Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed
Shein, akitoa taarifa maalum kwa wananchi kuhusu zoezi la kuhesabiwa la
Sensa, litakalofanyika siku ya Jumapili, Agosti 26, mwaka huu, ambayo
itawezesha na kufanikisha mipango ya
maendeleo kwa Taifa. (Picha ya Ramadhan Othman, Ikulu)
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
24.8.2012
RAIS wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein,
ameeleza kuwa matokeo ya sensa ndio yanayoipa Serikali taarifa halisi na
ya kitaalamu juu ya idadi ya watu na taarifa nyengine muhimu katika
kutayarisha mipango ya maendeleo.
Dk.
Shein aliyasema hayo leo katika taarifa yake aliyoitoa kupitia vyommbo
vya habari kwa wananchi kuhusu umuhimu wa wananchi katika kushiriki
kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makaazi itakayofanyika
tarehe 26 Agosti, mwaka huu.
Kwa
matiki hiyo, Dk. Shein alieleza kuwa kujua idadi ya watu katika eneo
fulani kunaiwezesha Serikali kukadiria mahitaji ya huduma kwa wakaazi
wake ambapo kinyume chake ni kutoa huduma pungufu kwa vile hakuna
takwimu sahihi ya wakaazi hao.
Dk.
Shein alisema kuwa si jambo la kufurahisha kusikia kuwa baadhi ya watu
ambao wanawashawishi watu wengie wasishiriki katika zoezi hilo muhimu na
kusisitiza kuwa wananchi wa Zanzibar sio wageni katika zoezi hilo kwani
wameshashiriki kwa vipindi kadhaa na kupata mafanikio ambapo sensa ya
mwanzo iliyowajumuisha watu wote ilifanyika mwaka 1948.
Alisema
kuwa suala la kuzingatia ni kuwa sensa haina uhusiano wo wote na
matakwa ya watu kibinafsi bali ina lenga kuleta mafanikio kwa watu wote
kwani hilo ni jambo la msingi sana kwa lengo la kuiwezesha Zanzibar
kujua idadi halisi ya wananachi wake na kuwafikishia maendeleo.
“Sote
lazima tuweke mbele mapenzi na uzalendo kwa nchi yetu tukielewa kuwa
sisi ndio wapangaji, watekelezaji na wasimamzi wa mipango yetu ya
maendeleo kwani bila ya kushiriki katika utekelezaji wa majukumu hayo
nchi yetu itawachwa nyuma na mataifa mengine yatasonga mbele kwa kasi,
jambo ambalo siyo vyema kuliruhusu”, ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Dk.
Shein alitumia fursa hiyo kwa mara nyengine tena kuwasihi wananchi wote
kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo muhimu hapa nchini.
Aidha,
Dk. Shein alisema kuwa sensa zote ni muhimu, lakini sensa ya mwaka huu
ina umhimu wa kipekee kwa kuwa taarifa zitakazokusanywa zitatumika
kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya
mwaka 2025 kwa Tanzania Bara na mwaka 2020 kwa Zanzibar pamoja na
Mkakati wa Kukuza na Kupunguza Umasikini MKUKUTA na MKUZA.
Dk.
Shein alieleza kuwa Zanzibar imepiga hatua kubwa katika nyanja mbali
mbali za kiuchumi, kisiasa, utawala bora, haki za binaadamu na ustawi wa
jamii licha ya kuwepo kwa baadhi ya changamoto kadhaa.
Dk.
Shein alisema kuwa taarifa kutoka Ofisi ya Rais inayoshughulikia Fedha,
Uchumi na Mipango ya Maendeleo zimebainisha mafanikio makubwa katika
kukuza uchumi katika kipindi cha miaka miwili iyiliyopita.
Alieleza
kuwa pato la jumla la mtu binafsi limeongezeka kutoka wastani wa Tsh.
782,000 mwaka 2010 hadi kufikia Tsh. 960,000 mwaka 2011. Aidha, taarifa
za hivi karibuni zinaonesha kuwa uchumi wa Zanzibar umekuwa kwa asilimia
6.8 katika mwaka 2011 ikilinganishwa na asilimia 6.5 ya mwaka 2010.
Pamoja
na hayo, Dk. Shein alieleza kuwa jitihada mbali mbali zimefanyika
kupunguza tatizo la mfumko wa bei ambapo katika miezi ya mwanzo ya mwaka
huu ilionekana hali kuwa sio nzuri na kutokana na juhudi hizo mfumko
wa bei umeweza kudhibitiwa hadi kufikia asilimia 9.4 kwa mwezi wa Juni
kwani awali ya mwaka 2011 na 2012 ilifikia hadi asilimia 16.6.
Akiendelea
kutaja mafanikio hayo, Dk. Shein alisema kuwa mafanikio yamejitokeza
kwa upande wa ujenzi wa miundombinu, kuimarika kwa huduma za maji safi
na salama na pia kuzidi kusambaa kwa huduma za umeme kwa wananchi wengi
zaidi hasa wa vijijini.
Pia,
Dk. Shein alisema kuwa Zanzibar imepiga hatua katika uimarishaji wa
sekta ya kilimo baada ya Serikali kutekeleza ahadi yake ya kutoa ruzuku
kwa wakulima ambapo asilimia 75 ya gharama imebebwa na Serikali.
Alieleza
kuwa hatua iliyofikiwa hivi karibuni ya kuwandolea wananchi mchango wa
Tsh. 40,000 kwa waja wazito wanaojifungua kwa njia ya operesheni,
imetokana na kuwa na takwimu sahihi zenye kuonesha idadi yao na kiasi
cha fedha kinachopatikana.
Sambamba
na hayo, Dk. Shein aliwashukuru viongozi wa ngazi mbali mbali katika
jamii ambao muda wote wameendelea kuwahamasisha wananchi ili washiriki
katika sensa ya mwaka huu, huku akiwashukuru wananchi wote kwa
ushirikiano mkubwa walioutoa wakati wa maandalizi ya zoezi la sensa
tangu lianze katika hatua mbali mbali.
Aidha,
Dk. Shein alisisitiza kuwa kwa azma ya kuitakia mema Zanzibar, ni vyema
kila mtu ashiriki katika kuhesabiwa na kufanikisha zoezi hilo “Hii ni
dhamana yetu sote”,alisema Dk. Shein.
Mbali
na hayo Dk. Shein aliwataka Maafisa wa sensa na wote watakaoshiriki
katika zoezi hilo kuwa na bidii ya kazi yao, nidhamu, ustahamilivu na
uchangamfu wakati wote na wawafahamishe na wawaelimishe watu yanayopaswa
kufanywa na maelezo yanayohitajika.