lake  lilipopata stori   hiyo ya utapeli  waliweka mtego eneo la Ipogolo ambapo askari huyo feki alikuwa amepiga kambi la kitapeli kwa  kuwasanua mavumba wazazi wenye uchu wa  watoto  wao kuwa mageda (ma Askari).

Alisema  kuwa  vijana  hao ambao  mmoja  Nyakunga ambae ni mkazi wa Ilula Mtua katika  wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ni kijana  aliyepata  kusoma kozi ya ualimu mkoani Shinyanga  na kuwa ndie  alikuwa akijifanya na askari  polisi na muda  wote  alikuwa akivaa sare za jeshi  hilo.

Mungi  alisema  kuwa  kijana  huyo na mwenzake  wamepata  kuwaliza  watu wengi  sana Iringa na Morogoro na  kuwa mtu wa mwisho  wamemliza kiasi cha Tsh 900,000 na kuwa njia  wanayotumia ni Nyakunga kama askari  baada ya  kumpata  mazazi na mtu mwinye uhitaji na ajira ya  polisi amekuwa akipiga simu kwa boss  wake Bw Mbehale na kuiweka simu hiyo katika mfumo wa Laudi spika ili mtu anayetapeliwa  kupata  kusikiliza vema mazungumzo hayo.

“ Nyakunga kama askari  feki  baada ya  kumpata mteja  wa kumtapeli amekuwa akiweka simu yake katika  sauti  kubwa na huyo boss  wake amekuwa akisikika akipanga gharama za mtapeliwa  kulipia na baada ya  kutoa  pesa  wamekuwa  wakiingia mitini kwa kumta ahadi feki….mfano anapopiga simu anajifanya samahani boss naomba maelekezo ya mwisho huyu mzazi /kijana anataka kazi anapaswa kutimiza nini kwa  sasa kabla ya kuitwa katika usaili ”.

Hata  hivyo kamanda Mungi alisema  kuwa ni  vema  wananchi kuchukua  tahadhari juu ya utapeli huo na kuwa kazi za polisi kwa  sasa haziingizwi kwa mtindo huo na kuwa jeshi  hilo lina utaratibu wake wa kuingiza  vijana ikiwa ni pamoja na kuwachucha toka  sekondari  kwa kujaza fomo huku wale  wa elimu ya  juu  upo utaratibu na  wale  wanaochukuliwa kwa utaalam  wao pia  wanautaratibu wao  na si vinginevyo.

Alisema  kuwa  hakuna  usaili  wa askari  unaofanywa  mitaani ama  wilayani  hivyo vijana  hao  walikuwa  wakifanya utapeli  na ni vema  wananchi  kuchukua tahadhari  kubwa .

Pia  alisema jeshi lake  linafanya uchunguzi  ili  kubaini eneo  ambalo matapeli hao  walipata  sare  hizo za  jeshi la  polisi na mbinu  waliyotumia  kuzipata sare  hizo ikiwa ni pamoja na kuwafikisha  mahakamani.

Hata  hivyo kwa  upande wao matapeli  hao  walidai kuwa   ni kweli  wanafanya kazi na ualimu na mmoja na mmiliki wa  studio eneo la Kihesa mjini  Iringa na  kuwa sare  hizo  walizipata kutoka kwa rafiki yao ambae ni askari polisi aliyewatuma kuzifikisha kwa ndugu yao askari .

KAMPUNI YA BANTU SPORTS AND FITNESS ENTERPRISE WATOA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO KWA SHULE YA MSINGI MIONO, CHALINZE PWANI



Viongozi wa Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, wakipanda mti wakati wa Uzinduzi wa Kampuni hiyo iliyoambatana na utoaji wa Msaada wa Vifaa vya Michezo na vya mafunzo ya kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na kutunza mazingra katika Shule ya Sekondari Miono na Kikaro zilizopo Chalinze Mkoa wa Pwani.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kevin William na Alex Mode wa Shule ya Kikaro wakichuana kuwania mpira baada ya kupokea msaada wa Vifaa vya Michezo na vya mafunzo ya kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya uliotolewa na Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwamtumu Mahiza kulia akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kikaro, Alex Mode, mbuzi aliyetolewa na Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise inayotoa elimu ya kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo pia kampuni hiyo imetoa vifaa mbalimbali vya michezo katika shule mbili hizo. Miono Kikaro zilizopo Chalinze Mkoa wa Pwani.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari, Kikaro wakiwa wamembeba juu juu mbuzi waliopewa na Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, inayotoa elimu ya kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo baada ya kuifunga timu ya Shule ya Sekondari Miono kampuni hiyo pia imetoa vifaa mbalimbali vya michezo katika shule mbili hizo.
Mbia wa Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, inayotoa elimu ya kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo Mashuleni, Said Said kulia akimkabidhi msaada wa vifaa vya kuelimisha wanafunzi jinsi ya kuepukana na matumizi ya madawa ya kurevya Mwalimu wa Shule ya Sekondari Miono, Ally Miango shuleni hapo juzi.