NGUMI KUPIGWA IJUMAA OKTOBA 4 UKUMBI 361 MWENGE
Mabondia wa mgumi za kulipwa nchini walioibuka na ushindi wanatarajia kushiriki katika sherehe za kupongezwa na mashabiki wao Oktoba Nne Club 361Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi Mratibu mkuu wa Pambano la kuwapongeza mabondia hao Selemani Semunyu alisema mipango imekamilika ikiwemo mabondia watakaocheza ingawa maombi ni mengi ya mabondia wengi kutaka kushiriki kuonyesha furaha yao na kuwaunga mkono mabondia wenzao .
Aliwataja miongoni mwa mabingwa hao ni Abdalah Pazi ,Tonny Rashidi ,Bruno Vifua Viwili na Nassib Ramadhani kwa pamoja na bondia yeyote bingwa na wameletea taifa heshima kubwa wadau na mashabiki hakuna budi kuwapongeza.
" Serikali na Wabunge wamewapongeza lakini wadau na mashabiki sasa huu ndio wasaa wa kuwapongeza hata kama kuna zawadi ya kuwapa hii ndio sehemu moja lakini sie tunawapongeza kwa pambano" Alisema Semunyu.
Aliongeza kuwa pambano hili pia litatumika kupata mabondia watakaowania mikanda mwezi Desemba ambapo litafanyika pambano la funga mwaka.
" Watakaofanya vizuri katika pambano hili wataweza kupata nafasi katika pambano la mwezi wa 12 ambapo historia ya Ngumi nchini kwa kipindi cha hivi karibuni itawekwa " Alisema Semunyu.
Pia amewashukuru kamisheni ya ngumi za kulipwa kutoa kibali kwa wadhamini Smart Gin na kuomba wadhamini wengine kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha kurejesha hadhi ya mchezo wa ngumi nchini.
Kwa upande wake mratibu wa kiufundi wa mapambano hayo Yassin Abdalah Ustaadh aliwataja mabondia watakaosindikiza sherehe hiyo kuwa ni issa nampechehe (Dsm) vs alli hamisi (morogoro )
Ibrahim Makubi (Dsm)vs abdallah kingolwira ( morogoro )Maganga kulwa (mbagala) vs Said Sudi (M'nyamala) )Hashimu msungo vs Epson john Lewis Salumu omari vs ramadhani chicho
Aliongeza kuwa mapambano yanaweza kuongezeka kutokana na mabondia wengine kutafuta nafasi ya kutaka kushiriki Desemba lakini wengine nao wanataka kushiriki kuonesha furaha ya ushindi huo
No comments :
Post a Comment