Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00

Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, July 29, 2016

MAZOEZI MAKALI YANAENDELEA KATIKA KAMBI YA SUPER D COACH UHURU GYM KARIAKOO

Mabondia Faraji Sayuni kushoto na Hassani Kiwale wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM Kariakoo mabondia wote hawo watapanda uringoni agost 8 katika ukumbi wa kobelo pub manzese Dar Es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS

 Bondia Hassani Kiwale kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Faraji Sayuni wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika katika kambi ya Super DCoach Uhuru GYM Kariakoo Dar es salaam mabonda hawo watapanda uringoni Agost 8 kuwakabili wapinzani wao katika ukumbi wa kobelo pub manzese Dar Es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwasimamia mazoezi mabondia Faraji Sayuni kushoto na Hassani Kiwale wakati ya mazoezi yao yanayoendelea katika kambi ya Super D coach Uhuru GYM Kariakoo Dar Es Salaam 

Na Mwandishi Wetu
MPAMBANO wa ubingwa wa taifa wa kg 57 utagombaniwa na mabondia Kais Rashidi Na Faraji Sayuni siku ya Agost 8 katika ukumbi wa Kobelo Pub Manzese Dar Es Salaam  

mpambano uho wa raundi kumi za ubingwa umeratibiwa na Promot Miraji Uliza ambapo kutakuwa na mapambano mengine mbalimbali ya mchezo wa masumbwi nchini

mabondia wengine watakaopanda siku hiyo ni Abdallah Pazi atakaezipiga na Said Mkone wakati godrack Mrema atakumbana na Hassani Kiwale wakati Omari Uliza atazipiga na Bruno Fadhili na Said Jelemi atamkabili Azizi Kondo na Saleh Mkalekwa atacheza na Salum Ngula na Azizi Uliza atacheza na Mohamed Matimbwa

pamoja na mapambano mengine mengi

Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

CHADEMA YAMLILIA JOSEPH SENGA

SALAAM ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA JOSEPH SENGA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko na mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha mmoja wa waandishi wa habari za picha mwandamizi na mahiri nchini, Joseph Senga kilichotokea usiku wa jana akiwa kwenye matibabu nchini India.

Kama taasisi na kisha mtu mmoja mmoja kuanzia kwa wanachama na viongozi wa chama kwa hatua ya sasa tumejikuta tumeishiwa maneno ya kusema kuhusu kifo cha mwandishi huyu mwandamizi, lakini katikati ya mshtuko na majonzi tuliyonayo, tunaweza kusema kuwa kifo cha Senga, hasa siku kiliyotokea, kimedhihirisha jambo moja kubwa kuwa alikuwa SHUJAA WA DEMOKRASIA NA HAKI.

Kifo cha Senga kimetokea siku ambayo kulikuwa na matukio makubwa mawili kuhusu demokrasia na haki nchini.

Kwanza, wakati Senga anafariki usiku wa Jumatano, Julai 27, mchana wa siku hiyo hiyo Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, ilikuwa imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 15 jela askari anayefahamika kwa jina la Pacificius Simon kwa hatia ya kosa la kumuua bila kukusudia aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel ten, mkoani Iringa.

Matukio hayo matatu; kuuwawa kwa Mwangosi, hukumu ya aliyemuua na kifo cha Senga, yana uhusiano mkubwa wa karibu huku Senga akiwa katikati yake, kwamba;

Picha zote ambazo hadi leo zinaweza kupatikana dunia nzima kupitia mtandao wa intaneti zikionesha mauaji ya kikatili aliyofanyiwa Mwangosi, kuanzia ile ambayo inaonesha kundi la askari polisi likiwa limemzunguka Mwangosi huku mmoja wao akiwa amemlenga kwa bunduki ya kulipulia mabomu ya machozi, hadi zile ambazo zinaonesha mwili wa mwandishi Mwangosi ukiwa umefumuliwa na kutawanywa vibaya baada ya kulipuliwa, huku nyingine ikimuonesha mmoja wa askari akiugulia maumivu ya ‘bomu’ lililomuua Mwangosi, zilipigwa na Shujaa Senga.

Kwa watu waliokuwepo siku ya tukio hilo baya kuwahi kuikumba tasnia ya habari nchini, watakumbuka kuwa Senga alipiga picha zile akiwa katikati ya mirindimo na moshi wa mabomu, ngurumo za risasi za moto na kundi la askari wengi ambao walikuwa wanazidi hata idadi ya wanachama na viongozi wa CHADEMA waliokuwa wamekusanyika kwa amani kwenye ofisi yao kijijini Nyololo kabla hawajavurugwa na Jeshi la Polisi likiongozwa na RPC Michael Kamhanda.

Picha zile ambazo ziliiambia dunia nzima ukweli wa tukio hilo, ziliokoa watu wengi na bila shaka zilisaidia kutotokea kwa jambo kubwa ambalo watawala walishaanza kuonesha nia ya kulitekeleza, kupitia maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi, makao makuu na mkoani Iringa, ambao walitaka kuonesha kuwa CHADEMA ‘walijilipua’, ambapo maana yake ni kwamba wafuasi, wanachama na viongozi wa CHADEMA walikuwa na milipuko au vitu vya namna hiyo.  

Pili; Senga amefariki siku ambayo Watanzania bila kujali tofauti zao, wakiongozwa na CHADEMA walitangaza Operesheni UKUTA ambayo moja ya malengo yake ni kupigania haki za makundi mbalimbali ya Watanzania, wakiwemo waandishi wa habari dhidi ya mifumo kandamizi inayolelewa na watawala kupandikiza mbegu za utawala wa kidikteta nchini.

Kwa muda mrefu, kupitia chombo chake alichokuwa akikifanyia kazi hadi mauti yanamkuta, Free Media, CHADEMA kama inavyofanya kazi na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali, ilikuwa ikishirikiana na Senga kikazi, huku naye akifanya kazi yake kwa uwezo mkuwa, akizingatia miiko na misingi ya taaluma ya uandishi wa habari, kwa weledi mkubwa. 

Habari picha zake mbalimbali ambazo zimekuwa zikidhihirisha ukongwe wake katika tasnia ya habari, zikiwemo za matukio ya CHADEMA, zitakuwa historia itakayotunza jina lake miongoni mwa waandishi mahiri nchini ambazo waandishi chipukizi watajifunza.

Kwa masikitiko makubwa, CHADEMA inatoa salaam za pole kwa familia ya marehemu, Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media, wafanyakazi wenzake, tasnia ya habari nchini na Watanzania wengi walioguswa na msiba huo. Mwenyezi Mungu awatie moyo wa ujasiri kuyakabili majonzi mazito ya kifo cha mpendwa Senga.

Huyo ndiyo Joseph Senga. Shujaa wa demokrasia na haki. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema.

Imetolewa leo Alhamis, Julai 28, 2016 na;

Tumaini Makene
Mkuu Idara ya Habari na Mawasiliano

CHADEMA

MABONDIA KUTOKA KWA SUPER D COACH UHURU GYM

MABONDIA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA YA MAZOEZI YAO YANAYOFANYIKA KWA SUPER D COACH UHURU GYM KARIAKOO KUTOKA KUSHOTO NI HASSANI KIWALE 'MORO BEST' KG 51 MOHAMED KISEA KG 54 FARAJI SAYUNI KG 56 IDDI MKWELA KG 61 VICENT MBILINYI KG 63 GESPER MSEVENI KG 66 NA KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D'
BAADHI YA MABONDIA WALIOPO KATIKA KAMBI YA SUPER D COACH UHURU GYM
BAADHI YA MABONDIA WALIOPO KATIKA KAMBI YA SUPER D COACH UHURU GYM
KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D AKIWA NA  MABONDIA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA YA MAZOEZI YAO YANAYOFANYIKA KWA SUPER D COACH UHURU GYM KUTOKA KUSHOTO NI HASSANI KIWALE 'MORO BEST' KG 51 MOHAMED KISEA KG 54 FARAJI SAYUNI KG 56 IDDI MKWELA KG 61 VICENT MBILINYI KG 63 GESPER MSEVENI KG 66

KOCHA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KUSHOTO NI FARAJI SAYUNI NA HASSANI KIWALE
KOCHA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KUSHOTO NI FARAJI SAYUNI NA HASSANI KIWALE

Monday, July 25, 2016

MABONDIA WA KIKE KUPANDA URINGONI AGOST 7 UWANJA WA TAIFA KUWASINDIKIZA GALILE NA KALAMA

Promota wa mchezo w masumbwi nchini  Haruna Mussa 'Dippo' katikati akizungumza na mashabiki wa mchezo wa ngumi za kulipwa wakati alipowatambulisha kupigana kwa mabondia wa kike Halima Bandola na Joyce Awino watakao oneshana umwamwamba Agost 7 katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha SUPER D BOXING NEWS

Promota wa mchezo w masumbwi nchini  Haruna Mussa katikati akiwainua juu mabondia mbele ya mashabiki wa mchezo wa ngumi za kulipwa wakati alipowatambulisha kupigana kwa mabondia wa kike Halima Bandola na Joyce Awino watakao oneshana umwamwamba Agost 7 katika uwanja wa ndani wa  Taifa Picha SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA wa kike katika mchezo wa ngumi za kulipwa nchini Halima Bandola na Joyce Awino watapanda uringoni Agost 7 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa taifa

akizungumza na mashabikiwa mchezo wa masumbwi wishoni mwa wiki iliyopita promota wa mpambano uho Haruna Mussa 'Dippo'

amesema ameamua kuwa promoto watoto wa kike kwa ajili ya kuhamasisa wasichana kuupenda na kuucheza mchezo wa masumbwi kwani kwa sasa michezo ni ajira kwa vijana

aliongeza kwa kusema katika mpambano uho kutakuwa na mpambano wa kukata na shoka mabondia Kalama Nyilawila atavaana na Selemani Galile mpambano wa raundi kumi katika uzito wa kg 72

wakati mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Meshack Mwankemwa kutoka Mbeya atakumbana na Selemani Zugo mpambano wa ubingwa wa KG 66 raundi kumi   
 Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

RAIS DK. MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA SIKU YA MASHUJAA KITAIFA MJINI DODOMA

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka Sime katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016. PICHA ZOTE/IKULU
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka Ngao katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma  Julai 25, 2016.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kuweka silaha za jadi.
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiongea wakati wa Madhimisho ya Siku ya Mashuja.
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiongea wakati wa Madhimisho ya Siku ya Mashuja.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela baada ya kuongea na wananchi kwenye Madhimisho ya Siku ya Mashuja.

DVD MPYA KABISA ZA MASUMBWI SASA ZINAPATIKANA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI

DVD MPYA KABISA ZA MASUMBWI SASA ZINAPATIKANA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.burudan.blogspot.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

BONDIA IDDI MKWELA ALIVYO MSAMBALATISHA MWITA MACHAGE K.O RAUNDI YA KWANZA

Bondia Mwita Machage kushoto akipambana na Iddi Mkwela wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Mkwela alishinda kwa K.O ya raundi ya kwanza katika mpambano huo Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Iddi Mkwela kushoto akimshambulia Mwita Machage kwa makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Mkwela alishinda K.O ya raundi ya kwanza ya mpambano uho Picha na SUPER D BOXING NEWS
Refarii Saidi Chaku akimnyoosha mkono juu bondia Iddi Mkwela baada ya kumdunda kwa K.O ya raundi ya kwanza Mwita Machage kushoto ni bondia Vicent Mbilinyi Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akifuraia baada ya bondia Iddi Mkwela kusinda kwa K.O ya raundi ya kwanza wakati wa mpambano wake uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akifuraia baada ya bondia Iddi Mkwela kusinda kwa K.O ya raundi ya kwanza wakati wa mpambano wake uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kushoto ni Sako Mwaisege 'Dungu' Picha na SUPER D BOXING NEWS
kabla ya mpambano kuanza

NITAHAMIA DODOMA SEPTEMBA MWAKA HUU - WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  alipokuwa akiwasalimia na kuwashukuru mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma mapema leo asubuhi  waliojitokeza kushuhudia  maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA
*Asema akishahamia, Mawaziri na Naibu Mawaziri wote wafuatie mara moja
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atahamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka huu kuonyesha kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi.

Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Julai 25, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma.
“Jana nilimwita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kumwambia akamilishe matengenezo kwenye nyumba yangu kwa sababu ninataka kuhamia Dodoma ifikapo Septemba,” amesema na kushangiliwa na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma waliohudhuria maadhimisho hayo.
Amesema tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, kazi nyingi zimefanyika na wananchi wameziona na kwamba sasa hivi kazi iliyobakia ni utekelezaji wa ahadi alizotoa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.
“Wananchi kazi mmeziona na sasa tunaenda kwenye utekelezaji. Ninatoa agizo kuwa mawaziri na manaibu wote wahame mara moja kutoka Dar es Salaam na kuja Dodoma. Wana ofisi ndogo Dodoma na kwa kuwa wamekuwa wakiishi wakati wote wa Bunge, wahamie mara moja. Mimi nahamia Septemba, na utekelezaji wake nitausimamia kwa juhudi zote,” alisisitiza.
Amewataka wakazi wa Dodoma watumie fursa hiyo kutunza amani ya nchi na kudumisha umoja uliopo na pia akataka watumie fursa hiyo kujenga nyumba za kuishi za kutosha, nyumba za kulala wageni na hoteli za kitalii ili watu watumishi na wageni wanapokuja wasipate taabu mahali pa kuishi.
Wakati huo huo, mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli katika muda wa siku tatu amerudia kusisitiza nia ya Serikali kuhamia  Dodoma katika kipindi chake cha uongozi ili kutekeleza ndoto ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kutaka makao makuu ya nchi yawe Dodoma.
Akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma kwenye uwanja wa mashujaa huku akishangiliwa, Rais Magufuli amesema atahakikisha Dodoma inakuwa makao makuu ndani ya miaka minne na miezi minne iliyobakia kwenye awamu ya kwnza ya uongozi wake.
“Kama wabunge karibu 300 na mawaziri na manaibu wao ambao hawafiki 30 wanakaa hapa kwa miezi mitatu na maisha yanakwenda, kama makao makuu ya chama kinachotawala nchi yako hapa sioni sababu ni kwa nini Serikali ninayoiongoza iendelee kubakia Dar es Salaam,” amesema.
Mara kwanza kutoa kauli hiyo, ilikuwa ni Jumamosi iliyopita, Julai 23, 2016 wakati akitoa hotuba yake ya kwanza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mkutano Mkuu maalum wa chama hicho.
Rais Magufuli amesisitiza wananchi na wanasiasa kutunza amani na kudumisha amani iliyokuwepo nchini. Pia amewataka Watanzania wote kuendelea kuwaenzi mashujaa walioipigania nchi hii.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,    
DODOMA.
JUMATATU, JULAI 25, 2016.

Saturday, July 23, 2016

MABONDIA IDD MKWELA KUPAMBANA NA MWITA MACHAGE KESHO JUMAPILI JULAI 24 TANDIKA

Bondia Idd Mkwela kushoto akiwa na Mwita Machage baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya julai 24 katika ukumbi wa musoma bar Tandika Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Idd Mkwela kushoto akiwa na Mwita Machage baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya julai 24 katika ukumbi wa musoma bar Tandika Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akiwa na mabondia wake Mohaed Kisua kg 51 iDDi Mkwela kg 61 Vicent Mbilinyi Kg 63 na Shabani Kaoneka Kg 72  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Idd Mkwela atapanda tena ulingoni kesho jumapili katika mpambano wake mwingine wa Kg 61 atakapo mkabili Mwita Machage katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika

akizungumza baada ya upimaji uzito na afya kwa mabondia watakaocheza siku hiyo 

Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' amesema kuwa mabondia wengine waliopima na watagombania ubingw wa taifa ni Imani Mapambano atakaezichapa na Selemani Galile raundi kumi za ubingwa

katika mapambano haya tumeamua kuchukuwa mabondia chipkizi kwa ajili ya kuendelea kuamasisha mchezo wa ngumi sehemu mbalimbali nchini

hususani katika ukanda uhu wa Temeke ambapo tumekuwa tukichezesha vijana wanao chipukia kila wakati

 Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

TIGO YATOA MSAADA WA MADAWATI WILAYANI URAMBO

Mkuu wa wilaya ya Urambo Bi,Angelina Kwingwa akikata utepe ishara ya kupokea msaada wa madawati Miamoja kutoka kampuni ya Tigo kanda ya ziwa.
Mkuu wa wilaya ya Urambo Bi,Angelina Kwingwa Akitoa hotuba kwa wananchi wakati wa makabidhiano ya madawati wilayani hapo
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Urambo pamoja na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Bw.Ally Maswanya wakiwa wameketi katika madawati yaliyotolewa na Tigo kusaidia Shule za Msingi wilaya ya Urambo.
Mkuu wa wilaya ya Urambo Bi.Angelina Kwingwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa wakiwa wameketi kwenye Madawati  pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Ukombozi wilayani Urambo.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ukombozi
Kutoka kulia Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Ally Maswanya akimkabidhi  dawati  moja kati ya Madawati  miambili  Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nzega JACKOB  MTALITINYA,Kulia katikati ni Mbunge wa Jimbo la Bukene Suleiman Zedi.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwangoye

Wednesday, July 20, 2016

KAMBI YA SUPER D COACH UHURU GYM KUSHILIKI BONANZA VINGUNGUTI JULAI 30

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mabondia watakaoshirika katika bonanza la michezo mbalimbali litakalofanyika Vingunguti kiembembuzi julai 30 kwa ajili ya kuamasisha mchezo uho Picha na SUPER D BOXING NEWS
 Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na mabondia Idd Mkwela kushoto na Vicent Mbiliyi wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya 'Super D Coach Uhuru GYM' Kariakoo shule ya Uhuru Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS

MABONDIA kutoka katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM , iliyopo kariakoo shule ya Uhuru Dar es salaam chini ya kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini julai 30 mwaka uhu mabondia wake watashiriki katika bonanza maalumu walilo alikwa kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi nchini

mabondia hawo watakaoshiliki ni Ibrahimu Class .Idd Mkwela, Vicent Mbilinyi, Fadhili Boika,Mohamed Kisua,Shabani Kaoneka, Gasper Mseveni ambao watacheza siku hiyo

Bonanza ilo lililo ratibiwa na mwenyekiti Moses Mwakibolwa pamoja na wajumbe wake Alli Bakari 'Champion' Spear Mbwembwe ambaye ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu

akizungmzia bonanza hilo mmoja ya wajumbe Alli Bakari amesema kuwa lengo la bonanza hilo ni kuwatoa vijana kwenye makundi ya vijiweni uharifu pamoja na utamiaji wa madawa ya kulevya

Bonanza hili lililopewa jina la 'Hapa Kazi 2016' litafanyika nchi nzima lakini kwa kuanzia wameanza na wilaya ya Ilala 

pia kufanikisha jambo hili wamejipanga kushirikiana na tasisi mbalimbali ikiwemo kupata ufadhili wa makampuni pamoja na bank mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha vijana wote wanakutanishwa katika michezo na kuelimishwa jinsi ya kufanya kazi

siku hiyo kutakuwa na michezo mbalimbali ikiwemo ndondi mpira wa miguu kuvuta kamba kukimbiza kuku kwa wazee mpira wa pete kwa wasichana dhuna draft na michezo yote kwa ujumla

pia kutakuwa na zawadi ndogo ndogo kwa washiriki watakaofanya vizuri siku hiyo