Na Mwandishi Wetu
Bondia Selemani Galile amesaini mkataba wa kuzipiga na Paul kamata Novemba 30 katika ukumbi waChampion Nifht Club uliopo Gongolamboto Dar es salaam
Mpambano uho wa kumaliza ubishi umeandaliwa na Rajabu Mhamila 'Super D' kutoka Super D Boxing Promotion kwa ajili ya kukuza na kuendeleza vipaji vya mabondia mbalimbali kutoka kila upande wa Tanzania
Mbali na pambano hilo kutakuwa na mapambano mengine ya kumaliza ubishi na kukata ngebe ya nani zaidi ya mwenzie ambapo bondia Mbwana Chinenda atazipiga na Nassoro Nyange wakati Selemani Bangaiza atazidunda na Mohamedi Mpombo Frank John atazichapa na Lumeme Hussein na Bakari Mbede ataoneshana kazi na Idd Mbaraka na Iddi Juma atazipiga na Ismahil Haridi
Wakati Abdallah Zamba ataoneshana kazi na Abasi Amza Said Ndeki atazipiga na Rashidi Mnyagatwa Abdallah Luaga na Luqman Ramahani
Promota wa mpambano uho Super D aliongeza kwa kusema kuwa kutakuwa na burudani za aina yake pamoja na ngumi zitakazo burudisha zaidi
siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katika
mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini 'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchini kama vile Glove gumshirt clip bandeji bukta protecter na vifaa vingine
No comments :
Post a Comment