TBL KUMLIPA DAVID MGWASSA BILIONI MOJA NDANI YA WIKI MBILI
David Mgwasa akizungumza na wahandishi wa Habari mara baada ya hukumu yake kutolewa |
Na Mwandishi Wetu
TUME Usuluhishi na Uamuzi (CMA) imetoa tuzo kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi Tanzania (TDL), David Mgwassa (pichani juu kulia) baada ya kulipwa dola za Kimarekani 200, 000 ndani ya siku 14 kuanzia leo kama gharama za usumbufu baada ya kuachishwa kazi isivyo halali na Kampuni ya Tanzania Brewaries (TBL).
Pia TBL inatakiwa kumlipa Mgwassa Sh.milioni 412 kama fidia ya kusitishwa kwa haki zake na pia ilipe mkopo wa gari lenye thamani ya Sh.milioni 94 ambalo lilikopwa na Mgwasa akiwa kazini.
Uamuzi huo umetolewa na Mwamuzi, Bw. Alfred Massay katika shauri la mgogoro wa kazi lenye kumbukumbu namba CMA/DSM/ILALA/R.49/16, ambapo Mgwassa alifungua madai mbalimbali dhidi ya TBL, Sabmiller Africa na Sabmiller PLC-London.
Mgwassa pamoja na mambo mengine mbali mbali, alikuwa akilalamikia kuachishwa kazi isivyo halali na kuomba alipwe mishahara ya miezi 36 kama fidia na pamoja na malipo ya bonasi kwa miezi mitatu ambayo ni sawa na zaidi ya Sh.milioni 261.5.
Mgwassa aliajiriwa na TBL kati ya Februari mwaka 1982 na Juni mwaka 2015 na katika kipindi cha kusitishwa kwa mkataba wake wa ajira alikuwa akiilipwa mshahara wa Sh. 17,191,451.88 kwa mwezi. Hata hivyo, ajira kati ya TBL na Mgwassa ilifikia mwisho Juni 25 mwaka 2015 baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya mkataba wa kustaafu mapema.
Baada ya uamuzi huo kutolewa,Mgwassa aliyekuwa akiwakilishwa na Wakili Alex Mshumbusi alisema ameridhishwa na uamuzi huo.David Mgwasa akizungumza na wahandishi wa Habari mara baada ya hukumu yake kutolewa hapo akiwaonesha nakala ya ukumu hiyo |
No comments :
Post a Comment