Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, October 3, 2013

BLOG MPYA MAALUM KWA VIDEO A BONGO TU - ONLY FOR BONGO VIDEO'S







KUTOKA KAPITALI ONLINE MARKETING & ADVERTISING COMPANY INAWALETEA BLOG HII MAALUM KWA AJILI YA MUSIC WA BONGO TU ,LIVE SHOW ZA WASANII WA BONGO NA INTERVIEW ZAO
UKITEMBELEA BLOG HII UTAWEZA KUPATA VIDEO ZOTE KALI ZA BONGO
NA MATUKIO YANAYOHUSU WASANII KWA VIDEO
KWA WASANII WANAOHITAJI VIDEO ZAO ZIWEKWE KWENYE HII BLOG WANAWEZA WASILIANA NASI KWA
EMAIL: videozabongo@gmail.com

Maskini Niyonzima! Umeme wamtia hasara kwa kuunguliwa na vitu nyumbani kwake Magomeni Kondoa




Baadhi ya vitu vilivyoungua ndani ya nyumba ya Haruna Niyonzima wa klabu ya Yanga.
Nyumba anayoishi Haruna Niyonzima ambayo ilipatwa hitilafu ya umeme na kuuguza baadhi ya vitu kabla moto huo kuzimwa usilete madhara zaidi. Tukio hilo limetokea leo asubuhi jijini Dar.

Haruna Niyonzima akiwa nje ya nyumba yake hiyo.
Kiungo Haruna Niyonzima akiwa nje ya nyumba yake iliyonusurika kuteketea kwa moto uliozuka ghafla majira ya asubuhi ya leo.
NYOTA wa klabu ya Yanga, Haruna Niyonzima asubuhoi ya leo ameunguliwa nyumba yake iliyopo Magomeni Kondoa kwa kile kilichoelezwa hitilafu ya umeme ambapo baadhi ya mali zake ziliungua kabla ya kuokolewa.
Inaelezwa kuwa moto huo ulizuka wakati wakiwa wamelala na kwa bahati mfanyakazi wake wa ndani alikuwa ameshamka na kuona tukio kabla ya kutoa taarifa na kufanyika juhudi za kuuzima moto huo ulioungua masofa na samani nyingine za mwanandinga huyo.
Hata hivyo ni heri hakukuwa na madhara yoyote kwa wakazi wa nyuma hiyo zaidi ya mali zilizoungua ambazo hata hivyo bado hazijafahamika thamani yake.

Kikosi cha Usalama Barabarani chaendesha ukaguzi wa magari kwa wafanyakazi wa Airtel



Koplo Jumaa Mwalimu wa Kituo cha Polisi Oysterbay akikagua gari la mmoja wa wafanyakazi wa Airtel,  Bi. Susan Kajubili wakati  kikosi hicho, kilipoendesha zoezi la ukaguzi wa magari kwa wafanyakazi Airtel katika kutimiza lengo la wiki ya Nenda kwa usalama barabarani, liliyofanyika katika makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
Koplo Jumaa Mwalimu akikagua tairi la gari la mmoja wa wafanyakazi wa Airtel, James Majwala.
Mkaguzi wa Polisi Bw. Serengeti akiingia katika moja ya gari la mfanyakazi wa Airtel, Bi. Aminata Nakieta tayari kwa ukaguzi.

ZIARA YA WAZIRI MKUU WILAYANI KAKONKO - KIGOMA




Waziri Mkuu, MIzengo Pinda  akitazama  bunduki, risasi na  silaha mbalimbali  zinazolipuka vilivyokamatwa na  Jeshi la polisi  mkoani Kigoma kutoka kwa watu waliokuwa wakizilmiki kinyume cha sheria, Oktoba 2, 2013. Vifaa hivyo  viko kwenye Makao Makuu ya Polisi ya mkoa huo. Mheshimiwa Pinda yuko katika ziara ya siku sita mkoani Kigoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,  Mizengo Pinda  akiweka jiwe la Msingi la Hoteli ya  CMG Motel  wilayni Kakonko akiwa katika ziara ya mkoa  wa Kigoma Oktoba 2, 2013. Kushoto ni mmiliki wa Hoteli hiyo Mwita Gachuma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akifurahia kigoda  alichozawadiwa na wakazi wa wialya ya Kakonko  kabla ya kuwahutubia katika mkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Oktoba 2, 2013. Kushoto ni Mzee Mohamed Ismail ambaye alimkabidhi zawadi hiyo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiagana na wananchi wa wilaya Kakonko wilayani  humo akiwa katika ziara ya  mkoa wa Kigoma Oktoba 2, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

IRINE UWOYO AMSHINDILIA MWANAWE MIPOMBE




Picha aliyoipost mtandaoni Staa wa filamu za Kibongo,Irene Uwoya ikimuonyesha mtoto wake Krish Ndikumana akiwa ameshika glasi ya pombe imemfanya msanii huyo ashambuliwe baada ya mashabiki wake kutoa maoni kwamba hapaswi kufanya hivyo kama mzazi na kioo cha jamii kwani anamfundisha tabia mbaya mtoto wake huyo.…cio malezi ata kama ameshika au kunjwa kabisa. b a good mother….Huku mwingine akicomment ….Ayaaa atapombeka huyo

WADAU wa mambo ya utamaduni na michezo wameombwa kujitokeza kwa wingi


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WADAU wa mambo ya utamaduni na michezo wameombwa kujitokeza kwa wingi kufanikisha kufanyika kwa Tamasha la Utamaduni lililopangwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Mratibu wa Tamasha la Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga, Kambi Mbwana, pichani.
Hayo yamesemwa na mratibu wa tamasha hilo, Kambi Mbwana, alipozungumza na mwandishi wa mtandao huu mapema leo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya kutangaza mipango ya kuandaa tamasha hilo la aina yake na lenye mguso wa kuwakutanisha wadau wote kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo, Mbwana alisema endapo wadau wote, wakiwamo wafanyabiashara na wamiliki wa kampuni, taasisi za serikali watashirikiana katika hilo, mambo yatakuwa mazuri.
Alisema hali hiyo inamfanya aone haja ya kuwataka watu hao washirikiane kwa pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tamasha la utamaduni na michezo Handeni linafanyika kwa mafanikio na kuweka historia mpya.
“Watu wote wana umuhimu katika kufanikisha kwa tamasha hili, hivyo kila mmoja kwa nafasi yake tunaomba msaada wake hata wa kimawazo, ukizingatia kuwa kinachofanyika kwa sasa ni kuachiana majukumu tu.
“Tunawaomba wote wenye moyo wa kufanikisha wazo hili tushirikiane nao kwa namna moja ama nyingine, hasa kwa kuona wenye kampuni zao, mashirika na taasisi za serikali pia kutudhamini katika hili,” alisema Mbwana.
Kwa mujibu wa Mbwana, kufanyika kwa tamasha hilo kutakuwa ni sehemu nzuri ya kuwakutanisha wadau, wananchi wa Handeni na Tanzania kwa ujumla kwa ajili ya kujadiliana changamoto zinazowakabili kwa maendeleo yao.
Tamasha hilo la Utamaduni linaandaliwa chini ya Raha Company and Entertainment huku likifanyika kwa mara ya kwanza katika wilaya hiyo inayoongozwa na Mkuu wake wa Wilaya Muhingo Rweyemamu, wakati mbunge ni Dk Abdallah Omari Kigoda ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara.

KOCHA RAJABU MHAMILA SUPER D AKIWA KATIKA MAPAMBANO YAKE KABLA YA KUA KOCHA






Kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila (Super D) kushoto akitangazwa mshindi zida ya bondia Safari Berdard kipindi hicho

Super D Boxing Coach kushoto Akipambana na Rashidi Ali

Super D Boxing Coach kulia akipambana na Ajibu Salumu
Salam alykum kaka kwenye maktaba yangu ya picha nimekutana na picha hizo kaka si vibaya ukawakumbusha bondia machachari aliekuwa anasimamisha mashabiki vitini awapo ulingoni asante kwa ushirkiano wako tupo pamoja
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

MPAMBANO WA MASUMBWI KUFANYIKA PANANDI PANANDI ILALA OKTOBA 26




MPAMBANO mwingine wa masumbwi kufanyika katika ukumbi wa panandi panandi Oktoba
26 mpambano huo wa mchezo wa masumbwi utakaokuwa chini ya uratibu wa Kinyogoli Fondition utawakutanisha mabondia mbalimbali wenye majina na wanaotamba kwa sasa katika anga za masumbwi nchini

Akizungumzia mchezo huo kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini kutoka kambi ya ilala Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mpambano huo utawakutanisha bondia Yakubu Maganga atakae zichapa na Ubwa Salumu katika uzito wa kilo 75 huku Seif Ali akipambana na Hassani Labanda

pamoja na mipambano mengine ya masumbwi itakayo wakutanisha mabondia mbalimbali

Siku hiyo kutakuwa pia na huzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama.Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
 
DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
 
Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa  zawadi kwa mabondia na Kocha Super D  ambaye ame haidi kutoa, Gum Shit ,Clip Bandeji,DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta,Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakao onesha uwezo wa ali ya juu wa kutupiana masumbwi

Wednesday, October 2, 2013

MPAMBANO WA MASUMBWI KUFANYIKA PANANDI PANANDI ILALA OKTOBA 26


MPAMBANO mwingine wa masumbwi kufanyika katika ukumbi wa panandi panandi Oktoba
26 mpambano huo wa mchezo wa masumbwi utakaokuwa chini ya uratibu wa Kinyogoli Fondition utawakutanisha mabondia mbalimbali wenye majina na wanaotamba kwa sasa katika anga za masumbwi nchini

Akizungumzia mchezo huo kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini kutoka kambi ya ilala Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mpambano huo utawakutanisha bondia Yakubu Maganga atakae zichapa na Ubwa Salumu katika uzito wa kilo 75 huku Seif Ali akipambana na Hassani Labanda

pamoja na mipambano mengine ya masumbwi itakayo wakutanisha mabondia mbalimbali

Siku hiyo kutakuwa pia na huzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama.Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
 
DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
 
Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa  zawadi kwa mabondia na Kocha Super D  ambaye ame haidi kutoa, Gum Shit ,Clip Bandeji,DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta,Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakao onesha uwezo wa ali ya juu wa kutupiana masumbwi

Simba kuivaa Yanga bila First Eleven




Wachezaji wa Simba wakijifua asubuhi ya leo
Chollo, Adeyum saleh na wenzao wakijifua
Kwa tizi hizi Ruvu Shooting atoke salama Jumamosi...Mawe....!
Ramadhani Singano 'Messi' naye alikuwepo
Dua ni muhimu iwe kabla au baada ya mazoezi, vijana wa Simba wakiwa na benchi lao la ufundi likimshukuru Mungu kwa kumaliza salama mazoezi yao ya leo asubuhi
KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Abdallah Kibadeni 'King Mputa' amesema bado hajapata kikosi chake cha kwanza (First Eleven) cha timu yake, japo anaridhishwa na baadhi ya wachezaji kwa namna wanavyojituma mazoezi na uwanjani na kuisaidia timu.
Hata hivyo alisema anatumaini baada ya mechi nne zijazo atakuwa ameshafanikiwa kukipata kikosi hicho kwani alijiwekea lengo hilo ndani ya mechi 10 za Ligi Kuu Tanzania Bara inayozidi kushika kasi.
Kwa maana ni kwamba Simba itaikabili Yanga Oktoba 20 ikiwa bado haijapata kikosi chake cha kwanza.
Akizungumza kwenye mazoezi ya timu hiyo leo asubuhi, Kibadeni alisema bado hajafanikiwa kupata kikosi chake cha kwanza cha kukitegemea kwa vile anaendelea kuwaangalia nyota wake, ambapo alikiri wapo wanaomkuna kwa umahiri wao.
Kibadeni alisema kwa kuwa alijiwekea lengo la kukipata kikosi hicho katika mechi 10 anatarajia baada ya mechi nne kuanzia ile ya Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting, Prisons-Mbeya, Yanga na Coastal Union.
"Bado sijapata kikosi cha kwanza kwa sababu nilishatangaza tangu awali nitatumia mechi 10 kupata kikosi hicho na ndiyo kwanza tupo mechi ya sita, nadhani baada ya mechi nne zijazo ndipo nitakuwa na uhakika wa kikosi hicho, ila vijana wanajitahidi," alisema.
Kocha huyo mwenye rekodi nzuri nzuri kwa Simba na Tanzania kwa ujumla, aliizungumzia mechi yao ijayo dhidi ya Ruvu Shooting na kukiri itakuwa ngumu kama ilivyokuwa kwa JKT Ruvu kwa vile karibu timu zote za majeshi zinafanana, ila anashukuru baadhi ya nyota wake waliokuwa majeruhi wameanza kurejea uwanjani na kutumaini huenda akawatumia katika mchezo huo.
Wachezaji hao waliokuwa miongoni mwa majeruhi na jana walishiriki mazoezi ni kiungo Henry Joseph na beki wa pembeni Issa Rashid 'Baba Ubaya'.
"Nashukuru baadhi ya nyota wangu waliokuwa majeruhi wamerejea uwanjani na nina tumaini kuwatumia katika mechi ijayo dhidi ya Ruvu Shooting, japo nitaendelea kuwakosa Miraji Adam na Abdallah Seseme bado wanaendelea kujiuguza," alisema.
Kuhusu ushindani katika Ligi Kuu ya msimu huu, Kibadeni alisema ni mkubwa na ndiyo maana hata kwenye msimamo timu zimepishana kwa idadi ndogo ya pointi kitu alichosema kinafanya ligi isisimue na kutabiri siyo rahisi bingwa kutangazwa mapema kama ilivyokuwa mwaka jana.
"Ligi ni ngumu na ina ushindani mkubwa na karibu timu zote zimejizatiti  kunipa raha na hasa ikizingatiwa kuwa ligi ni ngumu na ina ushindani mkali kama ilivyokuwa msimu uliopita," alisema Kibadeni.

Tambwe atamba, 'Yanga kitu gani bwana, nitawatungua tu Okto 20'





Amisi Tambwe (kulia) akishangilia mabao yake na Betram Mombeki
MSHAMBULIAJI nyota wa Simba, Amissi Tambwe ameitumia salamu Yanga akiiambia kwamba ikae chonjo kwa ajili ya pambano la watani wa jadi wa soka nchini litakalofanyika Okotba 20, akiahidi kuwatungua ili kuendeleza rekodi yake ya mabao.
Mrundi huyo aliyesajiliwa Simba akitokea Vital'O ya Burundi alisema kwa vile lengo lake ni kufikisha idadi ya mabao 20 mwishoni mwa msimu kitu yoyote itakayokutana na Simba bila kujali kama ni Yanga au Ashanti United akili yake itakuwa kwenye kufumania nyavu tu.
Akizungumza na MICHARAZO leo mara baada ya mazoezi ya klabu yake uwanja wa Kinesi, Tambwe alisema licha ya kwamba hajaiona Yanga ikicheza katika msimu huu, bado anaichukulia kama timu nyingine zilizokutana na Simba ambapo hujitahidi kufunga mabao kwa lengo la kuisaidia timu yake kadhalika kutimiza lengo la kufunga jumla ya mabao 20.
"Sijabahatika kuwaona Yanga wakicheza tangu nitue nchini, lakini nafahamu ni timu kubwa na wapinzani wakubwa wa Simba, lakini hilo mimi sijali siku tutakayokutana nitakuwa na kazi moja tu ya kuwafunga kama ninavyozifunga timu nyingine," alisema.
Alisema yeye awapo dimbani akili zake ni namna ya kujipanga ili kufunga mabao kitu ambacho kimemsaidia kutwaa tuzo kadhaa za ufungaji bora katika ligi yao ya nyumbani na ile ya Kombe la Kagame, kitu anachotaka kitokee pia katika Ligi Kuu ya Tanzania.
Mshambuliaji huyo ambaye alishindwa kuendelea kufanya mazoezi na wenzake kwa kile alichoeleza kusumbuliwa na tumbo, alikiri ligi ya Tanzania ni ngumu na yenye ushindani mkali akidai karibu timu zote zilizocheza na Simba zilionekana kuwakamia kitu anachotarajia hata katika mechi ijayo dhidi ya Ruvu Shooting itakayoyochezwa Jumamosi.
"Ligi ni ngumu na ina ushindani mkubwa, siowezi kusema kuna timu iliyoonekana tishio zaidi ya nyingine ila zote zinacheza kwa malengo na kukamia zaidi, tunashukuru tunaoongoza katika msimamo mpaka sasa," alisema.
na karibu timu zote zina upinzani mkali huku akidai mpaka sasa katika mechi tano alizocheza hawezi kusema timu ipi ilikuwa kali zaidi Mchezaji huyo ndiye anayeoingoza orodha ya wafungaji kwa sasa katika ligi akiwa na mabao saba kutokana na mechi tano alizocheza kwa vile mechi ya awali ya fungua dimba kati ya Simba na Rhion Rangers alikuwa bado hajaruhisiwa kucheza nchini..

TANGAZO LA DAWA YENYE NGUVU Piga simu 0755875884, O713827689









DAWA YA NGUVU ZA KIUME NA MSIMKO KWA WANAWAKE WASIO NA HAMU YA TENDO LA NDOA AMBAYO HULETA MSISIMKO KWA WANAUME NA WAKE WAKUTANAPO.KWA SASA INAPATIKANA KWA BEI NAFUU HAPA JIJINI DAR ES SALAAM MAKUTANO YA MTAA WA KIPATA NA BARABARA YA MSIMBAZI
ALLY WA YANGA BOMBA UHURU NA MSIMBAZI 0787230551 AU 0652755838


PIGA NO O713827689, 0755074505 , au 0719 541366
,0652755838 UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM

BUGURUNI LOZANA STENDI YA TAX ULIZIA ADAMU KIBANDANI 0755875884
SHULE YA UHURU FIKA JENGO LA AZAM BAKHRESA ULIZA NGAEJA 0715110900

KARIAKOO SHULE YA UHURU STENDI YA MABASI YA TANDIKA ULIZIA ZUNGU MUHUZA TIKETI 0712743870 
0787406938

NA UKIWA ILALA SHARIF SHAMBA FIKA DSJ BANDA NAMBA 14 SIMU 0718718671

NA UKIWA KOTA ZA BANDARI KARIAKOO FIKA MKUNGUNI KIBANDANI KWA HUSEIN 0753893295

MWANANYAMALA FIKA JABA KLABU ULIZA MACHELLAH 0713470492
ENZOY INALETA HESHIMA

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHINI DK EMMANUEL NCHIMBI, MKURUGENZI WA IOM KANDA YA AFRIKA MASHARIKI NA PEMBE YA AFRIKA USO KWA USO JIJINI DAR ES SALAAM LEO




 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimfafanulia jambo Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Wahamiaji (IOM) Kanda ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, Ashraf El Nour alimpomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Kiongozi huyo wa IOM alifika ofisini kwa Dk Nchimbi kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ya wahamiaji. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Wahamiaji (IOM) Kanda ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, Ashraf El Nour alimpomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ya wahamiaji. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa IOM nchini, Damien Thuriaux. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimshukuru Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Wahamiaji (IOM) Kanda ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, Ashraf El Nour kwa kumtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ya wahamiaji. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa IOM nchini, Damien Thuriaux. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI.WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

SWAHILI TV TELEVISION YAKO YA KIZALENDO ILIKUWEPO KATIKA KUHAKIKISHA MATUKIO YOTE YANAWEKWA KATIKA KUMBUKUMBU MUHIMU ZA VONGOZI WETU




Mhe. Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba akijibu kwa ufasaha na kwa ustadi mkubwa kabisa maswali kutoka kwa wananchi waliohudhuria Mkutano wa Maendeleo ya Nchi yetu uliofanyika DMV Jumapili Sept 29,2013
 Liz Haynes akifuatilia Mkutano kwa Makini

 Mh. Mwigulu akifafanua jambo katika Mkutano wake na Watanzania DMV

 Mhe. Naibu Katibu Mkuu CCM Mwigulu Nchemba aliruhusu kila swali liulizwe na aliyajibu yote kwa ufasaha na kwa ustadi mkubwa hakuna mwananchi aliyerudi na dukuduku nyumbani. Pichani Kulia aliyeketi ni Msaidizi wa Rais Bw. Rajab Luhwavi

 Dada Georgina Lema akiuliza Maswali yake kwa hisia kali

TAMBUA DALILI ZA MWANAMKE ANAETOKA NJE YA NDOA



           Wataalamu wa maswala ya mahusiano wanaamini kwamba, mwanamke anapotoka nje ya ndoa yake, inakuwa rahisi sana kubainika au kufumaniwa kuliko ilivyo kwa mwanaume. 
Hii inatokana na ukweli kwamba, hisia zinakuwa na nafasi kubwa sana kwa mwanamke, kwani mwanamke huishi kwa hisia zaidi kuliko mwanaume. Bado nasisitiza kwamba, haipaswi na siyo sahihi mtu kuchukulia dalili hizi kama ushahidi wa mpenzi wake kutoka nje ya ndoa.  Uchunguzi wa kina kufuatia dalili hizi ni muhimu sana.

 Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya dalili zinazoweza kuonyeshwa na mwanamke ambaye anatoka au yupo kwenye harakati za kutoka nje ya ndoa yake:

 1. KUCHELEWA: Kuna wakati mwanamke anaweza kuaga kwamba anakwenda saluni au kusuka, badala ya kurejea kwa muda ambao umezoeleka, anachukua muda mrefu hata mara tatu zaidi. kuna wakati kwenda sokoni huchukua saa kadhaa bila kujali soko liko umbali gani. Kama ni mara moja sawa, lakini ikishakuwa zaidi ya mara moja huenda kuna tatizo la kukosa uaminifu.

 2. KUBADILI MAENEO: Hebu chukulia kwamba, mwanamke amezoea kwenda soko fulani la karibu, hospitali fulani ya karibu, saluni fulani ya karibu na hata nyumba fulani ya ibada ya karibu. Unapoona anahama maeneo ya karibu ya huduma na kwenda ya mbali, bila sababu ya msingi, huna budi kuanza kutuhumu mwenendo mbaya.
 Siyo lazima kuhama kokote kuwe na mwenendo mbaya, lakini kama kuhama kwenyewe kunatia shaka kwa sababu maelezo ya kuhama huko hayana msingi, mwanaume ana kila sababu ya kuchunguza kama hakuna usaliti unao anywa.

 3. UNUNUZI USIO WA KAWAIDA: Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake kwa ajili ya kupata fedha, basi atakuwa na mabadiliko makubwa katika mtindo wake wa manunuzi. 
 Atakuwa ananunua vitu vya thamani kubwa kuliko uwezo wake, atakuwa na fedha nyingi tofauti na ambazo angekuwa nazo na pengine kumiliki mali kama nyumba kwa siri.

4. KUANZISHA VURUGU: Kuna wakati mwanamke anayetoka nje ya ndoa huanzisha vurugu za makusudi na mumewe. Lengo la kuanzisha vurugu hizo ni ili apate nafasi ya kujifanya amezira na kuondoka nyumbani kwa muda. 

Huo muda anapoondoka nyumbani kujifanya kakerwa na vurugu hizo ndiyo muda ambao anautumia kwenda kwa hawara yake.

 5. KUSITISHA UAMINIFU: Mwanamke anayetoka nje ya ndoa, mara nyingi husimamisha kumwamini mumewe, yaani hayuko tayari kushiriki masuala ya siri, ambayo wanandoa huwa wanashiriki. 

 Husita kumshirikisha mumewe kwenye mambo yake mengi. Lakini pia husita kumuomba mumewe ushauri, kama alivyokuwa akifanya siku za nyuma.

 6. KUACHA KUVAA PETE: Kuna sababu nyingi ni kwa nini mwanamke anaweza kuacha kuvaa pete yake ya ndoa. Moja ya sababu hizo ni kusalitiwa na mumewe au ndoa yake kuwa kwenye misukosuko mikubwa sana. 
 Lakini nje ya misukosuko mikubwa ya ndoa, sababu nyingine inayoweza kumpelekea mwanamke kuvua mara kwa mara au moja kwa moja pete yake ya ndoa, ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa yake.
7. KUONESHA WASIWASI: Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake , ni lazima atakuwa na wasiwasi na mashaka yasiyo na sababu mbele ya mume wake. 

 Anaweza kuonesha kutotulia kwa aina fulani kana kwamba, anahofia kuna siri itatoka au kuna kitu ambacho tayari mume wake anakijua dhidi yake. Mara nyingi wasiwasi na mashaka humtawala sana mwanamke anayetoka nje , hasa katika hatua zake za awali za kutoka nje.

 8. KUZUNGUMZIA KUACHWA: Kuna wakati mwanamke anaweza kuwa anatoa kauli za kuonesha kwamba, kama mwanaume anaona vipi , wanaweza kuachana. 
 Kama kila penye ugomvi kidogo tu mwanamke anakimbilia kusema, “kama ni kuachana, tuachane tu” hiyo inaweza kuwa ni dalili mbaya kwa mwanamke anayetoka nje ya ndoa kwa sababu hana tena upendo na mumewe

TAZAMA TUKIO ZIMA LA WAFANYA BIASHARA KUGOMA KUNUNUA MASHINE ZA TRA ZENYE THAMANI YA THS 800,000 JIJINI MBEYA, MADUKA YAFUNGWA.




 Polisi wakiwa katika ulinzi mkali 
 Maduka yakiwa yamefungwa 
 Wafanya biashara wakiwa uwanjani kungoja kusikiliza nini  hatma yao
 Baadhi ya watu wakiwa wanakimbia Baada ya Mabomu ya machozi kuanza kurushwa kuepusha vurugu
 Mawe yakiwa yamepangwa kuzuia magari yasiende kokote
 Maduka yote yakiwa yamefungwa eneo la mwanjelwa kupinga ununuzi wa mashine hizo za TRA
 Vijana hawa wakiwa wana nawa uso baada ya Bomu la machozi kuwapitia 
 Jiwe kubwa likiwa limewekwa katika Barabara magari yasipite
 Hali tete Tayari vijana wameanza kuchoma mataili.....