Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, June 18, 2013

MARIA TUBETI ATWAA TAJI LA REDD'S MISS KAGERA 2013




Mshindi wa taji la Redds Miss Kagera 2013 Maria Tubeti (Katikati) akiwa na nyuso ya furaha mara baada ya kamati ya majaji kumtangaza mshindi katika kinyanganyiro kilichoshirikisha walimbwendwe 14, Wa pili ni Hilda Athanas na mshindi wa tatu ni Arodia Mahatane
Mshindi wa taji la Redds Miss Kagera 2013 Maria  Tubeti akifurahia kutwaa taji hilo lililokuwa limeshikiliwa na  Miss Talent Tanzania Babylove Kalalaa aliyeshinda mwaka jana 2012.
Eeeee jamani Hongera kwa kushinda...
Warembo wote 14 wa Redd's Miss kagera 2013 wakitambulishwa

Washiriki wa Shindano la redd's miss Kagera 14 wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Majaji walianza kutaja Tano Bora hapa.(Kutoka kulia ni jaji Abella Kamala mtangazaji wa Radio Kasibante fm, jaji wa katikati ni Bi Beata na wa kushoto ni Jaji Edgar)
Tano Bora
Maria  Tubeti akijibu swali
Warembo waliochagulia tano bara wakiwa na tabasamu baada ya kutajwa na kusonga mbele
Miss aliyeachia taji lake leo hii ambaye pia ni Miss Talent Tanzania Babylove Kalalaa
Majaji wakitaja Mshindi wa tatu, wa pili na

Epiq Open Mic kumekucha Dar



Vijana waliojitokeza wakiwa kwenye foleni. 
 Jopo la washauri likongozwa na Marco Chali (wa pili toka kulia), akifuatiwa na Dknob, Walter na mwisho kulia ni Godzila
 Mmoja wa vijana akiimba mbele ya washauri.
Mmoja wa wasichana akionyesha uwezo wake.

Vijana waliojitokeza wakijiandikisha.


NaMwandishi wetu


Baada ya kuzinduliwa kwa mafanikio wiki mbili zilizopita katika viwanja vya Mwembe Yanga, mamia ya vijana wamejitokeza mwishoni mwa wiki hili katika viwanja ya ofisi za Zantel kuhudhuria usaili wa Epiq Open Mic.
Huku ikiwa imebaki wiki kadhaa kabla ya kuanza kwa msimu mya wa Epiq BSS, Zantel kwa kushirikana na Marco Chali Foundation, wamezindua Epiq Open Mic ili kuwapa vijana nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.
Fursa hii, ya Epiq Open Mic, inawapa nafasi vijana wenye vipaji vya muziki fursa ya kusikilizwa na mtayarishaji wa muziki maarufu nchini, Marco Chali pamoja na jopo la wanamuziki kama Godzila na Dknob, ambao wanawashauri mambo kadhaa kuhusiana na muziki wao, na huku wale wenye vipaji zaidi wakipewa nafasi ya kurekodi na Marco Chali.
Akizungumzia Epiq Open Mic, Marco Chali anasema hii ni fursa ya vijana kujifunza misingi ya muziki, lakini pia kuweza kurekodiwa muziki wao.
‘Lengo la Epiq Open Mic ni kuwahamasisha vijana kushiriki katika kukuza vipaji vyao, kuongeza uelewa wa mambo ya muziki pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo katika muziki’ alisema Chali.
Marco Chali ambaye pia ni mtunzi na mwimbaji, ametayarisha nyimbo nyngi ambazo zimeshinda tuzo ndani na nje ya nchi za wasanii kama Ms. Trinity kutokea Jamaica, A.Y wa Tanzania, Prezzo wa Kenya, J Martins kutoka Nigeria na wengine wengi.
Kwa upande wake, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema kampuni ya Zantel inaaminini katika kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao.
‘Muziki ni ajira kwa vijana wengi, na kuamini hilo ndio maana kampuni ya Zantel imeamua kuwafikia vijana wote wenye vipaji na kuwapa nafasi ya kuonekana’ alisema Khan.

REDDS MISS KINONDONI TALENT 2013 KUFANYIKA ALHAMIS 21 JUNI UKUMBI WA SHEKINAH GARDEN JIJINI DAR




Warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutambulishwa mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani), kwa sasa warembo hao wameshaingia katika hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam kujinoa kwa ajili ya Redd's Miss Kinondoni Talent 2013 zinazofanyikia ukumbi wa Shekinah Garden Mbezi Beach na Fainali zinafanyika Juni 21 ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip.
---
Na Cathbert Angelo, Kajunason Blog.
SHINDANO la Redd’S Miss Kinondoni Talent 2013 linatarajiwa kufanyika alhamisi ya Juni 25 katika ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambalo litashirikisha warembo wapatao kumi na mbili ambao watachuana kumpata mrembo mwenye kipaji.
Akizungumza mratibu wa shindano hilo, Dennis Ssebo alisema maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri na kueleza mshindi atakabidhiwa zawadi zake kwenye fainali ya shindano hilo ambalo litafanyika Juni 21 mwaka huu katika uwanja wa hoteli ya Golden Tulip.
“Ninachoweza kusema shindano la mwaka huu litakuwa la aina yake kutokana na kusheheni warembo bomba wenye mvuto na hivyo kuonyesha kutakuwa na mchuano mkali miongoni mwao “Alisema Ssebo.
Warembo warembo wanaotarajiwa kumenyana ni kutoka katika vitongoji vya Sinza, Ubungo na Dar Indian Ocean ambao kwa pamoja wanaunda Redd's Miss Kinondoni 2013.
Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa wilaya ya Kinondoni maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata raha.
Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com, JestinaGeorge Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.

HATIMAYE KANUMBA MPYA AZALIWA.






Lulu akiwa amembeba Kanumba jnr

Mama Lulu na mama wa marehemu Steven Kanumba wanaonekana kuwa karibu sana siku hizi na hivyo watu kuzidi kuamini kuwa hawana tofauti tena na kusahau yaliyopita. Dada wa marehemu Steven Kanumba amejifungua hivi karibuni katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na mtoto huyo kupewa jina la Steven Kanumba Jr huku mama mzazi wa Elizabeth Michael(Lulu) na mama Kanumba wakiwa na furaha sana, Lulu pia alionyesha furaha yake kwa kuzaliwa mtoto huyo kama picha zinavyoonekana hapo chini. Tunawapongeza tena na tena wazazi hao kwa kuwadhihirishia wanajamii kwa mara nyingine kuwa kila mtu ana amani na mwenzake na hakuna tofauti yoyote kati yao. Mtoto huyo amepewa jina la Kanumba kama ishara ya kumuenzi muigizaji Steven Kanumba aliyekuwa maarufu Afrika mashariki na kuanza kujulikana kimataifa. Angalia picha...........


Sura zikiwa na Furaha

Mama Lulu, Lulu Na Mama Kanumba kwenye picha ya pamoja

Monday, June 17, 2013

KONYAGI YAWAPIGA MSASA WABUNGE KUHUSU BIASHARA VIROBA






 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa, akionesha kinywaji cha Afrika Kusini kilichofungwa kwenye viroba kama ambavyo Konyagi inafanya hapa nchini.Vinywaji kama hivyo vipo karibu nchi nyingi Ulimwenguni.

 Meneja wa Masoko wa Konyagi, Joseph Chibehe akielezea jinsi vinywaji vyao vinavyochangia mapato ta serikali
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo,Maji na Mifugo, Said Nkumba akichangia mada hiyo kwa kuviasa baadhi ya vyombo vya habari kuacha kuandika habari za kudidimiza viwanda vya haba nchini. Kulia ni Idd Azzan Mbunge wa Kinondoni na Dunstan Kitandula ambaye ni Makamu Mwenyekiti was  Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara.
                               Bidhaa mbalimbali zikiwa zimfungwa kwenye viroba
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa () akifafanua jambo katika semina ya wajumbe wa Kamati mbili za Bunge za Uchumi,Viwanda na Biashara  pamoja na Kilimo,Maji na Mifugo kuhusu baadhi ya vyombo vya habari vyenye uhusiano na nchi jirani vinavyotumika kupiga vita viwanda vya ndani kikiwemo cha Konyagi. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makala, akichangia mada katika semina hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Kassim Majaliwa na Said Nkumba.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Dunstan Kitandula akichangia mada hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa (kushoto) akimkabidhi jezi Idd Azzan kwa ajili ya timu ya Bunge iliyocheza na timu ya Konyagi kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma Jumamosi
 Mgwassa akikabidhi jezi ya timu ya Konyagi kwa Idd Azzan tayari kwa mtanange na timu ya Bunge
 Meneja Masoko wa Konyagi, Joseph Chibehe (kushoto) akimkabidhi W. Zuberi  msaada wa vyerehani, ambavyo alivipokea kwa niaba ya BNaibu Spika wa Bunge, Job Ndugai
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika, akisalimiana na timu ya Bunge muda mfupi kabla ya pambano lao na timu ya Konyagi, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

 George Mkuchika akisalimiana na wachezaji wa timu ya Konyagi
 Wachezaji wa timu ya Bunge wakisalimiana na wachezaji wa Konyagi
 Kikosi cha timu ya Bunge kilichochuana na Konyagi
Kikosi cha timu ya Konyagi kilichomenyana na Timu ya Bunge

KING CLASS MAWE ALIVYO MSAMBALATISHA BAUNSA WA MOROGORO



Bondia Patrick Kavako 'Baunsa wa Morogoro akiwa chini hoi baada ya kupata kipondo toka kwa Ibrahimu Class 'King Class Mawe' katika raundi ya tatu Class alibuka mshindi kwa KO picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Refarii Omari Yazidu akimwinua mkono juu bondoa Ibrahimu Class 'King CLass Mawe' kuwa mshindi baada ya kumuangusha bondia Patrick Kavako'Baunsa' wa morogoro katika raundi ya tatu. picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Patrick Kavako 'Baunsa' wa morogoro wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Class alishinda kwa KO ya raundi ya tatu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Bondia Mariam Abdallah kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Lulu Kayage wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita Kayage alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Lulu Kayage Kushoto akioneshanas ufundi wa kutupiana Makonde na MariamuAbdallah wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita lulu alishina kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia lulu Kayage akinyooshwa mkono juu baada ya kushinda

Mabondia Chipkiz wa kike kushoto Lulu Kayage na Mariamu Abdallah kulia wakiwa na viongozi wa ngumi nchini Ibrahimu Kamwe na Emanuel Mlundwa


Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Patrick Kavako 'Baunsa' wa morogoro wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Class alishinda kwa KO ya raundi ya tatu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com



Ibrahimu Class 'King Class Mawe'

Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akiwa na mashabiki wake

MRISHO MPOTO NA BENDI YA MJOMBA BAND KUFANYA KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA




1Msanii wa ngoma za asili na Mkurugenzi wa bendi ya Mjomba Band Mrisho Mpoto akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kinondoni Mkwajuni wakati alipotangaza kuhusu kundi lake kuanza kampeni kubwa ya kuhamasisha wananchi kuhusu usafi wa mazingira mijini na vijijini kwa kunawa mikono na sabuni, kujenga na kutumia vyoo bora na kuboresha mzingira kwa ujumla ili kuhakikisha elimu hiyo inawafikia walengwa kwa kubadili tabia na njia mbadala za mawasiliano kuhusu elimu hiyo, Upatikanaji wa maji safi na salama na usafi wa mazingira bado ni tatizo kubwa kwa watanzania walio wengi, mwaka 2010 aslimia 9 tu ya wananchi waishio vijijini na asilimia 22 ya wananchi waishio mijini waliweza kupata huduma bora za usafi wa mazingira. kati ya sababu zingine , ni watu kutozingatia faida za usafi wa mazingira Katika k kampeni hiyo Mrisho Mpoto na kundi lake la mjomba Bandi wanashirikiana kwa pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, kushoto ni Mariam Mahamudu Afisa Afya, Mazingira Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii , Kampeni hiyo itaanza na mikoa ya Dodoma, Mara, Njombe, Rukwa na Tanga kabla ya kuendelea mikoa mingine 2Mariam Mahamudu Afisa Afya, Mazingira Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii akizungumza katika mkutano huo kuzungumzia kuhusu kampeni hiyo, kulia ni Mrisho Mpoto Mkurugenzi wa Mjomba Band.

JUMA FUNDI VS NASIBU RAMADHANI KUPAMBANA SIKU YA IDI PILI



Bondia Juma Fundi kushoto akitunishiana isuri na Nasibu Ramadhani wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika sikukuu ya Idi pili wengine kushoto ni mratibu Duni Lianjara Promota wa Mpambano huo Side Mkigoma na kocha wa Nasibu Christpher Mzazi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
PROMOTA WA MPAMBANO WA MASUMBWI SIDE MKIGOMA KATIKATI AKIWAINUA MIKONO JUU MABONDIA JUMA FUNDI KUSHOTO NA NASSIBU RAMADHANI
Mabondia wakisaini mkataba