Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, April 29, 2012

CHEKA ALIVYOMGALAGAZA MAUGO BILA HURUMA

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA MPAMBANO WA CHEKA NA MAUGO

 Baadhi ya Maraisi wa vyama vya mchezo wa Masumbwi Nchini wakiangalia mchezo wa Mada Maugo na Francis Cheka ubingwa wa IBF AFRIKA kutoka kushoto ni Rais wa TPBO,Onesmo Ngowi wa TPBC pamoja na Emanuel Mlundwa wa PSTwww.superdboxingcoach,blogspot.com

 Ibrahimu Maokola kulia akipambana na Saidi Mbelwa Maokola alishinda kwa Point.Picha na www.superdboxingcoach,blwww.superdboxingcoach,blogspot.comogspot.com

Baadhi ya Marefarii kutoka Nnje ya nchi wakisubili kuchezasha mpambano wa ubingwa wa IBF Arika kati ya Mada Maugo na Francis Cheka jana.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya mashabiki waliokuwa wamekaa katika VIP wakiangalia mpambano
Mada maugo kushoto na Francis Cheka wakioneshana umwamba wa kutupiana masumbwiwww.superdboxingcoach,blogspot.com

Cheka akipiga ngumi bila mafanikio uku mada akiludi nyuma kujiami.www.superdboxingcoach,blogspot.com
Meya wa Manspaa ya Ilala Jery Slaa akimkabidhi funguo ya gari bondia Francis Cheka baada ya kuibuka na ubingwa wa k.o raundi ya 6 jana.www.superdboxingcoach,blogspot.com

KAIMU MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AZUNGUMZIA USAFI JIJINI
Kaimu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bi. Mwamtum Mahiza akiongea na
waandishi wa habari jana Ofisini kwake jijini Dar es salaam kuhusu hali
ya usafi katika jiji la Dar es salaam ambayo imekuwa hairidhishi kwa
muda mrefu hali hiyo imesababishwa na wananchi kutozingatia kanuni
sheria na taratibu za afya na usafi wa mazingira.

(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE).

TANGAZO LA DAWA YENYE NGUVU

DAWA YA NGUVU ZA KIUME NA MSIMKO KWA WANAWAKE WASIO NA HAMU YA TENDO LA NDOA AMBAYO HULETA MSISIMKO KWA WANAUME NA WAKE WAKUTANAPO.KWA SASA INAPATIKANA KWA BEI NAFUU HAPA JIJINI DAR ES SALAAM MAKUTANO YA MTAA WA KIPATA NA BARABARA YA MSIMBAZI
ALLY WA YANGA BOMBA UHURU NA MSIMBAZI 0787230551 AU 0652755838


PIGA NO O713827689, 0755074505 , au 0719 541366
,0652755838 UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM

BUGURUNI LOZANA STENDI YA TAX ULIZIA ADAMU KIBANDANI 0755875884

SHULE YA UHURU FIKA JENGO LA AZAM BAKHRESA ULIZA NGAEJA 0715110900

KARIAKOO SHULE YA UHURU STENDI YA MABASI YA TANDIKA ULIZIA ZUNGU MUHUZA TIKETI 0712743870

NA UKIWA ILALA SHARIF SHAMBA FIKA DSJ BANDA NAMBA 14 SIMU 0718718671

NA UKIWA KOTA ZA BANDARI KARIAKOO FIKA MKUNGUNI KIBANDANI KWA HUSEIN 0753893295

MWANANYAMALA FIKA JABA KLABU ULIZA MACHELLAH 0713470492

ENZOY INALETA HESHIMA
You might also like:

TIGO YAZAMINI MAADHIMISHO YA SIKU YA TAALUMA VYUO VIKUU MAKUMBUSHO


Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Leon Haule (kulia) akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu umuhimu wa Social Protection wakati wa maadhimisho ya siku ya Taaluma kwa Vyuo vikuu liliyofanyika Makumbusho ya Taifa kwa udhamini wa Tigo
Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Josephine Douglas(kulia) akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu umuhimu wa Social Protection wakati wa maadhimisho ya siku ya Taaluma kwa Vyuo vikuu liliyofanyika Makumbusho ya Taifa kwa udhamini wa Tigo

Mwenekiti wa Bodi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Charles Nyoni (katikati) akikata utepe wakazi wa ziara ya kuzungukia vibanda vya maonyesho wakati wa maadhimisho ya siku ya Taaluma kwa Vyuo vikuu liliyofanyika Makumbusho ya Taifa kwa udhamini wa Tigo.Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha IFM, Profesa Mjema na Mwanafunzi wa Chuo hicho, Dorthea Msofe.

SIMBA KUIVAA AL AHLY SHANDY YA SUDAN LEO UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM.Wawakilishi pekee waliobaki toka Klabu za Tanzania katika michuano ya Barani Afrika, Simba, leo wanatinga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya michuano ya CAF ya Kombe la Shirikisho kwa kucheza na Al Ahly Shandy ya Sudan.

Katika Raundi zilizopita, Simba walibwaga Kiyovu ya Rwanda kwa jumla mabao 3-2 katika Mechi mbili kisha kuwatoa ES Setif ya Algeria kwa bao la ugenini baada ya kufungana bao 3-3 katika Mechi mbili, Simba wakishinda Dar es Salaam bao 2-0 na kuchapwa 3-1 huko Mjini Setif, Algeria.

Nao Al Ahly Shandy waliwatoa Ferroviario de Maputo ya Msumbiji Raundi iliyopita na ingawa Klabu hii ya Sudan ni mara ya kwanza kucheza michuano ya Klabu Afrika lakini kwa mchezo ilioonyesha walipocheza na Ferroviario de Maputo na kushinda 1-0 ugenini Maputo na 2-0 kwenye Mechi ya marudiano, Timu hii si ya kubeza.

Timu hizi zitarudiana hapo Jumamosi Mei 12 huko Mjini Shandy, Mji ambao uko Kilomita 150 Kaskazini Mashariki ya Mji Mkuu wa Sudan, Khartoum.

Na katika mechi hiyo kiingilio cha chini ni sh 5,000/=
You might also like:

CHEKA AGALAGAZA MAUGO

 

MAUGO ADUNDWA NA CHEKA


BONDIA Francis Cheka ‘SMG’ kutoka Morogoro, kwa mara ya tatu mfululizo Jana Usiku amempiga mpinzani wake Mada Maugo kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya saba katika pambano lililokuwa la raundi 12, kwenye ukumbi wa PTA, Saba Saba, Dar es Salaam.
Maugo baada ya kupigwa ngumi nyingi katika raundi tatu mfululizo, kiasi cha kutabiriwa kukaa chini wakati wowote, mwanzoni mwa raundi ya saba hakurejea ulingoni.
Msaidizi wake, Karama Nyilawila alitupa taulo ulingoni akisema bondia wake hataendelea na pambano.
Refa John Shipanuka kutoka Zambia aliyelimudu pambano hilo, alimuinua mkono Cheka kumtangaza mshindi kwa TKO raundi ya saba.
Baada ya hapo, Maugo aliinuka kwenye kona yake na kwenda kumkumbatia Cheka na kocha wake, akisema kwamba amesalimu amri baada ya kuishiwa pumzi.
“Pumzi imekata, siwezi kuendelea,”alisema Maugo ambaye leo alionekana muungwana ingawa hakuwa tayari kusema atahitaji pambano la nne au la.
Akiwa mwenye furaha, Cheka alisema kwamba anamshukuru Mungu amemuwezesha kuendeleza ubabe wake kwa mabondia wa Tanzania na sasa anageuzia makali yake kwa Japhet Kaseba ambaye naye ameomba pambano la marudiano.
Katika pambano la jana, refa Shipanuka alimdhibitu Maugo mwenye desturi ya kuwakumbatia wapinzani wake ili kukwepa kupigwa na pia kupumzikia kwenye miili yao.
Kila alipokuwa akimkumbatia Cheka, Shipanuka alikuwa akifika na kuwaachanisha na kufanya mabondia hao watumie muda mwingi kupigana.
Pamoja na hayo, Maugo alilianza pambano hilo vizuri na katika raundi ya pili almanusra ashinde kwa Knockout (KO) baada ya kumkalisha mpinzani wake kwa ngumi kali.
Lakini SMG aliinuka na kuendelea na pambano, ingawa limchukua hadi raundi ya nne kuanza kuutawala mchezo.
Raundi ya kwanza hadi ya tatu, Maugo alifanya vizuri, lakini baada ya hapo mambo yalikuwa magumu na tangu hapo wengi walijua angepigwa wakati wowote.
Katika  mapambano ya utangulizi, mdogo wake Cheka, Cosmass Cheka alipigwa kwa pointi na Sadiki Momba katika pambano la uzito wa Light, wakati Hajji Juma alimpiga kwa pointi Emmilio Naffat uzito wa bantam.
Simba Watunduru alimpiga kwa KO raundi ya sita Mohamed Kashinde katika pambano la uzito wa Feather, wakati Amos Mwamakala alimpiga kwa pointi Said Muhiddin uzito wa Light.

RAIS KIKWETE AWA MWENYEJI WA MKUTANO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI ARUSHARais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakitia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo leo Aprili 28, 2012 katika hoteli ya Ngordoto jijini Arusha. 
Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakionesha hati baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo leo Aprili 28, 2012 katika hoteli ya Ngordoto jijini Arusha.  
 Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakikaribishwa chakula cha mchana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Richard Sezibera baada ya picha ya pamoja kufuatia kutia saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi wa nchi hizo leo Aprili 28, 2012 katika hoteli ya Ngordoto jijini Arusha

Tigo yawezesha wakazi wa Muheza


. Mmmoja wa washindi aliyejishindia zawadi ya simu kutoka Tigo
Kikundi cha Sarakasi kikipagawisha mashabiki waliofurika kwenye Tamasha la Tigo wilayani Muheza hivi karibuni.
Mwanamuziki H.Baba akiwaburudisha wakazi wa Muheza

CHEKA ‘AMPOLA’ GARI MAUGO AENDA KULIACHA POLISI


 Gari la Cheka likiwa Kituoa cha Polisi Magomeni baada ya kupata ajali jana usiku.
***************************
*Furaha ya ushindi wa Cheka kumchapa maugo yaishia kituo cha Polisi
*Alala Oysterbay Polisi adhaminiwa leo
 BAADA ya Bondia mahiri  Francis Cheka kuibuka na ushindi mnono wa TKO dhidi ya mpinzani wake Mada maugo na kukabidhiwa mkanda wa ubingwa wa Afrika Mashariki IBF na Gari lenye thamani ya Sh. Milioni 8, katika pambano lao lililofanyika jana usiku katika Ukumbi wa PTA, furaha ya bondia huyo iliishia mikononi mwa Polisi.
Ikiwa ni siku moja tu baada ya kuvishwa taji la ubingwa huo na kukabidhiwa mchuma wake, Cheka alikamatwa na Polisi masaa machache tu baada ya kukabidhiwa gari na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwake ambayo iliishia mitaa ya Manzese baada ya kupata ajali kwa kugonga Pikipiki na kuwajeruhi dereva wa pikipiki hiyo na abiria wake ambao walikimbizwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.
Pikipiki iliyogongana na gari la Cheka
Leo asubuhi baada ya kupata taarifa ya tukio hilo mtandao huu wa  ulifanya jitihada za kupata dondoo za tukio hilo na kufika Kituo cha Polisi Oysterbay ambako alikuwa ameshikiliwa Bondia huyo na kupata taarifa kuwa muda mchache tu uliopita kabla ya kuwasili mahala hapo aliondoka akiwa ameongozana na nduguze baada ya kupata dhamana.
Baada ya kupishana na bondia huyo mtandao ulitinga Kituo cha Polisi Magomeni na kufanikiwa kuliona gari hilo likiwa limeharibika na kuvunjika kioo huku Pikipiki hiyo iliyogongwa yenye namba za usajiri T507 BYR, ikiwa mahala hapo.
Akizungumza na Mtandao huu kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea jana usiku majira ya saa nane maeneo ya Manzese na kuwajeruhi dereva na abiria wake waliokuwa katika pikipiki hiyo.
Aidha Kenyela, alisema kuwa baada ya ajali hiyo Dereva wa gari hilo lenye namba za usajiri T 321 AAU, aliyefahamika kwa jina la Francis Cheka, alifikishwa kituo cha Polisi Oysterbay na kushikiliwa hadi asubuhi ya leo walipofika ndugu zake na kumuwekea dhamana.
Akielezea tukio hilo Kenyela, alisema kuwa Gari la Cheka lilikuwa likitokea maeneo ya Manzese kuelekea Ubungo na Pikipiki ikitokea Ubungo kuelekea Manzese na walipofika maeneo ya Tip Top Manzese, dereva wa pikipiki aliutan na kuhamia barabara ya pili ili kuelekea Ubungo na kugongana na gari hilo.
Aidha alisema kuwa dereva huyo wa pikipiki bado amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala akiendelea na matibabu huku abiria wake akitibiwa usiku wa jana na kuruhusiwa.
 Kenyela aliwataka madereva wa pikipiki kufuata na kuheshimu sheria za usalama Barabarani ili kuepuka ajali za kizembe za kila siku zinazokatisha maisha yao.HABARI NA PICHA KWA HISANI YA www.sufianimafoto.blogspot.com,

Friday, April 27, 2012

MAUGO VS CHEKA WAPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WAO KESHO SUPER D KUZAMBAZA DVD ZA NGUMI MPYA

Na Mwandishi Wetu
WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo wamewapima uzito   na bondia  Mada Maugo  na  Na Francis Cheka wote wamekutwa na KG.
KG.76.5 ambapo mpambano wao utafanyika Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.

Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa mpambano huo Yasini Abdallah alisema kuanikwa kwa mkanda huo na Gari kuwekwa Hadharani kutaashiria kupamba moto kwa pambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.

“Tunauanika Gari na mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda,” alisema Kaike.
Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.
Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D
.

--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

NANI KUIBUKA MBABE KESHO PTA
 CHEKA AKIWA NA WAPAMBE WAKE
 MADA MAUGO NA CHEKA WAKINYOOSHWA MIKONO JUU NA PROMOTA
 PROMOTA AKIWA NA MABONDIA HAO
Bondia Mada Maugo akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa wa IBF na Francis Cheka kushoto mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba kesho na mshindi atanyakua zawadi ya gari.picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
0 comments

WATANZANIA WAWILI WAOMBEWA ITC UGHAIBUNI
Wachezaji wawili Watanzania wameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya kucheza mpira wa miguu katika nchini za Denmark na Jamhuri ya Czech.


Chama cha Mpira wa Miguu cha Denmark (DBU) kimemuombea hati hiyo William Benard Okum kama mchezaji wa ridhaa ili ajiunge na timu ya Brabrand IF. Klabu ya zamani ya Okum ni Viko Pham FC ya Zanzibar.

Naye Samwel Jonathan Mbezi ameombewa hati hiyo na Chama cha Mpira wa Miguu cha Jamhuri ya Czech (FACR) ili aweze kuchezea timu ya Sokol Dolany akiwa mchezaji wa ridhaa. Katika maombi hayo, FACR imeonesha kuwa Mbezi kwa sasa hana timu anayochezea hapa nchini.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linafanya mawasiliano na pande husika kabla ya kutoa hati hizo kwa wachezaji hao kama walivyoomba DBU na FACR.

MECHI KUCHANGIA TWIGA STARS MEI 4
Mechi maalumu ya hisani kwa ajili ya kuchangia timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars), kati ya timu hiyo na wasanii wa filamu maarufu kama Bongo Movie itachezwa Mei 4 mwaka huu.

Kwa mujibu wa kampuni ya Edge Entertainment iliyoandaa mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni kwa kiingilio cha sh. 2,000, sh. 5,000 na sh. 10,000.

Twiga Stars kwa sasa hivi haina mdhamini na iko kambini katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ya Ruvu mkoani Pwani inashiriki michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) ambapo Mei 26 mwaka huu itacheza na Ethiopia jijini Addis Ababa. Fainali za AWC zitafanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.

MECHI ZA LIGI KUU WIKIENDI HII
Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea katika raundi ya 25 kesho (Aprili 28 mwaka huu) ambapo Coastal Union itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mtibwa Sugar ikiwa mgeni wa African Lyon kwenye Uwanja wa Chamazi.

Aprili 30 mwaka huu Azam na Toto African zitacheza Chamazi wakati Mei 1 mwaka huu Villa Squad itaumana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Chamazi.

Ligi hiyo itafunga msimu wa 2011/2012, Mei 5 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitakuwa uwanjani. Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs Polisi Dodoma (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha) na Ruvu Shooting vs Villa Squad (Mabatini, Mlandizi).

Mechi nyingine zitakuwa kati ya Coastal Union vs Toto African (Mkwakwani, Tanga), African Lyon vs JKT Ruvu (Manungu, Morogoro), Azam vs Kagera Sugar (Chamazi, Dar es Salaam) na Moro United vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro).

MKUTANO MAKOCHA SIMBA, AL AHLY SHANDY
Makocha wa timu za Simba na Al Ahly Shandy ya Sudan kesho (Aprili 28 mwaka huu) watakuwa na mkutano na Waandishi wa Habari kuzungumzia walivyoandaa vikosi vyao kwa ajili ya mechi ya Jumapili.

Mkutano huo utafanyika saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho itachezwa Uwanja wa Taifa kuanzia saa 10 kamili jioni.

Thursday, April 26, 2012

FRANSIC CHEKA ASAINI MKATABA WA KUPAMBANA NA JAPHET KASEBA SIKU YA SABASABA

 Bondia Fransic Cheka kushoto akisaini mkataba wa makubaliano ya kupambana na Japhet Kaseba siku ya sabasaba wanaoshughudia kushoto ni Mshauli wake Oscar George na Promota wa mpambano huo Kaike Silaju .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


f
BONDIA JAPHET KASEBA KATIKATI AKISAINI MKATABA WA KUPAMBANA NA FRANSIC CHEKA

BONDIA FRANSIC CHEKA AKIWA KATIKA POZI

Bondia Fransic Cheka kushoto akisaini mkataba wa makubaliano ya kupambana na Japhet Kaseba siku ya sabasaba Dar es salaam leo wanaoshughudia kushoto ni Mshauli wake Oscar George na Promota wa mpambano huo Kaike Silaju .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com