Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

Friday, June 1, 2012

REAKING NEWS: BONDIA MAGOMA SHAABAN AFARIKI DUNIA





BINGWA wa zamani wa dunia wa ngumi za kulipwa uzito wa Super Fly, aliyekuwa akitambuliwa na WBU, Magoma Shaaban Ngereza amefariki dunia usiku huu katika hospitali ya Bombo, mkoani Tanga, imeelezwa.
Bondia maarufu wa zamani nchini, Ally Bakari ‘Championi’ amesema, Magoma aliyezaliwa Oktoba 21, mwaka 1980 mjini Tanga, amefariki majira ya saa 12 jioni.
Championi alisema kwamba Magoma alikuwa anaumwa kwa muda mrefu na siku nne zilizopita alizidiwa na kukimbizwa katika hospitali hiyo, kabla ya umauti kumfika leo.
Hadi anafariki dunia, Magoma (pichani kushoto) alikuwa amepigana jumla ya mapambano 16, akishinda 13, manane kati ya hayo kwa Knockout (KO), amepigwa matatu na yote kwa KO na hakuwahi kutoka sare.
Magoma alipanda ulingoni kwa mara ya mwisho Julai 21, mwaka 2006 na Eugen Sorin Tanasie mjini Timisoara, Romania katika pambano ambalo alipigwa kwa Technical Knocout (TKO) raundi ya pili.
Taji lake la kwanza kutwaa lilikuwa ni la IBF Afrika, Septemba 12, mwaka 1998 akimpiga Mkenya Joseph Waweru kwa KO raundi ya kwanza, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mei 11, mwaka 2000 alimpiga bondia ‘matata sana’ Totin Lukunim wa Thailand na kutwaa taji la IBF Intercontinental, uzito wa Super Fly kwenye ukumbi wa PTA, Temeke, Dar es Salaam.
Agosti 3, mwaka 2001 ndipo alitwaa ubingwa wa dunia wa WBU baada ya kumpiga Ferid Ben Jeddou wa Tunisia kwa TKO raundi ya sita mjini Avezzano, Abruzzo, Italia, kabla ya kupoteza taji hilo kwa kupigwa na Gabula Vabaza Julai 26, mwaka 2002 katika ukumbi wa Hemingways Casino, East London, Eastern Cape, Afrika Kusini kwa KO raundi ya kwanza.
Mei 25, mwaka 2003 alipigwa na Mtanzania mwenzake, Mbwana Matumla kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam kwa TKO raundi ya nne.
Alijiunga rasmi na ngumi za kulipwa mwaka 1996, pambano lake la kwanza akicheza Juni 3, mwaka huo na kumpiga Athumani Omari kwa pointi, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mungi aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.

MABONDIA WA TANZANIA WAWEKWA KATIKA VIWANGO VYA KIMATAIFA



Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi cha Marekani (IBF/USBA) limewaweka mabondia wa Tanzania katika orodha ya viwango .
 
Mabondia hawa ambao watakuwa miongoni mwa mabondia 15 bora duniani katika uzito wao ni:
 
Francis Miyeyusho, Fadhili Ramadhani, Mbwana Matumla, Seba Temba, Allan Kamote, Pascal  Bruno na Francis Cheka.
 
Katika kikao cha Kamati ya Viwango (Ratings Committee) ambacho kilikaa jana chini ya Uenyekiti wa William James, IBF/USBA iliridhishwa na viwango vya mabandia wa Kitanzania na kutoa ahadi kuwa watawaangalia kwa karibu zaidi katika kipindi cha mwaka mmoja ujao ili kuwaongeza katika orodha ya viwango.
 
Hii ina maana kuwa mabondia hao waliowekwa kwenye orodha ya viwango vya IBF vya mabara wanaweza kupigania ubingwa wa IBF wa Afrika na mabara wakati wowote.
 
Afrika, Mashariki ya Kati ya Ghuba ya Uajemi iliwakilishwa kwenye kikao hicho na Rais wake Onesmo Ngowi toka Tanzania. Katika vikao hivi vya viwango ni Marais wa mabara na viongozi wakuu wa IBF wanaohudhuria peke yao.
 
Ngowi aliwapendekeza pia mabondia kadhaa wa Kenya, Uganda, DRC, Afrika ya Kusini, Namibia, Zimbabwe, Mali, Gabon, Benin, Bukina Faso, Ghana, Nigeria, Morocco, Cameroon, Ivory Cost, Tunisia, Misri, Dubai na Jordan.
 
Kumekuwepo na uchakachuaji mkubwa wa rekodi za mabondia katika bara la Afrika kwa mapromota na mawakala wa ngumi kuweka viwango vya mapambano ya uongo katika rekodi za mabondia wao kweney mtandao wa Boxrec. Hii inawapa wakati mgumi sana mabondia wa Kiafrika kupata mapambano ya ngumi ya kimataifa.
 
Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi inaongozwa na rais wake Onesmo Ngowi wa Tanzania.

SUALA LA AFYA YA UZAZI SALAMA LIPEWE KIPAUMBELE MCHAKATO WA KATIBA MPYA



Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Mwanasheria Tike Mwampipile akizungumza na washiriki wa semina ya mapendekezo ya kuwepo kwa   sheria ya Afya ya Uzazi Salama  katika mchakato wa maoni ya kuandikwa kwa Katiba Mpya iliyomalizika jana kwenye ukubi wa hoteli ya Blue Pear Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.
 
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO

JAMII iimeshauriwa kulipa kipaumbele suala ya mapendekezo ya kuwepo kwa   sheria ya Afya ya Uzazi Salama  katika mchakato wa kuwepo kwa Katiba Mpya , ambayo itawezesha watumishi wa afya ambao watasababisha vifo vya wakinamama wajawazito  au watoto wachanga kwa sababu za uzembe.
Kauli hiyo iliyoilitolewa (jana) na Mkurugenzi wa Mtendaji  wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA), Tike Mwampipile,   wakati  akifafanua ya mapendekezo  hayo  iliyoandaliwa  na chama hicho kwa waandishi wa habari kwenye semina ya siku mbili iliyofanyika , Ubungo Plaza jijiini Dares Salaam.Semina ya mafunzo hayo  ambayo iliyoanza jana  (juzi) na kumalizika leo(jana)
“ Wito wangu katika jamii ni ni ina wajikubu mkubwa wa kujua haki zao za msingi na kufahamu wapi pa kuzipata. Afya ya Uzazi Salama ni kitu muhimu ambacho hakijangaliwa kwa umakini. Hivyo katika mchakato wa Katiba Mpya suala hili liangaliwe kwa uzito kwa  na upana wake kujali mama ambaye analemta mtoto hapa duniani  ambaye anaweza kuwa na  Rais au Waziri Mkuu wa kesho,” alisema   Mwampipile.
 Aliongeza kuwa kuwepo kwa sheria hiyo kutasaidia kupunguza  idadi ya vifo vya wakinamama wajawazitio na watoto wachanga.
Kwa upande wake mtoa mada wa mapendekezo hayo,  Bernadetha Mkandya ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya TAWLA na Wakili wa Kujitegemea alisema  kuwa mwanamke ana haki ya   kuishi na kulindwa ,hivyo sheria hiyo italuiwezesha taifa kupata watoto waliolelewa katika mazingira bora na afya njema.   .
“ Tunataka tuwe na sheria ya iyatomlinda mwanamke wakati wa ujauzito na siku 42 baada ya kujifungua,”  ikiwepo kupanga idadi ya watoto atakaoweza kuwalea na muda wa kupata mtoto mmoja baada ya mwingine alisema.  
 Akifafanua zaidi kuhusu sheria hiyo alisema  itamwezesha mamamjamzito kupata huduma za afya ya uzazi salama bora na ambazo zitamwezesha kupata vifaa tiba vinavyotakiwa bila gharama yeyote.
Aidha Mkandya aliongeza katika sheria hiyo wamapendekeza kuwa umri wa uti mzima uwe ni miaka 18 ili kuwezesha mtoto wa kike kuolewa katika umri unaotakiwa hatua ambayo itasaidia kupunguza athari za afya ya uzazi  zinazotokana na umri mdogo. Alisisitiza kuwa ni muhimu kwa makundi yote katika jamii kushiriki katika kutoa maoni ya mchakato huo.
Mkandya aliongeza kuwa mapendekezo hayo  hayo yanaelekeza kuwepo kwa sheria ambayo itamwezesha mama mjamzito kusitisha ujauzito pale itakapogundulika kuwa unasabbaisha athari za kiafya kwa ruhusa ya daktari na ridhaa yake  au endapo atakuwa amebakwa na  kwa ridhaa yake kuwa hana uwezo wa kuendelea hudumia ujauzito huo na kumlea mtoto  pale atakapojifungua.
Pia ridhaa hiyo inaweza kutolewa na ndugu zake endapo mama huyo ni mlemavu wa

MKUTANO WA 29 WA SHIRIKISHO LA NGUMI LA KIMATAIFA (IBF) WAANZA RASMI NCHINI MAREKANI.



Rais wa IBF duniani Daryl Peoples wa Marekani katikati akiwa amesimama na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi wa Tanzania pamoja na promota maarufu wa ngumi wa Thailand Jimmy  Chaichotchuang walipotembelea Pearl Habour tarehe 30 May, 2012.

Mkutano wa 29 wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) umeanza rasmi katika Hotel ya Hawaii Hilton Village Resort jijini Honolulu, Hawaii, Marekani tarehe 29 May, 2012. Mkutano huu ulianza rasmi saa 3 za asubuhi katika ukumbi wa kimataifa wa Atlatic International Conference Center, kwenye jengo la Rainbow Towers katika hotel hii ya nyota tano.
Tarehe 29 ilianza kwa wajumbe wa mkutano huo kujiandikisha kuanzia saa 3 za asubuhi mpaka saa 11 jioni. Jioni wajumbe wote walikuwa na cocktail party ya get together katika ukumbi wa Rainbow Towers.
Mkutano huu unahudhuriwa na wajumbe 6000 toka nchi 204 duniani kote. Ujumbe wa Afrika ni moja ya ujumbe unaoshiriki katika mkutano huu maalum wa kuafiki programu ya Utalii wa Michezo itakatowakilishwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi.
Akiwakaribisha wajumbe walioanza kumiminika katika mkutano huo Rais wa IBF duniani Daryl Peoples wa Marekani aliwataka wakaribie Marekani na kutumia muda walionao katika jiji la Honolulu kufahamiana na kutembelea jiji hili.
Ratiba ya siku tano itajumuisha kuwa tarehe 29 ni siku ya kuanza kwa mkutano huo kwa wajumbe kujiandikisha. Jioni kutakuwa na party ya kukutana na kufahamiana. Tarehe 30 kutakuwa na ziara ya kutembelea Pearl Habour bandari iliyoharibiwa na majeshi ya Japan mwaka 1941na kuifanya Marekani ijiingize kwenye vita ya pili ya dunia.
Tarehe 31 ni siku rasmi ya ufunguzi wa mkutano huo ambapo Rais wa IBF duniani Daryl Peoples wa Marekani ataufungua rasmi. Wajumbe wengine watakaohutubia ni pamoja na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi.
Wengine ni Lindsey Tucker ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Ubingwa wa IBF,  William James ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Viwango wa IBF.
Nao Lou Priluka ambaye ni Katibu wa bodi ya wakurugenzi wa IBF atazungumza pia. Aidha Al Maiyer ambaye ni Mwakamu wa Rais wa IBF atazungumza. Ray Wheatler ambaye anaiwakilisha IBF katika bara la Asia atazungumza.
Rarehe 1 Juni kutakuwa na semina ya Utibabu pamona na Marefari. Tarehe 2 kutakuwa na semina ya Majaji pamoja na programu maalum kwa IBF zitawakilishwa. Mkutano huu utafungwa rasmi tarehe 2 Juni na Mstahiki Meya wa jiji la Honolulu.
Imetumwa toka Honolulu, Hawaii, Marekani na;
Onesmo A.M.Ngowi
IBF/USBA President for Africa
President, Tanzania Professional Boxing Commission(TPBC)
Director, Commonwealth (English Empire) Boxing Council (CBC)
Coordinator, Moshi Sister Cities Committee
Coordinator, International Education and Resources Network (iEARN) to TANZANIA

BAADHI YA WAREMBO WATAKAOPANDA JUKWAANI KATIKA SHINDANO LA MISS NYAMAGANA JIJINI MWANZA LEO



Aisha.
HIZI NI BAADHI YA SURA  ZITAKAZOPANDA JUKWAANI USIKU WA LEO IJUMAA,  KATIKA SHINDANO LA  MISS NYAMAGANA 2012. KATIKA UKUMBI WA GOLD CREST JIJINI MWANZA.
SHUGHULI NZIMA INASIMAMIWA NA STOPPERS ENTERTAINMENT.
BURUDANI ITATOLEWA NA LINAH, DITTO NA HAFSA KAZINJA.
MSHEHERESHAJI MKUU AU MC WA SHUGHULI NZIMA NI MASANJA MKANDAMIZAJI KUTOKA KUNDI LA ORIGINAL KOMEDI.
Amina.
Brenda.
Cecy.
You might also like:

MKUTANO WA SHIRIKISHO LA NGUMI LA DUNIA IBF WAENDELEA HUKO HONOLULU MAREKANI



 
Rais wa IBF/USBA duniani Daryl Peoples wa Marekani kushoto akiwa amesimama na Rais wa IBF bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi siku ya ufunguzi wa mkutano huo tarehe 31 May, 2012.
Rais Peoplers aliwakaribisha wajumbe na kuwasomea taarifa ya mwaka ya IBF/USBA ambapo zaidi ya mapambano ya ubingwa 349 yalifanyika chini ya IBF/USBA mwaka jana. 
 
Mkutano huo ulihutubiwa pia na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi. Aidha mwakilishi wa IBF katika bara la Ulaya Roberto Reya wa Italia naye alihutubia mkutano huo.
 
Katika mkutano huo taarifa ya kifo cha bondia wa Thailkand Thangthong Kiattaweesuk aliyekuwa na miaka 35 kilitolewa rasmi. Bondia Kiattaweesuk alikufa katika ajali ya gari akiwa na mkewe, mtoto mmoja na ndugu yake baada tu ya kushinda pambano lililompa nafasi ya kupigana na bingwa wa IBF wa dunia katika uzito wa Feather Geoffrey Mathebula wa Afrika ya Kusini.
 
Kiattaweesuk alimpiga bondia wa Kenya Geofrey Munica kwa KO raundi ya 10 katika pambano la kugommbea mkanda wa mabara wa IBF.
 
Pamoja na ufunguzi huo leo kutakuwa na semina ya utibabu pamoja na semina ya majaji. Mkutano huo utamalizika tarehe 2 Juni.
 
Mkutano huu unahudhuriwa na wajumbe 6000 toka nchi 204 duniani kote. Ujumbe wa Afrika ni moja ya ujumbe unaoshiriki katika mkutano huu maalum wa kuafiki programu ya Utalii wa Michezo itakatowakilishwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi.

Msondo kukamua Kitunda Juni 10



NA MWANDISHI WETU

BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo ngoma inatarajia kuwapa burudani kabambe wakazi wa Kitunda na maeneo jirani kwa kufanya onyesho kwenye ukumbi mpya wa Msige Pub Juni 10, mwaka huu.
Mratibu wa onyesho hilo, George Msige, alisema kuwa maandalizi yamekamilika na amewataka wapenzi wa burudani kujitokeza kwa wingi kupata vionjo vya wakongwe hao.
Alisema amevutiwa kuialika bendi hiyo kutumbuiza kwenye ukumbi huo uliopo Kitunda Kibeberu, kutokana na maombi aliyopewa na mashabiki wengi baada ya kufurahishwa na 'shoo' ya kwanza ya kundi la taarab la Five Stars wiki mbili zilizopita.
"Kwa hiyo wakazi wa Kitunda Kibeberu kuanzia sasa watakuwa wanapata burudani ya kila aina kwa nia ya kukata kiu yao hivyo, wajiandae kucheza nyimbo za bendi ya Msondo," alisema Msige.
Alisema kuwa Msondo itapiga vibao vya zamani na vipya ambavyo ni Suluhu wa Shabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu na Baba Kibene wa Eddo Sanga.
Mwimbaji nguli Maalim Gulumo 'Kamanda' na Saidi Mabela na wengineo watafanya vitu vyao siku hiyo ili kukonga nyoyo za mashabiki wao.
Msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila 'Super D' amethibitisha Msondo itaangusha burudani ya nguvu katika ukumbi huo ikitokea Masasi, Mtwara kuzindua ukumbi wa Emirate.

MISS MTWARA KUFANYIKA JUMAMOZI JUNI 2 MJINI MTWARA



Warembo watakaopanda jukwani kushiriki katika shindano la  kumtafuta Miss Mtwara 2012 siku ya jumamosi juni 2 katika ukumbi wa Makonde Beach mjini Mtwara, ambapo wamekuwa wakiendelea na mazoezi katika ukumbi huo kujiweka tayari kwa ajili ya shindano hilo.
Warembo watakaopanda jukwani kumtafuta Miss Mtwara 2012 Wakimsikiliza mkufunzi wao Isabela mpada (MISS RUVUMA 2006) siku ya jumamosi Juni2 katika ukumbi wa makonde beach
Warembo watakaopanda jukwani kumtafuta Miss Mtwara 2012 Wakimsikiliza mkufunzi wao Isabela mpada (MISS RUVUMA 2006),Pamoja na muandaaji wa shindano Rajab Mchatta. siku ya jumamosi Juni 2 katika ukumbi wa makonde beach

SAFARI LAGER YATANGAZA TAREHE NA ZAWADI ZITAZOKABIDHIWA KWA WAJASILIAMALI WASHINDI WA “WEZESHWA NA SAFARI LAGER”.



  Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akionyesha baadhi ya vifaa vitavyokabidhiwa kwa wajasiliamali waliofuzu katika grogramu ya ruzuku ya “Wezeshwa na Safari Lager” Dar es Salaam jana.Vifaa hivyo vitakabidhiwa mwishoni mwa wiki katika viwanja  vya CCM Ilomba Mkoani Mbeya.
  Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari.
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi tarehe na zawadi zitakazokabidhiwa  kwa wajasiliamali  ambazo ni vitendea kazi kwa wajasiriamali walioshinda katika shindano la “Wezeshwa na Safari Lager”.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema wajasiriamali watakabidhiwa ruzuku zao kwenye kanda walizofanyia mafunzo ya ujasiriamali. Bwana Oscar alisema, “Tutaandaa matamasha ya kuwazawadia wajasiriamali wetu ambapo tunawaalika pia wafanyabiashara wengine wa eneo lao ili kufurahi pamoja na wajasiriamali wetu”. Aliendelea, “Kituo cha Mbeya tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 02 June katika kiwanja cha CCM Ilomba, kituo cha Arusha tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 09 June katika viwanja vya Soweto, kituo cha Mwanza tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 16 June katika kiwanja cha Furahisha na tutamaliza na kituo cha Dar Es Salaam ambapo tamasha litafanyika siku ya Jumapili tarehe 23 June kwenye viwanja vya leaders Club.”
Akielezea mchakato wa kuwapata wajasiriamali hawa Bwana Shelukindo alisema baada ya kutangaza kuanza kwa shindano hili mwishoni mwa mwaka jana, jumla ya fomu za maombi 9,738 zilikusanywa. Fomu hizi zilikaguliwa na majaji wenye ujuzi wa mambo ya biashara na wajasiriamali 80 walichaguliwa kuingia katika hatua ya pili. Wajasiriamali waliochaguliwa walitembelewa na wataalamu ili kuthibitisha uwepo wa biashara zao, jumla ya wajasiriamali 54 walifaulu na ndio waliopatiwa mafunzo. Wajasiriamali 26 waliondolewa katika hatua hii kutokana na mapungufu mbalimbali kama kuomba kuwezeshwa wakati biashara sio za kwao, kutokuwa na biashara inayoendelea .
Akionyesha baadhi ya ruzuku zitakazotolewa kwa wajasirimali walioshinda bwana Oscar alisema, “wajasiriamali wetu wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wako wajasiriamali katika fani tofauti pia kama Mafundi wa kushona nguo za aina tofauti,  mafundi seremala, magari nk wako pia wajasiriamali wa kusindika vyakula, ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku, kutengeneza mizinga ya nyuki nk, wako wajasiriamali katika biashara za vyakula, kuuza vinywaji, umeme jua, teknolojia ya mawasiliano .
Bwana Shelukindo aliwataja tena wajasiriamali watakaopatiwa ruzuku ya vitendea kazi ili kupanua biashara zao. Katika kituo cha Dar Es Salaam wajasiriamali watakaokabidhiwa ruzuku ni Catherine Urio, Josephine Kisiri, Zainabu Juma Zayumba, Elizabeth Chami, Richard Kwiligwa, Hilary Meck Mremi, Damas Daniel Msoka, Innocent Mbelwa, Stumai Namanga, Dasina J Buzuka, Christabela Lymo, Dadan J Munisi, Faraji Bakary Mgwegwe, Issa Lema na Valerian Tigano Luzangi. Shelukindo aliwataja pia washindi wa kituo cha Arusha kuwa ni Ansilla Danny, Bibie Msumi, Rogers Msangi, Simon Kinabo, Sophia Khalfan, Yuda Mbando, Amani Lymo, Adam Akilinyingi, Joseph M. Mnemwa, Rose Tesha na Victoria Riwa.
Bwana Shelukindo aliendelea kuwataja wajasiriamali watakaojipatia ruzuku katika kituo cha Mwanza ambao ni Bora Mganda, Brighton Dismas Maricell, Mangana Kilahanya Kigombe, Prudence Mubito, Musa Mahushi George, Innocent K. Doi, Amos Edward Mwambola, Edith Mudogo, Aron Magembe, Yusuph A. Kawaga, Zamda Shabban, Oscar Bosco Kabobo, Yahaya Fundisa, Dainess Ngaiza na Boniface Joseph Minja. Na katika kituo cha Mbeya wajasiriamali waliofaulu kupata ruzuku baada ya mafunzo ni Rose Eliudi Maruila, Benedict Abel Matandiko, Vumilia Mtweze, Bahati Mbata, Hellen A. Mwanguku, Felix Phillip Kamuhabwa, Festo Mwakasege, Phares Richard Lymo, Iradi A. Msemwa, Gabriel Mwalugaja na Tatu Ngemela. Jumla ya ruzuku ya vitendea kazi vya thamani ya shilingi milioni 200 vitatolewa kwa wajasiriamali hawa.
Bwana Shelukindo alimaliza kwa kuwashukuru watanzania wote kwa kushiriki shindano la Wezeshwa na Safari Lager, alisema “Shukrani nyingi ziende pia kwa wanywaji wetu wa bia ya Safari Lager, bila wao hakika zoezi zima la Wezeshwa na Safari Lager lisingewezekana, tunawaomba waendelee kufurahia bia yetu”. Aliwakaribisha kuhudhuria matamasha haya na aliwaomba radhi wajasiriamali ambao hawakufaulu, na wale wanaoendelea kutuma fomu wasitume tena, wajiandae kushiriki shindano lijalo la Wezeshwa na Safari Lagerbaadae mwaka huu
 .
Meneja akizungumza na waandishi wa habari
You might also like:

DOGO ASLAY, ORIJINO KOMEDY WAPAMBA UZINDUZI WA KAMPENI YA 'TUKO WANGAPI?TULIZANA!



Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk.Fatma Mrisho wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kimataifa ijulikanayo kama ‘Tuko Wangapi?, Tulizana’.
 Dk.Mrisho ambayea likuwa mgezi rasmi katika uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya Golden Tulip amesema kwamba kampeni hiyo imelenga kuongeza idadi ya Watanzania wanaojua maana ya mtandao wa ngono, hatari ya kuambukizwa VVU kutokana na kuwa mmoja ya wanamtandao wa kuwa na wapenzi wengi kwa wakati mmoja.
 Dogo Aslay jukwaani
 Original Komedy wakiwa kazini


Bondia wa kike,Lulu Kayege ajifua kwa ajili ya kuwakabiri wapinzani wake



 Kocha wa Mchezo wa ngumi Kambi ya Ilala Kondo Nassoro akimfundisha bondia chipkizi wa kike,Lulu Kayege Dar es salaam leo kwa ajili ya kujiandaa  na mashindano ya kumi bora yatakayofanyika june 15 katika ukumbi wa panandi panandi Ilala Bungoni Dar es salaam.picha na www,superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia wa kike,Lulu Kayege akiwa katika pozi bondia huyo  anaenolewa katika Kambi ya Ilala na Makocha wazowefu wa mchezo wa Masumbwi Nchini Habibu Kinyogoli 'Masta, Rajabu Mhamila 'Super D' na Kondo Nassoro kwa sasa yupo fiti kwa ajili ya masindano mbalimbali nchiniwww,superdboxingcoach.blogspot.com

Wednesday, May 30, 2012

AMOSI MAKALA AKABIDHI BENDERA KWA WACHEZAJI WA GOFU



Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala ameitaka timu ya Taifa ya Wanawake ya gofu kuhakikisha inapeperusha vyema bendera ya nchi katika mashindano ya All Africa Challenge yanayotarajia kuanza Juni 5, Botswana.

Timu hiyo inatarajia kuondoka nchini kesho kutwa huku ikiwa na Wachezaji watatu sambamba na mkuu wa msafara ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Maendeleo na watoto ya bunge Mary Chitanda.

Timu hiyo inaondoka nchini ikiwa tayari imeisha wahi kushika nafasi ya pili katika mashindano hayo yaliyofanyika mwaka 2010 ambapo hufanyika kila baada ya miaka miwili.

Akizungumza Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo Makala alisema watumie matoke hayo ya awali kwa kufanya vyema zaidi na kuweza kupeperusha vyema bendera ya nchi.

"Kama katika taarifa yenu ionavyosema mashindano ya mwisho mlishika nafasi ya pili sasa tunaimani mashindano haya mtakuwa wa kwanza na kuweza kututangaza vyema katika bara hili la Afrika, hivyo nendeni makaipiganie nchi yenu na kwa manufaa ya michezo," alisema.

Naye kwa upande wake Kepteni wa timu hiyo Madina Idd alisema kama waliweza kushika nafasi hiyo ya pili na wakati huo walikuwa katika maandalizi mabovu hivyo kwa sasa wanawahakikishia Watanzania wataibuka na ushindi.

"Mwaka 2010 tulishiriki na hata kufanikiwa kushika nafasi hiyo na huku tulikua katika maandalizi ya kusuasua lakini kwa sasa naimani tutafanya vyema zaidi," alisema.

Sambamba na hilo Shirika la ndege la Precion Air leo limekabidhi tiketi saba kwa timu  hiyo zikiwa ni za kwenda na kurudi ikiwa ni pamoja na tisheti na kofia vyote vikiwa na jumla ya sh. milion 7.3.

WAZIRI AMOS MAKALA AIKABIDHI BENDERA TIMU YA (TAIFA TAIFA STARS)



Naibu waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh, Amos Makala akizungumza na waandishi wa habari leo hii jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi bendera kwa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars inayokwenda Nchini Ivory coast kucheza na timu ya taifa ya nchi hiyo  jumamosi ya wiki hii ambapo aliwataka wachezaji wa timu hiyo kuipa raha Tanzania kwa kishindo kizito na kuwatangazia kuwa wasiogope wachezaji wa Ivory coast makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA PHILEMONI SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Rais wa shirikisho la Mpira Tanzania TFF Bw, Leodger Tenga akiwatakia wachezaji hhao kila la heri katika safari yao na kuwatakia ushindi mwema.
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Kim Paulsen akiwahakikishia watanzania kuwa watakwenda kule Ivory Coast  kushinda kwani amewafundisha wachezaji wake namna ya kujiamini wenyewe na pia kuwa na nidhamu mchezoni ili waweze kupata ushindi.
Wachezaji wa timu ya Taifa waliohudhuria katika Tafrija hiyo ya kukabidhiwa Bendera.
Naibu waziri wa Utamaduni na Michezo Mh, Amos Makala (kushoto) akimkabidhi bendera ya taifa kapteni wa timu hiyo Mlinda mlango Juma Kaseja.

TUMBAKU HUUA WATU MILIONI 6 KWA MWAKA DUNIANI KOTE




NA MWANDISHI WETU
WAKATI Watanzania wakitarajia kudhimisha Siku ya Kutotumia Tumbaku Duniani kesho, imebainika kuwa tumbaku huua watu takribani milioni sita (6), kila mwaka.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Kumbana na Matumizi ya Tumbaku, Lutgard Kagaruki wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam kuhusu Siku ya Kutotumia Tumbaku Duniani.
Alisema maradhi yabayosababishwa na tumbaku huathiri nchi zite duniani, na ndiyo maana jumuiya ya kimataifa ikaungana na Mkataba wa Kimataifa wa Shirika la Afya Duniani wa kudhibiti matumizi ya tumbaku.
Kagaruki alisema  Mkataba huo umebeba misingi muhimu ya udhibiti wa matumizi ya tumbaku, itakayoweza kuokoa maisha ya watu milioni 200 ifikapo mwaka 2050, kama itatekeleza ipasavyo.
Alisema muingiliano wa kampuni za tumbaku umekuwa tishio kubwa kuliko yote kwa mikakati ya kutekeleza mkataba wa kimataifa wa kudhibiti matumizi ya tumbaku.
Kagaruki alibainisha kuwa mkataba huo unavipengele muhimu kwenye Kanuni namba  5.3 ambacho kinaeleza bayana mgongano mkubwa wa maslahi uliopo kati ya kampuni za tumbaku na afya ya jamii.

THABEET KUFUNDISHA KIKAPU WATOTO 200


NYOTA wa NBA, Hasheem Thabeet anategemea kutoa mafunzo ya siku mbili ya kucheza mpira wa kikapu kwa watoto 200 walio chini ya miaka umri wa miaka 17 kwenye  Uwanja wa Don Bosco kuanzia Juni 2 hadi Juni 3.

Thabeet anayechezea timu ya Portland Trail Blazers inayoshiriki Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) ataongoza kliniki hiyo yenye lengo la kuibua vipaji.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,Thabeet alisema  mafunzo ya mwaka huu yatakuwa ni tofauti kidogo na yale ya mwaka jana.

“Ninaimani kliniki hii itakuwa tofauti na ile iliyopita kwa sababu watoto wengi wamepata mwamko wa kucheza mpira wa kikapu baada ya kuona mafanikio ya wenzao,”anasema Thabeet.

Naye Meneja wa Sprite nchini Warda Kimaro wanadhamini wa mashindano hayo alisema baada ya mafunzo hayo vijana hao watakuwa kwenye mpango maalum wa kuendelezwa na kampuni yake.


Habari - Jackson Odoyo
Picha - globalpublishers.info
You might also like:

DIAMOND KUTUMBUIZA KATIKA SHINDANO LA MISS CHANG'OMBE



Baada ya  kufanya  show ya Big Brother  Afrika Kusini MSANII Abdul Naasib ‘Diamond’ni mmoja wa wasanii watakaotoa burudani kamambe kulipamba  shindano la Redd’s Miss Chang’ombe 2012 shindano litakalofanyika Juni 9 mwaka huu  katika ukumbi wa Quality Centre barabara ya Nyerere Jijini Dar es Slaam.
Wengine watakaopamba shindano hilo la aina yake ni  kundi la Original Commedy akina Joti na bendi ya mapacha watatu ambayo kwa sasa imekuwa moja ya bendi zinayokonga  nyoyo za mashabiki wengi wa muziki hapa nchini.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam msemaji wa Kampuni ya King Promoters  ambao ndiyo waandaaji wa shindano hilo Martin Mauya ameaema kuwa kwa sasa warembo hao wameendelea kufanya mazoezi katika viwanja vya klabu ya TCC Chang’ombe Jijini Dar es Salaam.
Shindano hilo linatarajia kushirikisha warembo bomba 14 watakaopanda jukwaani kuchuana vikali kumpata mrembo wa mkoa huo wa kimashindano wa Chang’ombe huku baadhi ya wadau wa fani hiyo ya urembo nchini wakitabiri kuwa mrembo wa Tanzania mara hii atatokea katika mkoa huo wa kimashindano.
Mauya  amewataja warembo wanaotarajia kupanda jukwaani ni Elizabeth Mushi, Restituta Faustine, Miriam Ntakisivya, Flora Kazungu, Flora Robert,  Like Abraham, Clara Diu, Margareth Gerald, Jesca Haule, Deborah Nyakisinda, Suzan Paul, Wensley Matius, Zulfa Bundara na Catherine Masumbigana.
‘Kwa sasa warembo hao wanafanya mazoezi na kurudi nyumbani lakini Juni 3 warembo hao wataingia rasmi kambini katika Hoteli moja kubwa Jijini kabla ya kuapnda hiyo Juni 9’ alisema Mauya.
Shindano hilo limedhaminiwa na REDD’S ORIGINAL, NEXUS CONSULTING AGENCY, DODOMA WINE, CXC AFRIKA, PAPAZII INTERTAINMENT, KITWE GENERAL TRADERS,CHERISH, BEN EXPEDITION, SCREEN MASTERS, ARDHI PLAN LIMITED.

Meneja mkuu wa kampuni ya tigo atembelea kampuni ya Clouds Media Group leo jijini Dar



Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez akizungumza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga pichani kulia,mara baada ya kumaliza ziara ndani ya kampuni hiyo  na kujionea mambo mbalimbali,shoto ni Ofisa Mahusiano wa Tigo Alice Maro.
 Meneja Mkuu wa kampuni ya simu za mikononi ya Tigo akifanya mahojiano mafupi na mtangazaji wa Choice FM,aitwaye Thandi Kathembe mapema leo jioni.
Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga (pili kutoka kulia),akifafanua jambo kwa Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez alieambatana na Ofisa Mahusiano wake, Alice Maro,kulia ni Dj Fetty.
Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akifafanua jambo kwa Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez (pichani kati),Kulia ni mmoja wa watangazaji wa Clouds FM,Ruben Ndege.
Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez akiperuzi moja ya jarida la Burudani hapa nchini la KITANGOMA,linalochapishwa na kampuni ya Prime Time Promotions LTD. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimuelekeza Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez namna ya baadhi ya vipindi vya Clouds TV vikiwa tayari kwa kurushwa hewani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimuelekeza Meneja Mkuu wa kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo,Diego Gutierrez namna ya baadhi ya vipindi vya Clouds TV vikitayarishwa kabla ya kwenda kurushwa hewani.

WANASHERIA WA KIMATAIFA WASAIDIA KUWAJENGEA UWEZO WANASHERIA WA KITANZANIA



 Mkuu wa Chuo cha Sheria cha Tanzania Dr. Gerald Ndiku akiongea katika ufunguzi wa mafunzo kwa ajili ya wanasheria wa hapa nchini kuwajengea uwezo na mbinu za uandika maandiko ya kisheria, namna ya kutengeneza vipengele vya upatanishi wa mizozo, mwenendo wa kesi mahakamani, mikataba ya kuuza na kununua, mikataba ya mikopo pamoja na mbinu na taratibu zake na maandishi mengine ya kisheria kwa ujumla.
 Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Bi. Angellah Kairuki akisoma risala yake kuashiria ufunguzi wa mafunzo ya sheria kupitia Chuo Cha Taifa Cha Sheria kupitia shirika la kujitolea lijulikanalo kwa jina la New Perimeter lililoanzishwa na DLA Piper kwa muda wa wiki 2 kwa wanafunzi wapatao 240 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Bw. Simon Boon kutoka DLA Piper- London Kitengo Maalum cha Restructuring ambaye pia ni kiongozi wa mradi akiongea machache.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Sheria cha Tanzania Dr. Gerald Ndiku, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Bi. Angellah Kairuki  wakiwa pamja na Bw. Lawrence Masha kutoka IMMMA Advocates.
 Wageni waalikwa wakiwa na wanafunzi.
Mshereheshaji wa sherehe hiyo, Bw. Sebo akiongea machache kabla ya kumaliza ufunguzi.
 Wageni wakiwa katika picha ya pamoja.
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Bi. Angellah Kairuki akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baaya ya kufungua mafunzo hayo.

WAZIRI AMOS MAKALA NA MATUKIO JIJINI DAR ES SALAAM



Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla akikabidhi bendera kwa Timu  ya Taifa ya mchezo wa Golf inayotarajiwa kusafiri kwenda  Gaborone Botwsana kwa ajili ya mashindano ya chalenji ya Afrika kwa upande wa Wanawake.Wapili kushoto ni  Mh. Mery Chatanda (Mbunge).(Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla akikabidhi kiasi cha shilingi milioni kumi kwa mama wa marehemu Steven Kanumba ikiwa ni rambirambi ya Serikali kwa familia. (Picha na Benjamn Sawe wa WHVUM)
You might also like: