Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Dotto Texas katikati akiwainua mikono juu mabondia Jakobo Maganga kutoka Tanga kushoto na Abdalla Pazi 'Dulla Mbabe' wakati wa kutambulisha mpambano wao utakaofanyika julai 15 jijini Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS Na Mwandishi Wetu MABONDIA Abdallah Pazi 'Dulla Mbabe' wa Dar na Jakobo Maganga wa Tanga wamesaini kuzipiga julai 15 katika jiji la Dar es salaam Tanzania akizungumza baada ya kuwasainisha mabondia hawo Promota Dotto Texas amesema kuwa ana ongea na mabondia watakaocheza utangulizi siku hiyo kwa kuwa mchezo uho utakuwa wa kujua nanio zaidi katika uzito wa KG 76 hivyo wapenzi na mashabiki wakae mkao wa kula kwani mpambano huu ni wa kujua nani ni nani katika mchezo wa masumbwi nchini haidha promota huyo alieleza kuwa punde watawatangazia mashabiki kuwa wachezaji wengine walio ingia mikataba kwa ajili ya kucheza siku hiyo ni nani na nani ila nina wahakikishia mapambano yote yatakuwa bora zaidi kwani ngumi kwa sasa zina ushabiki mkubwa sana nae bondia Maganga kutota tanga alieleza kuwa ameanza mazoezi kwa ajili ya mpambano uho kwani Pazi ni mtoto mdogo katika masumbwi na bado ajakomaa katika ngumi hivyo asitarajie ushindi kabisa hapa ni kipigo tu akijibu mapigo Pazi alisema kwake yeye ngumi sio taarabu kwani mikono ndio inayofanya kazi ivyo ameomba mashabiki kuja kwa wingi na promota ataalishe machela kabisa siku ya mpambano |
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
No comments :
Post a Comment