Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, August 13, 2015

SIKU YA KIMATAIFA YA VIJANA DUNIANI YAADHIMISHWA KWENYE VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR



Maandamano  yakiongozwa na bendi ya jeshi la polisi
 
Baadhi ya vijana kutoka shule mbalimbali wakiandamana kuingia katika viwanja vya mnazi mmoja wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishw  jijini Dar es Salaam. Mashirika mbalimbali  ya mataifa yanayofanya shughuli za vijana ni kamaUNFPA, IYF, UNIC, ILO, RESTLESS DEVELOPMENT, YUNA, AMREF, MARIE STOPES, pamoja na PSI.(Picha zote na Geofrey Adroph)
 
 Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na viongozi wengine wakipokea maandamano ya vijana wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi na wapili kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bibi. Natalia Kanem.
 
 Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja viongozi wengine wakipokea maandamano ya vijana wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.
 Viongozi katika meza kuu wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani iliyoadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem akizungumza na vijana wakati wa Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Katika hotuba yake aliweza kuzungumzia maswala ya watoto wa kike kubeba mimba wakiwa na umri mdogo ambao unapelekea kuacha masomo kutokana na ujauzito huo pia aliwasisitiza vijana kuwa na umoja kwani ndio nguvu kazi ya Taifa.
Mwendeshaji wa Sherehe hiyo Bi. Usia Nkhoma ambaye ni Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC)  akizungumza jambo na  vijana walioshiriki maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi(wa nne kutoka kulia) akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na vijana wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Wa tatu kutoka Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, Wa kwanza kulia ni Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum na wa pili kutoka kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem.
 Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akitoa shukrani kwa wawakilishi wa Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum na wa pili kutoka kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem.
Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwahutubia vijana walioshiriki maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake aliwasisitiza vijana kujitokeza katika uchaguzi unaotegemea kufanyoka mwezi wa kumi mwaka huu ili kuchagua viongozi makini watakaoweza kutetea masuala ya vijana na pia aliwasisitiza vijana kufanya kazi za kujitolea.
 Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum akiwasalimia vijana walioshiriki maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Bw. Hesein Melele(wa kwanza kuli) kijana ambaye ni mwakilishi wa asasi ya vijana chini ya umoja wa mataifa (YUNA) akiwasilisha maazimio yaliyofikiwa na vijana wakati wa kongamano lililofanyika Agosti 10 mwaka huu kujadili ujumbe wa siku ya kimataifa ya vijana duniani na kuandaa maazimio yaliyowasilishwa kwa mgeni rasmi leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja walipokua wakiadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani.
 Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani, Tatu Ahmed akitoa shukrani kwa wageni waalikwa waliofika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja walipokua wakiadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani.
Mratibu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutoka asasi ya vijana chini ya umoja wa mataifa (YUNA), Rahim Nasser akiwatolea ufafanuzi vijana waliofika kwenye banda la Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani  Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akimsikiliza kwa makini Mratibu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutoka asasi ya vijana chini ya umoja wa mataifa (YUNA), Rahim Nasser alipotembelea kwenye banda la Umoja wa Mataifa
 Mkufunzi wa Ujasiriamali/Biashara wa Program ya anzisha na imarisha biashara yako (SIYB) iliyochini ya Shirika la Kazi Duniani (ILO), Bw. MacDonald Lanzi (wa pili kutoka kulia) akimfafanulia jambo Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel. Wa pili kushoto ni Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum na wa kwanza kutoka kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem.
Mshauri na Mkufunzi wa Ujasiriamali/Biashara wa Program ya anzisha na imarisha biashara yako (SIYB) iliyochini ya Shirika la Kazi Duniani (ILO), Bw. Lawrence Ambokile(mwenye koti jeusi) akitoa ufafanuzi kwa Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipotembelea banda ilo
 Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akisaini kitabu katika kwenye moja ya bada la PSI Tanzania katika Viwanja vya Mnazi Mmoja walipokua wakiadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani. kushoto ni Dkt. Benedict Nyiro
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem akisaini kitabu katika kwenye moja ya bada la PSI Tanzania katika Viwanja vya Mnazi Mmoja walipokua wakiadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani. kushoto ni Dkt. Benedict Nyiro
 Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum akisaini kitabu katika kwenye moja ya bada la PSI Tanzania katika Viwanja vya Mnazi Mmoja walipokua wakiadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani. kushoto ni Dkt. Benedict Nyiro
Ofisa Habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC), Stella Vuzo(wa kwanza kushoto), Meneja mradi wa ICS Bi. Imisa Masinjila(wa pili kutoka kushoto)Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara hiyo Prof. Hermas Mwansoko(wapili kutoka kulia) pamoja na Imisa Masinjila wakizungumza jambo maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum(wa kwanza kushoto) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem(katikati) wakizungumza jambo na  Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi  wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania Bi. Hashina Begum pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi. Natalia Kanem wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya vijana waliofika kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Bw. Hesein Melele(katikati) kijana ambaye ni mwanachama wa asasi ya vijana chini ya umoja wa mataifa (YUNA) akiwa kwenye picha ya pamoja na vijana wenzake ambao ni Rehema Pascal(kushoto) pamoja na Felister
  
 
 
 
 
 
 
 

 Vijana kutoka vikundi mbalimbali wakitoa burudani wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 
 
 
Vijana wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Sunday, August 9, 2015

BONDIA LULU KAYAGE AIBUKA KIDEDEA AFRIKA YA KUSINI

BONDIA wa Kike Lulu Kayage mwishoni mwa wiki iliyopita alibuka kidedea nchini Afrika ya kusini baada ya kumdunda vibada   Lizbeth Sivhaga wa nchini humu
huu ni mpambano wake wa kwanza Lulu kucheza nje ya nchi na kufanikiwa kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili mchezo uho ulioanza kwa kasi ya mashambulizi ya uku na kule kila mmoja kutaka kumpiga mwenzie raundi za awali

ata hivyo ilivyofika raundi ya pili bondia Lulu Kayage alimwelemea sana mpinzani wake kwa makonde mfululizo na wasaidizi wake kumuokoa kwa kumtupia taulo hivyo kusababisha Lulu kushinda T.K.O ya raundi ya pili

ushindi wa Llulu Kayage ulichagizwa na kocha maarufunchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambapo siki mbili kabla ya kuondoka nchini alimzawadia vifaa mbalimbali vya mchezo wa masumbwi na kumwaidi ushindi kwa asilimia zote

bondia huyo anatarajia kurudi nchini agost 11 kwa ajili ya maandalizi ya mapambano yake mengine ya kimataifa wakati uho uho bondia Ramadhani Shauri amepoteza mpambano wake kwa kupigwa K.O ya raundi ya nne na bondia mzoefu Philip Ndlovu wa Afrika ya Kusini ambapo mpambano uho wa raundi nane ulijikuta ukisha katika raundi ya nne

Bondia Lulu Kkayage akiwashukuru mashabiki walio udhulia kwa kuwapigia magoti na kuwapungia mikono baada ya kumchakaza bondia Lizbeth Sivhaga wa Afrika ya Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na SUPER D BOXING NEWS

Refarii akiwa katikati uku akiwashika mikono mabondia Llulu Kayage na Lizbeth Sivhaga wa Afrika kusini kwa ajili ya kutangaza mshindi Lulu alishinda kwa TKO ya raundi ya pili kushoto ni Yassini Abdallah
Picha na SUPER D BOXING NEWS
Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' akimnyoosha mkono juu bondia Lulu Kayage baada ya kuibuka mshindi
Yassin Abdallah 'Ostadh' akimwinua juu mkono baada ya kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili

Saturday, August 8, 2015

MABONDIA LULU KAYAGE NA RAMADHANI SHAURI WAPIMA UZITO


Bondia lulu KayaGE AKIWA NA WAPENZI WA NGUMI aFRIKA YA kUSINI
Wakifuraia kwa pamnoja
 Mabondia Lulu Kayage kushoto Yasini Abdballa na Ramadhani Shauri

LULU KAYAGE NA RAMADHANI SHAURI WATUA AFRIKA YA KUSINI KWA AJILI YA KUPAMBANA AGOST 9

 Mabondia Lulu Kayage kushoto na Ramadani Shauri katikati wakiwa katika picha ya pamoja na Promota wao Afrika ya kusini mara baada ya kushuka katika ndege mwingine ni rais wa TPBO Yasini Abdallah
MABONDIA LULU KAYAGE NA RAMADHANI SHAURI WAKIPOKELEWA NA WENYEJI WAO

PROMOTA AKIPEANA MIKONO NA MABONDIA BAADA YA KUWAPOKEA UWANJA WA NDEGE AFRIKA YA KUSINI

Wednesday, August 5, 2015

SUPER D AZAWADIA BONDIA LULU KAYAGE VIFAA



Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimpatia zawadi ya vifaa vya mchezo wa ndondi kikingia kinywa pamoja na clip bandeji na fulana yenye ndembo ya taifa hiii ni kwa ajili ya kumpa sapoto bondia huyo anaenda kupigana afrika ya kusini agost 9 na bondia Lizbeth Sivhaga wa uko anaeshudia katikati ni rais wa TPBO Yassini Abdallah Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimpatia zawadi ya vifaa vya mchezo wa ndondi kikingia kinywa pamoja na clip bandeji na fulana yenye ndembo ya taifa hiii ni kwa ajili ya kumpa sapoto bondia huyo anaenda kupigana afrika ya kusini agost 9 na bondia Lizbeth Sivhaga wa uko anaeshudia katikati ni rais wa TPBO Yassini Abdallah Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimpatia zawadi ya vifaa vya mchezo wa ndondi kikingia kinywa pamoja na clip bandeji na fulana yenye ndembo ya taifa hiii ni kwa ajili ya kumpa sapoto bondia huyo anaenda kupigana afrika ya kusini agost 9 na bondia Lizbeth Sivhaga wa uko anaeshudia katikati ni rais wa TPBO Yassini Abdallah Picha na SUPER D BOXING NEWS


Na Mwandishi Wetu

KOCHA wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila amemzawadia bondia Lulu Kayage vifaa vya mchezo wa masumbwa baada ya bondia huyo kuchaguliwa kwenda kupigana Afrika ya kusini agust 9 mwaka uhu vifaa hivyo alivyokabidhiwa bondia huyo ni Gumshilt 'kikingiakinywa' clip bandeji pamoja na fulana yenyenembo ya Tanzania vifaa ambavyo ni lazima bondia awe navyo

Lulu kayage anaondoka nchini agous 7 kwenda afrika ya kusini kupambana na Lizbeth Sivhaga Mapambano haya yatafanyika kwenye mji wa Limpopo siku ya jumapili

akizungumza baada ya kupokea msaada huo Lulu alimshukuru Super D kwa kujitolea alichojaliwa kwa kuwa sio watu wote wenye mioyo ya kujitolea kama yeyey hivyo amemwakikishia kumpa zawadi ya ushindi ili aendelee kuwa na furaha mana ushindi wangi ni wa watanzania wote hivyo sito wahangusha

nae Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallahh 'ostadh' aliongeza kwa kusema Lulu atambatana na bondia Ramadhani Shauri atakaekwenda kupambana na bondia mzoefu Philip Ndlovu  siku hiyo hiyo msafara huo utakuwa na watu watatu ukiongozwa na mimi mwenyewe pamoja na mabondia wawili 

ata hivyo namshukuru kocha Super D kwa kumzawadia Lulu kwani tungepata watu wengi wa kujitolea kwa moyo mmoja kama yeye michezo yetu ingefika mbali zaidi Duniani

LULU KAYAGE KUZIPIGA AFRIKA KUSINI




Bondia Lulu Kayage (kushoto) akimrushia konde bondia  Hamisi Berege wakati wa mazoezi yaliyofanyika kwene Uwanja wa Msimbazi Rovers Ilala jijini


MABONDIA wawili wa ngumi za kulipwa wanatarajia kuondoka nchini kesho kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mapambano yatakayofanyika Agosti 9, mwaka huu.

Akizungumza jijini kocha wa ngumi za kulipwa, Rajabu Mhamila  'Super D' aliwataja mabondia hao kuwa ni Lulu Kayage na Ramadhan Shauri.

“Lulu na Shauri wamepata mapambano yatakayochezwa Agosti 9, hivyo wataondoka kesho kwa ndege ya shirika la Ethiopia “, alisema Mhamila.

Pia Mhamila alisema Lulu atapigana na Lizbeth Sivhaga na Ramadhan Shauri atapigana na bondia mzoefu Philip Ndlovu 

Mapambano haya yatafanyika kwenye mji wa Limpopo hivyo watanzania mnawaombwa kuwaombea mabondia hao ili waweze kupeperusha bendera ya taifa vema.

Wednesday, July 29, 2015

SELCOM YAONGEZA MAPATO YA TAZARA COMPUTER TRAIN KASI



 
 
KAMPUNI ya Selcom Tanzania imesema kwa kushirikiana na Tazara imefanikiwa kuongeza mapato ya fedha kwa mfumo wa ukatisha tiketi ulioanza kutumiwa na shirika la reli la Tazara.

Akizungumza na mwandishi  wa gazeti hili, Bw. Juma Mgori,  ambaye in Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko wa Kampuni ya Selcom Tanzania, alisema  kupitia vifaa vyao vya kukata tiketi (POS), wananchi wameondolewa adha kubwa waliyokuwa wakiipata wakati wa kukata tiketi katika shirika reli la Tazara.

Alisema kuwa, kutokana na mpango huo,  TAZARA imefanikiwa kuongeza mapato kwa abiria kukatiwa tiketi kwa mfumo wa mashibe hizo.

Mfumo huo ni rahisi na bora zaidi na hivi karibuni kampuni ya Selcom inatarajia kuzindua kadi zake mpya za malipo zijulikanazo kama SELCOM PAYPOINT CARD ambazo mbali na malipo mbalimbali na uwezo wa kutuma Pesa kwenye mitandao yote.

 Kadi hizo zinaweza kuwa njia sahihi kwenye njia za usafiri kama treni, mabasi ya mikoani na hata daladala.

Bw. Mgori alisema kuwa, kadi hizo ni salama na zenye uwezo mkubwa zikiwa zimethibitishwa na kuidhinishwa katika viwango vya nchini na hata vya kimataifa.

"Tunajivunia ubunifu wetu huu ambao unafanyika hapa nyumbani na kampuni ya kizawa na wataalamu wazawa. Ikumbukwe pia kadi hizi hivi sasa zinatumika na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa wale wastaafu kutoa Pesa zao na ziko kwenye majaribio.