Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, February 26, 2010

YANGA JUMAMOSI KULIPA KISASI DHIDI YA LUPOPO

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara na wawakilishi katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrka Yanga wameahidi kubuka na ushindi katika mchezo wa marudiano dhidi ya FC Lupopo, mchezo utakaopigwa Lubumbashi, DR Congo.
Akizungumza kwa njia ya simu Luis Sendeu amesema, maandalizi yote yamekamilika, licha ya leo wakati wakifanya mazoezi kuvamiwa na watu wa Lupopo ambao waliwataka kuacha mazoezi na kuwapisha kuufanyia usafi uwanja ikkiwa ni pamoja na kukata majani.
Hata hivyo Sendeu amesema malalamiko ya kuzuiliwa kufanya mazoezi wameyawasilisha kwa ujumbe wa CAF na wameahidi kuyafanyia kazi.
Aidha hapo jana walikumbwa na kizaza cha kupotelewa na mabegi katika uwanja wa ndege wa Nairobi nchini Kenya wakati wakibadilisha ndege kuelekea Lubumbashi, Congo tayari kuwavaa FC Lupopo.
Akizungumza na viwanjani hapo jana katibu wa kamati ya mashindano ya Yanga, Emanuel Mpangala mara baada ya kuwasili Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, amethibitisha hilo na kusema takriban wachezaji wanne wamepoteza mabegi yao akiwemo Jerison Tegete, Boniface Ambani na Godfrey Bony.
Kikosi cha Yanga kimeondoka na Jumla ya wachezaji 18 na Viongozi wa nane, ambapo waliondoka majira ya saa kumi Alfajiri kwa ndege ya shiraka la ndege la Kenya KQ.
Msafara huo uko chini ya Kitwana Manara kutoka shirikisho la soka Tanzania TFF, Kocha mkuu wa Yanga Kotadin Papic, Daktari wa Timu Shecky Mngazija, Katibu Mkuu Laurence Mwalusako, Luis Sendeu Afisa habari wa Yanga, Meneja wa Timu Kenneth Mkapa, Emmanuel Mpangala na Mhasibu wa Timu Godfrey Mwenje.
Kwa upande wa wachezaji, ni Magolikipa ni Obren Cuckovic na Yaw Berko, wengine ni Fred MBuna, Shadrack Nsajigwa, Nurdin Bakari, Athumani Iddi “Chuji”, Shamte Ally, Nadir Haroub “Canavaro”, Jerison Tegete, Amir Maftah, Abdi KAssim, George Owino, Mrisho Khalfani Ngassa, Steven Bengo, John Njoroge, Boniface Ambani, Wisdom NDlovu na Kigi Makasi.
Utakumbuka msikilizaji katika mchezo wa kwanza Yanga walizabwa nyumbani katika uwanja bora Afrika Mashariki na kati, Uwanja wa mpya wa Taifa 3-2.
Ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Yanga wanalazimika kuifunga Fc Lupopo magoli 2-0.
Wakati Yanga wakiwa wamecheza mchezo mmoja wa kirafiki na Zesco ya Zambia na kutoka sare ya bao moja kwa moja, FC Lupopo yenyewe iliondoka Lumbumbashi siku ya JUmatatu na kupiga Kambi katika mkoa wa Copperbelt nchini Zambia ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Yanga.
Lupopo walicheza mchezo wa kirafiki siku ya Jumapili na klabu ya Raon United na kuzabwa 2-1 kwenye uwanja wa Kabufu mjini Luanshya.
wafungaji wakiwa Ben Mwanza na Perry Sinkala wa Roan katika dakika ya 35 na 37, huku bao la kufutia machozi la Lupopo likifungwa na Junior Mubende katika dakika ya 14.

KICKBOXING LIGI KUANZA JUMAMOSI

Japfet Kaseba mwenye T-shirt ya njano akiwa na wapiganaji wengine wa mchezo kick Boxing walipozuru Radio Times FM, mwenye karatasi mi mdau wa viwanjani Amri Massare.
Zaidi ya mabondia nane leo wamepima uzito pamoja na Afya zao tayari kupambana katika ligi ya mchezo huo itakayoanza siku ya jumamosi majira ya saa kumi katika ukumbi wa DDC Magomeni jijini Dar es Salaam.
Mwandaji wa ligi hiyo ambaye ni bingwa wa dunia wa mchezo huo Japhet Kaseba amesema kwamba sambamba na upimaji wa mabondia wametoa mafunzo na semina kwa waalimu na waandishi habari.
Japhet Kaseba amesema maandalizi yote yapo tayari na kiingilio ni Tshs 4000 kwa VIP na kawaida 2000.
Aidha kaseba amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo ya mchezo wa kick Boxing ambayo yanafanyika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza.
Amesema anaamini itakuwa ni Burudani ya pekee kushuhudia vijana wenye vipaji lakini hawakuwahi kupewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao kutokana na mapromota uchwara ambao wamekuwa na tabia ya kutaka wapiganaji wenye majina kwa kutaka faida kubwa, na kuwasahau wengine ambao wanavipaji lakini hawana majina.

SIMBA KUKIPIGA NA ZESCO YA ZAMBIA JUMAMOSI, NA AZAM JUMAPILI

Wekundu wa msimbazi Simba inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Zesco ya Zambia jumamosi katika dimba la uhuru jijini Dar es Salaam.
Akiongea na kipindi cha michezo na burudani cha Radio Times FM Afisa habari wa Simba Cliford Ndimbo amesema kuwa mchezo huo ni maandalizi ya michuano kombe la Shirikisho barani Afrika CAF itakayoanza marchi mwaka huu.
Ndimbo ametaja viingilio katika mchezo huo kuwa VIP 10,000, na kuna viti vya Tshs 5000 na 3000.
Aidha amewataka mashabiki wa kandanda kujitokeza kwa wingi kuwaungana kama ambavyo wamekuwa wakiwaunga mkono katika michezo ya ligi kuu Tanzania Bara.
Siku ya JUmapili Machampion hao wa Zambia timu ya Zesco itacheza na klabu ya Azam FC ambayo inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.

Wednesday, February 24, 2010

SERENA WILLIAMS ASAIDIA KENYA

Makamu wa Raisi Kalonzo Musyoka amepongeza jihudi za mcheza Tenis nambari moja Duniani Serena Williams wakati akifungua shule nchini Kenya.
Musyoka amesema washirika wake ambao ni wanaongoza kwa usalishaji komputa kampuni ya Hewlett-Packard (HP) na Charitable organization - Build African Schools, limeahidi licha ya kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo litawawezesha vifaa vya komputa ikiwa ni pamoja na maabara ya mtambo wa kompyuta kwa ajili ya kupatikana internet.
Makamu huyo wa Raisi, ambaye amemualika kuungana na mfuko wake wa Kalonzo Musyoka Foundation kwa ajili ya kuwasaidiza wanafunzi udhamini wa masomo, na kusema itaweza kumnufaisha zaidi Ms Williams hasa kufuatia katiba mpya.
Musyoka anasema Serena Williams amegusa maisha ya watu wengi wa Kenya na amefanya makubwa kwa wakenya.
Ms Williams amesema ataendelea kusaidia Kenya sit u kufungua na kutoa misaada mashuleni lakini pia kujenga na kuwezesha vifaa vya Kompyuta ikiwa ni pamoja na nchi zingeni barani Afrika.
Ms Williams amefungua shule ya Wee Secondary School iliyopo Matiliku wilaya ya Makueni.

Friday, February 19, 2010

TIMU YA TAIFA YA TANZANIA ITAKAYOINGIA KAMBINI 27 MWEZI HUU HII HAPA

Golikipa
Shaban Hassan (Kado) Mtibwa
Jackson Chove JKT

WALINZI

Shadrack Nsajigwa Yanga
Salum Kanon Simba
Juma Jabu Simba
Stephen Mwasika Moro United

WALINZI WA KATI

Nadir Haroub (Canavaro) Yanga
Kevin Yondani Simba
Aggrey Morris Azam
David Naftari Simba

VIUNGO

Abdulhalim Humoud Mtibwa
Erasto Nyoni Azam
Juma Nyoso Simba
Shabani Nditi Mtibwa
Abdi Kassim Yanga
Mbwana Samata African Lyon
Kigi Makasi Yanga
NUrdin Bakari Yanga
Ibrahim Mwaipopo Azam

WASHAMBULIAJI

Mussa Hassan Mgosi Simba
Mrisho Ngassa Yanga
John Bocco Azam
Jerson Tegete Yanga

WANARIADHA KENYA WAPATA MSIBA

Mwanariadha wa zamani wa Kenya wa mbio za kati David Lelei amefariki Dunia katika ajali ya gari huku mwanaariadha mwenzake na bingwa wa zamani wa Dunia wa mbio za mita 10,000 Moses Tanui ameumia vibaya kifuani.
kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwanariadha anayeshikilia rekodi ya Dunia yam bio za marathon Paul Tergat, amesema Lelei, 39 na Tanui, 45, walikuwa wakiendesha gari toka Nairobi wakielekea nyumbani kwao Eldoret hapo jana na kkuligonga kilomita chache nje ya Nakuru, Mji wa nne kwa ukubwa nchini Kenya ikiwa na kilomita za mraba 200 magharibi mwa Nairobi.Tergat amesema walikuwa waktoka katika hafla mjini Nairobi na walikuwa wakisafiri kurudi nyumbani Eldoret wakati ajali ihyo ikitokea.
Akiongea kwa maaseikitiko anakiri kwamba wamempoteza Lelei, lakini Tanui amenusurika na amelazwa Nairobi Hospital.
Lelei alishinda medali ya shaba katika mbio za mita 1,500 mwaka 1999 katika michuano ya All African Games iliyofanyika Johannesburg, mwaka huo huo alimaliza akishika nafasi ya saba katika mbio za Dunia zilizofanyika Seville. Inakumbukwa alimaliza akiwa wa nne katika mbo za mita 800 mwaka 2001 katika michuano ya ndani ya Dunia huko Lisbon.
Tanui alishinda mbio za mita 10,000 na kutwaa ubingwa wa Dunia mwaka 1991 katika michuano iliyofanyika Tokyo. lakini pia alishinda mbio za marathon 1996 na 1998 zilizofanyika Boston.

KEWLI SASA MCHEZO WA NGUMI UNARUDI NCHINI

Bondia Denis Mwaisarage (kulia) akijaribu kutupa konde kwa mpinzani wake, Said Mtubukwa, wakati wa mazoezi ya kuchagua timu ya Taifa ya ngumi yaliyofanyika Dar es salaam jana (Picha na Rajabu Mhamila)Bondia Sanday Elias (kulia) akijaribu kutupa konde kwa mpinzani wake, Noel Akwilini, wakati wa mazoezi ya kuchagua timu ya Taifa ya ngumi yaliyofanyika Dar es salaam jana (Picha na Rajabu Mhamila)Kocha wa mchezo wa ngumi, Habibu Kinyogori (kushoto) akiwaelekeza jinsi ya kutupa ngumi wachezaji wa mchezo uho wa klabu ya Simba Dar es salaam juzi.(Picha na Rajabu Mhamila)

Tuesday, February 16, 2010

MISS TANZANIA HATIMAYE APATA DHAMANA

Miriam akiwa chini ya ulinzi kabla ya kuwekewa dhamana.
Hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar mchana huu ,imewaachia kwa dhamana Miss Tanzania 2009/10 Miriam Gerald na mpenzi wake Kennedy Victor 'Kanny'. Kufanikiwa kwa dhamana hiyo kumetokana na harakati za Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga ‘Ankal’ pamoja na ndugu wa kijana Keny ambao tokea Ijumaa iliyopita walikuwa wakihaha mahakamani hapo kuwawekea dhamana.
Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani hivi karibuni katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kujeruhi na kuharibu mali katika ukumbi wa TPDC uliopo Mikocheni jijini Dar.Miriam akipelekwa kusaini hati ya dhamana huku akiwa amejifunika
Picha kwa hisani kubwa ya GPL

MIPANGO YA KILI MARATHON 2010 YAIVA

Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Suleiman Nyambui (kushoto) akifafanua jambo kwa wandishi wa habari jijini leo kuhusu mbio za nyika za 2010 ambazo zitafanyika mwishoni wa mwezi wa Februari 2010 mkoani Kilimanjaro. kulia ni Meneja ya Bia ya Kilimanjaro George Kavishe.
Mbio hizo za nyika zimedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, Vodacom Tanazania pamoja na makampuni mengine nchini ikiwemo kampuni ya KK Security,Tanga Cement. Good Year, Kilimanjaro Water,Tanzanite One, DT Dobie Tanzania, TPC, New Africa Hotel na Keys Hotel, jumla ya shilingi milioni 22 zitashindaniwa na wanariadha mabimbali wanaotarajiwa kushiriki katika mbio hizo .

TAARIFA TOKA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA - TFF

1. MAREKEBISHO YA KATIBA ZA WANACHAMA

Kama inavyofahamika TFF iliagiza wanachama wake wote kukamilisha marekebisho ya katiba zao kulingana na maelezo yaliyotolewa na TFF. Wanachama wote wa TFF(Vyama vya mpira wa miguu vya Mikoa, klabu za ligi kuu na vyama shiriki).TFF iliweka tarehe 15 februari 2010 kuwa mwisho wa wanachama wote kuwasilisha marekebisho ya katiba zao ili TFF iweze kuyapitia marekebisho hayo na haomaye kukamilisha zoezi zima ifikapo februari 28, 2010.Hata hivyo kazi ya wanachama kuwasilisha marekebisho ya katiba zao imekuwa si nzuri na kwahiyo TFF imeona ni vema kuongeza muda wa juma moja (siku saba (7) hadi tarehe 22 Februari 2010.
Kwa nyongeza hii ya muda wa kuwasilisha marekebisho ya katiba inamaana kuwa mwanachama yeyote ambaye hata kamilisha ndani ya muda huo, hataweza kuhudhuria mkutano mkuu wa TFF utakaofanyika Februari 27 na 28, 2010.

wanachama waliyowasilisha hadi sasa ni kama ifuatavyo:

Mkoa: Mwanza, Mara, Morogoro na Tanga.
KLabu za ligi kuu: Tanzania Prisons, Simba SC, Azam FC, Majimaji, Ruvu Stars JKT.
Vyama shiriki: Hakuna.

2. TIMU YA TAIFA - TWIGA STARS

Timu ya taifa - Twiga Stars inakabiliwa na mashindano ya kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wanawake zitakazofanyika Afrika Kusini baadae mwaka huu.
Twiga Stars imepangwa kuanza kampeni yake ya kufuzu kwa fainali hizo za Afrika kwa kupambana na Ethiopia kati ya tarehe 5-7 Machi 2010, katika mchezo utakaochezwa huko Ethiopia na baadaye kurudiana majuma mawili baadaye. Iwapo itafaulu kuitoa Ethiopia, Twiga Stars itacheza na mshindi kati ya Kenya na Eritrea baadaye Mei 2010.
Twiga Stars imeingia kambini siku ya Jumatatu Februari 15, 2010. Twiga Stars itakuwa chini ya kocha Charles Boniface na Adolf Rishard na kambi imeweka katika hoteli ya Lamada, Ilala Dar es Salaam huku mazoezi wakifanya katika uwanja wa KArume.
Gharama zote za Kambi na safari ni zaidi ya shilingi milioni 70. Kama inavyofahamika Twiga Stars haina mdhamini. Kwa hali hiyo TFF inajitahidi kutafuta fedha kutoka sehemu mbali mbali ikiwemo kwa wadau na jamii kwa ujumla.
Tunapenda kutumia Fursa hii kwa jamii nzima ya mpira wa miguu kuisaidia Twiga Stars ili iweze kushiriki kikamilifu katika michezo ya kufuzu.
Kutokana na majukumu ya Twiga Stars mashindano ya timu za mikoa za wanawake yaliyokuwa yafanyike kuanzia katikati mwa Februari yameahirishwa hadi itakapotangazwa tena.

3. MTIHANI WA UWAKALA WA WACHEZAJI

Mtihani wa uwakala wa wachezaji uttafanyika Alhamisi April 15, 2010 saa nne Asubuhi.

waombaji wa mtihani huo wanapaswa:

Kuwasilisha barua ya maombi TFF
Kuwa na elimu isiyopungua kidato cha nne
Aeleze ushiriki wake katika masuala ya Mpira
Ada ya Dola za marekani 50.

4. TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA 2010 AFRIKA KUSINI

TFF imekwishawasilisha maombi ya tiketi kwenye ofisi inayoshughulikia tiketi za kombe la Dunia.
Jumla ya tiketi ambazo Tanzania imepangiwa kama moja ya nchi ambazo timu zake hazishiriki ni 290.
Hata hivyo maombi ya tiketi yanazidi idadi ya tiketi ambayo Tanzania imepangiwa. Kwa hiyo TFF imewasilisha maombi kwa FIFA kwa ajili ya kupata nyongeza ya tiketi.
Kwa upande wa tiketi 290, kinachosubiriwa sasa ni invoice ya FIFA ili waliyoomba waweze kulipia tiketi zao. Kulingana na utaratibu wa FIFA ni kwamba waombaji wote watatakiwa kulipia tiketi zao ndani ya siku 10 tangu siku TFF itakapopokea invoice.

Fredrick Mwakalebela
KATIBU MKUU - TFF

Monday, February 15, 2010

RADIO TIMES FM WALA VALENTINE NA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

Katika kusherehekea sikukuu ya wapendanao maaurufu Valentine hapo Radio Times Fm ilijumuika na watoto wanaoishi katika mazingira magumu toka vituo tofauti katika uwanja wa karume na kushow luv vya kutosha.Hawa ni watoto wakicheza katika siku ya Valentine pamoja na wafanyakazi wa Radio Times Fm.Ukweli walijiachia vya kutosha na kusahau hata kama wanatoka matika mazingira magumu.Huyu kkijana anaitwa Hamisi anatokea kituo cha kulelea watoto cha Dogo Dogo Center, hapa ilikuwa ni baada ya kushinda shindano la kucheza akiondoka na miondoko ya KIDUKWI.Hawa ni watoto wakkishindana kujaza maji katika chupa, ilikuwa burudani sana.hawa walikuwa wakishindana kukimbia huku wakiwa wamefungwa miguu, ama kweli upele ulipata mkunaji.wakati michezo mingine ilipokuwa ikiendelea, kwa watoto wenye vipaji vya uchoraji nao walionyesha umahiri katika staili ya aina yake ya kuwapendeza wenzao kwa michoro tofauti tofauti.Hebu ona watoto walivyopendeza na michoro ambayo inamaua ambayo naamini kabisa mchoraji anamaanisha mtoto anapaswa kuanza kujengwa tangu akiwa mdogo kupenda asili ya Mtanzania.Hapa ilikuwa ni mashindano ya kumpata nani mjanja ambaye atabaki peke yake akiwa ameketi katika kiti, picha ya kwanza kulia ndivyo mchakato ulivyoanza huku picha ya katikati ndiyo mshindi alivyopatikana.Hiki ni kikund cha Wanne Stars nacho kiliungana na Radio Times FM kushow luv na watoto wanaoishi katika mazingira magumu, ebwana jamaa ni wakali katika michezo ya utamaduni.Hapa wafanyakazi wa Radio Times FM wakijiandaa kuingia uwanjani tayari kusakata kandanda na watoto wanaoishi katika mazingira magumu, mwenye Singlend ni mkurugenzi wa Radio TIMES FM naye hakuwa nyuma.Panapo mkusanyiko wowote hatari inaweza kutokea, hawa ni watu wa msalaba mwekundu walikuwepo bega kwa bega na RAdio Times FM kuhakikisha wanatoa huduma ya kwanza.Hapa mzee wa viwanjani akipozi na jamaa aliyevalia sanamu la katuni niipendayo ya BEN 10, kazi ilikuwa moja tu ni kupiga picha kwa kwenda mbele.
Hata hivyo Shukrani za pekee ni kwa Marrybrown waliyotoa vifaa vya kuchezea watoto na kampuni ya SBC watengenezaji wa Pepsi ambao walitoa vinywaji.

Thursday, February 11, 2010

NGUZA MBANGO NA FRANCIS NGUZA WAACHIWA HURU, VIKING NA PAPII NGUZA WARUDI JELA!!

Maofisa Magereza wakiwasindikiza washtakiwa wa familia moja wa kosa la kulawiti watoto,kuingia katika Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam leo asubuhi. kuanzia kushoto ni Nguza Vickig na wanawe Papy Nguza,Nguza Mbangu,Francis Nguza.
Familia ya Mwanamuziki Nguza Viking imemuomba Raisi Jakaya Kikwete kuingilia kati suala la kuendelea kukaa gerezani kwa mwanamuziki huyo na mwanaye JohnSon Nguza maarufu Papii Kocha.
Ombi hilo limetolewa leo na shangazi wa nguza viking, bibi Mwisha Matuka Bizoo, baada ya mahaka ya Rufaa kuwaachia huru, watoto wao, Francis Nguza na Nguza Mbangu na kumrejesha Gerezani mwanamuziki huyo na mwanawe Papii Kocha.
Nguza Viking, na watoto wake watatu walihukumiwa kifungo cha maisha Jela mwaka 2004 na mahaka ya hakimu mkazi kisutu Jijini Dar es Salaam baad ya kupatikana na hatia ya kuwadhalilisha kijinsia waoto wa kike eneo la sinza jijini.Nguza na mwanae Papii Kocha wakirejeshwa lupango kutumikia kifungo cha maisha.
Hata hivyo, baada ya hukumu iyo kupitiwa upya na majaji wa tatu, Bwana Salum masati, Bwana Mbaruk Mbaruk, wakiongozwa na Bwana Nathalia Kimaro, makama hiyo imebaini kuwa watoto wawili wa Nguza Viking, Fransis Nguza na Nguza Mbangu walifungwa kimakosa.
Akisoma huku hiyo, Jaji Neema Chusi, amesema wakati makosa hayo yakifanyika jijini Dar es Salaam, Nguza Mbangu, alikuwa kwenye ziara za kimuziki, na Fransis Nguza, alikuwa Shuleni.

Wednesday, February 10, 2010

TFF YATANGAZA VIGEZO VYA KUMRITHI MAXIMO

Shirikisho la soka Tanzania (TFF) jana lilitangaza sifa nane za msingi ambazo kocha mpya wa timu ya taifa, Taifa Stars, anatakiwa awe nazo.
TFF imefikia maamuzi hayo baada ya wajumbe wa kamati ya utendaji wa shirikisho hilo kukutana wiki iliyopita na kukubaliana sifa ambazo mrithi wa Mbrazili, Marcio Maximo, anatakiwa awe nazo.
Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela, alisema jana kuwa kocha mpya ajaye anatakiwa awe na kiwango cha elimu kuanzia ya sekondari, uwezo wa kuzungumza, kusoma na kuandika Kiingereza, na awe elimu ya kiwango cha kuanzia diploma ya kufundisha soka kutoka katika chuo kinachotambulika. Na sifa ya ziada, awe na leseni ya ualimu wa soka inayotambulika kimataifa. Mwakalebela alitaja sifa nyingine kuwa ni awe na cheti cha ukufunzi wa makocha wa soka, umri kuanzia miaka 30 na pia awe na uzoefu usiopungua miaka mitano wa kufundisha timu za daraja la juu (timu za taifa ni sifa ya ziada).
Alisema pia rekodi nzuri ya kufundisha katika nchi zinazoendelea ni sifa ya ziada ya kocha huyo anayetaka kutuma maombi yake, huku sifa nyingine ikiwa ni kuwa mwadilifu na mwenye haiba.
"Pia awe na uwezo wa kuwasiliana na wasaidizi wake na wakuu wake wa kazi," alisema katibu huyo.
Aliongeza kuwa sifa nyingine ya kocha huyo mpya ni lazima awe na uwezo wa kutumia kinakilishi (kompyuta) na programu za kisasa.
Mwakalebela alisema pia ni lazima kocha huyo awe na maarifa ya kuongoza jopo la ufundi na mbinu za kisasa za ufundishaji wa mchezo huo.
Alisema kwamba makocha wote wanaotaka ajira hiyo mpya wanatakiwa kuanza sasa kutuma maombi yao na mwisho ya kufanya hivyo ni Februari 28. “Waombaji watume maombi yao kwa katibu mkuu wa TFF,” alisema.
Alisema kocha huyo atakuwa na majukumu ya kuandaa programu za muda mrefu, kati na fupi kulingana na mashindano yanayomkabili huku akilinda nidhamu ya wachezaji.
Kocha huyo mpya pia atakuwa na jukumu la kuendesha mafunzo ya ualimu wa mchezo huo hapa nchini pale atakapopangiwa kufanya hivyo huku pia akitakiwa kuwa karibu na makocha wa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Daraja la Kwanza.

SIMBA YATAKIWA KUFANYA UCHAGUZI KABLA YA MECHI 3

KAMATI ya Michezo ya Wilaya ya Ilala, imeiagiza klabu ya Simba ifanye uchaguzi wake mkuu ndani ya Machi 3 mwaka huu, vinginevyo Serikali itaingilia kati.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Mwenyekiti wa kamati hiyo, Prisca Kissila amesema, Kamati ya Michezo inauagiza uongozi wa klabu hiyo uhakikishe lazima unafanya uchaguzi ndani ya siku 90 kutoka Desemba 3 mwaka jana.
Amesema kwa hiyo watalazimka kufanya uchaguzi kabla ya Machi 3 mwaka huu, sera ya maendeleo ya michezo inawalazimisha kifungu namba sita lazima waheshimu kipindi cha uongozi.
Kissila amesema , katika kikao walichokaa juzi (jana) maagizo yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya kwa Kamati hiyo yafuate katiba ya Simba pamoja na sheria namba 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake namba 6 mwaka 1971 ya Baraza la Michezo la Taifa na kanuni za usajili namba 442 za mwaka 1999.
Aidha ameongeza kwamba uongozi wa Simba uliomaliza muda wake, ulitakiwa kuitisha mkutano simu 30 kabla ya kumaliza kipindi cha uongozi au baada ya siku 30, lakini uongozi haukufanya hivyo.
Kissila amesema, uongozi wa Simba umekiuka katiba ya chama chao pamoja na kanuni za Baraza la Michezo la Taifa, uliitisha mkutano mkuu ndani ya siku 46.
Aidha amesema muhtasari wa kikao haukuletwa kwa msajili tangu wamalize kikao chao, katiba yao inasema Kamati ya Utendaji itapanga tarehe ya Uchaguzi Mkuu na si Mkutano Mkuu, lakini uongozi wa Simba ulidai mkutano utapanga tarehe ya uchaguzi ni kinyume na katiba yenye ridhaa yao.
Hata hivyo kabla ya ofisi ya msajili haijatoa ufafanuzi kundi la baadhi ya wanachama wa Simba wakiongozana na aliyekuwa katibu Mwenezi, Said Rubeya 'Seydou' lilivamia ofisi ya msajili huyo huku wakiwasonga viongozi waliowakuta kwa kuwalalamikia kuwa ndio wanaokwamisha uchaguzi.
Hata hivyo Kissila amesema, viongozi wa Simba jana waliitwa na Mkuu wa Wilaya lakini wamekaidi agizo hilo, hivyo Mkuu huyo ameahidi kuwatafuta ili waweze kutoa tamko la terehe ya uchaguzi kama walivyoamuliwa.

Tuesday, February 9, 2010

RONALDINHO ATEMWA TIMU YA TAIFA BRAZILI

Mchezaji Ronaldinho huenda akaikosa michuano ya soka Dunia baada ya kuachwa katika kikosi cha Taifa cha Brazili ambacho kinajiandaa na michezo ya kirafikki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea Afrika Kusini.
Ataukosa mchezo utakaopigwa katika dimba la Emirates dhidi ya timu ya taifa ya Ireland utakaopigwa Machi 2.
Nyota huyo anayeichezea klabu ya AC Milan hajaichezea timu ya taifa ya Brazil tangu kuanza kwa mwaka 2009, lakini kwa sasa ameonekana kuimarika zaidi huku mashabiki wa soka wa Brazili wakishinikiza aitwe katika timu ya taifa.
Lakini kocha Dunga amekataa kufuata msukumo wa mashabiki pamoja na vyombo vya habari kumuita nyota huyo wa zamani wa Barcelona.
Dunga ambaye alikuwa kapteni katika kikosi cha Brazili kilichotwaa uchampion wa Dunia mwaka 1994 ameendelea kuwa waamini kina Michel Bastos (Lyon), Juan na Doni ambao wote wanacheza soka katika klabu ya AS Roma, Kleberson (Flamengo) na Gilberto (Cruzeiro).
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Robinho, ambaye anacheza kwa mkopo katika klabu ya Santos, amejumuishwa katika kikosi cha taifa pamoja na kiungo wa Liverpool Lucas. lakini hakuna nafasi kwa kiungo wa Manchester United Anderson.
Ronaldinho alikuwa mmoja wa wachezaji waliyokiwezesha kikosi cha Brazili kutwaa uchampion wa Dunia mwaka 2002 na ndiye aliyeitoa England katika michuano hiyo baada ya kumdanganya golikipa David Seaman kwa shuti la mpira uliyokufa.
Mkongwe wa soka wa Brazil Pele ni mmoja wa watu ambao waliomba Ronaldinho ajuimuishwe katika kikosi kitakachotinga katika fainali za Dunia.
Ronaldhinho amejitokeza mara 87 katika timu ya taifa ya Brazili, akifunga jumla ya magoli 32.
Lakini pia amefanikiwa kutajwa mara mbili kuwa mwanasoka bora wa Dunia mwaka 2004 na 2005 na amefanikiwa kutwaa tuzo ya Ballon d'Or ama (european player of the year) mara moja.
________________________________________
Brazil squad to face Ireland:
Goalkeepers: Julio Cesar (Inter Milan), Doni (Roma).
Defenders: Maicon (Inter Milan), Daniel Alves (Barcelona), Gilberto (Cruzeiro), Michel Bastos (Lyon), Juan (Roma), Lucio (Inter Milan), Luisao (Benfica), Thiago Silva (AC Milan).
Midfielders: Gilberto Silva (Panathinaikos), Josue (Wolfsburg), Felipe Melo (Juventus), Lucas (Liverpool), Kaka (Real Madrid), Ramires (Benfica), Elano (Galatasaray), Julio Baptista (Roma), Kleberson (Flamengo).
Forwards: Robinho (Santos), Adriano (Flamengo), Nilmar (Villarreal), Luis Fabiano (Seville).

Monday, February 8, 2010

MATUMLA APIGWA UJERUMANI NA BENJAMIN SIMON

Bondia wa ngumi za kulipwa anayeshikilia mkanda wa Dunia unaotambulika na Shirikisho la ngumi la IBF Benjamin Simon wa Ujerumani amemdunda bondia wa Tanzania Rashidi Matumla kwa pointi pambano lililofanyika jana usiku nchini Ujerumani.
Mwamuzi namba moja pawel kandyn ametoa pointi 118 kwa 110 mwamuzi namba mbili claus greysel pointi na 119 kwa 109 mwamuzi namba tatu Ben decrosy ametoa pointi 119 kwa 109.
Akizungumzia pambano hilo kocha wa Rashidi Matumla ambaye ndiye mwandaji wa safari hiyo Ally bakari Champion amesema kwamba mchezo huo kwa bondia wake ulikuwa mgumu lakini amecheza mchezo mzuri na amemtumia salam Bondia Franciss Cheka wa Morogoro.

Sunday, February 7, 2010

SAYORE AIBUKA MSHINDI GOFU ZAIN


Ali Mfuruki akipiga mpira kwelekea shimoni wakati wa mashindano ya kila wiki ya gofu ya Lugalo yanayofanyika kwenye viwanbya vya Gofu Lugalo, Zain inadhamini klabi ya Gofu ya Lugalo ili wasaidie kukuza mchezo wa Gofu nchini.
Mchezaji gofu wa klabu ya Lugalo Kibuna shabani akijiandaa kupiga mpira kwelekea shimoni, wakati wa mashindano ya kila wiki ya gofu ya Lugalo yanayofanyika kwenye viwanja vya Gofu Lugalo, Zain inadhamini klabu ya Gofu ya Lugalo ili wasaidie kukuza mchezo wa Gofu nchini.Generali mstaafu Gideon Sayore ameibuka mshindi wa jumla wa mashindano ya mchezo wa gofu yanayofanyika kila Ijumaa katika viwanja vya gofu vya Lugalo vya Jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Zain.
Sayore amejishindia simu mpya ya mkononi aina ya Zain Phone ambayo ndio ilikuwa zawadi ya juu pamoja na chupa ya wine kutoka Zain baada ya kupata pointi 38.Ofisa Uhusiano wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Daudi Helela alisema juzi kwamba jumla ya wachezaji 67 walijitokeza katika mashindano ya Ijumaa iliyopita.
‘’Wachezaji wanajitokeza wengi wiki hadi wiki na klabu sasa inasisimka kila Ijumaa. Tunawachezaji wenye vipaji ambao wanaweza kushirikia hata mashindano ya kimataifa. Hakika tunawashukuru Zain kwa udhamini wa Klabu yetu ya Lugalo.
Zain ina mkataba wa miaka mitatu kudhamini klabu ya gofu ya Lugalo, lengo la Zain ni kusaidia kukuza mchezo wa gofu ili upendwe zaidi nchini kama michezo mingine na imekuwa ikitoa zawadi mbali mbali ikiwemo zawadi kubwa kama simu za aina ya Blackberry ili kuwavutia wachezaji.

Wednesday, February 3, 2010

TID NA CHIDI BENZI NDANI YA NGOMA MOJA

Yapo majina ya wasanii wa kizazi kipya ambao ukisikia wameshirikiana(collaborate)kutengeneza kazi fulani, basi unakuwa na imani kubwa kwamba kazi hiyo ina nafasi kubwa ya kuwa nzuri. Hiyo inatokana na uzoefu na pia zingatio za kazi zao zilizopita,nafasi waliyonayo katika uwanja mpana wa sanaa ya muziki na mambo kama hayo.
Hivi karibuni nilipoletewa kazi mpya na kuambiwa kwamba wasanii waliomo katika kazi hiyo ni TID(Top in Dar) na Chid Benz, nilikuwa na uhakika kwamba kazi hiyo itakuwa imesimama.TID na Chid ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao binafsi nawaheshimu na sioni noma kusema kwamba nazipenda nyingi kati ya kazi zao.Habari nzuri ni kwamba hawakuniangusha katika kazi hii ya hivi karibuni inayokwenda kwa jina Huyu.
Kama zilivyo kazi nyingi za wasanii wetu siku hizi,hii pia ni hadithi ya mapenzi (bado natamani wigo wa yaliyomo(content) za kazi za wasanii upanuke zaidi na kugusa maeneo mengine yanayoizunguka jamii).Kinachoufanya wimbo huu uwe tofauti ni uwezo binafsi wa wasanii husika na hadithi yenyewe.
Kazi hii imepikwa pale Tetemesha Records(kule kule alikoibukia Hussein Machozi) chini ya George Mpanda au maarufu kama Kid Bwoy.

NGUMI: KUCHEZA TIMU YA TAIFA KAZI

Bondia wa timu ya taifa ya ngumi za ridhaa Joseph Mart akitupa ngumi kwa mpinzani wake Hapson Julias wakati wa mashindano ya kuchagua timu ya taifa yaliofanyika Dar es salaam.(Picha na Rajabu Mhamila)

SKUVI KUSAIDIA SOKA LA VIJANA

Mkurugenzi wa Kampuni ya SKUVI, Laibai Kallahe (kushoto) akimkabidhi jezi zenye thamani ya shilingi laki 1.3, Kocha masaidizi wa Timu ya kuinuwa vipaji vya watoto wadogo ya Serengeti iliyopo Kawe Dar es salaam mwishoni mwa wiki, Baton Daudi kwa ajiri ya lengo la kuendeleza na kukuza mchezo uho.(PIcha na Rajabu Mhamila)

TAMBO ZA MADA MAUGO ZA ZIMWA NA MANENO OSWAD MTAMBO WA GONGO

Bondia Mada Maugo alivyofulia kwa maneno Oswad Mtambo wa Gongo.Bondia Maneno Osward akichuwana vikari na mpinzani wake Mada Mahugo wakati wa pambono la kirafiki lililofanyika Dar es salaam Maneno alishinda kwa pointi.(Picha na Rajabu Mhamila)Bondia Mada Mahugo (kushoto) akilusha konde bila mafanikio kwa mpinzani wake Maneno Osward wakati wa pambano lao lililofanyika DAr es salaam Maneno alishinda kwa point.(Picha na Rajabu Mhamila)Bondia Anton Mathias kulia akitupa konde wakati wa mchezo wake na Nasabu Ramadhani lililofanyika Dar es salaam Nasibu arishinda kwa Point.(Picha na Rajabu Mhamila)

BWAGA MOYO WATOA SOMO DAR ES SALAAM

Muumin Mwijuma na Manda Parapanda wakiwajibika wakati wa onesho la bendi ya Bwaga Moyo lililofanyika katika ukumbi wa Afri Center Ilala, Dar es Salaa.

MSONDO WAJIPANGA NA NYIMBO MPYA

Wanamziki wa msondo music bandi wakifanya mazoezi ya nyimbo mpya ya 'Dawa ya deni kulipa' katika kambi yao iliyopo Amana kushoto ni Hamisi Kuyugwa na Sady Ally.(Picha na Rajabu Mhamila)
BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini Msondo Music bendi inatarajia kufanya ziara ya utambulisho wa albam yao mpya ya huna shukrani Mkoani Tanga mapema mwezi huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema sambamba na kutambulisha albamu hiyo pia ziara hiyo ni maalum kwa ajili ya kutakiana kheri ya mwaka mpya ikiwa ni pamoja na kusheherekea sikukuu ya wapendanao na wakazi wa Jiji hilo.
Alisema katika sherehe hizo mashabiki watapata nyimbo mpya ambazo wamezitunga kwa ajili ya alabamu yao mpya ya mwaka huu ikiwa ni pamoja na zile zilizopo katika albamu hiyo ya Hunashukurani huku ikisindikizwa na nyimbo zilizotamba katika miaka ya nyuma.
Alizitaja nyimbo hizo mbili mpya kuwa ni Lipi jema uliotungwa na Eddo Sanga na Dawa ya deni kulipa uliotungwa na Isihaka Katima 'dj papa upanga' ambao umefanyiwa kazi na kukamilika ambapo itakuwa ni zawadi kwa wakazi wa mkoa huo.Alisema sambamba na zawadi hiyo pia alizitaja nyimbo zilizokuwa katika alabamu ya Huna Shukrani kuwa ni pamoja na Kiapo (husein jumbe) haki yangu ipo wapi (Uluka Uvuluge) Mama Cos, uliotungwa na marehemu (Josephe Maina) Albino (Juma Katundu) Machimbo Isihaka Katima dj papa upanga) na Cheo ni Dhamana (Eddo Sanga)
Aidha aliwataja wanenguaji watakaokuwa wanatoa burudani katika safu hiyo kuwa ni Amina Said 'quen Emmy' Nacho Mpendu 'mama Nzawisa' na Amiri Saidi 'Dongo' aidha rapa wa bendi hiyo Romani Mng'ande 'Romario' atawachenguwa mashabiki watakaofika katika onesho hilo wakiongonzwa na mkurugenzi wa bendi hiyo Muhidini Gurumo,na kiongozi wa bendi hiyo Saidi Mabela.

ZAIN NA HUDUMA YA NIPE NIKUPE

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Zain Bwa. Kelvin Twissa, Ofisa Mwandamizi wa Kampuni hiyo Afrika na Mkurugenzi, Khaled Muktad, wakionesha vipeperushi wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya 'Nipe Nikupe' ambapo mteja atapata nyongeza ya muda wa maongezi kadri atumiavyo, Dar es Salaam.(Picha na Rajabu Mhamila)

Monday, February 1, 2010

BEBE COOL APIGWA RISASI BAADA YA SHOW YA R. KELLY

Mwanamuziki wa miondoko ya ragga muffin Moses Ssali, a.k.a Bebe Cool ameripotiwa kupigwa risasi siku ya jumamosi asubuhi na Polisi.
Hatahivyo Polisi na mwanamuziki huyo ambaye amelazwa chini ya uangalizi maalum.
Akizungumza akiwa amelala kitandani katika Hospitali ya Nsambya, Bebe Cool amekanusha taarifa iliyotolewa kwamba kulikuwa na ugomvi kati yake na Polisi ambaye alimpiga risasi.
Lakini pia amekanusha madai ya kwamba alikutwa akifanya mapenzi na wanawake wawili katika gari katika eneo ambalo hairuhusiwi kupaki, sehemu ambayo Polisi huyo alitaka kuwakamata kufuatia kuegesha gari sehemu ambayo siyo sahihi.
“Polisi amenipiga risasi mara nne. sikuwa na hatia. lakini hili linafanyiwa uchunguzi,” anasema Bebe Cool wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Tukio hilo la shambulio lilitokea nyuma ya Supermarket ya Nakummat muda mchache baada ya mwanamuziki kuondoka katika baa na mgahawa wa Effendy, ambao unatazamana na Centenary Park. Risasi alizopigwa pia zilimpata Polisi David Oluka ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mulago Hospital.
Mapema usiku huo, Bebe Cool alikuwa akiperform katika tamasha lililohudhuriwa na mwanamuziki nyota wa Marekani Robert Kelly katika klabu ya usiku ya Silk.
Hata hivyo Weasel wa kundi la Goodlife amedai kwamba Bebe alipigwa risasi baada ya kutaka kupambana na Polisi.

MARIGA: MKENYA WA KWANZA KUCHEZA LIGI KUU ENGLAND???

McDonald Mariga akiwa na klabu ya Parma FC akimtoka Jedaias Jeda aliyeanguka chini wa klabu ya Cagliari Calcio katika mchezo wa ligi kuu ya Italia maarufu Serie A katika mchezo dhidi ya Parma FC na Cagliari Calcio katika dimba la Ennio Tardini September 27, 2009 mjini Parma, Italy.
Kiungo wa kimataifa wa Kenya Macdonald Mariga anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na matajiri wapya wa England Manchester City akijiunga na klabu hiyo akitoa klabu ya Parma FC ya Italia.
Mariga atakuwa mchezaji wa kwanza toka Kenya kufanikiwa kucheza katika ligi kuu ya England.
Manchester City imeripotiwa kukamilisha taratibu zote na klabu ya Parma kwa ajili ya kumnunua kiungo McDonald Mariga aliyetokea kutamba na klabu hiyo kongwe nchini Italia.Mariga alijiunga na Parma mwaka 2007 kwa mkopo akitokea Helsingborgs, lakini baadae waliamu kumsajili moja kwa moja baada ya kuvutiwa na kiwango chake.
Kiungo huyo mkabaji amekuwa akizidi kuwa bora kila siku na amekuwa akiwindwa na klabu mbali kwa mida mrefu sasa ikiwa ni pamoja na Arsenal na Inter Milan.
Lakini kocha wa Manchester City Roberto Macini sasa ameripotiwa kufanikiwa kuwashawisho matajiri wa klabu hiyo kumnunua kwa dau la Pauni milioni saba.
Mama yake Mariga Mildred Wanyama ameripotiwa nchini akisema anamuombea mwanawe afanikiwe hilo.Manuel Pasqual wa klabu ya ACF Fiorentina akichuana na McDonald Mariga wa Parma FC wakati wa mchezo wa Serie A kati ya Fiorentina na Parma katika uwanja wa Artemio Franchi Novemba 21, 2009 mjini Florence, Italy.
Hata hivyo kufuatia Kenya kuwa nafasi ya 98 kiungo huyo mkabaji ameshindwa kupata kibali cha kufanya nchini England, hivyo dili kama kuingia mchanga vile.
klabu ya Inter Milan sasa itakuwa nanafasi kubwa ya kumnyakua.

SERIKALI YA TOGO - KUFUNGIWA NI KUDHARAU TAIFA

Serikali ya Togo imekasirishwa na kitendo cha kufungiwa na shirikisho la soka barani Afrika kwa miaka minne imetishia kuwashukulia hatua zaidi za kisheria.
"Haya ni maamuzi ya kushitukiza sana nah ii inamaanisha hawa watu yaani (Caf) hawana uchungu wowote na maisha ya binaadamu," Anasema waziri wa mambo ya ndani wa Togo Pascal Bodjona.
Ameongeza kuwa hatua hiyo ni dharau kwa taifa la Togo na familia za wale ambao ndugu zao walipoteza maisha pamoja na wote waliyoathirika na shambulio hilo.
Amesema wanasubiri taarifa rasmi ndipo watachukua hatua za kisheria kutatua tatizo hilo.
Shirikisho la kandanda Dunia limekataa kuzungumza chochote dhidi ya hatua ya kufungiwa Togo.
Taarifa ya Caf ilikuwa ikisema: "kamati ya utendaji imeifungia Togo kutoshiriki fainali mbili za mataifa ya Afrika na kukitoza chama cha soka cha nchi hiyo kiasi cha Dola za marekani 50,000."
Kocha msaidizai wa timu ya taifa ya Togo na Afisa habari walipoteza maisha wakati basi lao liliposhambuliwa mjini Cabinda Januari 8 walipoteza maisha na serikali kulazimika kuirudisha timu ya taifa nyumbani kwa ajili ya maombolezo ya siku tatu.