Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, June 29, 2013

NMB YAENDELEA KUZINDUA BUSINESS CLUB “SASA NI ZAMU YA KARATU”




Benki ya NMB imeendelea kuwa kinara katika kubuni na kuboresha huduma mbali mbali za kibenki, ili kuwawezesha wateja wake kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania.

 
Katika kulizingatia hili, NMB imezidi kuzindua klabu maalum za wafanyabiashara maarufu kama NMB Business Club. Hadi sasa zaidi ya NMB Business Club 29 zimekwisha zinduliwa nchi nzima.
Kupitia NMB Business Club wajasiliamali wanaowezeshwa na benki ya NMB wamekua wakipata nafasi ya kujifunza jinsi ya  kuandika michanganuo ya biashara zao na pia kuendelea kua vinara wa biashara.




Mkuu wa kitengo cha wajasiliamali wadogo wadogo na wakati wa NMB ,Filbert  Mponzi akimkabidhi mwenyekiti wa  NMB Business Club Paulith Jack  mara tu baada ya kuibuka kidedea kwenye mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa NMB Business Club Karatu .





Mhandisi mkuu wa Wilaya ya  Karatu, Tulinumpoki Mwakalukwa akitoa shukrani zake  kwa NMB mara baada ya kuzindua rasmi  NMB Business Club  wilaya ya Karatu. Kushoto ni Meneja wa NMB tawi la Karatu , Evarist Mtaro na mkuu wa kitengo cha wajasiliamali wadogo wadogo na wakati  wa NMB Filbert  Mponzi.





Sehemu ya wanachama wa NMB Business Club wilaya ya Karatu wakifurahia uzinduzi wa NMB Business Club.

Friday, June 28, 2013

GAPCO TANZANIA LTD YAENDEREA NA PROMOSHENI YA GAPCO RELSTAR OIL


Wasanii wa  JCB Dominion wakitoa burudani wakati wa promosheni ya Gapco Relstar Oil inanayotengenezwa na Kampuni ya Gapco T LTD Eneo laMwananyamala  Dar es salaam kutoka kushoto ni Omar Salimu Halima Masoud na Jafari Halawi picha na
www.burudan.blogspot.com

Mwakilishi wa Kampuni ya Gapco T LTD Bw.Stevin Mwakamele Akimkabidhi mmoja wa wateja Selemani Yusufu dumu la lita tano wakati wa promosheni ya Gapco Relstar inayoendelea katika jiji la Dar es salaam jana eneo la Mwananyamala
picha na
www.burudan.blogspot.com

Mwakilishi wa Kampuni ya Gapco ,Lightnes Samwel kulia akimkabidhi Mwendesha pikipiki Mrema Johnson Oil ya Gapco Relsta wakati wa promosheni inayoendelea jijini Dar es salaam Picha na
www.burudan.blogspot.com

Thursday, June 27, 2013

UCHAGUZI WA VIONGOZI WA BFT KUFANYIKA JULAI 7 MWAKA HUU




TANZANIA BOXING NEWS: UCHAGUZI BFT JULAI 7


Uchaguzi wa viongozi wa BFT uliopangwa Kufanyika tarehe 7/7/2013 jijini Mwanza, utafanyika kwa tarehe hiyo kama ulivyopangwa.

Kikao cha kamati ya utendaji ya BFT kilichofanyika juzi katika  ofisi za BFT kikiongozwa na Rais wa shirikisho Joan Minja kimesisitiza kuwa uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa na haujaairishwa kama baadhi ya kikundi 
cha watu wachache wanaojiita wadau wanavyoweka pingamizi na kupotosha  
kwa kuwashawishi wajumbe wa mkutanao mkuu hasa kutoka mikoani 
kutohudhuria mkutano huo wa uchaguzi,kwa manufaa yao binafsi na 
kinyume na katiba yetu.

Upotoshaji huo unafanywa na  Akaroly Godfrey aliyekuwa  kiongozi katika uongozi uliojiudhuru kutokana na kashfa za kusafirisha madawa ya kulevya 
na kusababisha Tanzania kufutwa uanachama na chama cha ngumi cha 
dunia (AIBA) na kusababisha  kutoshiriki mashindano,mikutano na 
shughuri zote za kimataifa za chama cha ngumi cha Dunia AIBA. Naomba 
wadau na serikali kuwa makini na watu wanaoshawishi kwa lengo la 
masilahi yao binafsi na kusababisha michezo kudolola badala ya kusonga 
mbele.

Fomu za uchaguzi zilishaanza kutolewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) toka tarehe 4//2013 na zitaendelea kutolewa hadi tarehe 4/7/2013 jijini 
Mwanza na tarehe hiyo  ndio itakuwa siku ya mwisho ya kuchukua na 
kurudisha fomu, tarehe 5/7/2013 itatakuwa siku ya usaili na utafanyika jijini mwanza, tarehe 6/7/2013 kupitia pingamizi na kuzitolea maamuzi na tarehe 7/7/2013 ndio siku ya uchaguzi.
Kimsingi taratibu zote za kuitisha uchaguzi kwa mujibu wa katiba yetu zimezingatiwa na zimekamilika.

Aidha BFT inatoa tamko kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufika katika 
uchaguzi uchaguzi, ili kupata viongozi halali kwa mujibu wa katiba, 
waendelee na shughuri za kuendeleza mchezo wa ndondi na kuaandaa timu 
ya taifa kushiriki katika mashindano ya Afrika nchini Mauritius Sept. 2013

BFT inatoa wito kwa watu wote wenye sifa, nia, moyo na uwezo wa kuongoza wajitokeze kuchukua fomu za kugombea uongozi kwani wakati ndio huu.

MISS KANDA YA NYANDA ZA JUU 2013 KUPATIKANA JUMAMOSI HII







  Kinyang’anyiro cha kumpata Miss Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kinatarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa Mikutano wa Mtenda SunSet uliopo Soweto Jijini Mbeya.   Mratibu wa Shindano hilo Fredy Herbet, amesema baada ya warimbwende kutoka Mikoa yote inayounda Kanda kukaa kambini tangu Juni 25, Mwaka huu na kupata mafunzo mbali mbali wanatarajia kuivunja Juni 29, Mwaka huu baada ya Msindi kupatikana.   Ameongeza kuwa Shindano hilo limeandaliwa na Lake Victoria Arts & Culture Promotion chini ya Udhamini wa TBL kupitia kinywaji chake cha REDDS, SBC kupitia  Mountain Dew, Man Company, My Choice Botique, Ebony Fm na Bomba Fm radio.   Amesema kinyang’anyiro hicho kitasindikizwa na burudani kutoka kwa bendi ya FM Academia ya Jijini Dar Es Salaam na kuongeza kuwa kiingilio kitakuwa  shilingi 10,000/= kwa watu wa kawaida na 25,000/= kwa VIP.   Amewataja washiriki wanaong’ang’ania kuibuka kidedea kwa kuiwakilisha Kanda katika shindano la kumpata Miss Tanzania Mikoa wanakotoka kwenye mabano na namba aliyoshinda Mkoani kwake  kuwa ni pamoja na Lina J. Allan (Rukwa 1), Aneth B Mapugilo(Mbeya 2), Jesca Mikambi(Katavi 2), Nuru Baraka ( Katavi 1) na Neema Mality (Iringa 1).   Wengine ni Lucy George (Iringa 3), Nuriath Suleiman (Njombe 1), Evamary Gamba( Rukwa 2) Lilian Samson (Iringa 2), Naba Magambo (Mbeya 4), Jacklin J Luvanda (Mbeya 1) na Winfrida Felix Miss Njombe namba 2.   Kwa Upande wake Mwalimu wa Walimbwende hao Naomi Jones  ambaye ndiye anayeshikilia taji hilo amesema kambi iko vizuri na washiriki wote wanafuata maelekezo vizuri hivyo Majaji wawe makini kumtafuta Msindi kutokana na wote kuwa na sifa zinazofanana.
Na:Mbeya yetu 

SHILOLE AMTIMUA MDOGO WAKE BAADA YA KUDUNGWA MIMBA






STAA wa sinema za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ (pichani) amemtimua mdogo wake aliyekuwa akiishi naye aitwaye Mary baada ya kunasa ujauzito.
Chanzo makini kilicho karibu na staa huyo kimepenyeza habari kuwa, Shilole alifikia maamuzi hayo baada ya kumuonya binti huyo aachane na mwanaume aliyemjaza mimba hiyo lakini hakusikia hivyo akaona bora amtimue.
 
“Kamtimua baada ya kumuonya mara nyingi bila mafanikio akaona isiwe tabu bora aepuke aibu,” kilisema chanzo hicho.

Alipoulizwa kuhusiana na ishu hiyo, mdogo huyo wa Shilole alikiri kutimuliwa na sasa amehamishia makazi kwa jamaa yake anayefahamika kwa jina la Tonny Montensi anayeishi Sinza, jijini Dar.

RAIS WA SRI LANKA MANIDA RAJAPAKSA AWASILI NCHINI LEO






Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuweasili nchini kwa ziara ya kikazi leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik.
Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa akisalimia na Msaidizi wa Rais Masuala ya Kidiplomasia,Balozi Liberata Mulamula wakati Rais Kikwete alipokuwa akiwatambulisha baadhi ya viongozi na wasaidizi wake kwa mgeni wake muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi leo asubuhi.
Mtoto Faith Warioba anayesoma katika shule ya awali ya Montessori jijini Dar es Salaam akimlaki kwa maua Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi nchini huku Rais Dkt.Jakaya Kikwete akishuhudia.

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA




 Mbunge wa Jimbo la Ilala, jijini Dar es Salaam, na mmoja wa Wenyeviti 
wa Bunge, Mussa Zungu Azzan akiongoza kikao cha Bunge
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kutoka Mkoani Arusha, Catherine 
Magige akiwa Bungeni mjini Dodoma Juni 26,2013.
 Mbunge wa Nzega, Dk. Hamisi Kingwangalla (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa CCM nchi za SADC, Kelvin Nyamori (katikati) na Mbunge 
wa Kisesa, Luhanga Mpina, nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana.
 Mbunge wa Viti Maalu, Faida Mohamed Bakar akizungumza jambo na 
Mbunge wa Tandahimba, Juma Njwayo nje ya ukumbi wa Bunge mjini 
Dodoma jana.
Mbunge wa Viti Maalum, Faida Mohamed Bakar akifurahia jambo na 
Wabunge wenzake  Juma Njwayo wa Jimbo la Tandahimba, na Dk. 
Hamisi Kingwangala wa Nzega(kushoto) nje ya ukumbi wa Bunge 
mjini Dodoma jana.
 Wapigapicha za Habari wakiwa kazini Bungeni
 Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe akisalimiana na Mbunge wa 
Viti Maalum, Josephine Gezabuke (kulia) nje ya Ukumbi wa Bunge 
mjini Dodoma jana. Kushoto ni Waziri wa Makamu wa Rais, Mazingira,
 Dk. Terezya Huvisa.
 Wabunge wakitoka Bungeni jana

MAKUMBUSHO MABINGWA AIRTEL RISING STARS KINONDONI




Nahodha wa timu ya Makumbusho United Hamza Mohamed akipokea kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, kutoka kwa Ofisa Maendeleo wa TFF Bw. Salum Madadi baada ya kuibamiza timu ya Mtakuja 5-1 katika mchezo wa mwisho wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 uliofanyika kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2013.

Nahodha wa timu ya Makumbusho United Hamza Mohamed akinyanua juu kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, baada ya kuibamiza timu ya Mtakuja 5-1 katika fainali ya mashindano hayo ngazi ya mkoa iliofanyika kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2013.


Wachezaji wa timu ya Makumbusho United wakishangilia baada ya kutwaa kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2013. Makumbusho walishinda 5-1 dhidi ya Mtakuja.

Baadhi ya mashabiki wa kishangilia timu zao katika michuano ya Mkoa ya Airtel Rising star 2013
Baadhi ya mashabiki wa kishangilia timu zao katika michuano ya Mkoa ya Airtel Rising star 2013

ILO NA TACAIDS WAENDESHA KONGAMANO LA KUJADILI MIKAKATI YA KUWAWEZESHA WANAWAKE, WASICHANA NA WAVULANA KIUCHUMI KATIKA HARAKATI ZA KUPUNGUZA HALI HATARISHI ZA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI NCHINI.




IMG_2657
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo amesema kupitia msaada kutoka Serikali ya Sweden wa kifedha ILO iliweza kuwahusisha wasichana na wavulana katika makundi mbalimbali wenye vipato vidogo kupata uelewa wa Afya ya Uzazi kupitia Makongamano, Semina na Mafunzo mbalimbali yaliyoendeshwa na shirika hilo la kazi Duniani.
Ameongeza kuwa “tuliwasaidia kuwaunganisha na vikundi vya kuweka na kukopa ili waweze kupata mitaji midogo midogo ya kufungua biashara ndogo ndogo katika harakati za kuwafanya wajitegemee na kuepekana na vishawishi vya Ngono isiyokuwa Salama.
Bw. Musindo amesisitiza Umuhimu wa TACAIDS kuandaa makongamano kama haya ili kuwawezesha wasichana na wavulana wadogo kupata ufahamu uelewa na mafunzo ya uzazi wa Afya na jinsi ya kuelewa mabadiliko yao ya kimaumbile.
“Ni matumaini yangu mwingiliano huu wa Utamaduni wa kupambana na Ukimwi, Kinga na Uwezeshwaji wa Kiuchumi umefanyika vizuri, hasa katika kuyalenga makundi yaliyo katika mazingira magumu itasaidia kuongeza kasi ya kupunguza maambukizi mapya kama ilivyoripotiwa na ripoti ya UNAIDS mwaka 2012 Duniani kwamba maambukizi mapya yamepungua kwa Asilimia 20”. Amesema.
IMG_2710
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo kwenye Kongamano hilo.
IMG_2731
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Kijakazi Mtengwa akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo amesema mikakati ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi inaweza kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake, Wasichana na Wavulana wadogo.
Amesema Jamii lazima itambue kuwa juhudi zaidi zinahitajika ili nchini yetu iweze kufikia malengo ya 0.3 yaani Tanzania ambayo haina maambukizi mapya ya VVU, Ukimwi usiwe sababu ya vifo, vile vile pasipo unyanyapaa wala ukatili kwa mtu yeyote anayeishi na Virusi vya Ukimwi.
IMG_2702
Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dr. Fatma Mrisho akizungumza na washiriki amesema Takwimu zinazonyesha Wanawake wako katika hali ya hatari ya kuambukizwa zaidi kuliko wanaume ambapo mpaka sasa ni Asilimia Sita ya Wanawake nchini huambukizwa wakati wanaume ni Asilimia 3 nchini nzima.
Dr. Mrisho alisisitiza umuhimu wa kumwezesha mwanamke kiuchumi kama ndio moja ya suluhisho la kumfanya kutokuwa tegemezi katika jamii.
“Amesema takwimu zinazonyesha katika nchi nyingi za Kiafrika umaskini unachagia sana kuenea kwa Ukimwi maana Wanaume wengi hutumia umasikini wa Wasichana au Kinadada kuwarubini kwa fedha na kufanya nao Ngono isiyosalama”.
Dr. Fatma Mrisho amepongeza juhudi za ILO na kuwataka mashirika mengine na wadau wa mapambano dhidi ya Ukimwi kuiga juhudi zilizofanywa na ILO za kuandaa makongamano ya kiuchumi ili kumwezesha Mwanamke na wavulana wadogo kujitambua na kuelewa jukumu lao katika mapambo ya VVU na Ukimwi nchini.

GAPCO .T. LTD KUTOA ELIMU YA OIL YA GAPCO RELSTAR NCHI NZIMA





Mwakilishi wa Gapco  Afrika Mashariki Bw. Suraj Vikash akizungumzia promosheni hiyo

Na Mwandishi wetu 
Mwakilishi wa Gapco  Afrika Mashariki Bw. Suraj Vikash  amesema Dar es salaam leo juu ya oil mpya ya virainishi vya injini pamoja na mitambo ambayo inafaa kwa magari madogo makubwa na faida zake ni nyingi ikiwemo ulinzi  thabiti wa injini,na maisha marefu utumiaji mdogo wa oil na aitopoteza ulaini wake inaondoa uchafu ugando kwenye injini

ambapo mteja anafuraia mwendo wa starehe injini safi zaidi umbali mrefu hizo ni baadhi ya sifa za oili ya gapco relstar bidhaa hiyo gapco Tanzania LTD  ni moja ya makampuni inayosambaza bidhaa hiyo ya oil  ambayo inauzwa kwa jumla na rejareja na kwa Tanzania wao ni mawakala wakuu wa mafuta ya virainishi vya injini
gapco relstar ni bidhaa bora ya virainishi vya injini mbalimbali

oil hiyo inayotengenezwa na kampuni ya
gapco Tanzania LTD ambayo ilianza kutoa bidhaa hiyo mwaka 2010 imekuwa chachu na yakutegemewa ndio mana wameamua kuleta bidhaa hiyo nchini hili watu waijue 

kuwa ni bidhaa pekee katika vyombo vyao ikiwemo magari,pikipiki pamoja na vyombo vyote vinavyotumia vipuli Gapco relstar imeweka nia ya kuwasambazia watanzania Oil hiyo  ya virainishi vya mashine katika mikoa yote nchini kwa ajili ya kulinda fedha zao wateja kwa kuwa inadumu kwa muda mrefu ambapo kwa sasa kuna matangazo ya barabarani kwa Tanzania nzima kuwapatia elimu ya manufaa kwa ajili ya kutumia oil hiyo wapate unafuu katika kutumia bidhaa hiyo alisema Bw.Vikash wakati anatangaza bidhaa hiyo ambayo itawasaidi watu mbalimbali
 
'Umbali mrefu kwa thamani ya pesa yako'

GAPCO .T. LTD KUTOA ELIMU YA OIL YA GAPCO RELSTAR NCHI NZIMA





Mwakilishi wa Gapco  Afrika Mashariki Bw. Suraj Vikash akizungumzia promosheni hiyo

Na Mwandishi wetu 
Mwakilishi wa Gapco  Afrika Mashariki Bw. Suraj Vikash  amesema Dar es salaam leo juu ya oil mpya ya virainishi vya injini pamoja na mitambo ambayo inafaa kwa magari madogo makubwa na faida zake ni nyingi ikiwemo ulinzi  thabiti wa injini,na maisha marefu utumiaji mdogo wa oil na aitopoteza ulaini wake inaondoa uchafu ugando kwenye injini

ambapo mteja anafuraia mwendo wa starehe injini safi zaidi umbali mrefu hizo ni baadhi ya sifa za oili ya gapco relstar bidhaa hiyo gapco Tanzania LTD  ni moja ya makampuni inayosambaza bidhaa hiyo ya oil  ambayo inauzwa kwa jumla na rejareja na kwa Tanzania wao ni mawakala wakuu wa mafuta ya virainishi vya injini
gapco relstar ni bidhaa bora ya virainishi vya injini mbalimbali

oil hiyo inayotengenezwa na kampuni ya
gapco Tanzania LTD ambayo ilianza kutoa bidhaa hiyo mwaka 2010 imekuwa chachu na yakutegemewa ndio mana wameamua kuleta bidhaa hiyo nchini hili watu waijue 

kuwa ni bidhaa pekee katika vyombo vyao ikiwemo magari,pikipiki pamoja na vyombo vyote vinavyotumia vipuli Gapco relstar imeweka nia ya kuwasambazia watanzania Oil hiyo  ya virainishi vya mashine katika mikoa yote nchini kwa ajili ya kulinda fedha zao wateja kwa kuwa inadumu kwa muda mrefu ambapo kwa sasa kuna matangazo ya barabarani kwa Tanzania nzima kuwapatia elimu ya manufaa kwa ajili ya kutumia oil hiyo wapate unafuu katika kutumia bidhaa hiyo alisema Bw.Vikash wakati anatangaza bidhaa hiyo ambayo itawasaidi watu mbalimbali
 
'Umbali mrefu kwa thamani ya pesa yako'

Tuesday, June 25, 2013

MPAMBANO WA MASUMBWI UBINGWA WA DUNIA



WATOTO YATIMA WA NGEZE EDUCATION CENTER KUJUMUIKA NA WATOTO WENZAO KATIKA MICHEZO




 Watoto yatima wa kituo cha Ngeze education center kilichopo maeneo ya kinondoni kwa  msisiri watajumuika na watoto wenzao katika tamasha la Raha za jana na leo linalojumuisha burudani ya bendi za muziki wa dansi.

Wasanii nguli wa filamu na bongoflava wanaokubalika kwa watoto watakuepo kula,kuimba na kucheza na watoto wote watakaodhulia katika tamasha hilo amabapo kiingilio kwa watoto wadogo kitakuwa ni bure ambapo wazazi wao watalipa kiasi cha tshs 8,000 tu.

Jumla ya bendi sita zitapanda jukwaani moja kuonyesha ukali wake,pia zile nyimbo mpya kutoka katika bendi hizo utazisikia zikipigwa live,bendi hizo ni Twanga Pepeta"African Stars",Mashujaa musica Band ikiongozwa na Chalz baba " wazee wa tuzo tano",Bantu group ikiongozwa na   ikiongozwa na "komandoo Hamza kalala".

Bendi zingine ni King kikii"wazee sugu",OTTU jazz band"MSONDO",King Kikii "wazee sugu" na DDC Mlimani park "SIKINDE" tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 6 mwezi wa saba katika viwanja vya posta vilivyopo kijitonyama jijini Dar es salaam.
 
 Milamgo ya viwanja hivyo itafunguliwa saa tano asubuhi ambapo michezo ya watoto itaanza na kuisha saa kumi na mbili jioni ambapo burdani za bendi zikiendelea mpaka usiku wa manane.

ZANTEL YAZINDUA HUDUMA YA DAKTARI KWENYE SIMU YA MKONONI



Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali Watu cha Zantel, Francis Kiaga akifafanua jambo wakati wa ushirikiano na Kampuni ya BR Solution na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuwawezesha watanzania kupata huduma ya ‘Daktari kwa njia ya simu’ ikiwa na lengo la kupata ushauri kwa masaa 24 mahali popote nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa BR Solutions, Richard Toba na Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan. (Picha na Habari Mseto Blog)
Mkurugenzi Mkuu wa BR Solutions, Richard Toba (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan.
Dk. Aidan Njau akifafanua jambo, Sajid Khan. 

DAR ES SALAAM, Tanzania

KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Zantel imezindua ushirikiano na Kampuni ya BR Solution na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuwawezesha watanzania kupata huduma ya ‘Daktari kwa njia ya simu’ ikiwa ni kupata ushauri kwa masaa 24 mahali popote nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Zantel jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali watu cha Zantel Francis Kiaga alisema, wameamua kuingia ubia na Wizara pamoja na BR ili kuwasaidia watumiaji wa Zantel kuongea moja kwa moja na madaktari endapo watakuwa na tatizo linalowasumbua ambalo wanahitaji ushauri.

“Huduma hii ya ‘Daktari kwa njia ya simu’ sisi kama Zantel tunaimani itawanufahisha watanzania kupata ushahuri kwa bei laisi juu ya matatizo yanayowasumbua na ndio maana tumeamua kubolesha maisha ya wateja wetu kwa teknolojia ya simu za mikononi kwa kuwa tunatambua Watanzania wengi wanatumia simu,”alisema Kiaga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa BR Solution Francis Njau alisema, huduma hiyo itashughulikia magonjwa kama, Ukimbi, Cancer, Moyo, Malaria, Afya ya Uzazi na huduma ya kwanza ambayo bado wanajipanga zaidi jinsi ya kuwafahamisha watanzania jinsi ya kufanya tofauti na kumwelekeza mgonjwa kwenda duka la madawa bila ya kwenda hospitalini kwanza.

“Tukumbuke Zantel walishawahi kushinda tuzo za ubunifu katika kutumia teknolojia katika kubolesha afya na huduma kupitia huduma yake ya Mobile Baby katika tuzo la kongamano la Makampuni ya simu mwaka jana,”alisema.

Kwa upande wa Daktari Aidan Njau wa Aghakan Hospitali alisema, wamejipanga kuhakikisha wanawapa ushauri mzuri watanzania ambao watapiga simu au kutuma meseji ambayo itatangazwa hapo badae na kudai kuwa huduma hiyo itakuwa sio kumpata dawa mgonjwa kwa kuwa fani yao hairuhusu kumpa mgonjwa dawa bila ya kumpima.

“Katika kipengele cha huduma ya kwanza kuna ushahuri ambao tutamwambia mgonjwa atakapopiga simu, ila kumwambia tumie dawa ni ngumu kwa kuwa mtu anaweza kupiga simu anasema anaumwa kichwa ukamwambia tumie Diklofenak alafu kumbe ana vidonda vya tumbo ambapo ni hatari zaidi,”alisemaTumaini.

MICHAEL JACKSON AIBUKIA BONANZA LA TBL'S FAMILY DAY JIJI DAR



 WMsanii wa kikundi cha  sanaa cha Afrigay Talent Base cha Magomeni Dar es Salaam, Michael Jackson wa Tanzania, akiwaongoza wenzake kutoa burudani wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), pamoja na familia zao Kunduchi Water Park, Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Fedha wa TBL, Kelvin (kulia), akimkabidhi George Magombeka zawadi ya saa ya ukutani baada ya kuwa mshindi wa riadha katika bonanza hilo la kukata na shoka lililofanyika Kunduchi, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo (kulia) akimkabidhi zawadi  .Mbwana Milanzi baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa mbio za magunia katika hafla ya Siku ya wafanyakazi wa TBL kufurahi na familia zao kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam
 Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo  akimkabidhi zawadi  .mmoja wa washindi wa riadha kwa upande wa wananwake. Kulia ni Mhandisi Ujenzi wa TBL, John Malisa.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifurahi na familia zao kwa kucheza kushindana kuvuta kamba katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam, wakati wa sherehe 'Tbl's Family Day'. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

NMB YAFADHILI UMITASHUMTA MANISPAA YA SUMBAWANGA



Benki ya NMB imefadhili UMITASHUMTA kwenye manispaa ya Sumbawanga kwa kutoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni tisa. Lengo kuu la ufadhili huu ni kusaidiana na UMITASHUMTA katika kuibua na kuendeleza  vipaji vya michezo kwa shule za msingi nchini Tanzania.
 Meneja wa NMB Tawi la Sumbawanga, John Chinguku akimkabidhi  Ofisa Elimu, Modesta Zambi  sehemu ya vifaa vya michezo vitakavyotumika kwenye UMITASHUMTA  manispaa ya Sumbawanga. Makabidhiano haya yalifanyika hivi karibuni kwenye manispaa hiyo.
Maofisa wa Benki  ya NMB  na maofisa wa Manispaa ya Sumbawanga wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB  Tawi la Sumbawanga, John Chinguku (tatu kulia)  mara baada ya kukabidhi vifaa vya michezo.
 Mipira iliyokabidhiwa.

WANASOKA MAARUFU NCHINI WAHITIMU KOZI YA UKOCHA YA NGAZI YA KATI LEO