Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, August 20, 2014

AZAM FC YATUPWA NJE KAGAME CUP YALAZWA PENATI 4-3 NA EL MARREIKH YA SUDAN



Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa AfrikaMashariki na Kati, Kombe la Kagame,  Azam FC ya Chamanzi jijini Dar es Salaam imetupwa nje ya michuano hiyo mikubwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kucharazwa mikwaju 4-3 dhidi ya El Marreikh ya Sudani katika mchezo wa pili wa robo fainali.Wachezaji ambao walielezwa awali kuwa wanasumbuliwa na vyama za paja lakini wakashuka katika dimba la Nyamirambo mjini Kigali Rwanda ndio walioigharimu Azam FC licha ya mlinda mlango  Mwadin Ally kufanya kazi nzuri ya kupangua penati ya wapinzani wao. 

Wachezaji walioipa tiketi ya kurejea nyumbani Azam FC kujiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga SC ni beki Shomary Kapombe na mshambuliajiLionel Saint- Preux kutoka Haiti.
Aidha kocha wa mabingwa hao wapya wa soka la Tanzania, Mcameroon JosephMarious Omog ameonekana amekuwa akiandaa Azam FC kitaalamu mnokuelekea mchezo huo, ambapo mbali na mambo mengine aliwaelekeza mifumona aina tofauti ya uchezaji, ikiwa ni pamoja na kutumia mipira mirefu na mifupi.
Omong aliwaandaa wachezaji wake pia kwa kupiga penalti, lakini hakuna kilichofua dafu kutokana na upigaji wa kimakosa uliofanywa na Kapombe aliyepaisha penati yake juu na gonga mwamba na Preux aliyepiga mpira mwepesi na kumwezesha mlinda mlango wa Merreikh kuificha bila shaka.

MANENO YA DIAMOND KWA WEMA SEPETU YAMCHOMA AUNTY EZEKIEL



Star wa filamu nchini Aunty Ezekiel anadaiwa kuchomwa vilivyo na maneno ya Diamond kwa Wema Sepetu yanayodaiwa kumgusa yeye pia moja kwa moja kama rafiki wa Wema...
Diamond juzi alisema  kuwa Wema anapenda sana starehe na mashoga wapenda kujirusha badala ya kufanya kazi ili kujiletea maendeleo kwa kutumia fursa aliyonayo sasa.Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na Aunty kikizungumza  jana kwa sharti la kutotajwa jina kilisema kuwa baada ya Aunty kuona alichoandika Diamond aliachia msonyo wa kufa mtu kuonyesha hakupendezwa hata kidogo huku akibaki kuumia.
"Aunty alipoona alichoandika Diamond alichia msonyo huoo! unajua maneno ya Diamond yamejaa ukweli mtupu, yalikuwa kama mkuki kwa Aunty, Aunty ni mtu wa starehe sana si umeona hata ndoa yake haina uhai, ukweli unauma, yeye na Wema wanapaswa kujiangalia upya Diamond amempa Wema ushauri mzuri sababu anampenda"
Chanzo hicho kilisema kuwa Aunty anataka kukata ukaribu wake na Wema ili kuepusha maneno kwasababu ameshazoea kuishi kwa kujirusha.
"Urafiki wa Wema  na Aunty muda si mrefu utakuwa kama ule wa Kajala, Aunty anataka kumuacha Wema na bwana'ke yeye achukue hamsini zake"kilisenma chanzo hicho
Hata hivyo Aunty alipotafutwa  ili kutoa ufafanuzi hakupatikana .

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WAHANI MSIBA WA MAREHEMU JAJI MAKAME



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweha saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe Agosti 19, 2014.
 Mama Salma Kikwete akiweha saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame,  Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe  Agosti 19, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwafariji wafiwa walipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame,  Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam  Agosti 19, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na watoto wa marehemu pamoja na Jaji Mstaafu Mark Bomani alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki,  jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe Agosti 19, 2014.

Tuesday, August 19, 2014

EXTRA BONGO KUSINDIKIZA MASAI SAFARI BANDI KATIKA UZINDUZI WA ALBAM YAO



Wapiga magitaa wa bendi ya masai safari band wakichalaza magitaa wakati wa mazoezio yao ya kujiandaa na uzinduzi wa albam yao ya kwanza kushoto Josephe Bivence na Juma Ali

Wapiga magitaa wa bendi ya masai safari band wakichalaza magitaa wakati wa mazoezio yao ya kujiandaa na uzinduzi wa albam yao ya kwanza kushoto Josephe Bivence na Juma Ali
Na Mwandishi Wetu
 BENDI ya masai safari ya jijini Dar es salaam inatarajia kuzindua albam yake ya kwanza kabisa

watakayozindua siku ya augost 30 katika ukumbi wa raunch time ya jijini akizungumzia uzinduzi wa albam hiyo rais wa bendi hiyo Fransic Mwaisela amesema kwamba siku hiyo watasindikizwa na bendi mbalimbali wakiongozwa na bendi ya Extra bongo inayo ongozwa na Ali Choki

alizitaja nyimbo zilizomo katika albam hiyo ni sita itakayozinduliwa siku hiyo ikiwa nyimbo ambayo iliyobeba albam ni akuna kama baba ya pili ni njia panda,mikono ni kazi,ndoa ni mpango wa mungu,usiwasikilize wambeya,kilio changu nyimbo hizo ndio zitakazokuwa katika albam hiyo itakayo zinduliwa mwishoni mwa mwezi huu


aliongeza kwa kutaja wasanii wengine watakaokuwepo siku hiyo ni Omari Tego,Maua Tego pamoja na wasanii mbalimbali wa bondo flefa watakaosindikiza uzinduzi uho

bendi hiyo kwa sasa ipo kwenye mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kutoa burudani kabambe siku ya uzinduzi wa albam ya bendi hiyo

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' BINGWA WA WPBF AFRICA



BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' BINGWA WA WPBF AFRICA

SIMTANK YAKABIDHI ZAWADI KWA WATEJA WAKE



 Mr. Shrima of Innocent hardware receiving 4th category award Bajaj Boxer motorcycle from Mr. Alpesh Patel CSMO(Chief Sales & Marketing)
Mr. Dilip on be half of Aim Steel Arusha receiving 4th category award Bajaj Boxer motorcycle from Mr. Alpesh Patel CSMO
Mrs. Elizabeth of Lazy Shop receiving for 6Th category award Samsung S4 Mini from Genesis Mushi Sales executive of Silafrica.
 Bi Fatma Wahenga akitoa shukrani za dhati kwa uongozi mzima wa kampuni ya SIMTANK baada ya kupokea zawadi ya gari aina ya Suzuki carry kama motisha baada ya kuibuka mnunuzi mkubwa wa SIMTANK eneo la buguruni DSM, kushoto ni Afisa masoko na mauzo wa SMTANK Alpesh Patel Kulia ni msherehashaji wa hafla hiyo iliyo fanyika serena hotel DSM havi karibuni.
Mkurugenzi mtendaji wa Silafrica SIMTANK Bw. Shah akimkabidhi mfano wa funguo wa gari aina ya Suzuki Carry kwa bi. Fatma Wahenga baada ya kuibuka mnunuzi mkubwa wa SIMTANK eneo la buguruni DSM ambapo washindi wengine walijishindia gari aina ya noah, pikipiki na sim za mkononi.
Wasanii kutoka Kundi la THT wakitoa burudani katika sherehe hiyo

ZAWADI ZA PIKIPIKI NA MAGARI ZITAKABIDHIWA SIKU CHACHE ZIJAZO BAADA YA KUKAMILIKA KWA USAJILI.

Simtank inatambua mchango mkubwa kutoka kwa wateja nwake hivyo imejiwekea utaratibu wa kurudisha sehemu ya faida zake kwa wale walioweza kununua kwa kiasi kikubwa SIMTANK kwa mwaka.

Kampuni ya SilAfrica ambao ndio watengenezaji na wauzaji wa matanki ya Kuifadhia majii aina Ya SIMTANK wafanya sherehe kwaajili ya kuwakabidhi zawadi wateja wao wanaonunua matank yao kwa idadi kubwa. Kampuni hiyo imekua ikifanya hivyo kila mwaka ikiwa kama njia ya Kuwapongeza na kuboresha uhusiano wao baina ya kampuni na Wateja wao vilivile sherehe za kuwapongeza na kuwapa zawadi hufanyika kila mwaka kwaajili pia ya Kutambua mchango wao kwa kampuni hiyo ya SilAfrica ambao ni watengenezaji wa Matanki ya kuhifadhia Maji ya SIMTANK

DVD MPYA KUTOKA SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION




DVD MPYA YA MAHASIMU WAWILI NI MADA MAUGO VS THOMAS MASHALI

Diwani Sagamiko aandaa warsha kwa wenyeviti na makatibu UWT Kinondoni


Kuluthum Sagamiko akihojiwa na waandishi wa habari
mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo 


 Eva Mwingizi akihojiwa na waandishi wa habari mara
baada ya kufungua warsha hiyo.

  viongozi hao wakisikiliza watoa
mada (hawapo pichani) wakati wa warsha hiyo



DIWANI wa Viti Maalum Msasani, Kuluthum Sagamiko ameandaa warsha kwa ajili ya wenyeviti na makatibu wa Umoja wa Wanawake (UWT) wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya mafunzo ya kujiimarisha kichama na ujasiriamali
kwa wanawake.
Warsha hiyo ilifanyika Dar es salaam jana, ambapo jumla ya viongozi
hao kutoka kwenye kata 34 za wilaya hiyo walishiriki na kuweka
mikakati ya pamoja.  Akifungua warsha hiyo, Naibu Katibu Mkuu Bara, Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Eva Mwingizi, aliwataka  kuwa mstari wa mbele na kusimama katika nyanja zote ikiwemo siasa na biashara bila woga.
Alisema uwiano sawa wa asilimia 50 kwa 50 katika uongozi hauwezi
kufikiwa endapo  wanawake wenyewe watasita kujitokeza kugombea nafasi
mbalimbali. "Nimefurahi leo kuwaona wanawake wamekutana pamoja, kwa sababu warsha kama hizi zinawajengea uwezo,kina mama wanaweza na wakijengewauwezo basi wanafanya vizuri katika nyanja zote.
"Kina mama ni mtaji mkubwa popote pale, ni tegemeo kwenye maeneo
mengi, hawa ni jeshi,ukitaka kufanikisha jambo, na kuwatumia kinamama
basi jambo hilo lazima lifanikiwe, kwahiyomafunzo ya kufanya
wajitambuezaidi ni muhimukwao,"aliongeza.
Alisema  ingawa UWT ipo kisiasalakini walifikiria kuwainua kina mama
kwa kuanzisha kitengo cha miradi, ambapopamoja namambomengine
kinawaunganisha na taasisi mbalimbali za mikopo ilikuinua biashara
zao. Naye muandaaji wa warsha hiyo, Diwani wa Viti Maalum Msasani, Kuluthum Sagamiko,alisema lengo ni kuwajengea uwezo wanawake  hao wanaotoka katika kata, kwakuwandiowenye watu .
"Pia wajitambue nakujipanga nachangamoto hususan  cha uchaguzi na
maisha kwa ujumla, hasa wakati huukuelekea katikachaguzi za
kitaifa,"aliongeza. Licha ya kupata mafunzo ya kisiasa,Kuluthum  alisema pia kunamkufunzi  wa mamboya biashara, ili kuleta msukumozaidi,kwa kuamini kuwa mwanamke mwenye uchumi ananguvu  zaidi.
"Kwenye wilaya yetuyaKinondoni, tumepoteza majimbo mawili na kata 11,
kupitia wanawake hawa, wenye nguvu nauelewa itakuwa rahisi kurudisha
maeneo tuliyopoteza kwa upinzani,"alisema.

Mambo yapamba moto kuelekea fainali za Miss Temeke 2014


 Vimwana wa Miss Temeke 2014 wakiwa kwenye pozi la picha,ikiwa ni sehemu ya maandalizi yao ya kuelekea kwenye kinyang'anyiro chao kitakachofanyika kwenye Ukumbi wa TCC klabu Chang'ombe jini Dar es Salaam Agosti 22,2014.Jumla ya washiriki 17 watapanda jukwaani siku hiyo kuwania taji hilo huku Globu ya Jamii ikimzawadia kitita cha Sh. Mil 1 Mrembo atakaeonekana ana mvuto wa picha (Miss Photogeni 2014).
Wakiwa wamepozi wenyewe.
Wakitembea kwa mwendo wa madaha mithili ya Twiga mbugani.

Monday, August 18, 2014

SERIKALI YASHAURIWA KUTUNGA SERA YA KUDHIBITI POMBE


.



DSC_0279
Banda la Mtandao wa mashirika yapatayo 30 ya kupambana na matumizi ya kupita kiasi ya pombe nchini (Tanzania Network Against Alcohol Abuse) kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imeshauriwa kutunga sera madhubuti ya udhibiti wa pombe katika jamii ili pamoja na mambo mengine kuhakikisha vijana wanalindwa dhidi ya bidhaa hiyo kwenye soko.
Akizungumza na Moblog Tanzania jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo kikuu wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana, Msemaji wa Mtandao wa kupambana matumizi ya pombe kupita kiasi (Tanzania Network Against Alcohol Abuse) Bw, Mathias Kimiro amesema kwamba kuna umuhimu wa serikali kutunga sera mpya ya pombe ili kuzuia madhara kwa vijana na taifa kwa ujumla.

“Kwa kawaida matumizi ya pombe kupita kiasi ina madhara makubwa katika afya ya mtumiaji lakini vile vile ina madhara kwenye familia kupitia kaya moja moja na kusababisha mateso kwa familia hasa watoto,” amesema Bw Kimiro

Amesema kwamba umuhimu wa kuwa na sera madhubuti ya kudhibiti pombe katika jamii ni kuangalia upya ni kwa kiwango ngani matangazo ya pombe yanavyohamasisha unywaji kupita kiasi kwenye jamii. Bw Kimiro aliongeza kwamba mashirika yasiyo ya kiserikali yataendelea kuwakumbusha mamlaka zinazohusika umuhimu wa kuwa na sera ya kudhibiti pombe katika jamii pamoja na kuangalia madhara ya matangazo kwa wasomaji wa mabango.
DSC_0300
Mkurugenzi Mtendaji wa Makangarale Youth Theatre, ambao ni taasisi chini ya Tanzania Network Against Alcohol Abuse (TAAnet), Bw. Ismael Mnikite akifafanua jambo kwa Mgeni Rasmi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Bibi Venerose Mtenga wakati wa maadhimisho hayo.

Waziri Gaudensia Kabaka aipongeza TPB kutoa mikopo kwa wastaafu




Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta (TPB), Sabasaba Moshingi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka na baadhi ya viongozi meza kuu wakiwa wameshikana mikono na kuinyanyua juu ikiwa ni ishara ya kuwaunganisha wastaafu kwenye fursa mara baada ya uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta (TPB), Sabasaba Moshingi, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka na baadhi ya viongozi meza kuu wakiwa wameshikana mikono na kuinyanyua juu ikiwa ni ishara ya kuwaunganisha wastaafu kwenye fursa mara baada ya uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza katika uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza katika uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka meza kuu mara baada ya waziri huyo kuzinduwa rasmi mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka meza kuu mara baada ya waziri huyo kuzinduwa rasmi mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (wa nne kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi (wa tano kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (wa nne kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi (wa tano kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu ulioandaliwa na Benki ya Posta (TPB) wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF leo jijini Dar es Salaam.

WAZIRI wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka ameipongeza Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa kuandaa mpango maalumu wa kutoa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF ikiwa ni fursa itakayowainua kiuchumi wastaafu hao.
Waziri Kabaka ametoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizinduwa rasmi mpango wa mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Penseni wa LAPF, mpango utakaowawezesha wastaafu sasa kuchukua mikopo na kuendelea kukidhi maitaji yao kipindi hicho. Akizungumza kabla ya uzinduzi huo, Waziri Kabaka alisema Benki ya Posta na Mfuko wa Penseni wa LAPF hauna budi kupongezwa kwa hatua ya kulikumbuka kundi la wastaafu ambalo kimikopo lilikuwa limesahaulika.

“…Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru Benki ya Posta Tanzania pamoja na Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa kubuni mpango huu maalum wa kuwasaidia wastaafu kimaisha na kuwawezesha kumudu gharama za mahitaji yao na kukabiliana na ukosefu wa muda mfupi wa fedha wanazohitaji kwa kuwapatia mikopo,” alisema Waziri Kabaka.

Aliongeza kuwa mpango huo utawasaidia wastaafu kipindi cha maisha yao mapya ya kustaafu kwani licha ya muda huo wengi kuwa na kipato kidogo cha mapato lakini gharama za maisha kwao hazipungui na badala yake huendelea kupanda, jambo ambalo lilikuwa changamoto kubwa kwao.

“…Ninafarijika kuona kwamba Benki ya Posta pamoja na LAPF mmeliona hili na kulifanyia kazi, na hatimaye kuja na huduma hii ya mikopo. Lengo mahususi la mpango huu ambao kwa kiasi fulani umeanza kutekelezwa ni kuwapa faraja na kuwasaidia wastaafu katika kukidhi mahitaji yao mbalimbali, ili kuweza kuboresha maisha yao na maslahi kwa ujumla,” alisema waziri huyo.
Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi akizungumza katika hafla hiyo, alisema mkopo huo ni wa kwanza na wa aina yake katika soko la mabenki nchini hivyo wanaamini utatoa hauweni kwa wastaafu wa LAPF.
Akifafanua zaidi alisema mstaafu anayehitaji kuwa na dhamana huku riba inayotozwa kwa mkopo huo kuwa ni ndogo yaani asilimia 12 tu kwa mwaka ukilinganisha na mikopo mingine. “…Mkopo huu umewekewa bima, hivyo endapo mkopaji atafariki familia yake haitaendelea kudaiwa. Hivyo wastaafu wote wa mfuko wa LAPF wanaweza kupata mikopo hii ambayo marejesho yake ni kati ya mwaka mmoja hadi miaka mitatu,” alisema Moshingi.

Alisema huduma za mikopo hiyo ni za haraka na bora na zitatolewa kwa matawi yote ya Benki ya Posta Tanzania hivyo kuwataka wahitaji wote wastaafu wa Mfuko wa Penseni wa LAPF kwenda katika matawi hayo popote nchini kupata maelezo ya nini cha kufanya kabla ya kupata mkopo huo.

Hata hivyo TPB kwa kushirikiana na LAPF wamezishauri taasisi za fedha nyingine zikiwemo Benki kuangalia namna ya kuweka mipango ya kusaidia wastaafu nchini kwani kundi hilo lina kiasi kikubwa cha fedha ambacho kikitumiwa vyema kinaweza kuleta mchango mkubwa katika uchumi wan chi ya Tanzania. Hafla hiyo pia iliyohudhuriwa na viongozi waandamizi na wafanyakazi wa TPB na Mfumo wa Penseni wa LAPF ilishirikisha pia baadhi ya wastaafu ambao baadhi walieleza wameanza kunufaika na mpango huo wa mikopo kwa wastaafu.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

MAULID WA KITENGE AMWAGA WINO LEO KATIKA STUDIO ZA REDIO YA E-FM, SASA KUSIKIKA E-FM



Mtangazaji mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge akipeana mikono na Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela wakati wa kubadilishana mikataba baada ya kusainishana jioni hii katika makao makuu ya Radio hiyo,yaliopo Kawe jijini Dar es Salaam.

Mtangazaji mahiri wa habari za michezo wa siku nyingi Maulidi Baraka Kitenge amejiunga na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam leo.

Kutokana na tafiti ya ipsos ya mwaka 2013,inasemekana kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha redio one,ndie mtangazaji bora wa michezo nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela,ameeleza kufurahishwa kwake kwa mtangazaji huyo kinara kuhamia katika kituo hicho.

“Mpaka sasa Maulidi Kitenge ameshasign mkataba na kituo chetu na anatarajia kusikika hivi karibuni katika kipindi cha michezo hapa EFM”, alisema mkuregenzi huyo.

Maulidi Kitenge au jezi nambari tisa mgongoni, amejiunga na magwiji walio bobea katika fani hiyo akiwemo Dizo one,Dennis Sebo,Sos B,Kanky Mwaigomole na Dj Majay.

ENZOY DAWA YA NGUVU YA KIUME INARETA HESHIMA




TIBA YA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME NA KIKE UVUMBUZI WAKE KITABU HIKI HAPA




KITABU AMBACHO KINATOA TIBA ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME NA KIKE KWA KUTUMIA VYAKULA VYA ASILI IKIWEMO MATUNDA NA MBOGA MBOGA ZA MAJANI SASA KIPO MITAANI KINAPATIKANA MITAA YA UHURU NA MSIMBAZI KWA MAITAJI YA KITABU HIKI NA DAWA MBALIMBALI ZA KUTIBU MARADHI PAMOJA NA MATATIZO PIGA SIMU  0787406938

TANGAZO LA DAWA YENYE NGUVU ENZOY





DAWA YA NGUVU ZA KIUME NA MSIMKO KWA WANAWAKE WASIO NA HAMU YA TENDO LA NDOA AMBAYO HULETA MSISIMKO KWA WANAUME NA WAKE WAKUTANAPO.KWA SASA INAPATIKANA KWA BEI NAFUU HAPA JIJINI DAR ES SALAAM MAKUTANO YA MTAA WA KIPATA NA BARABARA YA MSIMBAZI
ALLY WA YANGA BOMBA UHURU NA MSIMBAZI 0787230551 AU 0652755838




PIGA SIMU KWA MR.MKUNJE O713827689, 0755074505 , au 0719 541366
,0652755838 UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM


BUGURUNI LOZANA STENDI YA TAX ULIZIA ADAMU KIBANDANI 0755875884
SHULE YA UHURU FIKA JENGO LA AZAM BAKHRESA ULIZA NGAEJE 0713873412
MWANANYAMALA FIKA JABA KLABU  ULIZA MACHELLAH 0713470492
ENZOY INALETA HESHIMA
Photo: whatsapp 0713406938
whatsapp 0713406938

MAULID KITENGE AACHA KAZI ITV NA RADIO ONE LEO.



MTANGAZAJI machachari wa habari za michezo kupitia kituo cha Televisheni cha ITV na Radio One, Maulid Baraka Kitenge (pichani) leo kupitia akaunti yake ya Twitter ametangaza rasmi kubwaga manyanga (kuacha kazi) katika Kampuni hiyo aliyokuwa akiifanyia kazi baada ya kuitumikia kwa kipindi cha miaka 14. chini ni ujumbe wake aliouandika kupitia akaunti yake ya Twitter.

Sunday, August 17, 2014

KUNDI LA BONGO DANSI LA SHEREHEKEA MWAKA MMOJA WA KUANZISHWA KWAKE NA VIJANA JAZZ



Baadhi ya wana bongo dansi wakiwa katika picha ya pamoja na bendi ya vijana jazz wakati wa kusherehekea mwaka mmoja wa kundi hilo tangia lianzishwe kwenye mtandao wa kijamii wa fecebook ambapo kundi hilo mpaka sasa lina wanachama 3,086 mashabiki wa bendi mbalimbali wa mziki ya dansi nchini picha na www.burudan.blogspot.com
Baadhi ya wanachama maarufu wa bongo dansi kushoto ni Abdulfareed Hussein ,
Senetor Mwinyi na William Kaijage walipokutana katika sherehe za mwaka wa kundi hilo zilizofanyika vijana kinondoni Dar es salaam picha na
www.burudan.blogspot.com
wafulumusha magitaa wa bendi ya Vijana Jazz wakiwajibika wakati wa sherehe za kutimiza mwaka mmoja kwa kundi la Bongo Dansi ambao ni mashabiki wa mziki wa dansi nchini wanaokutanishwa katika mtandao wa kijamii wa fecebook kushoto ni Shomari Ally na Said Kizunga picha na www.burudan.blogspot.com
Wasanii wa bendi ya Vijana Jazz wakiserebuka
Mpiga tumba wa bendi ya vijana jazz Ally Rajabu kushoto na Mpiga drams wa bendi hiyo Samata Hassani waki wajibika wakati wa onesho lao
Waimbaji wa bendi wa Vijana Jazz wakiimba kutoka kushoto ni Saburi Athumani,Julius Mwesiwa,Abdallah Mgonahanzeru na Husein Boom wakitoa burudani wakati wa kundi la mashabiki wa mziki wa dansi nchini la bongo dansi lilipokuwa linatimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kweke katika mtandao wa kijamii wa fecebook lina wanachama 3,086 mashabiki wa bendi mbalimbali wa mziki ya dansi nchini picha na www.burudan.blogspot.com

Waimbaji wa bendi ya vijana Jazz wakitoa burudani kwa kundi la Bongo Dansi kutoka kushoto ni Julius Mwesiwa na Komweta Maneti picha na www.burudan.blogspot.com
Baadhi ya wana Bongo Dansi wakiwa katika meza wakiendelea kupata burudani za vijana jazz

Mwana familia wa Bongo Dansi William Kaijage akisema chochote wakati wa sherehe hizo kulia ni mwimbaji wa bendi ya vijana jazz Abdallah Mgonaanzeru
Wasanii wa Vijana Jazz wakimkaribisha Miraji Shakashia katikati
Wana bongo Dansi wakimkaribisha mwenzao Rajabu Zomboko katikati kushoto ni William Kaijage na kulia ni
Senetor Mwinyi wakati wa kundi hilo lilipotimiza mwaka mmoja kamili tangu lianzishwe kwake kwenye mtandao wa kijamii wa fecebook


Mwimbaji wa bendi ya Vijana Jazz Komweta Maneti kushoto akiserebuka na wana bongo Dansi wakati wa onesho lao