Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00

Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, October 2, 2012

MELI MPYA YA KISASA YA AZAM MARINE YENYE UWEZO WA KUBEBA ZAIDI YA WATU 1000 NA MAGARI 200 YAWASILI NCHINI

Meli ya Azam Marine inayoitwa Azam SeaLink 1 ikiwasili katika bandari ya Visawani Zanzibar kwa mara kwanza.

Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wakipiga picha Meli hiyo iliyowasili Visiwani Zanzibar leo.

Mzee Said Bakheresa (mwenye nguo nyeusi) akikagua mazingira ya Meli hiyo baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar leo.

Sehemu ya Parking yenye uwezo wa kuingiza magari 200.

Muonekano wa ndani wa Lounge ya kupumzikia wasafiri.

Muonekano wa nje. (Picha na Omar Said wa Kampuni ya Bakheresa).

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar

Kampuni ya Azam Marine inayomiliki boti ziendazo kasi hapa nchini, leo imeingiza meli mpya na ya kisasa itakayochukua zaiidi ya abiria 1500 na magari 200.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine, Bw. Hussein Mohammed Saidi, amesema leo mjini Zanzibar kuwa meli hiyo ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, zanzibar na Pemba itatoza nauli nafuu kwa abiria wake.

Amesema meli hiyo ambayo inatarajiwa kuanza safari zake mara baada ya kukamilisha taratibu za mamlaka mbalimbali.

Meli hiyo inayoitwa AZAM SEALINKI ni ya kisasa katika ukanda huu wa Mwambao wa nchi za Kusini na Pembe ya Afrika.

Bw. Hussein amesema Meli hiyo ambayo imetengenezwa nchini Ugiriki na inatayarishiwa eneo maalumu litakalotumika kwa kupakia na kushusha abiria na mizigo yakiwemo magari.

Amesema meli hiyo itasafiri kwa muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam na Zanzibar na saa 4 kutoka Zanzibar na Pemba ama saa 7 kutoka dar es salaam na Pemba.

Amesema pamoja na kuwasili kwa Meli hiyo, Kampuni ya Azam pia inatarajia kuleta meli nyingine ya abiiria inayojulikana kama Kilimanjaro namba 4.

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Visiwa vya zanzibar wamepongeza ujio wa meli hiyo lakini wakaitaka serikali kuendelea kudhibiti uingizwaji wa meli chakavu na kukuu ili kuepuka uwezekano wa kutokea ajali za mara kwa mara.

Bwana Rajabu Khamisi mkazi wa Pemba na Bi. Rehema Omari wa mjini Zanzibar, wamesema kuna haja ya Serikali kusimamia ukomo wa nauli ili kila mwananchi aweze kusafiri kutoka sehemu moja na nyingine kwani wamesema vipato havilingani.

Monday, October 1, 2012

MASTA JUMANNE AWAKUMBUSHA WATU KUFANYA MAZOEZI

Na Mwandishi Wetu

MSANII Jumanne Wilsoni 'Masta Jumanne' anawashauli vijana kuja kujiunga katika mazoezi anayotoa katika ukumbi wa Ilala Sheli CCM ambapo anafundisha mchezo wa Taiching Kumfuu ambayo inawasaidfia kuwalinda mbali na kuwalinda inasaidia pia kujenga mwili kwa mazoezi

na sehemu nyingine iliyopo Ilala CCM Mchikichini 'Masta jumanne' ametoa wito kwa vijana kujitokeza kufanya mazoezi katika stail mpya alizokuja nazo toka china hivi karibuni amboyo amekuja na mbini mbalimbali za Taichi Kung-fu kwa ajili ya kufanikisha kujilinda wakati wowote kwa  watu wabaya

Masta Jumanne aliyejifunzia michezo hiyo nchini China na ni mtu wa kwanza kuingiza stail hiyo nchini kwa ajili ya kukuza vipaji vya mchezo wa Taichi Kung-fu

Ambapo alianza kufundisha mwaka 2003 katika majeshi ya Tanzania na sasa anawafundisha Raia mbalimbali kwa ajili ya kujilinda Masta jumanne ambaye anatamba na filamu ya mapigano ijulikanayo kwa jina la Malipo ni Duniani 'Amesema kuwa filamu hiyo ametoa ili kuonesha Dunia jinsi ilivyo na malipo yake ni hapa hapa Duniani

na sasa yupo mbioni kutoa filamu ya nipo trayari kufa inayotarajia kutoka mwishoni mwa mwezi uhu iliowashilikisha raia wa kichina ambayo ipo katika matasifa mawili ya Tanzania na China

Mpaka sasa ameshawafundisha vijana wengi wapatao 60 ambao wamepitia mafunzo kutoka kweke

Masta Jumanne kabla ya kwenda kujiendeleza zaidi na mafunzo ya mchezo huo katikla nchi mbalimbali alikuwa ajifunza nchini Zambia kabla ajaenda china kukamilisha mafunzo yake ya ufundishaji

Ametoa wito kwa watu mbalimbali kujitokeza katika mafunzo yake kwa kuwa wengi aliowafundisha wamepata mafanikio mbalimbali kupitia kwake ikiwemo kupata ajira katika makampuni mbalimbali ya ulizi na usimamizi wa shunghuli mbali mbali za kitaifa

KWA WANAOTAKA KUJINGA NAS MAFUNZO HAYA WAWASILIANE MOJA KWA MOJA NA MASTA JUMANNE SIMU NAMBA 0713938461
KWANI MAZOEZI UONDOA PRESHA,KISUKALI,KUPUNGUZA UNENE,KUPOOZA,MATATIZO YA VIUNGO, SASA WANAPATIKANA KATIKA JENGO LA CCM ILALA SHELI GHOROFA YA KWANZA

TIKETI YANGA, SIMBA KUANZA KUUZWA KESHO

Tiketi kwa ajili ya mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa keshokutwa (Oktoba 3 mwaka huu) zitaanza kuuzwa kesho (Oktoba 2 mwaka huu) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
 
Mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku.
 
Vituo vitakavyotumia kuuza tiketi hizo kuanzia saa 4 asubuhi ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Uwanja wa Taifa, Kituo cha Mafuta OilCom Ubungo, Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio/Samora, Dar Live Mbagala na Kituo cha Mafuta Buguruni.
 
Kiingilio cha chini kwenye mechi hiyo ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000. Watazamaji watakaoketi kwenye viti vya rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja.
 
Sh. 10,000 ni kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000. Kwa upande wa VIP B tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio kitakuwa sh. 30,000.
 
Wakati huo huo, mwamuzi Mathew Akrama kutoka Mwanza ndiye atakayechezesha mechi hiyo. Waamuzi wasaidizi ni Samuel Mpenzu kutoka Arusha na Ephrony Ndissa wa Dar es Salaam wakati mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es Salaam.

AIRTEL KWA KUSHIRIKIANA NA EQUITY BENKI YATOA MIKOPO KWA WAFANYABIASHA WADOGOWADOGO

 Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex, Bw. Abdubakar Rakesh akizungumza katika uzinduzi wa utakaowawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la machinga complex jijini Dar es Salaam. Mpango huo utawawezesha wamachinga hao kupata mikopo nafuu kwa ajili ua kuendesha na kukuza biashara zao ambapo benki ya Equity kwa kupitia huduma ya Airtel Money na wao kuwa wakifanya marejesho ya mikopo hiyo kwa kutumia Airtel Money.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Ear Promotion ambao wanasimamia na kuratibu mradi huo, Bw. Brian Kikoti aliwasifu benki ya Equity pamoja na Airtel kwa kuungana nao katika kusaidia kusimamia ufanisi wa soko la wafanyabiashara wadogo wadogo.
 Umati wa watu waliohudhuria katika uzinduzi wa utakaowawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la machinga complex jijini Dar es Salaam.
 Bi. Sara Yohana aliyemwakilisha mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam akisoma risala katika uzinduzi wa utakaowawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la machinga complex jijini Dar es Salaam.
Meneja Mahusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema kuwa wataendelea na mikakati ya kusaidia jamii Nyanja mbali mbali za kimaendelea kwa kupitia huduma ya Airtel Money katika mradi wa upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia simu ya mkononi.
Dar es Salaam Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Equity bank pamoja na Kampuni ya Ear promotion mwishoni mwa wiki hii imezindua mradi utakaowawezesha  wafanya biashara wadogo wadogo wa soko la machinga complex jijini Dar es saalam  kupata mikopo nafuu kwaajili ya kuendesha na kukuza biashara zao ambapo mikopo hiyo itatolewa na benki Equity kwa kupitia huduma ya Airtel money na wao kuwa wakifanya marejesho ya mikopo hiyo kwa kutumia Airtel money
Akizungumza wakati wa halfa ya uzinduzi wa mradi huo, Meneja uendeshaji wa benki ya Equity bw, David Mukaru  alisema” equity benki iko  mstari wa mbele kuisaidia  jamii katika huduma za kibenki ikiwemo mikopo ya riba nafuu hasa akina mama wa vikundi mbalimbali.
Benki yetu imekuwa sehemu ya maendeleo ya kukuza biashara na mtaji wa wafanyabiashara wadogo hadi wakubwa nchini. Leo kwa kushirikiana na Airtel kupitia huduma ya Airtel money tunawawezesha wafanyabiasha wa soko hili la machinga complex zaidi ya  efu tano kupata mikopo ya riba nafuu ambayo kwa hakika itakuza mitaji na kuwapatia ufanisi zaidi katika biashara zao”. 
Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja uhusiano wa Airtel bwn Jackson Mmbando alisema ”Airtel tunaendelea na mikakati yetu ya kusaidia jamii katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo kwa kupitia huduma  ya Airtel money, katika mradi hu Airtel tunarahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia simu yako ya mkononi, tunawawezesha wafanyabiashara hawa kupokea na kufanya marejesho ya mikopo yao kwa kupitia huduma ya Airtel money”
“lengo letu  Airtel ni kurahisi uendeshaji wa mikopo hii,  kuhakikisha usalama wa fedha, na kupunguza usumbufu wa wafanyabiashara hawa kutembea umbali mrefu kufanya marejesho ya mikopo hii”.  aliongeza Mmbando.
Naye mwenyekiti wa wafanyabisahara wa soko la machinga complex bw. Abdubakar Rakesh alisema ”ninaishukuru  kampuni ya Airtel pamoja na Equity benki kwa kutufikia sisi wafanya biashara wadogowadogo kwa kupitia mradi huu wa mikopo nafuu. ni kwa muda mrefu wafanyabiashara wa soko la machinga complex wamekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata mikopo nafuu ambayo itawawezesha kukuza mitaji na kuweka bidhaa mbalimbali zitakazo wavutia wateja kufanya manunuzi katika soko hili, hivyo kwa kupitia mradi huu tunaamini tutafanikisha matarajio yetu ya kuwa na soko la kisasa lenye miundo mbinu na hadhi kwa wafanyabishara na wateja wetu.
Naye bw, Brian Kikoti Mkurugenzi wa Ear promotion Kampuni inayosimamia na kuratibu mradi huo amewasifu Equity Benki pamoja na Airtel kwa kuungana nao katika kusaidia kusimamia ufanisi wa soko hilo na la wafanyabiashara wadogowadogo.
Mbali na ushirikiano huu wa kibiashara na  Equity bank,  Airtel tayari inashirikiana na mashirika mbalimbali yakiwemo GEPF , LAPF, DAWASCO, TANESCO, USA EMBASSY, COCACOLA na mengine mengi katika kutoa huduma zao kupitia huduma ya Airtel money.

PUNGUZA "STRESS" ZA WIKI NZIMA NA SKYLIGHT BAND KILA IJUMAA THAI VILLAGE MASAKI JIJINI DAR.

Baadhi ya Wanamuziki wa SKYLIGHT BAND wakishambulia Jukwaa mwishoni mwa wiki katika show ya kukata na shoka kwenye kiota chenye upepo mwanana cha THAI VILLAGE Masaki jijini Dar es Salaam. Pichani ni Rappa Sam Machozi akisindikizwa na Wenzake Aneth Kushaba AK 47 pamoja na SONY MASAMBA.

Sam Machozi kazini. Hapa unapata kila kitu Style zote za muziki kuanzia Dancehall, Reggae, R & B, Azonto na nyinginezo bila kusahau Kwaito.

Mdogo mdogo wapenzi wa Skylight Band wakaanza kujimwaga kwenye dancing floor.
Uzao wa Bongo Star Search binti mwenye kipaji na sauti nyororo Mary Lukas.
Vijana machachari wadogo wakifanya mambo makubwa.
Joniko Flower, Aneth Kushaba AK 47 sambamba na SONY MASAMBA.
Tumba zikikung'utwa kisawa sawa.
Hawa ndio Malkia wa Skylight Band wenye sauti za kumtoa nyoka pangoni. Kushoto ni Mary Lukas sambamba na Meneja wa Band Aneth Kushaba AK 47 wakiwajibika.
Aneth Kushaba AK 47 akiimba kwa hisia kali.
Taratibu dancing floor ikiendelea kupendeza.
Sam Machozi sambamba na marapa wenzake.
Hapa ni kikongo kimelala anaitwa SONY MASAMBA.

NAIROBI SHOWCASE -SWAHILI FASHION WEEK 2012

BIASHARA YA MAGAZETI YAHUJUMIWA JIJINI DAR. WAUZAJI HUKODISHA MAGAZETI KWA BEI YA TSH 250 HALAFU HUYAFUATA BADALA YA KUYAUZA.

Moja ya maeneo yanapouzwa magazeti jijini Dar es Salaam.              
UCHUNGUZI uliofanywa na blog hii jijini Dar es Salaam hasa maeneo ya Kariakoo kumekuwepo na biashara isiyo ya haki inayofanywa na wauza magazeti ambayo kwakiasi fulani inawahujumu wamiliki wa makampuni hayo.
 Kiutaratibu magazeti yanatakiwa kuuzwa kwa bei halali iliyoandikwa kwenye gazeti na mteja anapaswa kulipia bei hiyo na siyo zaidi na wala pungufu ya bei hiyo. Kilichonisukuma kufanya uchunguzi huo ni pale nilipomuona muuzaji mmoja wa magazeti akipita kuyaacha magazeti kwenye baadhi ya maduka baadaye huyapitia tena na kupewa Tsh250/ tu ikiwa ni malipo kwaajili yakulisoma gazeti hilo.

Raha za Pwani ilikwenda mbali zaidi na kuzungumza na baadhi ya vijana wa mtaa wa Kipata nakunieleza kuwa biashara hiyo ni yakawaida tangu magazeti yalivyopandishwa bei na kuuzwa hadi bei ya Tsh 800.

Mbali na Changamoto ya Mitandao ya Kijamii blogs facebook na mingine mingi bado kunaibuka adui mwengine kwa biashara hiyo ya magazeti hali inayoweza kuhatarisha sekta hiyo mbele ya safari ndefu ya maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

TRENI YA SHIRIKA LA RELI LA TANZANIA NA ZAMBIA(TAZARA) ITAKAYOTUMIKA KWA USAFIRI WA DAR ES SALAAM – PUGU MWAKANGA-KURASINI YAFANYIWA MAJARIBIO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Mhandisi Omar Chambo akishuka kwenye Kichwa cha treni kitakachofanya Safari zake Dar-Mwakanga-Kurasini mapema mwezi wa kumi.Majaribio ya sehemu ya mabehewa hayo yalifanyika jana. Treni hiyo kwa

Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA)na wa Wizara ya Uchukuzi wakiwa ndani ya Mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio kwa ajili ya Usafiri wa treni Jijini Dar es Salaam jana.
Treni maalum kwaajili ya usafiri wa jiji la Dar es Salaam ikiwa tayari imeshafanyiwa matengenezo kuanza kazi na kufanyiwa majaribio jijini humo jana.
Meneja Mkuu wa Kanda ya Tanzania wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA), Mhandisi Abdalla Shekimweri akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo jana wakati wa majaribio ya Mabehewa matatu yakayofanya safari zake kutokea Dar-Kurasini-Mwakanga.Mabehewa hayo ni sehemu tu ya mabehewa yatakayokuwa yakifanya safari

TANGAZO TANGAZO LA KUJIUNGA KWENYE MAZOEZI

TANGAZO TANGAZO LA KUJIUNGA KWENYE MAZOEZI

MCHEZO WA MASUMBWI, TAA INAYOZIZIMA – SEHEMU YA NNE

Na Onesmo Ngowi

Masumbiwi au kwa majina mwengine ndondi au ngumi na kwa majina ya mitaani ndogwa, mawe n.k. ni mchezo unapoendwa sana na watu wengi. Aidha mchezo huu ni kati ya michezo inayoogopwa sana duniani. Mchezo wa ngumi uko hatarini kupoteza maana yake ya asili yaani kucheza kama burudani, kuwakilisha nchi na kujenga ushupavu wa mchezaji. Mamilioni ya watu wanaojazana kuutazama wasingependa kabisa kujiingiza kuucheza mchezo wa ngumi. Sasa endelea………………………………….! 

MATUMIZI YA SHERIA MPYA ZA NGUMI 

                Ni katika mwaka 1866 wakati ambapo mtawala wa Queensbury (Marguees of Queensbury) huko Uingereza alisaidia kutunga sheria mpya zilizotumika kuuendesha mchezo wa ngumi sheria ambazo kwa heshima zilipewa jina lake. Sheria hizi ziliweka bayana mambo yafuatayo:
Uzito wa kila bondia ulianzia Fly ambao ni chini ya kilo 50, bantam kilo 54, featherweight kilo 57, lightweight kilo 60, welterweight kilo 67, middleweight kilo 75, light heavy kilo 80 na hevyweight uzito ambao haukuwa na kikomo.
Sheria za ulingoni: zilipunguza muda uliotumika kwenye raundi za mpambano wa ngumi kuwa dakika 3, na pia ziliweka kikomo kwa mabondia kuangushana chini kama wacheza mieleka. Zilifanya pia matumizi ya gloves kuwa ya lazima. Uzito wa glovu nao ulianzia oz 8, 9, 10, 12 na 15.
Pamoja na ukweli kwamba sheria hizi mpya za hazikuweza kuzuia kwa mara moja kupigana kwa kutumia mikono mitupu (bare-knuckle). Ushindi wa bondia maarufu wa Kingereza James J. Corbet dhidi ya bingwa maarufu aliyejulikana kwa kucheza kwa mikono mitupu John L. Sullivan mwaka 1892 ndipo matumizi ya gloves yalipoanza kutumika rasmi katika mapambano yote ya ngumi.
                Katikati ya karne ya 20 kuelekea kwenye karne ya 21 sheria mpya za ngumi zilitungwa baada ya kuanzishwa kwa mashirikisho mbalimbali ya ngumi ambayo kila moja lilikuja na sheria zake. Kwa uchache sheria hizi zilipunguza raundi za ngumi mpaka kufikia 15 kwa ubingwa wa ngumi na kuweka sheria kali za sehemu ambazo bondia anaweza kumpiga mwingine.
                Aidha sheria hizi ziliweka kikomo katika uzito mbalimbali ambapo kulianzishwa uzito kama light fly, fly, super fly, light welter, junior middle, super middle n.k. Vile vile sheria hizi mpya zilizuia matumizi ya madawa mbalimbali ya kuongeza nguvu kwa mabondia.
Katika mashindano makubwa ya kimataifa hususan Olimpiki wakati wa ngumi za ridhaa sheria za matumizi ya madawa ya kuongeza ngumi ziliwekewa kipaumbele. (Wakati huu madawa mengi ya kuongeza nguvu yamepigwa marufuku karibu katika michezo yote).
                Aidha mabondia mbalimbali ambao waligombea mikanda ya ubingwa walitakiwa walingame uzito na aliyezidi ilibidi apewe muda maalum wa kuupungunza hadi afikie uzito wa mwenzie.
                Ni mwishoni mwa karne ya 20 ndipo mashindano makubwa ya utitiri wa mashirikisho ya ngumi hususan ngumi za kulipwa yalipoanzishwa kwa fujo za aina yake.
Mwanzoni kulikuwepo na shirikisho moja tu nalo lilikuwa Chama cha Ngumi duniani (WBA). Baada ya muda wa miongo kadhaa Baraza la Ngumi Duniani (WBC) nalo lilianzishwa. Mwanzoni mwa miaka ya 80 Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) nalo lilianzishwa.
                Sababu kubwa ambazo zinatajwa na watu mbalimbali za kuwepo kwa utitiri wa mashirikisho haya ni ubinafsi. Lakini ukiangalia kwa makini kuanzishwa kwa mashirikisho haya kumeweza kwa kiasi kikubwa kuwapa nafasi mabondia wengi kujulikana kimataifa.
Hebu fikiria kuwa katika nafasi ya ubingwa wa shirikiso moja kuna nafasi 17 tu za ubingwa. Kwa maana nyingine mabondia 17 tu ndio wanatakiwa wajulikane kuwa ni mabingwa wa dunia kwa wakati mmoja.
                Idadi kamili ya mabondia walioko dunia nzima haijulikani lakini inaweza kufikia malaki kama sio mamilioni kadhaa. Itakuwa vigumu sana kwa mabondia wote kuweza kufikia ubingwa wa dunia katika maisha yao kama kungekuwepo na shirikisho moja tu.
Japokuwa kuna hisia kuwa mashirikisho mengine yamezidiwa umaarufu na mengine lakini kunasaidia kuwapa nafasi nzuri mabondia wengi kujulikana duniani. Kwa sasa inakadiriwa kuweko kwa mashirikisho kama 15 na ukizidisha kwa 17 utaona tayari mabondia wengi zaidi wanaweza kuwa mabingwa wa dunia kwa wakati mmoja. Japokuwa bingwa mmoja wa dunia anaweza kujulikana kwa zaidi ya shirikisho moja.

SHERIA ZA BAADHI YA MASHIRIKISHO YA NGUMI

Mashirikisho mengi ya ngumi yanatumia sheria zinazofanana. Yote yanatumia sheria za “Marguees of Qunensbury” yaani mabondia wapigane wakiwa wamevaa glovu mikononi zenye uzito unaofanana. Wawe na uzito sawa na ngumi zipigwe kuanzia juu ya mkanda.
Ikumbukwe kuwa mengi ya mashirikisho haya yalianzishwa miaka ya karibuni. Kabla ya shirikisho hata moja la ngumi kuanzishwa ngumi zilikuwa zinatawaliwa (zinaendeshwa) na kamisheni za mitaa, manispaa na nchi mbalimbali. Hata wakati mabondia wa zamani wanatwa ubingwa wa dunia kwao hakukuwa na njia mbadala ya kuwakutanisha na mabondia wengi waliokuwa kwenye viwango vimoja na wanotoka katika nchi mbalimbali.
Ikumbukwe pia kwamba neno ubingwa wa ngumi linamaanisha ushindi wa tuzo katika kiwango chako. Kama unawashinda mabondia karibu wote walio kwenye kiwango chako unakuwa bingwa wa kiwango hicho. Viwango huwekwa na mashirkisho yanayosimamia ngumi.
Kwa mfano mabondia wanaowekwa kwenye viwango fulani vya ngumi wanatakiwa wawe wamecheza mapambano kadhaa yenye hadhi ya kitaifa na kimataifa.
Shirikisho la Ngumu la Kimataifa (IBF) linataka walio kwenye viwangio vyake wawe wameshindana na mabondia wenye hadhi ya kimataifa. Viwango vya IBF vinaanzia 1-15 kila uzito.  Bondia anayeingizwa kwenye viwango vya IBF ni lazima awe amecheza mapambano zaidi ya 15 yenye hadhi ya kimataifa ya kushinda asilimia 75 ya mapambano yote.
Yapo mashirikisho mengine yenye utaratibu tofauti na wa IBF na ambayo masharti ya kuingizwa kwenye viwango vyake sio magumu sana. Pengine ndio maana mashirikisho ya IBF, WBA, WBC na WBO yanaheshimika zaidia duniani kwa kuwa masharti ya kuwekwa kwenye viwango vyake na kucheza ubingwa wake ni magumu zaidi.
Kwa ajili ya sheria kuwa ngumu mashirikisho haya yana makubaliano ya kuwaruhusu mabondia kucheza ubingwa unaotambuliwa na mashirikisho yote manne kwa pamoja (unification titles). Yaani bondia anaweza kugombania ubingwa mmoja unaotambuliwa na IBF, WBA, WBU na WBO na kuvaa mikanda minne. Mabingwa hawa wanajulikana kama undisputed champions (mabingwa wasiopingika)
Sina maana kwamba ubingwa wa mashirikisho mengine hauna maana bali yamezidiana kwa umaarufu na heshina tu. Bingwa wa dunia ni bingwa kwa wapenzi wake na wapinzani wake.
Wako mabingwa wa mashirikisho mengine kama IBA, IBC, WBF, WPBF ambao wamekuja baadaye kuwa mabingwa wa sasa wa WBC, WBA, IBF na WBO. Mfano mmoja ni bingwa wa sasa wa WBC Vitali Klitschko toka Ukraine ambaye kwa muda mrefu alikuwa bingwa wa dunia wa WBO. Iaendelea………………………….!
Mwandishi wa makala haya ni; Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Shirkisho la Ngumi za Kulipwa Afrika Mashariki na Kati (ECAPBF), Shirikisho la Ngumi la Kimataifa bara la Afrika, Masharilki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi (IBF/AFRICA) na Mkurugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) E-mail: ibfafrica@yahoo.com

MAHAFALI YA KAMALDIN MBUGUNI

 Kamaldin Suleima Mbuguni akiwa na baba yake Mbuguni na mama yake Ananora katika sherehe ya mahafali ya darasa la saba mwishoni mwa wiki Blog Hii inampongeza na kumtakia safari njema katika maandalizi ya elimu ya Sekondari.
                                  amaldin Mbuguni akiwa na baba yake Suleiman Mbuguni.
 
 Kamaldin akilishwa keki na binti wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga Iman Madega ambaye  wamemaliza pamoja katika Shule ya Msingi Shree Hindu Mandal.
Wazazi wa mtoto Kamaldin (Katikati) kulia ni Baba yake Suleimana Mbughuni na kushoto ni mama yake
KAMALDIN MBUGUNI akiwa na cheti chake cha kuitimu
Mahafali ya Shule ya Msingi Hindu Mandal Kijitonyama, Kulia ni mtoto Kamaldin Suleiman Mbughuni

Hizi ndizo keki za Graduation ya Hindu Mandal