Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, August 2, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUTURISHA MIGOMBANI UNGUJA




 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa dini ya Kiislam, katika swala ya Magharibi wakati alipojumuika na waumini hao katika Futari ya pamoja aliyowaandalia na kufuturu nao Migombani Unguja mjini Zanzibar jana.
 Wake wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal (wa pili kulia) na Mama Asha Bilal (katikati) wakijumuika na waumini wa dini ya Kiislam, wakati wa futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kwa waumini hao iliyofanyika Migombani Unguja, mjini Zanzibar jana. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislam, baada ya kufuturu nao futari ya pamoja aliyowaandalia Migombani Unguja mjini Zanzibar jana.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislam, baada ya kufuturu nao futari ya pamoja aliyowaandalia Migombani Unguja mjini Zanzibar jana.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akipiga picha ya pamoja na baadhi ya kinamama, baada ya kushiriki nao katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, iliyofanyika jana Migombani Unguja mjini Zanzibar.

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, akipiga picha ya pamoja na baadhi ya kinamama, baada ya kushiriki nao katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, iliyofanyika jana Migombani Unguja mjini Zanzibar.

BANDI YA MUZIKI YA K-MONDO OUND YARUDI KWENYE ANGA ZA BURUDANI MASHABIKI MKAO WA KULA.




Wanamuziki wa bendi ya K-mondo Sound,wakiburudisha jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuitambulisha bendi hiyo mbele ya waandishi wa habari, huku ikiwa na ujio mpya na ladha mpya za burudani kwa wapenzi wa muziki wa Dansi nchini.
Hivi ni vionjo kwa uchache tu.

DAR ES SALAAM THIS MORNING WITH EPIQ BONGO STAR SERCH.



Majaji wa Shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Epiq Bongo Star Serch linaloondelea kwenye vianja vya Coco Beach wakihakikisha kila kitu kinakwenda sawa kuchukua taarifa sahihi za washiriki hao.
Washiri hao wakiimba pamoja kabla yakwenda kuwaona majaji.
Vyomba vya asili kama kawaida navyo vipo kwenye mchuano huo mshiriki pichani akipiga gitaa la asili.

Wednesday, August 1, 2012

TIGO YAZINDUA PROGRAMU YA MAJARIBIO YA 'TIGO KILIMO'




Taarifa kwa vyombo vya Habari

Tigo yazindua suluhu kwa wakulima kupitia mtandau wa simu za mikononi

Agosti 1, 2012, Dodoma. Tigo leo imetangaza uzinduzi wa programu ya majaribio inayojulikana kama ‘Tigo Kilimo’ ambayo inakusudia kuwapatia wakulima taarifa  stahiki kwa wakati muafaka za kilimo kupitia simu zao za mikononi.

Tigo Kilimo inatumia teknolojia ya ujumbe wa maadishi ( sms) ambayo itawapatia wakulima wadogo wadogo fursa ya kipekee kuboresha shughuli zao. Kupitia Tigo Kilimo wakulima watapata taarifa za hapo kwa hapo kuhusu hali ya hewa na taarifa nyinginezo  za kilimo. Hii itawasaidia kuongeza mavuno na kupunuguza utofauti ya mavuno  na sehemu nyingine za ulimwengu.

“Kwa kutumia  mtando wa simu za mikononi kuleta suluhu kwenye maswala ya  Kilimo wakulima wataunganishwa kwa ukaribu zaidi na italeta ufanisi zaidi katika shughuli za kilimo ,” alisema Yaha Ndojore , Meneja Mradi wa huduma za Tigo Kilimo , Tigo Tanzania .  “Kutokana na miundombinu na mawailiano hafifu kwenye sehemu kubwa za nchi zinazoendelea , wakulima wanataabika kupata taarifa muhimu za kilimo , pamoja na mafunzo na ushauri kuhusu maswala kama wadudu na magonjwa , hali ya hewa na mbinu tofauti za kilimo . Kupitia huduma hii , Tigo itatoa fursa ya suluhu mpya na  nafuu  yakusaidia hizi changamoto.” Alisema

Kama mdhamini mkuu wa mawasiliano ya maonyesho ya Nane Nane na kusheherekea  Wiki ya Maonyesho ya Kilimo,Tigo inawapatia wakulima mawasiliano ya Tigo Kilimo bure kwa mwezi mzima wa Ogasti.Wakulima wanaweza kupata huduma hii kupitia simu zao za mikononi kwa kupiga  *148*14# na kupata listi ya huduma za Tigo Kilimo. Hapa watapata lisiti ya taarifa mbali mbali kwa ujumla kuhusu hali ya hewa , udani wa menjimenti wa udongo , njia ya kudhibiti wadudu kwa zaidi ya aina 20 za mboga , matunda na nafaka , taarifa kuhusu utunzaji wa mifugo nk. Kwenye awamu ya pili ya huu mradi Tigo itaongeza huduma kama vile bei ya bidhaa sokoni, na kuanzisha huduma kwa wateja wakulima, ambao wataweza kupiga wakiwa na maswali mbali mbali 

Simu za mikononi zinarahisisha mawasilano. Tigo inaweza kuwafikia wakulima viijini na taarifa muhimu kupita huduma hii. Kwa kupitia Tigo Kilimo , wakulima wanapata ujuzi wa kuboresha kazi na stadi zao ambazo zitasaida kuongeza mazao , kupunguza gharama na kuongeza kipato, na wakati  huo huo kupata faidia kwa kutumia simu za mikononi.


KuhusuTigo

Tigo ilianza biashara 1994 kama mtandao wa kwanza wa simu za mkononi Tanzania. Sasa inapatikana katika mikoa yote 26 tanzania Bara na Zanzibar. Tigo imejitahidi kuwa na ubunifu katika uendeshwaji wa huduma zake za simu nchini Tanzania kwa kutoa huduma zenye gharama nafuu katika mawasiliano  mpaka katika kutoa huduma za intanet zenye kasi na huduma za fedha kwa njia ya simu kupitia  Tigo Pesa.

Tigo ni sehemu ya Millicom International Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz

SIMBA WAANZA MAZOEZI KUJIANDAA NA LIGI KUU


 Wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam kwa ajili ya  kujianda na Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara inayoyarajiwa kuanza mwezi Septemba.

KUTOKA KWA MDAU ABDALLAH MRISHO - VODACOM MMEKOSEA KATIKA HILI



Mmoja wa washindi wa tuzo hizo, Masoud Kipanya (kulia), akipokea zawadi zake kutoka kwa Kelvin Twisa, huku akishuhudiwa na mmoja wa wasimamizi wa zoezi hilo kutoka Vodacom.
Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Vodacom kwa kuja na wazo zuri la kutambua michango na umuhimu wa mitandao ya kijamii, hususan blogs na web site na kuamua kuwatunuku.

Pamoja na pongezi hizo, lakini mmekosea katika utekelezaji wake. Kwa mtizamo wa wahusika wengi (Blogers), tuzo mlizotoa baadhi zimeenda kwa wasiostahili na mmeacha wengi waliostahili kupata tuzo hizo.

Ingawa hamkuweka wazi vigezo vyote, lakini baadhi ya mlivyovitaja ni pamoja na blog kuwa inayofanyakazi (active), ambayo inaweka habari mpya kila siku, iwe inayoandika vitu halisi na siyo vya kukopi au kutafsiri kutoka BBC na mitandao mingine ya Kiingereza na kupesti.

Hali kadhalika mkasema kuwa web site au blog hiyo inachokiandika kiwe kimeandikwa na mtu mwenye ujuzi nacho, mkatoa na mfano kuwa kama ni mapishi, basi yaandikwe na mtu mwenye kujua mapishi. Pia mtandao huo uwe maarufu.

Bila shaka kwenye ulimwengu wa mitandao, unaposema mtandao fulani ni maarufu, ina maana unatembelewa na visitors wengi kwa siku, mtandao hauwezi kuwa maarufu kisha ukawa na visitors 500 au 800 tu kwa siku.

Bloggers maarufu nchini wanajuana na wanahesabika, inakuwa kichekesho inapokuja kutangazwa blog fulani ndiyo maarufu wakati haijulikani hata miongoini mwa bloggers wenyewe, achilia mbali wasomaji wengine.


Hawa ndiyo washindi wenyewe:
  1. Mikocheni Report,
  2. Issa Michuzi
  3. Wanamuziki Tanzania.
  4. Kipanya.co.tz
  5. Vijana FM
  6. Millardayo.com
  7. Taste of Tanzania
  8. Jamii Forums
  9. Mambo Magazine
  10. DJ Fetty Blog
Kwa mtizamo wa wengi, katika orodha hiyo ya watu kumi, ni wanne tu ndiyo walistahili na waliobaki hawakustahili kabisa, kwa sababu licha ya kuwa hawajulikani sana, lakini pia huoni hata namna ambavyo Vodacom, kama kampuni, inaweza kunufaika nao iwapo mtaamua kujitangaza kupitia kwao.

Kuna Bloggers wameachwa ambao wao ku blog ndiyo maisha yao, wanalala, wanaamka, wanatembea, wanakula, wanakunywa, wanakaa wana blog tu. Wao na Blog, Blog na wao. Hakuna taarifa, breaking news au picha za matukio yote muhimu zinazowapita hapa nchini na hata katika kuripoti matukio ya promosheni ya Vodacom kwenye mitandao yao wako mstari wa mbele. Wengine kazi yao ni kukopi na kupesti kazi za wengine!

Pengine hatuyajui malengo ya Vodacom, kwa sababu kama kweli mnanataka kuthamini michango ya 'social media' na wao kunufaika na media hizo, basi mmekosea katika hili.

Waulizeni mliowatuma, wamefanya research ya kutosha na kuona hao washindi wana visitors wangapi na pageviews ngapi kwa siku? Je, Google Analytics Report zao zinaoneshaje? Na, je, habari na picha wanazoziweka kwenye mitandao yao, kweli ni za kwao, au wamekopi na kupesti tu kutoka kwingine?

Naomba mliopewa kazi ya kuandaa tuzo hizi myachukue haya kama changamoto na kuyafanyia kazi ili msiharibu kazi nzuri inayofanywa na Vodacom nchini Tanzania na wala hatuyasemi haya kwa sababu ya chuki binafsi, bali kwa ukweli na uwazi tu!


Wassalaam!

Global Publisherstz.com
"Great achievement, involves great risks"
Abdallah Mrisho
The General Manager
Global Publishers&General Enterprises Ltd
"The House Of Favorite Newspapers"
P. O. Box 7534, Dar es salaam
Tel: +255 22 2773356-7
Mobile: +255 754 290167, 0784 888982
Web Site: www.globalpublisherstz.com
www.abdallahmrisho.blogspot.com
You might also like:

DAWA MPYA YA UKIMWI YAANZA KAZI




Hamida Hassan na mitandao ya kijamii


DAWA mpya inayokinga na kuua kwa kasi virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi, tayari imeshaanza kutumika, hii ni kwa mujibu wa ripoti za mitandaoni.
Dawa hiyo ambayo toleo lake la kwanza ipo kwenye muundo wa vidonge, inaitwa Truvada na tayari imekwishaanza kufanya kazi nchini Marekani.
Kitendo cha Truvada kukubalika na Mamlaka ya Usimamizi wa Chakula na Dawa nchini Marekani (FDA), kinatoa picha kuwa sasa vidonge hivyo vinaweza kuuzwa sehemu yoyote duniani.
Kamishna wa FDA, Margaret Hamburg, amesifu Truvada na kueleza kwamba itapunguza wastani wa maambukizi mapya pamoja na vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Hamburg alisema kuwa hivi sasa nchini Marekani kumekuwa na kasi ya maambukizi mapya, kwani kila mwaka kumekuwa na wastani wa watu 50,000 wanaobainika kupata Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Watafiti waliogundua Truvada wanaeleza kuwa dawa hiyo kwa sehemu kubwa inakinga VVU na upande mwingine inasaidia kuua virusi vya Ukimwi kwa mtu ambaye tayari amekwishaathirika.
Hata hivyo, FDA na watafiti hao, hawajaeleza kama Truvada inatibu moja kwa moja, isipokuwa wanasisitiza: “Inamkinga mtu kupata maambukizi mapya, inamsaidia mwathirika kwa kuua VVU pamoja na kumkinga dhidi ya magonjwa nyemelezi.”

GARI MOSHI LAWAKA MOTO INCHINI INDIA HUKU WATU ZAIDI YA 30 WAKIUAWA



Treni ikiteketea kwa moto wakati juhudu za uokozi zikiendelea

 WATU zaidi ya 30 wameuawa Kusini mwa India katika mji wa Chennai kwa kuteketea kwa moto baada ya gari moshi walilokuwa wanasafiria kuwaka moto Julai 30, 2012. 

Mkasa huo umetokea Jumatatu asubuhi wakati gari moshi hilo lilipokuwa linatokea mjini New Delhi na kusababisha abiria wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.

Maafisa wa uokoaji kwa sasa wanaendelea na shughuli za kuwatafuta watu zaidi ambao huenda wamekwama ndani ya gari moshi hilo huku idadi ya wafu ikitarajiwa kuongezeka.

Walioshuhudia mkasa huo wanasema, waliona gari moshi hilo likiwaka moto likiwa safarini, mkasa ambao umeleta kumbukumbuku ya ajali nyingine ya gari moshi iliyotokea mwezi Mei mwaka huu baada ya magari Moshi kugongana na kusababisha zaidi ya watu 20 kuuawa.

Taasisi inayoshughulika na maswala ya ajali za terni nchini humo inasema kuwa tangu mwaka 2009,  watu 25,705 wameuawa kutokana na ajali za gari moshi.

Ajali mbaya zaidi ya gari moshi iliyowahi kuikumba nchi hiyo ilikuwa mwaka 1981 ambapo watu 800 waliuawa baada ya gari moshi la abiria kuzama katika mto katika jimbo la Bihar.

Serikali ya India inasema iko katika harakati za kuimarisha sekta ya safari za reli kwa kuimarisha usalama wa magari moshi.

Assah Mwambene Mkurugenzi Mpya wa Idara ya Habari - MAELEZO



Bw. Asah Andrew Mwambene ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuanzia tarehe 01 Julai, 2012. Bw. Mwambene anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Clement Mshana ambaye mwaka jana aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Bw. Mwambene (41) kabla ya uteuzi huu alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Aidha, Bw. Mwambene amewahi kufanya kazi katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) akiwa mwakilishi wa Kampuni hiyo huko Zanzibar.

Idara ya Habari (MAELEZO) ndiyo Msemaji Mkuu wa Serikali hapa nchini.


IMETOLEWA NA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI
NA MICHEZO

AGOSTI 1, 2012

Mzee Mwinyi kuongoza harambee ya Islamic Help ya kuchangia yatima wa Kisemvule Agosti 03, Serena Hotel



Afisa Programu wa Asasi ya Islamic Help, Adam Rajab (wa pili kushoto), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu hafla ya Futari na chakula cha usiku iliyoandaliwa na Asasi hiyo Ijumaa Agosti 3.2012 katika Hoteli ya Serena, kwa ajili ya kuchangisha fedha za ujenzi wa nyumba katika kijiji cha watoto yatima 'Childrens Eco Village' huko Kisemvule ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Kushoto ni Afisa Utawala wa Islamic Help, Saamia Shikely (Kutoka wa tatu kushoto) ni; Meneja wa Islamic Help Tanzania, Ishak Muhsin, Mwanachama Mshauri wa Bodi, Salehe Ally na Mkurugenzi wa Vision Investment, Ally Nchahaga. Picha na Daily Mitikasi Blog
******************
Nasaidia ili kuleta mabadiliko'  ‘ unasikika mwito wa kushiriki katika futari na chakula cha jioni kilichoandaliwa na Asasi ya  Islamic Help Tanzania ili kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wa  ‘ Children’s eco village’ huko Kisemvule, Dar es salaam.
Hafla hiyo itafanyika tarehe 3 Agosti  2012 kuanzia saa 12.00 jioni katika Hoteli ya Serena jijini  Dar es Salaam. Rais mstaafu Mheshimiwa  Ali Hassan Mwinyi, atakuwa mgeni rasmi ambapo Kiasi cha zaidi ya wageni 400, wakiwemo wahisani na wakereketwa wengine wanatarajiwa kuhudhuria katika hafla hiyo .
Makazi ya watoto ya The Children’s Eco village yana jumla ya nyumba  16 kwa ajili ya watoto yatima  160.

Makazi hayo yako katika eneo la ekari 30 lenye uoto mwanana wa kijani na hali nzuri ya tabia nchi Ni katika eneo hilo la kuvutia ndiko ambako mradi unatarajia kujenga makazi rafiki kimazingira yaliyosheheni vionjo vyote vya vivutio vya kisasa.

Ujenzi  unakusudiwa kuzingatia kwa kiwango cha hali ya juu matumizi madogo ya nishati pamoja na ya ardhi . Aidha mradi unatarajiwa kutumia teknolojia ya nishati rafiki kwa mazingira, mbinu nzuri za usimamizi wa utupaji taka, na teknolojia ya urejelezaji.

Matumizi ya ardhi yaliyo rafiki kwa mazingira pamoja na yabiogesi yatakuwa ni uhakikisho wa  kuweko  kwa mazingira salama na yenye tija kwa shughuli za uzalishaji.

 Kituo cha mafunzo pamoja na shamba vitaanzishwa  kwa awamu kama shughuli za kuingiza kipato kwa kijiji cha makazi ya watoto  pamoja na kuwa  mfano wa ujenzi wa maendeleo ya jamii na wa uwezo  kwa vijiji vya jirani.

Islamic Help
Islamic Help ni Asasi ya misaada  isiyo ya kiserikali (ASIZE) iliyoandikishwa huko  UK . Asasi hii imekuwa ikitoa misaada mbalimbali ya kiutu kwa zaidi ya nchi ishirini. Kama shirika la maendeleo linaloinukia, hivi karibuni tulishinda  tuzo ya  Oscar ya filamu fupi bora iliyojulikana kama ‘ Saving face’ on Acid burn victims. Tumekuwa tukifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 2008 , hasahasa tumekuwa katika kisiwa cha  Mafia  tukijihusisha na  programu ya ukusanyaji fedha kwa  kujitolea, uhamasishaji na ufikiaji.

Progarmu hiyo ambayo imekuwa ikifahamika kama  ‘ Mission to Mafia’ imefanikiwa kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 600 kutoka kwa zaidi ya vijana  55 wa UK na kutekeleza miradi  ya maji, afya, malezi ya yatima na shughuli nyingine. Aidha tangu tufungue ofisi zetu jijini Dar es Salaam tumefanikiwa kutekeleza miradi iliyogharibu zaidi ya shilingi milioni 950.
 
Kwa taarifa zaidi kuhusu  Islamic Help na mradi yake, tafadhali tembelea tovuti yetu ifuatayo www.islamichelp.co.tz au piga simu Namba 0787 487333, kwa Afisa mawasilino wetu  Nadhir Bahyan  au tuma baura pepe kwa anuani: nadhir@islamichelp.co.tz 

EPIQ BONGO STAR SERCH NDANI YA DAR SASA, Vijana wafurika Coco beach. Mistari ni mirefu sana usaili kuendelea kesho.


Jaji wa Shindano hilo Salama Jabir akiwasikiliza washiriki kwa makini.

Vijana wa jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye foleni ya kusubiri kwenda kufanya usaili ili kushiriki shindano la Epiq Bongo Star Serch jijini humo leo.



Mtangazaji wa Televishen CAESAR DANIEL , LEON COETZER na SWEDE  wa Bench Mack  Productions wakiwahoji washiriki hao.

OPERESHENI YA TANESCO YAFIKA ENEO LA KARAKATA UKONGA SASA.



Fundi wa Shirika la Umeme Tanesco Deo Chitamu akikata Umeme kwenye moja ya nyumba eneo la Karakata Ukonga jijijnini Dar es Salaam kwenye zoezi la kukamata wezi wa umeme na kukata umeme kwa wadaiwa sugu linaloendelea kwenye kanda ya Tanesco Ilala ambapo zoezi hilo sasa linaendelea hapa.
Deo Chitamu akikata nyaya hizo.

Ujumbe wa Makene kuhusiana na tuzo za bloggerz zilizotolewa na Vodacom.



Hivi majuzi niliskia kuwepo kwa tuzo za waandishi wa habari za mtandaoni maarufu kama waandishi wa magazeti tando (blogs). Katika Tuzo hizo ambazo ziliandaliwa kwa vigezo wanavyovijua Vodacom, wametajwa washindi fulani. Kama mdau wa kawaida katika magazeti tando, miongoni mwa waasisi wa Bloger wa kwanza kabisa wa Kitanzania naamini kwa sasa kama nchi hii itakuwa inaendeshwa kishkaji, kirafiki, kima kundi na ikaachwa bila kukemewa basi siku si nyingi tutapoteza ladha ya mashindano yanayopima viwango na ubora wa kazi hali itakayofanya nchi kubakia kuwa ya wababaishaji kila siku.
Eneo hili la magazeti tando niliwahi kulilalamikia kutokana na kukosekana ubunifu hasa inapotokea habari moja inajaa kila blog kama ambavyo ipo katika magazeti ya Tanzania. Kwa kuona hili hili nashangaa blog iliyo na kazi ya kubandika picha za magazeti ya kila siku ama habari za wasanii walio nje au kuchota mawazo ya watu katika FB na twitter, au kusubiri taarifa za Maafisa Habari ikaibuka mshindi kwa kuwa tu eti inaonesha kuwa na wasomaji wengi. Kwamba hamjui kuwa ukiseti weblog yako ihesabu wanaoitembelea itahesabu bila kujali ni nani anaingia mara ngapi? 

Kwa mantiki hii kigezo cha idadi ya watu si muwli kuonesha kuwa huyu ni mahiri katika kutoa taarifa katika Blog yake.

Natoa rai, kuwa mliopata nafasi ya kuwa na nguvu katika makampuni msitumie nafasi hizo vibaya kwa kutaka kuidhinisha udhamini wa blog kwa rafiki zenu na kisha kupoteza ladha ya ubunifu katika blog. Najua mmefanya hivi sana katika maeneo kama ya sanaa za urembo na kwingineko lakini kumbukeni hili limezidi na haliwezi kuvumiliwa! Jamhuri hii ilikuwepo kabla yenu na hiki mnachojivunia kwa kuwa kimetengenezwa na urithi wa Baba zenu msitarajie kitabaki kuwa hivi kila siku. Tendeni haki japo kidogo jamii hii itawaheshimu.

Kwa masikitiko na hasira kidogo nawasilisha!
Bonny Makene Road to PhD. 
http://www.fullshangweblog.com/

Rotary Club ya Dar es Salaam yaipiga jeki CCBRT



Rais wa Rotary Club ya Dar es Salaam  Bw. Vinay Choudary ( kushoto)
akikabidhi mfano wa hundi ya kiasi cha dola 10,000 kwa Mkuu wa
hosipitali ya CCBRT Bw, Erwin Telemans ambapo msaada huo ni kwaajili
ya kusaidia kununua vifaa vya viungo bandia katika hosipitali ya CCBRT
iliyopo jijini Dar es Salaam makabidiano hayo yamefanyika leo katika
hosipitali hiyo.
Meneja Kitengo cha Viungo bandia Bw, Maunice Rondo kulia akifafanua
mbele ya wadau wa Rotary Club ya Dar es Salaam namna ya mguu wa Bandia
unavyotengenezwa na kutumia.

Kiongozi Mkuu wa CCBRT Erwin Telemans wakwanza kulia akisisitiza
jambo mbele ya viongozi wa Rotary Club ya Dar es Salaam

MATUKIO KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO




Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe akielekea ndani ya ukumbo wa Bunge mjini Dodoma Aug,1,2012 kwaajili ya kusoma Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa Fedha,2012-2012 (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais- Asiye na Wizara Maalumu Prof, Mark Mwandosya akitoa shukurani Aug,1,2012 kwa Serikali na Wananchi waliomuombea wakati akiwa mgojwa hadi kupata nafuu na kuweza kuhudhuria tena katika vikao vya Bunge ,mjini Dodoma. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akijibu hoja mbalimbali  Bungeni leo kuhusu wizara yake, (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Kabwe Zitto (kulia) akitoa maelezo binafsi kwa waandishi  wa habari Aug. 1,2012 kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yake hususan kuelekea katika kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati. Pichani mwengine ni  Prof. Koyela Kahigi (CHADEMA). Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO,

Yanga, Push Mobile zamwaga bajaj, pikipiki kwa Yanga



Mwandishi Wetu
 
MABINGWA wa kombe la Kagame, Yanga kwa kushirikiana na kampuni ya Push Media Mobile wamekabidhi zawadi za bajaj na pikipiki kwa mashabiki wa timu hiyo walioshinda katika bahati nasibu inayojulikana kwa Young Africans loyalty SMS campaigns for 2012.
 
Washindi hao ambao walitangazwa rasmi katika mechi ya ya fainali ambayo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC na kutwaa kombe hilo kwa mara ya pili ni Roby Revecatus kutoka Mwanza na Amir Jafari (Tabora) ambao walikabidhiwa pikipiki kila mmoja na Finyasi  Vincent  aliyeshinda bajaj.
 
Mabashabiki hao walikabidhiwa zawadi zao makao makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani na Afisa Habari wa  klabu hiyo Louis Sendeu na meneja wa shindano hilo, Talib Rashid kutoka kampuni ya Push Mobile.
 
Rashid alisema kuwa wamefarijika kukabidhi zaidi hizo ambazo zimekwenda sambamba na shamrashamra na ushindi wa timu hiyo.
 
Alisema kuwa kampuni yao iliendesha shindano hilo kwa lengo la kuwapa ufahamu zaidi mashabiki wa timu hiyo kuhusiana na historia ya Yanga na mambo mengine muhimu ya klabu hiyo.
 
“Baada ya Bajaj na pilipiki, shindano linalokuja litakuwa la kuwania gari, hivyo nawataka kukaa mkao wa kula ili kushiriki katika shindano hilo,” alisema Talib.
 
Naye mshindi wa Bajaj, Finyiasi Vicent aliipongeza Push Mobile na Yanga kuendesha bahati nasibu hiyo ambayo imewafanya wao kusheherekea pamoja na ubingwa wa timu hiyo.
 
“Ni faraja kwetu kwa kukadhiwa zawadi zetu sambamba na ushindi wa kombe la Kagame, mimi na wenzangu tunajiona kuwa wenye bahati kubwa kwa kupata fursa hii,” alisema Vincent.
You might also like:

MSHINDI WA GARI YA PILI APATIKANA KATIKA DROO YA MWISHO YA KAMPENI YA VUMBUA DHAHABU CHINI YA KIZIBO.



Mkurugenzi mpya wa kampuni ya bia ya Serengeti bw.Stephen Gannon ( kushoto ) akiongea na waandishi wa habari alipohudhuria kwa mara ya kwanza droo ya mwishon ya promosheni ya Vumbua Hazina Chini ya Kizibo iliyoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti tangu mwezi wa tano 2012 hadi leo. Kulia ni Mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano wa kampuni hiyo Bi Teddy Mapunda.Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw Ephraim Mafuru (kushoto) akiongea na mmoja wa washindi katika droo hiyo ya mwisho kwa njia ya simu ya kiganjani.(katikati) ni meneja wa bia ya Serengeti bw. Allan Chonjo na kushoto ni wasimamizi na wakaguzi kutoka bodi ya taifa ya  michezo ya kubahatisha.
Hii ndiyo gari yenyewe aina ya Ford Figo iliyojipatia mshindi leo

Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti kampuni ya bia ya Serengeti akiongea mna mmoja wa washindi katika droo ya mwisho ya Vumbua dhahabu Chini ya Kizibo iliyomalizika leo, kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti  Lager Allan Chonjo na katikati ni Tumainieli Malisa kutoka kampuni ya PWC 
 Imekuwa ni desturi kwa wateja, wadau, wapenzi na watanznia wote wenye mapenzi mema na kampuni ya bia ya Serengeti kutega masikio ya na kutenga muda wao mwingi kusikiliza redio, kutazama tuninga na kusoma kupitia kwenye magazeti na mtandaoni juu ya nani kajishindia nini kati ya zawadi zinazotolewa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL iliyokuwa ikiendelea tangu ilipoanza 2/05/2012 mpaka leo 01/08/2012 inapofikia tamati yake.

Katika kipindi chote hicho, watanzania wengi wamekuwa wakifurahia kuwa watumiaji wakubwa wa bidhaa ama vinywaji vinavyozalishwa na kampuni ya bia ya Serengeti hasa vinywaji vile vilivyoainishwa katika promosheni hiyo kutokana na kufululiza kutokea kwa washindi mbalimbali waliojishindia zawadi zikiwemo Gari mpya, bajaj, pikipiki jenereta pamoja pesa taslimu.

 Asubuhi ya leo promosheni hiyo ilifika tamati katika  ofisi za CMC Motors jijini Dar es Salaam ambao ndio wauzaji na wasambazaji wa gari aina ya FORD FIGO lililopo kwenye promosheni hiyo ya ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ kwa kuchezesha droo ya mwisho kabisa.Droo hiyo kama ilivyo ada, ilipata kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers.

Awali akimkaribisha mkurugenzi mpya wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw.Steve Gannon anayechukua nafasi ya aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Richard Wells   na baadaye kuongea na waandishi wa habari katika mara baada ya kuchezesha droo hiyo ya mwisho mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Ephraim Mafuru amesema zawadi nyingi zimekuwa zikienda kwa washindi wengi nchini kote. 

Amewashukuru sana wateja na watanzania kwa ujumla kutokana na mwitikio na ushirikiano wao mzuri waliouonyesha katika kipindi chote cha promosheni hiyo. “Kwa niaba ya kampuni ya bia ya Serengeti nachukua fursa hii kuwashukuru sana tena sana wateja wetu na watanzania wote kwa ushirikiano wao mzuri waliotupa katika kipindi chote cha promosheni na kwamba tunatambua uwepo wao katika shughuli zetu zinazoendelea” alisema Mafuru huku akiongeza kuwa mwisho wa promosheni hii ni mwanzisho wa promosheni zingine nyingi.

Kwa upande wake mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo Bw. Steve Gannon amesema amefurahishwa sana na jinsi kampuni hiyo inavyofanya kazi yake hasa inavyotekeleza sera zake za kuwa karibu na wateja wake bila kubagua, “Nimefurahishwa sana na jinsi kampeni hii maalum inayolenga kubadilisha maisha ya watanzania kwa ujumla. Hata kama tumefikia mwisho wa kampeni hii, naomba watanzania wote wajue kwamba kuna promosheni nyingi sana za aina hii ambazo tutaendeleza na kuendelea kuinua maisha ya watanzania kwa ujumla.   ” alisema Gannon.

Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti Premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni  ya “ VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’, nchi nzima kwa muda  wa miezi kumi na Promosheni hiyo imeweza kuleta mabadiliko yakinifu kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla
You might also like:

MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN KUELEKEA KATIKA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI



Ndugu Waandishi,
Nalazimika kukutana nanyi kutoa maelezo juu ya tuhuma zenye shinikizo la kisiasa zinazoelekezwa kwangu binafsi kwamba hata mimi nimeshiriki katika vitendo vya rushwa, kwa nafasi yangu kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma. Taarifa hizo, kama kawaida ya uzushi mwingine wowote  zimesambazwa kimkakati na kwa kasi kubwa kiasi cha kuukanganya umma.
Nafahamu nabeba dhamana kubwa ya uongozi, taswira yangu ya uongozi daima imeakisi njozi na matumaini ya wananchi wa Kigoma Kaskazini, wananchi wanyonge na vijana kote nchini bila kujali itikadi zao za kisiasa, jinsia zao, makabila yao na rika zao. Hivyo, nawajibika kupitia kwenu kuwatoa hofu juu ya hisia potofu zinazopandikizwa kwao na wale wasiopenda kuona baadhi yetu tukiwaunganisha na kuwasemea watanzania wasio na sauti, dhidi ya vitendo vya hujuma na vyenye dhamira ovu kwa taifa.
Mkakati huo wa kuniunganisha na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wanaotuhumiwa kwa kupokea Rushwa unatekelezwa kwa njia zifuatazo:
  1.   Kumekuwa na kauli za watendaji wa serikali ambao wamekuwa wakizieneza na hususan kutoa taswira kwamba baadhi ya kauli zangu zinatokana na ushawishi wa rushwa;
  2.   Kuna taarifa ambazo zimeandikwa tena katika kurasa za mbele za baadhi ya vyombo vya habari  zikidai ’’Zitto kitanzini’’ ama ’’Zitto sawa na popo nundu’’  zikiashiria kwamba na mimi ni mla rushwa; na
  3.   Waandishi wa habari na jamii kwa ujumla wamefikia kuaminishwa habari hizi kiasi cha wengine kuuliza kwa nini Mhe. Zitto Kabwe hakutajwa katika orodha iliyotolewa na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani.

Wananchi waishio katika mabonde ya mito watakiwa kuvitunza



Na Gladnes Mushi wa Fullshangwe-Arusha

Wananchi waishio katika mabonde ambayo ndio vyanzo vya maji
 nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa wanayatunza mazingira ya mabonde ili
 kuwezesha kupatikana mazingira mazuri yatakayopelekea  kupatikana na
maji ya uhakiika pamoja na Mvua.


 Hayo yamesemwa na mtaalamu wa maji katika bonde la mto pangani Bw.
Jero Boam Riwa  wakati akiongea na  wadau wa maji wakati  wakiwa
kwenye ziara ya kutembelea vyanzo mbali mbali vya maji wilayani
arumeru.

Alisema kuwa uharibifu wa mabonde ni tatizo kubwa ibika kmbalo
linafanya kuhar ibika kwa mazingirhia hali ambayo inachangia kuwepo
kwa mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaasababisha  nchi kukumbwa na
ukame.



 Amesema kuwa rasilimali Maji inahitaji sana Utunzaji wa maji
 na isipotunzwa kila kitu kinarudi nyuma ikiwemo kilimo kwanza umeme hivyo
 kunaumuhimu mkubwa wa taasii kushirikiana katika kuzuia ili kuzuia taifa
 kuangamia.


 Pamoja na hayo amewataka watanzania kutambua sheria ya
 hifandhi ya vyanzo vya maji inayotaka kukaa umbali wa mita zipatazo 60 kutoka
 katika chanzo chochote kile cha maji ili kutunza mazingira hayo
ambapo ni muhimu sana kaitka swala zima la kuthibiti uhariabifu wa
mazingira

BODI YA MASHINDANO MISS UTALII TANZANIA YATHIBITISHA MAWAKALA, NAKUTANGAZA NAFASI ZA UWAKALA 2011/2012



Bodi ya Taifa ya mashindano ya Miss Utalii,katika kutekeleza mkakati wake wa kujiimarisha na kujipanga kwa ajili ya mpango mkakati mpya wa muda mfupi na muda mrefu wa miaka mitano na wa miaka kumi,imethibitisha waandaaki wa mashindano hayo katika mikoa na kanda 17, huku ikitangaza nafasi za wandaaji katika mikoaa na kanda mbalimbali Tanzania bara na Tanzania Visiwani. Katika kupitisha makampuni na majina ya waandaaji hao wa ngazi za mikoa, bodi imezingatia uwezo ,umakini na uwepo wa ofisi na waandaaji katika wilaya,mikoa na kanda husika. Pia bodi imezingatia kuwa na waandaaji makini ambao wanaweza kuendana na mfumi mpya wa kitaasisi wa mashindano haya, mfumo ambao unatoa fulsa ya mgawanyo wa madaraka na uwajibikaji wa pamoja na kila mmoja katika ngazi yake. “ Bodi sasa imeamua kujenga taasisi imara ya kiheshimika na kukubalika kitaifa na kimataifa,ni wakati sahihi sasa kwa mashindano haya kuchukua nafasi yake ya kuwa shindano bora na kubwa kuliko yote nchini,Afrika na duniani kwa ujumla, na hili litawezekana tu kwa kuwa na taasisi imara na makini iliyojengwa na watu na makampuni makini. Wale waandaaji wababaishaji,mamluki na wahuni sasa Miss utalii Tanzania sio mahala pake”. Aidha bodi imewataka wasandaaji wote kukamilisha taratibu na matakwa ya kanuni na taratibu za mashindano haya,kabla ya kufanya kwa mashindano ya ngazi zao,ikiwemo kwenda kujitambulisha na kuchukua vibali vya maafisa utamaduni. Aidha bodi imewaomba maafisa utamaduni wa ngazi zote kutotoa vibadi kwa waandaaji hao kabla ya kukamilisha taratibu iliwemo kukabidhi zawadi za washindi na washiriki siku saba kabla ya tarehe za shindano husika. Mikoa na kanda hizo na majina ya waandaaki katika mabano ni Arusha,Mara na Kanda ya Kaskazini ( NAman LIMITED COMPANY LTD), Kilimanjaro na Manyara (NEW VISION PLAN COMPANY LTD),Kagera ( FIOONA FASHION Limited) Mbeya ( WABUNIFU ENTERTAINMENT), katavi ( KATABI COMPANY LIMITED), Dar es Salaam,Kinondoni,Ilala na Temeke ( Tanzania Film Directors Association (TAFIDA)) Vyuo Vikuu Dar es Salaam (Eriado Point View) ,Iringa na Kanda ya Kusini (DELIMA Hotel & Tourism School),Vyuo Vikuu Kanda ya Mashariki ( L.J MEDIA COMPANY), Mwanza (Fania Beauty and Salon Company). Mikoa ambayo haijapata waandaaji baada ya maombi ya waliotuma kutikuwa na sifa, hivyo wenye sifa wajitokeze kuomba kuandaa ni : Njombe, Pwani, Lindi, Mtwara, Tanga Morogoro, Dodoma, Singida, Shinyanga, Simiyu, Geita, Tabora, Rukwa, Kigoma, Kanda ya Kati, Kanda ya Mashariki, Zanzibar, Kanda ya Kusini Nyanda ya Juu, Kanda ya Magharibi, ,Vyuo Vikuu Kusini,Vyuo Vikuu kaskazini,Vyuo Vikuu Magharibi,Vyuo Vukuu Kati,na Vyuo Vikuu. Makampuni na watu wanaotaka kuandaa mashindano haya ya Miss Utalii Tanzania wawasiliane nasi kupitia barua pepe ya missutaliitanzania@gmail.com ,ukurasa wetu wa facebook wa miss tourism/missutalii tanzania na au ofisi za vyombo mabalimbali za vyombo vya habari. Fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012, sasa zitafanyika siku ya mkesha wa sherehe za uhuru 8/12/2012 baada ya kuahitishwa kupisha utaratibu na kalenda mpya ambapo sasa kila mwaka Fainali za taofa zitafanyika siku ya mkesha wa sherehe za uhuru. Mikoa na kanda zote zinatakiwa kuwa zimekamilisha fainali zake kabla ya Novemba 15 kila mwaka.

RAHA ZA PWANI



Akhsante kwa ushirikiano wenu, naimani tutaendelea kushirikiana kwenye kazi pamoja wapezi blog hii

Karibuni sana kwenye blog yenu ya RAHA ZA PWANI muda wowote mkiwa na matukio ipo tayari kutoa taarifa za matukio hayo kwa jamii.

RAHA ZA PWANI

Fahari ya Tanzania

www.saidpowa.blogspot.com

 saidpowa@yahoo.com

0716322981

0787779095

Dar es Salaam Tanzania.

WAZAZI WANAFUNZI WAZUNGUMZIA MGOMO WA WALIMU


Zainabu Mhamila 'Super D Mmoja wa wanafunzi wanaopinga Mgomo wa Walimu kutoingia Madarasani ambaye amesema kuwa shule yao ya Msimbazi Mseto Walimu wao wamendelea kufundisha kama kawaida na kuwasikitikia wanafunzi wa shule nyingine walimu kuto kuingia Madarasani kufundisha watoto hawo ambao awana makosa yoyote
IKOTA MHAMILA
RAJABU MHAMILA 'SUPER D' AMBAYE NI MZAZA WA IKOTA ANAPINGA KITENDO CHA WALIMU KUTOINGIA MADARASANI KUWAFUNDISHA WANAFUNZI