Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, May 27, 2013

Kichanga cha siku nne chaokotwa shimoni alikokaa kwa siku 6





UKISHANGAA ya Mussa basi utayaona ya Firauni, usemi huu umethibitika Songea baada ya Mtoto Bahati Upendo mwenye siku 3 toka azaliwe aliyekuwa amewekwa kwenye mfuko wa mbolea kisha kutupwa kwenye shimo kuokolea akiwa hai licha ya kuishi shimoni humo kwa sita sita.
 
Ndani ya shimo hilo amekaa siku 6 bila kula wala kunywa hadi alipo okotwa na wasamaria wema...
Hivi sasa yuko Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma akiwa Salama  Salimini .
Yeyote Mwenye nafasi ya kumsaidia mtoto huyu anaweza kwenda moja kwa moja Hospitali au wasiliana na namba zifuatayo,  mchango  utafuatwa 0755061588 au 0755 731 234.
Dawati la Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma wakiwa na Wauguzi kuangalia usalama wa Mtoto huyo aliye Tupwa. Kutoka kulia ni Muguzi Rukia Twahili anaye fuata Devota Umbela na aliye mshika mtoto Mwenyekiti wa Mtandao wa Police Wanawake Fadhila Chacha na wa mwisho kushoto ni A nna Chaima

USAHIRI WA SHINDANO LA BIBI BOMBA WAFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA LEADERS CLUB, TAMASHA LA NYIMBO ZA MAKABILA LINAENDELEA



Mshiriki wa shindano la Bibi Bomba, Bi. Veronica Kayombo (katikati) akionesha umahiri wa kuimba nyimbo wakati wa mchujo wa kuwatafuta washiriki 10 watakaoingia katika nyumba kwa ajili ya shindano hilo lililoandaliwa na Clouds Tv na kudhaminiwa na Airtel. Kushoto ni Anna Nicolous na Rozalia Marko
 Majaji wa Shindano la 'Bibi Bomba' kutoka (kushoto) Zamaradi Mketema, Babuu wa Kitaa, Regina Mwalekwa na Benny Kinyaiya, wakifuatilia washiriki wakati wakijieleza kuhusu ufahamu wa shindano hilo, lililoanza leo katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, wakati wa Tamasha la Nyimbo za Makabila 'Tamadunika' linaloendelea hivi sasa viwanjani hapa.
 Mmoja kati wa washiriki 32, akijieleza wakati wa mahojiano rasmi viwanjani hapo....
  Mmoja kati wa washiriki 32, akijieleza wakati wa mahojiano rasmi viwanjani hapo....
 Baadhi ya wanacrew wasimamizi wa shoo hiyo, wakiwa eneo la tukio.....
 Babu wa Kitaa, (kushoto) akiburudika kwa miondoko ya sebene na mmoja wa washiriki wa shindano hilo.
 Sehemu ya washiriki waliojitokeza kushiriki shidano hilo...
 Mshiriki akijieleza......
 Watazamaji wakifuatilia shindano hilo......
Waongozaji wa Tamasha hilo, wasema lolote, Mbwiga Mbwiguke na Suzzy Bartazar, wakijiandaa kusherehesha Tamasha hilo la Nyimbo za Makabila.
 Benny Kinyaiya, akitoa maelezo mafupi kwa washiriki wa shindano la Bibi Bomba.......
 Gea Habib, akifafanua jambo kwa washiriki wa shindano hilo....
 Sehemu ya watazamaji......
Sehemu ya watazamaji waliojitokeza kushuhudia Tamasha hilo.....
Picha na www.sufianimafoto.com

DEO NJIKU ALIPOMSAMBALATISHA OMAR RAMADHANI MOROGORO



Bondia Deo Njiku kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Omari Ramadhani wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Taifa Njiku alishinda kwa TKO ya raundi ya pili na kuwa bingwa mpya wa Taifa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' akiwepo kushudia mpambano huo uliofanyika Morogoro

Mabondia wa Utangulizi wakisafisha jukwaa kabla ya mtanange wenyewe

Chembu Upcat Kidevu lazima ukae ndivyo inavyo someka picha hii

Omari Ramadhani kushoto akipambana na Deo Njiku wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Taifa Njiku alishinda kwa TKO ya raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI KUMPA POLE KUFUATIA VIFO VYA ASKARI WALIOFARIKI MTWARA



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Mkuu wa jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati alipofika kwa mazungumzo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkuu wa jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati alipofika kwa mazungumzo leo.
****************************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amekutana na Mkuu wa jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Said Mwema ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Mei 27, 2013.

 Katika mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais ametumia nafasi hiyo kumpa pole Mkuu wa Polisi kufuatia ajali ya gari la iliyosababisha vifo vya askari wanne wa Jeshi hilo, waliokuwa njiani kutoka Nachingwea kuelekea Mkoani Mtwara kwa kazi maalum ya kudhibiti vurugu zilizojitokeza Mkoani humo juma lililopita.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alisema, askari hao watazidi kukumbukwa kwa kuwa walikuwa mstari wa mbele kuhakikisha majukumu yao kwa Taifa hili yanafanikiwa. Mheshimiwa Makamu wa Rais alisema pia kuwa, serikali inathamini sana mchango wa Jeshi la Polisi sambamba na majeshi mengine kutokana na kufanya kazi kwa kujitolea na kwa kutambua kuwa ulinzi na usalama wa Taifa ni jambo muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Mkuu wa Polisi kuwa, kazi inayofanywa na jeshi lake ni kubwa na kwamba Watanzania wanaithamini sana. Pia aliongeza kuwa katika nchi zote wananchi wanaojitolea kufanya kazi katika vyombo vya usalama, ni miongoni mwa wazalendo wakubwa wanaopaswa kuenziwa kwa kuwa wamekubali kuweka maisha yao kwa ajili ya nchi na watu wake.

Katika mkutano huo, Makamu wa Rais alitumia nafasi hiyo kupata taarifa kuhusu hali ya usalama mkoani Mtwara na pia kubadilishana mawazo kuhusu kuhakikisha maeneo ya nchi yetu kubakia salama wakati wote. 

Imetolewa na Boniphace Makene
           Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais

Saturday, May 25, 2013

Issere Sports yatoa jezi, mipira kwa vijana Kondoa



Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally Isere (kulia) akimkabidhi jezi seti moja mwakilishi, Dige Shaaban Nkusa kwa ajili ya timu ya vijana wa kijiji cha Mwembeni wilayani Kondoa ili kuimarisha michezo vijijini.

 

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Isere Sports imetoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. mil. 1.7 kwa ajili ya kuendeleza vijana katika wilaya ya Kondoa.

Akikabidhi vifaa hivyo jana, Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Isere alisema ametoa vifaa hivyo ili kuwasaidia vijana kupenda michezo ili kujenga afya na kujikinga na vitengo cha kihalifu.


 

Abbas alisema vifaa alivyotoa ni kwa ajili ya vijiji vya Changaa kwa Mafunchi ambako wamepewa jezi, mipira na soksi, katika kijiji cha Mwembeni kata ya Hondomairo wilayani Kondoa wamekabidhiwa vifaa kama hivyo.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya vijana wa Changaa, Issa Lubuva alisema umefika wakati kwa wananchi waishio mijini kuwakumbuka vijana waliobaki nyumbani kwa kuwapatia vifaa vya michezo.

Naye Dige Shaaban aliyepokea vifaa kwa niaba ya kijiji cha Mwembeni alisema wachezaji wengi wapo vijijini lakini hawajapata fursa ya kuonesha vipaji vyao hivyo vifaa hivyo vitasaidia kutoa wachezaji kutoka wilaya ya Kondoa.

Madabida mgeni rasmi Tamasha la wasanii chipukizi la Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)



                                                      Press Release
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida atakuwa mgeni rasmi katika tamasha la Mastaa chipukizi zaidi ya 320 litafanyika Jumapili 26, 2013 katika ukumbi wa Starlight Hotel kuanzia saa 4 asubuhi.

 

Peter Mwenda

                             

Mwenyekiti wa Shiwata, Caasim Taalib alisema Madabida ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) atapata nafasi ya kuona vikundi mbalimbali vya sanaa kikiwepo kikundi cha  Kaole, Splendid, Super Shine Taarab pamoja na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava, Maigizo,Ngoma, Dansi na Sarakasi nao wamethibitisha kushiriki.
Taalib alisema wasanii wakongwe wa bongo flava walioalikwa ni Stara Thomas, Safi Theatre Group, Ommy G na waigizaji wakongwe wa Kaole na Splendid wataonesha umahiri wao katika fani ya sanaa Kauli Mbiu ikiwa ni Kilio cha Msanii .
Vikundi vingine vitakavyonesha vipaji vyao ni Kepteni  Shaibu, Tanzania Disabled, Uyoga Boga Village, Ndafu Arts Group, CGC, Magengistar Crew, Dodo Arts Group, Culture Arts Group, Wachapa Kazi Academy, Soweto Picture, Shiwata Commedy, Mwavionelachi, Manuari Arts Group, Tandale Morden Taarab na Begeja Wushu,
 Taalib alisema tamasha hilo ambalo limepata kibali cha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pia wamealikwa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania,Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Shirikisho la Muziki Tanzania na Shirikisho la Sanaa za maonesho Tanzania.
Mwenyekiti aliwaomba viongozi wengine wa bendi za muziki, taarab, vikundi vya sanaa,mapromota,maprodusa na wadau wote kushiriki katika tamasha hilo ili kujenga ushirikiano wa pamoja.
Peter Mwenda 
Ofisa Habari wa SHIWATA
0715/0752-222677

TASWIRA MBALIMBALI SHINDANO LA MISS KIBAHA



 Safu ya wanenguaji wa kiume wa bendi ya mashujaa wakiburudisha.
 Safu ya Majaji wakigonganisha vichwa  kabla ya kumpata Makia wa Kibaha 2013.
 Washiriki  kumi wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya ukumbi wa Container Maili Moja Kibaha.
 Rapa wa bendi ya Mashujaa  walFaurson na mcheza shoo wakitoa burudani katika shindano hilo.
 Lilian Tungaraza 'Internet' mcheza shoo mahiri wa Mahujaa akitunzwa katika moja na mashabiki .

Internet kazini,
 Internet aliendelea kukomaaa meza moja hadi nyingine.

Mheshimiwa Diwani wa kuteuliwa wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kibaha  Celine Wilson ,ambaye pia alikuwa Chief Judge katika shindabno hilo hapa kabla ya kumtangaza mshindi.
 Mratibu wa Shindano hilo Khadija nikionesha Crown atakayovaa mrembo kabla malkia hajatajwa.
Nzera akifurahi mara baada ya kutajwa kuwa ameshinda taji la Redd's Miss Mibaha 2013.

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AMJULIA HALI SHEHA ALIYEMWAGIWA TINDIKALI


RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AMJULIA HALI SHEHA ALIYEMWAGIWA TINDIKALI


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein, akimsikiliza, Sheha wa Shehia  ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja, Mohamed Saidi Kidevu,(kulia) aliyelazwa Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar baada ya kumwagiwa Tindikali na Mtu asiyejuilikana huko maeneo ya Tomondo juzi wakati alipokuwa akirudi kuchota maji na kuelekea nyumbani kwake. Sheha huyo anaendelea kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Mnazi mmoja (wa pili kulia) ni  Kaka yake Sheha Sudu Mgeni Saidi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein,akimuangalia Sheha wa Shehia  ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja,Mohamed Saidi Kidevu,(kulia) jinsi alivyoathirika na Tindikali aliyomwagiwa na Mtu asiyejuilikanwa  huko Tomondo juzi wakati alipokuwa akirudi kuchota maji na kuelekea nyumbani kwake, wakati Rais alipomtembelea kumjulia hali Sheha huyo yupo katika Hospitali ya Mnazi mmoja .Kushoto Dkt.Slim Mohamed Mgeni. Picha na Ramadhan Othman Ikulu.

RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA MAONYESHO YA MFUMO WA MATOKEO MAKUBWA 'SASA' AWAMU YA KWANZA



 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wakati wa Ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa 'Sasa' Awamu ya Kwanza leo Mei 24, 2013
 Msanii maarufu wa kughani, Mrisho Mpoto, wakibinjuka Sarakasi, wakati kikundi chake na Bendi yake ya Mjomba ilipokuwa ikitoa burudani katika Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa 'Sasa' Awamu ya Kwanza, yaliyofunguliwa na Rais Jakaya Kikwete, leo Mei 24, 2013.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwasili kwenye Ukumbi wa Jumba la Makumbusho ya Taifa, leo Mei 24, 2013 kwa ajili ya Kufungua rasmi Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa 'Sasa' Awamu ya kwanza
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mchambuzi Sera Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mipango, Lorah Madete, wakati walipokuwa wakitembelea Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa Awamu ya Kwanza, baada ya kuyafungua rasmi leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Mtafiti Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Shetto, wakati walipokuwa wakitembelea Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa Awamu ya Kwanza, baada ya kuyafungua rasmi leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Friday, May 24, 2013

SPLASH WAJA NA IDENTTTY CARD




TAIFA STARS MCHANA WAITWA IKULU KUTETA NA RAIS



TIMU ya Taifa 'Taifa stars" ambayo ipo kambini kujiandaa na mchezo wa marudiano na Morocco wa kutafuta kufuzu fainali za dunia 2014 nchini Brazil imealikwa Ikulu kula chakula cha mchana leo.

Taarifa ambazo Lenzi ya Michezo imezipata zinasema Taifa stars imeitwa na Rais leo mchana kula chakula cha mchana paamoja na mambo mengine ambayo yatafahamika baadae.

Stars asubuhi imefanya mazoezi kwenye uwanja wa Karume ikiwa na wachezaji 21 kwani Mwinyi Kazimoto aliumia mguu na Salum Abubakar amefiwa na baba yake mlezi hivyo amekwenda kuhudhuria msiba huo


NZERA KITANO REDD'S MISS KIBAHA 2013




Katikati  Redds Miss Kibaha Nzera Kitano , kushoto mshindi wa pili Ester Albert na kulia ni Rachel Joh ambaye ni mshindi wa tatu.
Na Ripota Wetu, Kibaha
ALIYEKUWA mshiriki namba 6 katika shindano la kumsaka Redds Miss Kibaha 2013 Nzera  Kitano ameibuka kua Redds Miss Kibaha 2013 katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Conteainer  Kibaha Maili Moja mkoani Pwani Mei 17 mwaka huu
Nzera ambae alionekana kuwa mchezi tangu mwanzo wa shindano aliweza kupenya katika hatua ya nusu fainali ambapo aliingia katika warembo watano bora kati ya washiriki 10 waliokuwa wakishindana kuwania taji hilo.

 Aidha kwa ushindi huo  Nzera amepata zawadi ya fedha taslimu sh.300,000 pia amepa ofa ya kwenda kuchagua vipodozi na mapambo ya aina mbalimbali katika duka la Shear Illusion lilipo Mlimani City pamoja na king’amuzi kutoka kampuni ya Multichoice ambapo atafungiwa bure.
 
Mshindi wa pili ni Ester Albert ambaye amepata fedha taslimu kiasi cha sh.200,000 pia atapata ofa ya kulipiwa ada ya shule au kutafutiwa kazi na mdau ambaye hataki kutaja kwenye vyombo vya habari.
 
Mshindi wa tatu ni Rachel John aliyepata fedha taslimu sh. 150,000 huku nafasi ya nne ikienda kwa Sylvia John huku nafasi ya tano ilikwenda kwa Beatrice Bahaya.
 
Kwa ushindi huo warembo wote watano wamepata nafasi ya kwenda kushiriki kwenye shindano la Redds Miss Pwani watakakochuana na warembo wa Bagamoyo kuwania tiketi ya kwenda kushiriki katika shindano la Kanda ikiwa ni katika kuwania  tiketi ya shindano la taifa.
Shindano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Linda Media Solution (LIMSO) na kudhaminiwa na
Redds Miss Kibaha ilidhaminiwa na Tanzania Distilleries Konyagi kupitia kinywaji cha Dododma Wine, Redds Premium Cold, Fredito Entertainment, CXC Africa, Michuzi Media Group |(MMG), Aco Catering & Servises, Pr Studio, ASET ,Santorine Holiday Resort na Amazon Night Club.
Bendi ya Muziki wa dansi ya Mashujaa ilitumbuiza na kuwachengua mashabi wa urembo wa mkoa wa Pwani.