Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, March 27, 2013

SIRI YA KUUAWA KWA ZITTO KABWE




Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘ SIRI YA KUUAWA ZITTO YAFICHUKA’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ Dk. Slaa atajwa kumtuma Ben Saanane kummaliza’. 

Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa. Napenda kusema yafuatayo:

Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.

Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.

Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.

Nne, Nawashauri viongozi wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.


Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Dar-es-Salaam
Jumatano, Machi 27, 2013

EAST AFRICA BAR WATAA UBINGWA WA MASHINDANO YA SAFARI LAGER NYAMA CHOMA MJINI MOSHI



Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Dr.Ibrahim Msengi(wa pili kulia) akimkabidhi Meneja wa Bar ya East Africa,Godfrey Mawala(kulia)Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.Wapili kulia ni Mpishi Mkuu Wilfred William na Meneja Mauzo wa Moshi, Edmundi Rutaraka
 Mashabiki wa Bar ya East Africa wakishangilia mara baada ya kutangazwa washindi wakati wa shindano la Safari Nyama Choma lililofanyika katika Viwanja vya CCM Mkoa Mwishoni mwa wiki.
EAST AFRICA BAR, wametwaa ubingwa wa mashindano ya Nyama Choma Mkoa wa Moshi, baada ya kuzigaragaza baa nne zilizotinga fainali ya mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Safari Lager.
Kwa kutwaa ubingwa huo katika fainali zilizofanyika juzi Jumapili kwenye Viwanja vya CCM Mkoa , baa hiyo ilizawadiwa fedha taslim Sh milioni moja pamoja na cheti.
Waliokuwa mabingwa watetezi wa mashindano hayo mkoani hapa, Makanyaga Bar, walishika nafasi ya pili na kuondoka na kitita cha Sh 800,000 na cheti, wakati White Star Pub walishika nafasi ya tatu na kupata zawadi ya Sh 600,000 na cheti.
Walioibuka na nafasi ya nne ni baa ya Forest Bar iliyozawadiwa Sh 400,000 na cheti, wakati baa ya Lamina ilishika nafasi ya tano na kuzawadiwa Sh 200,000 na cheti.
Akizungumza kabla ya kumtangaza mshindi, Jaji Mkuu wa fainali hizo, Douglas Sakibu, alisema kuwa walitoa mafunzo kwa baa zote hizo juu ya mambo wanayopaswa kuzingatia katika uchomaji nyama.
Alivitaja vigezo walivyotumia kupata mshindi kuwa ni usafi wa mchomaji, vifaa na mazingira, maandalizi ya nyama kuanzia uchaguzi, uhifadhi wake na wa vifaa.
Vingine ni uchomaji na upangaji nyama, ladha na ulaini wake, mazingira ya eneo, mtiririko wa maji na uhifadhi wa taka.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, alisema kuwa ni fahari kubwa kwa TBL na bia ya Safari Lager kwa ujumla kufanikisha shindano hilo mkoani ambao ndio mkoa wa mwisho.
“Tulianza kwa kuwataka watu wapige kura kupendekeza baa zinazofaa kuingia katika shindano la nyama choma kwa mkoa huu wa Moshi tukapata baa hizi tano zilizoingia fainali ambapo leo tutampata mshindi.
“Tunajua watu huwa wanakwenda katika baa na kula nyama hivyo tukaona ni vema tuanzishe mashindano haya ili walaji nyama choma wapate nyama bora,” alisema.
Alisema kuwa bia ya Safari Lager ina miaka takriani 36 na bado imeendelea kuwapo hadi sasa ambapo  ndio inayoongoza kwa mauzo.
Kwa upande wake, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Dr.Ibrahim    Msengi, aliisifu TBL kupitia Safari Lager kwa kuandaa mashindano hayo, akisema kuwa serikali inatambua mchango wa kampuni hiyo katika kujenga uchumi wa Taifa kupitia tukio hilo na mengineyo kama mashindano ya Pool Safari Lager, Safari Wezesha na hata udhamini wao katika michezo mbalimbali kama soka na mingineyo.
“Mashindano haya ni mazuri kwani yanawajengea wateja wa nyama mazingira mazuri na salama katika kutoa huduma hii ya nyama choma,” alisema.
Alizitaka baa ambazo hazikufika fainali, kutokata tamaa na badala yake kujipanga kwa ajili ya mashindano ya mwakani, kwa kurekebisha yale waliyokosea mwaka huu.

Simba chali Kaitaba, Azam ikitakata Dar




WAKATI wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa, Azam wakitaka jijini Dar kwa kuigaragaza Prisona ya Mbeya kwa mabao 3-0, mabingwa watetezi Simba wamejikuta wakiangukia pua mjini Kagera baada ya kudunguliwa bao 1-0 na wenyeji wao Kagera Sugar.
Azam walipata ushindi huo kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Chamazi, na kuweza kupunguza pengo la pointi kati yao na vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wanaoongoza wakiwa na pointi 48.
Mabao mawili na kinara wa ufungaji bora kwa sasa Kipre Tchetche na moja ya John Bocco 'Adebayor' yalifanya Azam ikifikishe pointi 40 na kuweka matumaini ya kuikamata Yanga ambayo haikushuka dimbani leo.
Bao la kwanza la Azam lilifungwa na Kipre katika kipindi cha kwanza kabla ya Bocco kuongeza la pili kipindi cha pili na Kipre kuongeza bao la tatu dakika za jioni na kuifanya Azam kutakata kabla ya kuvaana na Barrack YCII watakaorudiana nao katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika siku ya Jumamosi.
Wakati Azam wakimeremeta Dar, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Simba yenyewe walikiona cha mtema kuni baada ya kulambwa bao 1-0 na Kagrea Sugar katika pambano jingine lililochezwa uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.
Bao la sekunde chache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili lililofungwa kwa kichwa na beki Amandus Nesta akiiunganisha kona ya Salum Kanoni iliifanya Kagera kufika pointi 34 sawa na Simba.
Hata hivyo Kagera imekamata nafasi ya nne kutokana na kuzidiwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa na Simba ambao wamezidi kuwasononesha mashabiki wao ambao wamekuwa hawana raha kwa timu yao kuwa na matokeo mabaya msimu huu tofauti na matarajio yao.
Ushindi huo wa Kagera imekuwa muendelezo wa kuvinjuka 'vigogo' kwenye uwanja wake wa nyumbani kwani hata Yanga walipoenda mjini humo walipigwa bao 1-0 na kuibua tafrani kwa waandishi wa habari waliotuhumiwa kuhujumu pambano hilo.
Kagera mbali na kuikamata Simba kiponti pia imeziengua timu za Mtibwa Sugar na Coastal Union ambazo sasa zimeporomoka katika nafasi walizokuwa wakizishikilia hadi nafasi ya tano na sita badala ya zile za nne na tano walizokuwa wakishikilia awali.
Baada ya kipigo hicho Simba inatarajiwa kusafiri mpaka jijini Mwanza kuvaana na timu ya Toto Africans ambayo huwa inawasumbua kwenye dimba la CCM Kirumba.

Tuesday, March 26, 2013

KING CLASS MAWE ATAMBA KUMGALAGAZA MWAMAKULA MEI MOSI



SUPER D KUSHOTO AKITOA MAELEKEZO KWA KING CLASS
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Ibrahimu  Class 'King Class Mawe' anaendelea kujiandaa 
kumkabili Amosi Mwamakula katika pambano la utangulizi wakati wa
mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.
Pambono la raundi nane linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA
Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi mwaka huu, linatarajiwa kuwa la vuta
nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.
Kocha wa King Class Mawe, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa
bondia wake anajianaa vema kwa ajili ya  kumchakaza Mwamakula bila ya huruma ili
kuendelea kujiwekea rekodi nzuri.
"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya
vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na  Mashali" alisema
Super D.Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD  za mafunzo ya mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Fransic Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe. nyingine zitakuwa
zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

JK AFUNGA MAFUNZO YA JKT KWA VIONGOZI




Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbunge wa viti maalum Ester Bulaya leo katika kambi ya RUVU JKT.Rais Kikwete amefunga rasmi mafunzi hayo leo yaliyofanyika kwa wiki tatu.
Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT huko kibaha Mkoani Pwani leo.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi kutoka kwa kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu wakati wakimaliza mafunzo
ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa
Tanga.
Picha Zote za Tanga na Hussein Semdoe.
wakwanza katika mstari wa kushoto ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anayefuata ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, wakiwa kwenye Paredi ya kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT Kikosi cha
835 Mgambo JKT kambi iliyopo katika Kata ya Mgambo ilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
wakwanza kushoto ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani pamoja na Mbunge
wa Kigoma Kaskazini, ZItto Kabwe, wakihitimu mafunzo ya JKT katika kambi ya 835 Mgambo JKT iliyopo Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya
JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu
wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Biharamulo, Dk Athanas Mbassa, akiapa wakati wa kumaliza
mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. 
Mbunge wa Kiwani Pemba, Abdallah Haji Ali, , akiapa wakati wa
kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akiapa mbele ya kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu, hayupo pichani, wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge Viti maalum Raya Khamis , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya
JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu
wilayani Handeni.
Baadhi ya Wabunge walikuwa wakichukua mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waheshimiwa wabunge waliohitimu mafunzo maalumu ya JKT leo
Mbunge wa Mtera Mh. Livingstone Lusinde  Kibajaji"  (wa tatu toka kulia) akipiga kwata leo huko Ruvu

(COMMUNITY CENTRES) VITUO VYA KIJAMII BADO VINAHITAJIKA KATIKA MAENDELEO YA JAMII YETU



Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya Maafisa Habari kutoka sekta mbalimbali wakiwa kwenye warsha,wakijadiliana na kutafuta  njia   mbadala itakayosababisha wananchi kujua mambo mbalimbali ya kimaendeleo  ya nchi ili kujua hali halisi ya uchumi wa nchi inavyoendelea na mengineyo.
Pichani ni baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii wakijadiliana moja ya mada iliyohusu haia ya kurudisha vituo vya kijamii (Community Centres),katika masuala mazima ya kuilemisha na kuifahamisha jamii mambo mbali yakiwemo ya kimaendeleo,Warsha hiyo ilifanyika kwa  kwa hisani kubwa ya kitengo cha mawasiliano cha wizara ya fedha na wanahabri wengine wakiwemo wa mitandao ya kijamii,ambapo mijadala mbali mbali ya jinsi ya kuwasiliana na wananchi wa kawaida   ilikuwa ikijadiliwa.

Na Ahmedy Michuzi - Jiachie Blog.
Ipo haja ya kurudisha vituo vya kijamii ( Community Centres). Ipo haja ya kurudisha vituo vya kupashana habari vya kijamii(Community Centres) ili kuboresha utaratibu wa wananchi wa kawaida kupata taarifa za kimaendeleo kwa wakati muafaka. Tangu kuondoka kwa utaratibu wa vituo hivi ambavyo vilikuwa vikisaidia kuwapasha wananchi walio mbali na miji, taarifa mbali mbali kuhusiana na maendeleo ya nchi, kumekuwa na hali ya sintofahamu zinazopelekea wananchi hawa kupotoshwa na wanasiasa na kusababisha wananchi hawa kutokuwa na imani na serikali.

Zamani, wananchi walikuwa wakivitumia vituo hivi ambavyo vilikuwepo katika kila kata, hata kwa kuangalia tu taarifa za habari na vipindi mbali mbali vya kimaendeleo, jambo ambalo siku hizi halipo kabisa. Hii ni moja ya hoja iliyojadiliwa na wamiliki wa mitandao ya kijamii kwa kushirikiana na kitengo cha mawasiliano cha wizara ya fedha ambapo, mijadala mbali mbali ya jinsi ya kuwasiliana na wananchi wa kawaida ilikuwa ikijadiliwa.

Katika Warsha hiyo ya siku ambayo pia ilihudhuriwa na maafisa habari kutoka sekta mbali mbali za kimaendeleo, wadau walikuwa wakitafuta njia mbadala itakayosababisha wananchi kujua mambo mbalimbali ya kimaendeleo  ya nchi ili kujua hali halisi ya uchumi wa nchi inavyoendelea. 

Akifungua mjadala, Ingiahedi Mduma, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano cha  Wizara ya fedha, amesema taarifa za kimaendeleo za nchi ni haki ya kila mwananchi kujua na ndio maana sasa wameamua kukaa chini na kuumiza kichwa katika kutaka kujua jinsi ya kuwafikia asilimia kubwa ya wananchi, mijini na vijijini. Warsha hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro Parh Hotel, maeneo ya Misugusugu, wilayani Kibaha, mkoa wa Pwani ambapo pia mikakati mbali  mbali ya kimaendeleo ilijadiliwa.

ABOMOLEWA NYUMBA NA KUCHOMEWA VYOMBO VYA NDANI AKIDHANIWA MSHIRIKINA ILEMI MBEYA



Wananchi wenye hasira kali wakibomoa nyumba ya mama Atupele Kalile akidhaniwa kuwa mchawi maeneo ya ilemi Mbeya
Kazi ya kubomoa nyumba ya mama huyo inaendelea
Wengine wameshaingia ndani na kuanza kutoa vyombo nje tayari kwa kuvichoma
Mtoto wa mama Atupele akijaribu kuokoa vitu vya mama yake visichomwe moto na wanakijiji
Vyombo vinazidi kutolewa ndani ilivichomwe moto
Tayari wameshaanza kuchoma moto vyombo vya mama Atupele
Mwingine anaendelea kubomoa nyumba ya mama Atupele
Wamefyeka shamba lake lote la mahindi
Wengine wanapongezana kwa kazi waliofanya
Kushoto mama Atupele Kalile anaedhaniwa kuwa ni mshirikina akiwa na mtoto wake





MWANAMKE mmoja aliyejulikana kwa jina la Atupele Kalile (60) mkazi wa Mtaa wa Masewe Kata ya Ilemi Jijini Mbeya amenusurika kifo baada ya wananchi wa Mtaa huo kutaka kumpiga kisha kubomoa nyumba yake wakimtuhumu kwa ushirikina.
  
Wananchi hao kumtuhumu Mwanamke huyo kuhusika na upotevu wa motto mwenye umriwa miaka mitatu(3) (Judith Chengula) aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha Februai 22, Mwaka huu.
  
Kwa mujibu wa wakazi hao walisema Mtoto huyo alipotea majira ya saa 11 jioni baada ya kupoteana na dada yake  Anitha Mgaya wakiwa wametokea kanisani ambapo hadi sasa mototo huyo hakuweza kupatikana licha ya juhudi kubwa za wakazi hao kumtafuta bila Jitihada.
  
Walisema katika vikao kadhaa vilivyoitishwa mtaani hapo kwa ajili ya kutafuta mbinu za kupatikana kwa mtotolakini Mwanamke huyo hakuonesha ushirikiano jambo ambalo lilizua hofu miongoni mwa wakazi hao hali iliyopelekea kuhisiwa kuhusika na tukio hilo.
  
Walisema katika kikao kilichofanyika Machi 23 Mwaka huu majira ya Asubuhi mtaani hapo wananchi hao waliendelea kusisitiza kuwa Mwanamke huyo achukuliwe hatua kwa kuwa ndiye anayehusika na upotevu wa motto ambapo iliamriwa kwenda nyumbani kwake kufanya upekuzi.
  
Walisema baada ya kufika nyumbani kwake na kufanya upekuzi walikuta vitu vinavyohisiwa kuwa vinahusika na ushirikina ambavyo ni vitovu vya watoto wachanga watatu ambapo Mwanamke huyo baada ya kuulizwa alishindwa kutolea ufafanuzi hali iliyosababisha wananchi kupandwa na hasira na kuanza kumpiga.
  
Kutokana na tukio hilo Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa huo Nedy Mwamlima alimnusuru Mwanamke huyo katika kipigo kutoka kwa wananchi kwa kumpeleka katika kituo kikuu cha Polisi kwa usalama zaidi.
  
Baada ya mtuhumiwa huyo kunusuriwa na kukimbizwa katika kituo cha Polisi wananchi hao hawakupoza jazba zao ambapo waliamua kuteketeza nyumba ya mtuhumiwa ikiwa ni pamoja na kufyeka mazao yaliyokuwa yamepandwa jirani na nyumba yake.
Hata hivyo hasira za wananchi hao hazikuishia hapo bali walimsakama Mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina la Agnes Sika ambaye ni mke wa Mchungaji wa kanisa la Pentecost Groly  kwa madai kuwa ni rafiki wa mtuhumiwa na amekuwa akimfichia siri.
  
Jeshi la Polisi liliwahi kufika eneo laTukio na kumnusuru Agnes asipatwe na madhara ikiwa ni pamoja na kutochomewa nyumba yake ambayo tayari wananchi hao walionekana kuikimbilia kwa ajili ya kutaka kuibomoa.
  
Aidha Jeshi la polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano zaidi pamoja na upelezi ambapo Baba mzazi wa Mtoto anayesadikiwa kupotea katika Mazingira ya kutatanisha akisema anamwachia Mungu  baada ya juhudi za kumtafuta kushindikana.


picha na E. Kamanga

RAMADHAN KIDO AOMBA KURUDIANA NA MCHUMIATUMBO 'ARIVENJI'



BAADA ya kuchapwa katika mchezo wao wa kwanza uliokuwa na kila aina ya majigambo kwa mabondia, Ramadhan Kido na Mchumiatumbo, hatimaye sasa bondia mbavu nene Ramadhan Kido, anasema kuwa anamhitaji tena mbavunene mwenzake Alphonce mchumiatumbo, ili aweze kumuonyehs akuwa alimuotea na kumchapa kwa bahati mbaya katika mchezo wao ulipita.

Mabondia hao walichapana katika pambano lao la kwanza lililofanyika uwanja taifa na kumalizika kwa Bondia Kido, aliyekuwa amedhaminiwa na Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan, kuchapwa kwa KO,ambapo sasa amepania kulipa kisasi.

''Mchumiatumbo amenifanya nameshindwa kulala kwa muda mrefu sana tangu aliponipiga katika pambano lililopita, jambo ambalo limenifanya kujifua kufa na kupona kujiweka fiti ili niombe marudiano niweze kurivenji.

Siku zote nimekuwa nikimfikiria yeye kanipigajepigaje jibu sipati,nimeamua kurudi tena ulingoni kwa kujipima na Mussa Mbabe, katika pambano letu litakalofanyika siku ya jumapili Aprili 7, mwaka huu katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala.

Najua Musa ni bondia mzuri lakini siwezi kupoteza mara mbili mfululizo huu ni mwiko wangu nitahakikisha nafia ulingoni na ntajituma  kwa nguvu zangu zote na kuhakikisha namchapa kwa KO mbaya, bila huruma hata nikiua sawa tu nina uchungu sana na ngumi na nataka nimuoneshe Mchumiatumbo kuwa nakuja kivingine,na nikipigwa katika pambano la mwananyamala ni bora niache ngumi kabla ya kurudiana na Mchumiatumbo''. alisema Kido

MASHINDANO YA SHIMIWI KUFANYIKA SEPTEMBER 21 HADI OCTOBER 5 MKOANI DODOMA





SHIRIKISHO la michezo kwa wizara, idara ,taasisi na mashirika ya serikali limewataka viongozi wa michezo kudhibitisha mapema ushiriki wao katika mashindano kabla ya AUGASTI mwaka huu na kutuma majina ya michezo watakayoshiriki.
Katibu mkuu wa SHIMIWI RAMADHANI SULULU amesema mashindano hayo yamepangwa kufanyika SEPTEMBER mwaka huu mkoani DODOMA lakini yamekuwa yakigubikwa na mamluki jambo ambalo halikubaliki katika mashindano hayo 
SULULU amesema shiriki wanatakiwa kuanza mazoezi mapema ,lakini kulipa ada ya uwanachama shilingi laki sita, ada ya ushiriki laki nne na mchango wa ujenzi wa kiwanja laki mbili.
Mchezo inayoshindaniwa ni soka, netiboli kukimbia, kuvuta kamba, darts, drafti, baiskeli, karata pamoja na mchezo wa bao.

SEMINA YA VIONGOZI WA MICHEZO YA COPA COCA COLA YAFUNGULIWA RASMI




Tanzania Football Federation (TFF) President Leodegar Tenga emphases a point as he addresses over 60 delegates from across Tanzania at the opening ceremony of the Copa Coca-Cola Directive Seminar held at the National Stadium in Dar es Salaam Tuesday, March 26, 2013

Coca-Cola Brand Manager Tanzania Maurice Njowoka delivers his speech at the opening ceremony of the Copa Coca-Cola Directive Seminar held at the National Stadium in Dar es Salaam Tuesday, March 26, 2013.

 Washiriki wa semina wakimsikiliza mgeni rasmi Rais wa Tff Tenga akiwaasa kuhusiana na kuwatumia wachezaji waliozindi umri kwani wachezaji wanatakiwa chini ya miaka kumi na tano

Washiriki wa semina kutoka TANZANIA BARA na VISIWANI wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TFF akiwemo Rais wa Tff pamoja na viongozi wa serikalini semina hiyo imefanyika katika ukumbi uliopo katika uwanja wa Taifa Jijini DSM


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewataka viongozi wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuhakikisha wanaingiza wachezaji wenye umri sahihi katika michuano ya U15 FIFA Copa Coca-Cola 2013.

Ametoa mwito huo leo (Machi 26 mwaka huu) wakati akifungua semina elekezi ya michuano ya Copa Coca-Cola ambayo kuanzia mwaka huu itakuwa ikishirikisha watoto wenye umri chini ya miaka 15.

Rais Tenga amesema hakuna jambo la kipuuzi kama kuchomekea wachezaji ambao wamezidi umri unaotakiwa kwa vile lengo la michuano ya aina hiyo ni kubaini vipaji na kuwafanya watoto wapende kucheza mpira wa miguu.

“Kwanza nawashukuru kwa kutenga muda wenu na kuhudhuria semina. Lakini ni vizuri pia mkahakikisha mnakuwepo kwenye mashindano ili kutekeleza haya ambayo tutakubaliana katika semina hii. Mkileta mtu mwingine anaweza kutuanzishia mambo mengine badala ya yale tutakayokubaliana,” amesema Tenga.

Pia ameishukuru kampuni ya Coca-Cola ambaye imekuwa ikidhamini michuano hiyo tangu mwaka 2007 ambapo semina hiyo elekezi inayoshirikisha makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na waratibu wa mikoa wa michezo ya UMISSETA ni ya saba mfululizo.

Ratiba ya michuano hiyo kuanzia mwaka huu imebadilika ambapo sasa itaanzia ngazi ya wilaya Aprili wakati fainali katika ngazi ya Taifa itachezwa Septemba

SOLOMON MUKUBWA, NTABOBA WATUA DAR KUWASHA MOTO TAMASHA LA PASAKA



Mwimbaji wa nyimbo za injili, Solomon Mukubwa, akihojiwa na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya kushiriki katika Tamasha la Pasaka, ambapo katika Tamasha hilo mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri Mkuu Peter Pinda.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Faraja Ntaboba, akiimba kwa hisia moja ya nyimbo zake mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati Maalumu inayoratibu tamasha hilo la kimataifa, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu maandalizi ya tamasha hilo.
**********************************************
Na Mwandishi wetu, Dar

WAKATI muimbaji Sipho Makhabane wa Afrika Kusini akitarajiwa kutua nchini siku ya Ijumaa wiki hii, waimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamewasili jana jijini Dar es Salaa, tayari kwa ajili ya kushiriki katika Tamasha la Pasaka, litakaloanza Machi 31 kwenye Uwanja wa Taifa jijini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Kamati Maalumu inayoratibu tamasha hilo la kimataifa, Alex Msama aliwataja waimbaji waliowasili jana kuwa ni Solomoni Mukubwa (Kenya) na Faraja Ntaboba (DRC).

Msama aliwataka wapenzi, mashabiki na wadau wa muziki wa injili kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo, ambalo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ili kuunga mkono juhudi za kampuni yake kuandaa tamasha hilo kwa malengo mbalimbali ikiwemo kueneza injili ya Mungu na kusaidia makundi maalumu.

Kuhusu waimbaji, Msama alisema kuwa hadi kufikia Ijumaa, wakali wote wa nyimbo za injili kutoka nje watakuwa wamewasili jijini tayari kwa tukio hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Dar es Salaam na mikoa yote ambayo tamasha huilo litarindima.

Aidha, mkali wa aina hiyo ya muziki kutoka Kenya, Mukubwa, alisema kuwa amejiandaa vya kutosha katika tamasha la mwaka huu ambalo limebeba ujumbe wa Upendo na Amani.

“Wakati wa Uchaguzi wa Nchini Kenya tuliimba na kuhamasisha Amani na Upendo na kwa kupitia tamasha hili tutaimba nyimbo za kuhamasisha Amani na Upendo hapa Tanzania,” alisema Mukubwa. 

Naye mwimbaji kutoka DRC, Ntaboba alisema kuwa, watu wajitokeze kwa wingi katika tamasha hilo na kupata burudani itakayokwenda sambamba na mafundisho ya dini.

Msama aliongeza kuwa idadi ya waimbaji imeongezeka baada ya kujitokeza kwa nyota mwingine aliyemtaja kwa jina moja la Ntutuma kutoka Kenya, ambapo baada ya tamasha hilo kutikisa kwenye jijini Dar es Salaam, itakuwa zamu ya Dodoma, Iringa, Mbeya, Mwanza kabla ya mashambulizi kuhimishwa mkoani Mara.