Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, November 21, 2014

K-VANT GIN YADHAMINI BURUDANI ZA MALAIKA BAND TTC CLUB MWISHONI MWA WIKI


 Meneja wa Kanda ya Pwani wa Kampuni ya Megatrade watengenezaji wa kinywaji cha K-Vant gin, ,Geofrey Mkunde kushoto  akimkabidhi katoni ya kinywaji hicho Vendelin Meela wakati wa tamasha kubwa liliodhaminiwa na kampuni hiyo ambapo Malaika band
 walikuwa wakitoa burudani katika ukumbi wa Ttc club Chang'ombe mwishoni mwa wiki iliyopita kampuni hiyo imekuwa ikidhamini burudani mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia raha wateja wao baada ya kazi za kutwa nzima wengine na maofisa kutoka kampuni hiyo
Mkuu wa mauzo wa Kanda ya Pwani wa Kampuni ya Megatrade watengenezaji wa kinywaji cha K-Vant gin, ,Albert Kingu kushoto  akimkabidhi katoni ya kinywaji hicho Vendelin Meela wakati wa tamasha kubwa liliodhaminiwa na kampuni hiyo ambapo Malaika band
 walikuwa wakitoa burudani katika ukumbi wa Ttc club Chang'ombe mwishoni mwa wiki iliyopita kampuni hiyo imekuwa ikidhamini burudani mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia raha wateja wao baada ya kazi za kutwa nzima wengine na maofisa kutoka kampuni hiyo

Saturday, November 15, 2014

REDBULL WAMLETA BINGWA WA KUPIGA MISELE NA PIKIPIKI KUTOKA AFRIKA KUSINI


MWANAMICHEZO ambaye anacheza kwa kutumia chombo cha moto Pikipiki  Bryan Capper yuko nchini kwa mwaliko maalum akitoka nchini kwao Afrika kusini ametoa wito kwa watanzania kucheza mchezo huo ambao mbali ya kufurahisha pia unatumia akili na kukufanya uwe mkakamavu wakati wote.
Akizungumza leo asubuhi  katika viwanja vya Coco Beach  Jijini Dar es Salaam ambako ndiko alikoanza kuonesha onyesho lake la kwanza  na kuonesha umahiri wake katika uendeshaji wa pikipiki  yupo nchini kwa kudhaminiwa na Kampuni ya Red Bull, atakuwa nchini kwa ziara ya  siku tatu.
Kesho  Jumapili atakuwa katika viwanja vya Mlimani City na  Jumatatu atahitimisha ziara yake katika eneo la Ubungo Tanesco.
Capper amesema kwamba amefurahia kuweza kufika nchini Tanzania  pia tayari ameshafanya maonyesho yake katika nchi za Kenya na Uganda.
Wakati huohuo Rais wa Tanzania Motorcross Acrobatic Club , Blagina Mwihava alisema kwamba wamemleta  mwanamuchezo huyo ambaye wana imani kubwa ataleta msisimko mkubwa kwa vijana wa kitanzania kuweza kupata hamasa ya kucheza mchezo huo wenye mvuto.    
 “Hii itakuwa ni shoo kwa watanzania  ili waweze kuvutika kucheza mcheo huu wa aina yake .

Ziara ya mchezaji huyo imeratibiwa na Kampuni ya Mohans  inayosambaza kinywaji cha Redbull nchini maonesho hayo yote  ni ya wazi.

MISS TANZANIA 2013 HAPPINESS WATIMANYWA AAHIDI KUNG'ARA MISS WORLD


Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited, Bw. Hashim Lundenga (kulia) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu safari ya Mrembo wa Tanzania wa mwaka 2013 kuelekea katika Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2014) nchini Uingereza.
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
  
MREMBO wa Tanzania wa mwaka 2013, Happiness Watimanywa ameahidi kuing’arisha Tanzania katika mashindano ya ulimbwende ya Dunia yatakayofanyika mapema mwezi ujao huko nchini Uingereza.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, mlimbwende huyo amewaeleza waadishi kuwa, kutokana na uzoefu wa kazi zake alizokuwa akifanya kwa jamii kwa muda kipindi cha mwaka mmoja ikiwemo misaada ya hali na mali anayoipata toka  Bodi ya Utalii Tanzania pamoja na wahisani wengine nchini amewaahidi Watanzania kuibuka na ushindi katika kinyang’anyiro hicho huko nchini Uingereza ili kuitangaza Tanzania.
Alieleza kuwa, tayari Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza utakuwa tayari kumpokea pindi atakapowasili nchini humo kwa lengo la kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ya ulimbwende yatakayowahusisha walimbwende toka Ulimwengu  mzima.
“Nimejifunza mambo mengi hasa kipindi wakati nasafiri sehemu mbalimbali nchini pamoja na kufanya kazi za kusaidia jamii katika kipindi chote, hivyo nawaahidi watanzania ushindi katika mashindano hayo yatakayofanyika huko Uingereza pia mnipigie kura zenu za wingi”, alisema Watimanywa.
Naye Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited, Bw. Hashim Lundenga ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, alisema kuwa mashindano ya Urembo wa Dunia ni mashindano ya Kimataifa ambayo yanawakutanisha walimbwende toka nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania, hivyo alitoa wito kwa watanzania wote kuunga mkono kwa kumpigia kura nyingi mwakilishi ambaye ndiye mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2013, Hapinness Watimanywa ili ajinyakulie taji hilo la dunia ili aweze kuipa sifa Tanzania kimataifa.
Mashindano ya Urembo ya Dunia yanatarajiwa kufanyika mapema tarehe 14 Desemba, 2014 huko nchini Uingereza ambapo mrembo huyo wa Tanzania anatarajia kuanza safari yake ya kuelekea nchini humo tarehe 15 Novemba, 2014 tayari kwa ajili ya mashindano hayo.

KAMPUNI YA MAFUTA YA ENGEN YAADHIMISHA MIAKA 21 TANGU KUANZISHWA KWAKE




Wafanyakazi wa Kampuni ya Mafuta ya ENGEN Tanzania leo Novemba 14,2014 wameungana na wafanyakazi wenzao Barani Afrika kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 21 ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo,ambayo husherehekewa kila Mwaka ifikapo tarehe kama ya leo.Engeni ni Kampuni iliyojikita katika uuzaji wa Mafuta bora ndani na nje ya Tanzania,huku ikiendelea kujivunia kwa Ubora wake.Pichani ni Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni hiyo ya Engen hapa nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya jengo lao Kurasini jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya ENGEN Tanzania,Mubita Akapelwa (wa pili kulia) akikata keki wakati wa Kusherehekea Miaka 21 ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo,ambayo husherehekewa kila Mwaka ifikapo tarehe kama ya leo,iliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Ofisi za Kampuni hiyo,Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Shaaban Kayungilo.

Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Shaaban Kayungilo akichua kipande cha Keki iliyokatwa vyema na Dada Jullieth Lwato (alieshika sahani) wakati wa Kusherehekea Miaka 21 ya kuanzishwa kwa Kampuni hiyo,ambayo husherehekewa kila Mwaka ifikapo tarehe kama ya leo,iliyofanyika kwenye Makao Makuu ya Ofisi za Kampuni hiyo,Jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAHARIRI VYOMBO VYA HABARI KWA MAZUNGUMZO JIJINI DAR ES SALAAM.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya Habari (hawapo pichani) wakati alipokutana nao nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana kwa mazungumzo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya Habari wakati alipokutana nao nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana kwa mazungumzo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile na Mhariri wake, Jackton Manyerere (kulia) mara baada ya kumalizika mazungumzo na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari yaliyofanyika kwenye Makazi ya Mhe Makamu wa Rais Oysterbay, jijini Dar es Salaam, jana usiku.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Wahariri wa Gazeti la Mwananchi mara baada ya kumalizika mazungumzo na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari yaliyofanyika kwenye Makazi ya Mhe Makamu wa Rais Oysterbay, jijini Dar es Salaam, jana usiku.
 Mhariri wa gazeti la Jamhuri, Jackton Manyerere, akichangia mada wakati wa mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, yaliyofanyika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam, jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wahariri hao baada ya mazungumzo.

Friday, November 14, 2014

MASHINDANO NG'OMBE CUP YAENDEREA MAFIA MKOA WA PWANI



LIGI ya ng'ombe cup imeimalizika kwa atua ya kwanza  baada ya kumalizika mchezo wa mpira wa miguu baina ya jah fc na bayani fc ambapo katika matoke bayani ilibuka na ushindi wa magoli 2.0 matokeo hayo yameifanya bayani kutinga 8 bora ambapo imeungana na timu za rhino,utende fc,bayan,mfuluni,killas
,jah fc, pince boys, na potwe fc mashindano hayo yataendelea tena jumatatu taharifa hii kwa niaba ya mwenyekiti wa mashindano  ya ngo'mbe cup mafia kisiwani

mashindano hayo yanafanyika  dawe ndege wilayani kilindoni mafia mkoa wa pwani na kudhaminiwa na diwani wa  halmashauli wilaya ya mafia, Msomi Ally Kuku yataendelea tena jumatatu kwa kuzikutanisha timu mbalimbali zilizotinga hatua ya 8 bora

Thursday, November 13, 2014

BONDIA THOMAS MASHALI ASAINI KUZIPIGA NA ABDALLAH PAZI JANUAR MOSI FRENDS CORNER


Bondia Thomasi Mashali kushoto akitia saini ya kupigana na Abbdallah Pazi kulia baada ya makubaliano na promota Kassim Texas katikati mpambano utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BLOG
Bondia Abbdallah Pazi kulia akitia saini ya kupigana na Thomasi Mashali kushoto baada ya makubaliano na promota Kassim Texas katikati mpambano utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BLOG

Bondia Thomasi Mashali kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano juzi  ya mpambano wao kufanyika January Mosi 2015 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaa Picha na SUPER D BLOG
Promota Kassim Texas katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Thomas Mashali kushoto na Abdallah Pazi kuashilia makubaliano ya mpambano wao utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese Picha na SUPER D BLOG



Bondia Thomasi Mashali kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano juzi  ya mpambano wao kufanyika January Mosi 2015 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaa Picha na SUPER D BLOG

JONAS MKUDE ASAINI MKATABA MPYA WA MIAKA MIWILI SIMBA



Kiungo wa timu ya Simba SC, Jonas Gerald Mkude (katikati) akisani mkataba mpya mbele ya Rais wa Simba , Evans Aveva (kulia), Zachalia Hans Pope (kushoto)
Jonas Gerald Mkude (katikati) akiweka saini ya dole gumba katika mkataba mpya mbele ya Rais wa Simba , Evans Aveva (kulia), Zachalia Hans Pope (kushoto).
KIUNGO wa Simba SC, Jonas Gerald Mkude amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Simba SC na kusema bado nipo sana Msimbazi.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Silver Pippe, Kawe, Dar es Salaam Mkude amesema kwamba amesaini klabu hiyo baada ya kufikia kiwango cha fedha alichotaka.
Mkude mwenyewe hakusema ni kiasi gani amepewa, lakini habari ambazo mtandao huu mezipata zinasema kiungo huyo amepewa Sh. Milioni 60, ingawa mwenyewe alianzia Milioni 80.

MKURUGENZI WA TCRA PROFESA NKOMA AWAPA SOMO WAMILIKI WA BLOGS NCHINI



Baadhi ya wamiliki wa blogs wakiwa katika mkutano huo ulioandaliwa na TCRA, jijini Dar es Salaam

Make Money at : http://bit.ly/best_tips
Mmiliki wa Blog ya Bongo Weekend, Khadija Kalili akichangia hoja wakati wa mkutano huo. Baadhi ya wamiliki wa blogs wakiwa katika mkutano huo ulioandaliwa na TCRA, jijini Dar es Salaam

Make Money at : http://bit.ly/best_tips
 Mmiliki wa Blog ya Bongo Weekend, Khadija Kalili akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
 Baadhi ya wamiliki wa blogs wakiwa katika mkutano huo ulioandaliwa na TCRA, jijini Dar es Salaam
Baadhi  ya  wamiliki wa  Blogs wakiwa  katika   warsha ya  TCRA
Viongozi  wa  TCRA  wakifuatilia maswali  ya  wamiliki  wa  Blogs  Tanzania
Baadhi ya  wamiliki  wa  Blogs Tanzania  wakiwa katika warsha  ya  TCRA  kuelekea  uchaguzi  mkuu
Baadhi  ya  wamiliki wa  Blogs wakiwa  katika   warsha ya  TCRA Wana Blogu wakiwa makini ni Peter Mwenda na Super D
Wamiliki  wa  Blogs wakiwa katika  warsha ya  TCRA
Wamiliki  wa  Blogs wakiwa  katika  warsha  katika  ukumbi wa Mlimani City leo
Baadhi ya  wanahabari  wakifuatilia  warsha  hiyo
Washiriki wa  warsha  ya  TCRA  wakiwa  katika  warsha  hiyo

Profesa Nkoma  alisema  kuwa iwapo  wamiliki wa Blogs  nchini  wataanzisha  chama  chao  upo  uwezekano mkubwa  wa TCRA  kuwasaidia mchakato  huo na pia kuendelea  kuungana na chama  hicho  kwa kuendelea  kutoa elimu  zaidi.
Mbali ya  kuwataka  kuanzisha  chama  hicho  bado  aliwataka  wamiliki  wa blogs  nchini  kuendelea  kuifanya kazi  hiyo kwa  kuheshimu misingi ya maadili .
Pia  alisema  kuwa  TCRA  wataendelea  kuwa na mkakati  wa  kuendelea  kutoa elimu  na kukutana na wamiliki  wa Blogs ili kukumbushana maadili  zaidi.
Akielezea  kuhusu uwajibikaji wa  blogs nchini kuelekea  uchaguzi mkuu wa  mwaka 2015 alitaka   kuhakikisha  wanatoa nafasi  sawa  kwa vyama  na  wagombea  wote  bila  upendeleo.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AKABIDHI TUNZO KWA WASANII BORA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi tunzo ya Msanii ya Mafanikkio katika maisha ya usanii (LIFE TIME ACHIEVEMENT AWARD) Bibi Martina Edward kwa niaba ya Said George Tingatinga kwenye hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 13,2014 Ikulu Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi tunzo ya Msanii bora katika masuala ya kijamii (HUMANITARIAN AWARD) Bw. Patrick Kungalo kwa niaba ya Fr. Canute Mzuanda kwenye hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 13,2014 Ikulu Dar es salaam. Makamu wa Rais alikutana na jopo la waandaaji wa siku ya Msanii, Kampuni ya Haak Neel Production, Baraza la Sanaa la Taifa na Wizara ya Habari, Vijana Michezo na Utamaduni na kutoa zawadi ya fedha shilingi milioni kumi ambazo aliahidi siku kilele cha siku ya Msanii Tanzania iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Oktoba 25,2014
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akiwa katika picha ya  pamoja na washindi wa tunzo ya msanii bora na Viongozi wa Wizara ya Habari baada ya kukabidhi tunzo hizo katika hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 13,2014 Ikulu Dar es salaam.

BODI YA FILAMU TANZANIA YAZITAKA KAMPUNI ZA FILAMU KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI ZA FILAMU.



1
Katibu Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo akiongea na wahusijka wa Kampuni ya Kajala Entertainment wakati alipofanya nao mkutano leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapa Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu ya Mbwa Mwitu.
2q
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kajala Entertainment, Kajala Masanja akijitetea mbele ya Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania wakati aliitikia wito wa Ofisi ya Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuelezwa juu ya Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu yake ya Mbwa Mwitu.
3
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kajala Entertainment, Kajala Masanja akijitetea mbele ya Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania wakati aliitikia wito wa Ofisi ya Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuelezwa juu ya Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu yake ya Mbwa Mwitu.
4
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kajala Entertainment, Kajala Masanja akiweka sahihi ya kukubali kufanya marekebisho katika filamu yake pamoja na malipo ya faini mbele ya Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania wakati aliitikia wito wa Ofisi ya Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuelezwa juu ya Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu yake ya Mbwa Mwitu.
5
Meneja ambaye pia ni Mratibu wa Kampuni ya Kajala Entertainment, Bi. Leah Mwendamseke akiweka sahihi katika fomu maalum ya kukubali kufanya marekebisho katika filamu iliyokaguliwa na Bodi hiyo mbele ya Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania wakati aliitikia wito wa Ofisi ya Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuelezwa juu ya Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu ya Mbwa Mwitu.
6
Katibu Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo akiagana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kajala Entertainment wakati alipofanya naye mkutano leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapa Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu ya Mbwa Mwitu.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DSM)