NGUMI KUPIGWA OCTOBAR 20 CCM MWIJUMA MWANANYAMALA
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA mbalimbali kutwangana Octoba 20 katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala wakiongwazwa na mpambano wa Issa Nampepeche atakaezipiga na Hashimu Chisora mpambano wa ubingwa raundi kumi
akizungumzia mpambano uho mratibu Ibrahimu Kamwe 'BigRaght' amesema kuwa siku hiyo ni kwa ajili ya burudani ya mchezo wa masumbwi kwani kutakuwa na mapambano mbalimbali ya kuvutia na mabondia wanaotamba katika vitongoji mbalimbali hivyo kama mpenzi wa mchezo wa masumbwi hii si yakukosa
kwani mbali na pambano hilo kuu kutakuwa na mpambano mwingine wa kukata na shoka kati ya Shabani Madilu atakaezipiga na Selemani Bangaiza na bondia machachari anaekuja kwa kasi ya ali ya juu Hamisi Maya atazipiga na Zumba Kukwe kutoka Kibaha Mkoa wa Pwani mpambano mwingine utawakutanisha Mbena Rajabu atakae oneshana umwamba na Fredy Masinde na Josephe Mbowe atazikunja na Mwinyi Mzengela siku hiyo mbali na mapambano hayo kutakuwa na mapambano mengine mbalimbali siku hiyo
aliongeza kwa kusema BigRight Sports and Arts Promotion imejizatiti kuinua vipaji vya mabondia chipkizi na kuwaendeleza wale walio katika chati ya juu kwa kuwandalia mapambano mbalimbali yakiwemo ya ubingwa wa taifa na yale ya ubingwa wa kimataifa
siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katika
mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchini kama vile Glove gumshirt clip bandeji bukta protecter na vifaa vingine
No comments :
Post a Comment