Kamisheni
ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) imetoakibali kwa bondia wa kimataifa
wa Tanzania Francis Miyeyusho kucheza pambano langumi nchini Uingereza.
Miyeyusho atazipiga na bondia Luke Wilton wa Uingereza tarehe 27 mwezi
huu katika hoteli ya Holiday Inn iliyo katika mtaa wa jijiniBelfast,
Ireland ya Kaskazini. Mpambabno huo ni wa kugombea mkanda wa kimataifawa
Masters katika uzito wa Super Fly.
Miyeyusho anatarajia kuondoika nchini tarehe 22 mwezihuu siku ya Jumapili na shirika la ndege la Uingereza (British Airways).
Francis
Miyeyusho ni bondia wa kimataifa aliye kwenyeviwango vya mashirikisho /
vyama mbalimbali ya / vya ngumi duniani. Shirikishola ngumi la
Kimataifa IBF limemweka kwenye nafasi ya 5 katika orodha yamabondia 15
bora wa mabara duniani.
Hii
ni mara ya kwanza kwa Francis Miyeyusho kuchezanchini Uingereza na
mabondia wa huko na anatagemea kuonyesha umahiri mkubwakatika mpambano
huo.
Kamisheni
ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) inamtakiasafari njema Miyeyusho
katika safari yake ya kuitangaza Tanzania katika medaniya michezo ya
kimataifa.
Ikumbukwe kwamba ni Ngumi za Kulipwa pekee ambazozimekuwa zinaig’arisha na kuitangaza vyema Tanzania katika miaka ya karibuni.
Katika
mpambano huo, wimbo wa Taifa la Jamhuri yaMuungano wa Tanznaia utapigwa
mbele ya maelfu ya watanzamaji pamoja namamilioni wengine ambao
watakuwa wanaangalia kwenye luninga.
TPBC
imeanzisha rasmi mkakati wa kutumia mchezo wangumi za kulipwa
kuitangaza Tanzania kama sehemu salama ya kufikia kwa wataliina
wawekezaji (destination market for tourism and direct
investments)"Sports Tourism" kwa maana ya "Utalii wa Michezo"
Aidha tunamuombea mungu Miyeyusho aende salama naafanikiwe kurejea na mkanda wa International Masters nchini Tanzania.
No comments :
Post a Comment