Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, November 15, 2018

PAUL KAMATA NA SELEMANI GALILE KUZICHAPA NOVEMBA 30 GONGOLAMBOTO


Na Mwandishi Wetu

Bondia Selemani Galile amesaini mkataba wa kuzipiga na Paul kamata Novemba 30 katika ukumbi waChampion Nifht Club uliopo Gongolamboto Dar es salaam

Mpambano uho wa kumaliza ubishi umeandaliwa na Rajabu Mhamila 'Super D' kutoka Super D Boxing Promotion kwa ajili ya kukuza na kuendeleza vipaji vya mabondia mbalimbali kutoka kila upande wa Tanzania

Mbali na pambano hilo kutakuwa na mapambano mengine ya kumaliza ubishi na kukata ngebe ya nani zaidi ya mwenzie ambapo bondia Mbwana Chinenda atazipiga na Nassoro Nyange wakati Selemani Bangaiza atazidunda na Mohamedi Mpombo Frank John atazichapa na Lumeme Hussein na Bakari Mbede ataoneshana kazi na Idd Mbaraka na Iddi Juma atazipiga na Ismahil Haridi

Wakati Abdallah Zamba ataoneshana kazi na Abasi Amza  Said Ndeki atazipiga na Rashidi Mnyagatwa Abdallah Luaga na Luqman Ramahani

Promota wa mpambano uho Super D aliongeza kwa kusema kuwa kutakuwa na burudani za aina yake pamoja na ngumi zitakazo burudisha zaidi

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd


Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini  'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchini kama vile Glove gumshirt clip bandeji bukta protecter na vifaa vingine

SUPER D COACH AMFUA MBWANA CHINENDA KWA AJILI YA KUZIPIGA NOVEMBA 30


Mbwana chinenda kg 57


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimwelekeza bondia Mbwana chinenda  jinsi ya kupiga ngumi iliyo nyooka 'Jab' wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kuzipiga na   Nassoro Nyange Novemba 30 katika ukumbi wa  ukumbi wa Champion Nifht Club uliopo Gongolamboto Dar es salaam Picha na Super D Boxing News


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimwelekeza bondia Mbwana chinenda  jinsi ya kupiga ngumi ya mkunjo wa chini 'Upcat'  wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kuzipiga na Nassoro Nyange   Novemba 30 katika ukumbi wa  ukumbi wa Champion Nifht Club uliopo Gongolamboto Dar es salaam Picha na Super D Boxing News

Wednesday, November 7, 2018

RAMADHANI SHAURI NA AZIZI ULIZA WASAINI KUZIPIGA DESEMBA 31




Mratibu wa mpambano wa masumbwi nchini Chaurembo Parasa Katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Azizi Uliza kushoto na Ramadhani Shauri baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Desemba 31 katika uwanja wa Kinesi uliopo Shekirango Picha na Super D Boxing News

Mabondia Azizi Uliza kushoto wakitazamana kwa usongo mara baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Desemba 31 katika uwanja wa Kinese Shekilango

Mratibu wa mpambano wa masumbwi nchini Chaurembo Parasa Katikati akiwa na mabondia Ramadhani Shauri kushoto na  Azizi Ulizabaada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Desemba 31 katika uwanja wa Kinesi uliopo Shekirango Picha na Super D Boxing News


Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Ramadhani Shauri na Azizi Uliza wame saini mkataba wa kuzipiga Desemba 31 katika uwanja wa Kinesi Dar es salaam uliopo maeneo ya Shekilango

akizungumza mratibu wa mpambano uho Chaurembo Palasa amesema kuwa wamejizatiti kuinuwa mabondi yeye na kampuni ya Ijuka Sports ambao wanajishughulisha na kuinuwa mchezo wa masumbwi nchini

aliongeza kwa kusema kuwa mabondia wengi wana ndoto ya kufika Marekani kucheza mchezo wa ngumi sasa kampuni hii imeanza na mapambano haya ili mradi mabondia wapate nafasi ya kupigana Marekani ambapo mchezo huu unakubalika kwa asilimia mia moja bila kupingwa mabondia watakaofanya vizuri watakwenda kupigana U.S.A

aliendelea kwa kusema siku hiyo mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka wakati Hussein Itaba atazipiga na Kanda Kabongo na Tonny Rashidi atazipiga na Nassoro Madimba kutoka Bagamoyo maeneo ya Kiwangwa na Rolen Japhert atazikunja na Mohamedi Kashinde 'Simba wa Mbagala' nae Baina Mazola ataoneshana umwamba na Faraji Sayuni

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd


Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchini kama vile Glove gumshirt clip bandeji bukta protecter na vifaa vingine