Na Mwandishi Wetu
BONDIA wa kike Mwanne Haji ambaye
amejitokez kupambana na mabondia kwa kike wa Dar es salaam baada ya
kuwasumbuwa sana mabondia wenzake wanaotoka Chunya Mkoa wa Mbeya na sasa
kujikita katija jiji lakitokea katika GYM ya Zugo iliyopo Gongolamboto
bondia uyo wa kike ambaye amesha panda
uringoni kupambana na baadhi ya mabondiwa wa mkoani amesema amekuja kwa
ajili ya mchezo wa msumbwi jijini hivyo mabondia wa kike wakae pembeni
kwani sasa ata wasambalatisha mmoja baada ya mwingine
alitolea mfano wa mabondia wanaotamba
Dar es salaam kwa kupigana wenyewe kwa wenyewe kila wakati ni Lulu
Kayage,Halima Ramadhani, Fatuma Yazidu
sasa wakae foleni kwani atawapa vipigo
mmoja baada ya mwingine bondia uyo mpaka sasa amecheza michezo mitatu
ambapo mchezo wake wa kwanza alicheza na Vailet Modest na kufanikiwa
kumtwanga kwa point mchezo wake wa pili alicheza na Telesia Kiwale na
mchezo wake wa tatu alicheza na Jennifer Pius na kumsambalatisha kwa
pointi
hivyo amewaomba mapromota wajitokeza kumsaidi kupambanishwa na mambondia aliowataja hapo juu kwa uzito wa kg 49
mbali na hivyo ametowa wito kwa tasisi
mbalimbali pamoja na kmpuni kujitokeza kudhamini mchezo wa masumbwi
kwani unapendwa na mashabiki lukuki nchini