Bodi ya Taifa ya mashindano ya Miss
Utalii,katika kutekeleza mkakati wake wa kujiimarisha na kujipanga kwa
ajili ya mpango mkakati mpya wa muda mfupi na muda mrefu wa miaka mitano
na wa miaka kumi,imethibitisha waandaaki wa mashindano hayo katika
mikoa na kanda 17, huku ikitangaza nafasi za wandaaji katika mikoaa na
kanda mbalimbali Tanzania bara na Tanzania Visiwani.
Katika kupitisha makampuni na majina ya waandaaji hao wa ngazi za mikoa,
bodi imezingatia uwezo ,umakini na uwepo wa ofisi na waandaaji katika
wilaya,mikoa na kanda husika. Pia bodi imezingatia kuwa na waandaaji
makini ambao wanaweza kuendana na mfumi mpya wa kitaasisi wa mashindano
haya, mfumo ambao unatoa fulsa ya mgawanyo wa madaraka na uwajibikaji wa
pamoja na kila mmoja katika ngazi yake. “ Bodi sasa imeamua kujenga
taasisi imara ya kiheshimika na kukubalika kitaifa na kimataifa,ni
wakati sahihi sasa kwa mashindano haya kuchukua nafasi yake ya kuwa
shindano bora na kubwa kuliko yote nchini,Afrika na duniani kwa ujumla,
na hili litawezekana tu kwa kuwa na taasisi imara na makini iliyojengwa
na watu na makampuni makini. Wale waandaaji wababaishaji,mamluki na
wahuni sasa Miss utalii Tanzania sio mahala pake”. Aidha bodi imewataka
wasandaaji wote kukamilisha taratibu na matakwa ya kanuni na taratibu za
mashindano haya,kabla ya kufanya kwa mashindano ya ngazi zao,ikiwemo
kwenda kujitambulisha na kuchukua vibali vya maafisa utamaduni. Aidha
bodi imewaomba maafisa utamaduni wa ngazi zote kutotoa vibadi kwa
waandaaji hao kabla ya kukamilisha taratibu iliwemo kukabidhi zawadi za
washindi na washiriki siku saba kabla ya tarehe za shindano husika.
Mikoa na kanda hizo na majina ya waandaaki katika mabano ni Arusha,Mara
na Kanda ya Kaskazini ( NAman LIMITED COMPANY LTD), Kilimanjaro na
Manyara (NEW VISION PLAN COMPANY LTD),Kagera ( FIOONA FASHION Limited)
Mbeya ( WABUNIFU ENTERTAINMENT), katavi ( KATABI COMPANY LIMITED), Dar
es Salaam,Kinondoni,Ilala na Temeke ( Tanzania Film Directors
Association (TAFIDA)) Vyuo Vikuu Dar es Salaam (Eriado Point View)
,Iringa na Kanda ya Kusini (DELIMA Hotel & Tourism School),Vyuo
Vikuu Kanda ya Mashariki ( L.J MEDIA COMPANY), Mwanza (Fania Beauty and
Salon Company).
Mikoa ambayo haijapata waandaaji baada ya maombi ya waliotuma kutikuwa
na sifa, hivyo wenye sifa wajitokeze kuomba kuandaa ni : Njombe, Pwani,
Lindi, Mtwara, Tanga Morogoro, Dodoma, Singida, Shinyanga, Simiyu,
Geita, Tabora, Rukwa, Kigoma, Kanda ya Kati, Kanda ya Mashariki,
Zanzibar, Kanda ya Kusini Nyanda ya Juu, Kanda ya Magharibi, ,Vyuo Vikuu
Kusini,Vyuo Vikuu kaskazini,Vyuo Vikuu Magharibi,Vyuo Vukuu Kati,na
Vyuo Vikuu.
Makampuni na watu wanaotaka kuandaa mashindano haya ya Miss Utalii
Tanzania wawasiliane nasi kupitia barua pepe ya
missutaliitanzania@gmail.com ,ukurasa wetu wa facebook wa miss
tourism/missutalii tanzania na au ofisi za vyombo mabalimbali za vyombo
vya habari. Fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012, sasa
zitafanyika siku ya mkesha wa sherehe za uhuru 8/12/2012 baada ya
kuahitishwa kupisha utaratibu na kalenda mpya ambapo sasa kila mwaka
Fainali za taofa zitafanyika siku ya mkesha wa sherehe za uhuru. Mikoa
na kanda zote zinatakiwa kuwa zimekamilisha fainali zake kabla ya
Novemba 15 kila mwaka.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
18 hours ago
No comments :
Post a Comment