Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, January 3, 2012

RAIS KIKWETE AOMBOLEZA VIFO VYA AZIZ SHEWEEN NA BALOZI ATHUMAN MHINA


Rais Jakaya Kikwete, akiweka sahihi kwenye kitabu cha maombolezo ya kifo cha Aziz Sheween, Mikocheni jijini Dar es salaam, Jumatatu jioni nyumbani kwa marehemu Ofisa huyo wa Mambo ya Nje Mkuu Daraja la kwanza katika Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, aliyefariki dunia huko Riyadh, Saudi Arabia.
Rais Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo alipofika Madale jijini Dar es salaam, jana Jumatatu jioni nyumbani kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Balozi Athumani Mhina aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana alipokuwa akipelekwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kutibiwa shinikizo la damu.
Rais Kikwete, akiagana na baadhi ya wanafamilia ya marehemu ya Aziz Sheween, baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu huyo Ofisa Mambo ya Nje Mkuu Daraja la I katika Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, aliyefairiki juzi huko Riyadh, Saudi Arabia.
Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuia ya Wazazi ya CCM,
Balozi Athumani Mhina enzi za uhai wake.


KATIBU Mkuu wa Jumuia hiyo, Khamis Dadi alisema Balozi Mhina alifariki usiku wa kuamkia jana aliokuwa akipelekwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kutibiwa shinikizo la damu.

Dadi alisema Mhina alikuwa akipelekwa hospitali baada ya hali yake kubadilika ghafla kutokana na maradhi ya shinikizo la damu.Alisema mwili wa marehemu, ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na kwamba mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho.


Dadi alisema marehemu atazikwa kijijini kwao Mnyuzi wilaya ya Korogwe mkoani Tanga na kwamba mwili wake utasafirishwa leo kwenda kijijini huko.Alisema kabla ya kusafirishwa, wakazi wa Dar es Salaam watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho nyumbani kwake Mada

Monday, January 2, 2012

KONYAGI watoa msaada kwa wahanga wa Mafuriko.Kikundi cha Konyagi Cocioty chaonyesha ukakamavu ktk kugawa misaada!!




Diwani wa Kata ya MKigogo Mr Chengura akipokea akikabvidhi msaada kwa Mwathilika wa Mafuriko yaliyo tokea jiojini Dar es salaam.Alifanya hivyo baada ya kupokea kutoka kwa Benadeta Daudi ambaye ni Mwakilishi wa Kampuni ya Konyagi kupitia kikundi cha uhamasishaji cha konyagi

Wana kikundi cha Konyagi Cocioty Hadikieleweke wakipiga picha na wahanga hao






Watoto walichangamkia mipira iliyo tolewa na Konyagi

Mtoto john akiogopa kamera yetu.naye ni sehemu ya waathilika wa Mafuliko

Diamond aswekwa rumande Iringa

MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul a.k.a Diamond na wacheza show wake wawili wamejikuta wakifunga mwaka vibaya baada ya kutupwa rumande kwa kosa la kumshambulia na kuharibu mali za mwandishi wa habari wa mkoani Iringa Francis Godwin.

Sakata la Diamond kumshambulia mwanahabari huyo maarufu hapa nchini lilitokana na hatua utata uliokuwa umejitokeza katia uwanja wa Samora mjini Iringa ambako Diamond alipaswa kufanya onyesho lake ya kuuanga na kuukaribisha mwaka 2012 .

Hata hivyo onyesho hilo lilionyesa kuwa na kila aina ya utapeli baada ya ratiba kuonyesha kuanza saa 8 mchana na kumalizika mida ya saa 12 za jioni na baada ya hapo uwanja huo ulipaswa kutumiwa na umoja wa Makanisa mkoani Iringa kwa ajili ya mkesha wa kufunga mwaka na mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma ndie alikuwa mgeni rasimi.

HIvyo kutokana na msanii huyo kushindwa kuonekana hadi mida ya saa 11.50 jioni mashabiki kiduchu ambao walikuwa wameingia katika uwanja huo walilazimika kumvaa mmoja kati ya wahusika katika onyesho hilo ambaye alikuwa akichukua fedha za kiingilio mlangoni na kuanza kuhoji sababu ya onyesho hilo kukwama na msanii Diamond na Afande Sele ambao walipaswa kupagawisha kutoonekana hadi mida hiyo na kuhoji sababu ya tiketi za chama cha soka mkoa wa Dar e s Salaam (DRFA) ambazo zinaonyesha kuna mchezo wa kirafiki kati ya Asante Kotoko ya Ghana na Marafiki wa Uhuru mchezo uliochezwa 12/11/2011 uwanja wa Taifa na kiingilia ni shilingi 5000 huku wao wamefika kuona wasanii na sio mechi.


Hata hivyo haikuchukua muda ghafla Costa ambayo ilikuwa imembeba Diamond na wacheza show wake bila Afande Sele iliwasili uwanjani hapo na kufanya mashabiki kupunguza jazba.


Kutokana na hali ya utulivu kurejea uwanjani hapo mwandishi wa habari huyo ambaye ni mmiliki wa blogu maarufu nchini ya www.francisgodwin.blogspot.com
na makampuni ya New Habari LTD alimfuata na kwa nia ya kutaka kufanya nae mahojiano na kujua sababu za kuchelewa katika show hiyo hapo ndipo Diamond alipogeuka mbogo na kupokonya kamera ya kuirusha chini baada ya kufuta picha .

Baada ya hapo mashabiki walimlazimisha Diamond kupanda jukwaani kuimba vinginevyo wangemchapa hivyo kulazimika kupanda jukwaani huku akisimamiwa kwa bakora na mawe ,pamoja na kupanda jukwaani bado alishindwa kuimba baada ya wale waliokodisha vifaa vya muziki kugoma kupiga muziki kwa madai muda wao umekwisha huku watu wa mkesha wa makanisa nao wakipinga jukwaa la ibada ya mkesha kutumika kwa mambo ya kidunia hali iliyozua utata .


Hali hiyo ilimfanya Diamond kuchanganyikiwa zaidi na kushindwa kushuka jukwaani kwa kuhofia kichapo toka kwa mashabiki kutokana na hali hiyo mwandishi alianza kufanya mahojiano na kuchukua picha za mashabiki kusubiri na kumsimamia msanii huyo kabla ya kuruka jukwaani na kikosi chake na kuanza kumchapa mwandishi huyo ambaye pia alionyesha kukabiliana nao kwa kiasi na kusaidiwa na mashabiki .

Kutokana na tukio hilo mwandishi huyo wa habari Godwin alipoteza camera yake yenye thamani ya shilingi milioni 1.5, simu moja yenye thamani ya shilingi 300,000 huku Laptop yake ndogo aina ya Acer ikiharibiwa na msanii huyo.


Tukio hilo lilifikishwa polisi na Diamond kufunguliwa mashtaka ya kushambulia kwa RB namba IR/RB/ 7700/2011 na baada ya muda mida ya saa 1.30 usiku jeshi la polisi lilikwenda kumkamata msanii huyo na vijana wake wawili ambao walikuwa katika Hotel ya Staff Inn Anex mjini hapa wakijipumzisha na kupelekwa mahabusu hadi asubuhi .


Mratibu wa show hiyo Mike T akiomba msamaha kwa mwandishi huyo alisema kuwa msafara wa Diamond ulikuwa ukitokea Mbeya katika uwanja wa Sokoine ambako pia Show ilikwama kutokana na mvua kubwa kunyesha na baada ya hapo walianza safari kwa ajili ya kuja Iringa na kukwama kufika kwa wakati kutokana na basi lao la kwanza kuharibika na kulazimika kukodi Costa na kufika kwa mida mibaya Iringa na kuwa baada ya Iringa Msafara huo ulitaraji kwenda jijini Dar es Salaam kuzindua Albam yake .

SIMU YA MCHINA YAMLIPUKIA NA KUMUUNGUZA HAULE



Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe (kulia) akimjulia hali mfanyabiashara wa mafuta katika Kijiji cha Luilo Ludewa, Joseph Haule ambaye amelipuliwa na mafuta baada ya simu yake ya kichina kulipuka,majeruhi huyo anatibiwa katika Hospital ya Wilaya ya Ludewa, mkoani Iringa. (PICHA ZOTE NA FRANCIS GODWIN)
Filikunjombe na baadhi ya wananchi wakimjulia hali Joseph Haule
Joseph Haule akiwa amelazwa Hospitali

MDAU WA WWW.ELIMUBORA.COM AMALIZA KOZI YA WEB DESIGN



Evance ambae anaratibu website ya www.elimubora.com akiwa anapokea cheti baada ya kuhitimu kozi fupi nchini India. Amewataka watanzania hususan wadau wa masuala ya IT kufuatilia udhamini mbalimbali wa kozi fupi utolewao na chuo hicho kwa taarifa zaidi ingia katika libeneke lake la www.elimubora.com

RAIS JAKAYA AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU WAWILI NA NAIBU KATIBU MKUU MMOJA IKULU DAR LEO



Rais Jakaya Kikwete aklimwapisha Mh Eliakim C. Maswi kuwa Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini katika hafla iliyofanyika Iukulu leo jijini Dar es salaam. (PICHA NA IKULU) Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akimpongeza na kumkabidhi zawadi ya ua Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliackim Chacha, baada ya kuapishwa leo Ikulu Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Paul, Katibu Mkuu Ikulu, Peter Alanambula Ilomo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliackim Chacha, kabla ya kuapishwa wakati Makamu akiingia katika Ukumbi huo kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa makatibu hao walipokuwa wakisubiri kuapishwa rasmi kushika nafasi hizo Ikulu Dar es Salaam leo Januari 2, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima, Katibu Mkuu wa wizara hiyo aliyeapishwa leo Januari 2, 2012, Ikulu Dar es Salaam pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kuapishwa Katibu huyo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Rais Jakaya kikwete akimwapisha Mh Peter Ilomo kuwa Katibu Mkuu Ikulu PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mh Suzana Mlawi PICHA NA IKULU
Rais Dk. Jakaya Kikwete wa pili wa tatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa rais Dk. Gharib Bilal wa pili kutoka kushoto na makatibu walioapishwa leo kutoka kulia ni Mh Peter Ilomo Katibu Mkuu Ikulu, Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mh Suzana Mlawi,Balozi Ombeni Sefue katibu mkuu kiongozi na mwisho kushoto ni Mh Eliakim C. Maswi Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini PICHA NA IKULU

Sunday, January 1, 2012

MATUMLA AMGALAGAZA CHEKA KWA POINTI


Bondia Cosmas Cheka na Mohamed Matumla wakioneshana ufundi wa kurusha masumbwi wakati wa mchezo wao uliofanyika uwanja wa Jamuhuri Morogoro juna Matumla walishinda kwa pointi.

Bondia wa kike Asha Nzoa akishangilia baada ya kutangaza msindi kwa kumtwanga mpinzani wake Slma Kihobwa katika mpambano wa utangulizi kabla ya Mohamedi Matumla na Cosmas cheka awajapanda ulingoni jana katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro
Asha Nzoa kushoto akioneshana ufundi wa kutupa masumbwei na Salma Kihobwa
kutoka kushoto ni Rashid Matumla,Mohamedi Matumla,Mbwana Matumla na Mkwanda Matumla
Mohamed Matumla

Mohamed Matumla Kuichoto na Cosmas Cheka wakioneshana uwezo wa kutupa Masumbwi jana
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akikingiana ngumi na Rais Wa PST Emanuel Mlundwa kabla ya kuanza kwa mpambano jana
Bondia Rashid Matumla (kushoto) akimpa mawaidha mwanae wa kwanza Mohamed Matumla wakati wa mpambano wake na Cosmas Cheka kulia ni Mbwana Matumla akimkandakata
Mbwana Matumla kulia akimganga bondia Mohamedi Matumla wakati wa Mpambano wake na Cosimas Cheka Mohamedi alishinda kwa point

Bondia mohamedi Matuimla akishangilia ushindi baada ya kutangazwa kumchapa Cosmas Cheka
Bondia Cosmas Cheka na Mohamed Matumla wakioneshana ufundi wa kurusha masumbwi wakati wa mchezo wao uliofanyika uwanja wa Jamuhili Morogoro juzi Matumla walishinda kwa pointi.

UZINDUZI WA KIWANJA KIPYA CHA DAR LIVE

Kiwanja kipya cha michezo mbalimbali ya watoto kinachojulikana kama Dar Live kimezinduliwa leo huko Mbagala Zakhem jijini Dar es salaam , kiwanja hiki ni moja ya viwanja vizuri vinavyolifanya jiji la Dar es salaam kuwa na burudani katika maeneo mbalimbali hivyo kupunguza adha ya wakazi wa maeneo husika, kufuata burudani mbali kama ilivyokuwa mwanzo ambapo walikuwa wakienda Kunduchi Wet in Wild, South Beach Kigamboni au Beach Comber, jambo lililokuwa linawapa wakati mgumu kidogo watu wanaoishi maeneo ya Mbagala na Temeke kwa ujumla wake lakini sasa wamepata kiwanja cha kupeleka watoto kucheza. Katika kiwanja hicho pia kuna ukumbi wa Burudani na jukwaa kubwa la kisasa kabisa ambapo leo katika kuzindua kutakuwa na burudani kutoka kwa Juma Nature, Mh. Temba, Ali Choki na Extra Bongo pamoja na kundi zima la muziki wa Taarab la Jahazi Morden Taarab. Mimi leo nilijimuvuzisha na warembo wangu wapendwa Ivon kulia na Diana ili nao wajisikie kidogo katika siku hii ya kusherehekea mwaka mpya wa 2012, lakini mama Mkurugenzi yeye amesema ngoja apumzike baada ya kujumuika na wezake katika mkesha wa kuombea taifa kwenye uwanja wa Taifa usiku wa kuamkia leo hivyo tukasema sawa mama mkurugenzi pumzika.
Hapa ni vifaa mbalimbali vya michezo ya watoto vilivyopo katika kiwanja hicho cha Dar Live.
Hii ni moja wa toi la ndege ambalo watoto wamekuwa waakipenda kucheza humo pia katika kiwanja hicho.
Watu mbalimbali wakipumzika na kupata kinywaji na chakula katika kiwanja hicho.
Watoto wakicheza
Watoto wakicheza katika bembea.
Watu wakipishana kuingia na kutoka ni wazi kwamba watu wengi watafika ili kujionea mambo mbalimbali hapo Dar Live leo.
Picha za wasanii mbalimbali zimepambwa katika kuta za Dar Live yote hii ni kupendezesha kiwanja hicho.

Saturday, December 31, 2011

WACHEZAJI WATIMU YA TAIFA YA NDONDI WAILOTEULIWA KUSHIRIKI KINYANGA"NYIRO CHA KUTAFUTA NAMBA YA KUSHIRIKI OLIMPIKI 2012

Kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila Super D akiwa na vifaa vya mchezo huo
Moja ya kambi za mazoezi ya mchezo wa ngumi
KOcha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila Super D akiwa na vifaa vya mchezo huo


Vijana chipukizi wakijifua katika kambi ya mazoezi ya ngumi
Kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila Super D akiwa na vifaa vya ngumi

Kocha Kondo nassoro akimwelekeza bondia chipukizi Zainabu Mhamila (Ikota) huku nyuma akielekezwa jinsi ya kutembea na kocha Habibu Kinyogoli wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala Dar es Salaam



MAJINA YA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA NGUMI WALIOTEULIWA KWA AJIL YA MAANDALIZI YA MASHINDANO YA KUFUZU KWENDA KUWAKILISHA TAIFA KATIKA MASHINDANO YA OLMPIKI LONDON UINGEREZA Julai 2012.


KUTOKA NGOME BOXING TIMU:
1. .SELEMAN KIDUNDA.
2. PETER STANLEY
3. .MORIS MHINA
4. 3.KILLER MOHAMED
5. .ABDALAH KASSIM
6. SUNDAY ELIAS
7. DENIS MARTINE
8. ABDALAH KITENGE
9. HUSSEIN MNIMBO
10. HARUNA SWANGA
11. SAID PUME
12. HASHIM SAIMON
13. RAJABU MADINDA
14. ABDALAH SHABANI
15. ABDU RASHID
16. FRANK NICOLOUS
KUTOKA MMJKT BOXING TIMU:

1. EMILLIAN PATRICK

2. MAXIMILIAN PATRICK
3. ISSA ABDALAH KOBA
4. HAMDAN ISSA
5. SAID HOFU
6. KASSIM HUSSEN
7. BONIFACE MLINGWA
8. DOGO MUSSA
9. GRORGE COSTANTINO
10. JOHN CHRISTIAN
11. VICTOR NJAITI
12. ISMAIL ISACK
13. ELIAS MKOMO
14. WAMBURA AMIRI
KUTOKA MAGEREZA BOXING TIMU:
1. UNDULE LANG"SON

2. NURU IBRAHIM
3. SELEMAN BAMTULA
4. MICHAEL PASCHAL
5. SHABAN ALLY
6. MUSIN KIMWAGA
7. OSWARD CHAULA
8. ANTON IDOA
9. LUSAJO MWAIPOPO
10. MOHAMED CHIBUMBUI
KUTOKA SIFA BOXING TIMU
1. IDDI PIALALI

2. ANCE JOHN
3. SHABAN MAFIGA
4. DOTO SHOKA
KUTOKA POLISI BOXING TIMU
1. YAHAYA MALIKI
KUTOKA URAFIKI BOXING TIMU:
1. FADHIR HASSAN

KUTOKA TEMEKE BOXING TIMU:
1. EDWARD ASAJILE

2. ABDALAH MFAUME
KUTOKA NYAMBELE BOXING TIMU (DODOMA)
1. ANTONY NYAMBELE

KUTOKA MTONI BOXING TIMU
1. CHUKI MOHAMED

NB: MAZOEZI KWA WACHEZAJI 51 WALIOTEULIWA YATAANZA MARA TU BAADA YA KURIPOTI BFT NA KUPANGIWA KITUO CHA KUFANYIA MAZOEZI KATI YA VITUO TULIVYOANISHA VYA UWANJA WA NDANI WA TAIFA,MAGEREZA UKONGA, MGULANI JKT,NGOME,NA URAFIKI.
MWISHONI MWA Januari 2012 KUTAFANYIKA MASHINDANO MAALUM YA MCHUJO KWA HAO WACHEZAJI WALIOTEULIWA ILI KUPATA WACHEZAJI 20.

15-22/2/2012 TIMU HII ITASHIRIKI MASHINDANO YA TAIFA YATAKAYOSHIRIKISHA MIKOA YOTE YA TANZANIA BARA KWA LENGO LA KUSHIRIKISHA MIKOA YOTE ILI TUPATE WAWAKILISHI WA SURA YA KITAIFA.

BAADA YA MCHAKATO HUO NA KURIDHIKA NA WACHEZAJI WALIOFIKIA VIWANGO WATAINGIA KAMBINI KWA AJILI YA MAZOEZI KABAMBE YA MWISHO IKIWA PAMOJA NA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MAJARIBIO YA KIMATAIFA KABLA YA KWENDA CASABLANCA MOROCCO KATIKA MASHINDANO YA KUFUZU KWENDA KATIKA MASHINDANO YA OLIMPIKI.MASHINDANO YA KUFUZU MOROCCO YATAFANYIA KUANZIA TAREHE 27/4-6/5/2012.NA KATIKA MASHINDANO TUNATEGEMEA KUPELEKA WACHEZAJI 10 WA UZITO WA KUANZIA FLY WEIGHT HADI SUPER HEAVY WEIGHT


MAKORE MASHAGA

KATIBU MKUU(BFT)

Mob: +255 713 588818

Email: mashagam@yahoo.com