Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani Khijjah akizungumza na viongozi mbalimbali wa dini kuelezea umuhimu na ushiriki wao katika kufanikisha sensa ya watu na makazi itakayofanyika kitaifa mwezi Agosti mwaka huu wakati wa mkutano wa viongozi wa dini unaoendelea jijini Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.
Baadhi ya viongozi wa dini wanaoendelea na mkutano wao jijini Dar es salaam wakipitia vitabu na vipeperushi vyenye jumbe mbalimbali kuhusu zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika nchi nzima mwezi Agosti mwaka huu baada ya wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoa semina fupi kuhusu ushiriki wa viongozi hao katika kufanikisha sensa hiyo .
Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na uchumi Ramadhani Khijjah alipokuwa akizungumzia umuhimu wa sensa ya watu na makazi 2012 na namna serikali ilivyojipanga kukamilisha zoezi hilo kwa ufanisi.
Mkurugenzi mkuu ofisi ya taifa ya takwimu Dkt. Albina Chuwa akisisitiza jambo kuhusu sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka huu wakati wa semina ya viongozi wa dini jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani Khijjah (kushoto) akiandika maswali yaliyoulizwa na viongozi wa dini kuhusu namna serikali ilivyojipanga kukamilisha sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwezi Agosti 2012. Wengine ni mkurugenzi mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu Dkt. Albina Chuwa (katikati) na kamishna wa sensa Bi. Hajjat Amina Mrisho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani Khijjah (kushoto) akizungumza jambo na mkurugenzi mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu Dkt. Albina Chuwa wakati wa mkutano wa mkutano wa viongozi wa dini unaoendelea jijini Dar es salaam. Ofisi ya taifa ya takwimu imekutana na viongozi hao kufuatia umuhimu na ushawishi wao katika jamii ili waweze kushiriki kikamilifu katika kufanikisha sensa ya makazi itakayofanyika mwezi Agosti 2012.
No comments :
Post a Comment