Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, September 28, 2009

MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA MASHINDANO YA KIMATAFA YA NETBALL

Timu ya Taifa ya Netball ya Tanzania imeanza vema michuano ya kimataifa ya Netball katika uwanja wa Taifa kwa kuichapa Lesotho jumla ya magoli 33 - 19
Lesotho hoi, wakimbizwa mbaya uwanja wa Taifa katika mashindano ya kimataifa
KAMA ANASEMA ....ACHAA
KWANINI HIVI TUSIFANYE VIZURI KIMATAIFA ?
HAPA KWELI LAZIMA TUTISHE... ONA KAZI HII
Mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ya Netiboli,(Taifa Queens), ambaye ni nahodha wa timu hiyo Jackline Sikozi (kushoto) akimtoka mchezaji wa timu ya Taifa ya Lesotho, Malestephano Matrepe wakati wa ufunguzi wa mashindano ya netiboli ya kimataifa yaliyofunguliwa Dar es salaam jana.9Picha na Rajabu Mhamila)Mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ya Netiboli,(Taifa Queens), Judith Kaginja (kushoto) akitafuta njia ya kumtoka mchezaji wa timu ya Taifa ya Lesotho, Lumbata Pitro wakati wa ufunguzi wa mashindano ya netiboli ya kimataifa yaliyofunguliwa Dar es salaam jana Tanzania ilishinda kwa 33 kwa 19.(Picha na Rajabu Mhamila)Mke wa raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akiwasalimi wachezaji wakti wa ufunguzi wa michuano ya Netball ya kimataifa.

MISS TANZANIA KATIKA MICHEZO

Mshiriki wa shindano la Vodacom miss Tanzania Stela Chidodi, akijiandaa kupiga mpira Dar es salaam wakati wa siku ya michezo kwa warembo hawo.(Picha na Rajabu Mhamila)
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Urembo Vodacom miss Tanzania wakiwa katika mchezo wa kuvuta kamba wakati wa siku ya michezo ya washiriki hawo iliyofanyika Dar es salaam jana.(Picha na Rajabu Mhamila)

WADAU HAPO VIPI...? USAFI

Mchuuzi wa Takataka akizoa katika mtaa wa Mkunguni Dar es salaam kama dhana ya kuimarisha usafi katika mkoa huu.(Picha na Rajabu Mhamila)

TASAF NA MPANGO WA KIJAMII

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (tasaf) Bw.Servacius Likwelile, (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam kuusu Mpango wa kijamii wa Uhawilishaji fedha kwa kaya masikini utakaozinduliwa kesho Kibaha Mkoa wa Pwani (kushoto) ni Mkurugenzi mwendeshaji wa Mfuko uho Bw. Erasto Machume.(Picha na Rajabu Mhamila)
TANZANIA SOCIAL ACTION FUND
Press Release

OFFICIAL LAUNCH OF THE COMMUNITY BASED CONDITIONAL CASH TRANSFER (CB CCT) PILOT PROGRAMME, MAILI MOJA GROUND, KIBAHA, PWANI REGION,
TUESDAY, 29 SEPTEMBER 2009

MPANGO WA KIJAMII WA UHAWILISHAJI FEDHA KWA KAYA MASKINI

1.0 Official Launch of the Community Based Conditional Cash Transfer Pilot Programme
Following completion of initial/preparatory activities, namely sensitization, baseline data collection (by consultant), targeting, supply side capacity assessment, enrolment, training on payment including opening of back accounts by CMCs and development of the MIS modules for respective stages; official launch of the CB-CCT Pilot Programme is scheduled for Tuesday, September 29, 2009 at Kibaha Maili Moja Ground., from 09:30 am – 11.30 am. The Minister of State in the President Office (Good Governance), Hon Sophia Simba will officiate at the Launch.

Saturday, September 26, 2009

AFRICAN LYON YAFANYA KWELI KAMA LIVERPOOL

HILI NI BENCHI LA UFUNDI LA KLABU YA AFRICAN LYON WA PILI TOKA KULIA NI KOCHA MRENO EDWARD ALMEIDA AKIFUATILIA MCHEZO.
AFRICAN Lyon imezinduka katika mechi ya Ligi Kuu soka Bara baada ya kuilaza Toto African mabao 6-1 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Huku wakiwa kwenye mvutano na Kocha wao kutoka Ureno, Eduardo Almeida kutoka Ureno kutokana na Lyon kufanya vibaya jana mambo yalibadilika.
Lyon ikiwa na pointi moja baada ya mechi nne jana ilicharuka na huku ikiongozwa na Mremo huyo ambaye baadhi ya vyombo vya habari viliripoti amefukuzwa iliibuka na ushindi mkubwa tangu ligi hiyo ianze msimu huu.
Timu hiyo yenye makazi yake Mbagala iliwanyanyasa watoto wa Yanga, Toto kama ilivyofanya Liverpool kwa Hull City katika Ligi Kuu ya England jana kwa kushinda 6-1.
Bao la African Lyon lilipatikana dakika ya kwanza kwa shuti la mpira wa adhabu uliopigwa na Rashid Gumbo na kumshinda kipa Hussein Katandula.
Dakika ya 29, Robert Sentongo aliifungia Lyon bao la pili baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Idrisa Abdallah.
Toto ilipata bao la kwanza dakika ya 61, lililofungwa na Maulid Hanim baada ya kuwalamba chenga mabeki wa Lyon na kuusukumia mpira wavuni.
Hata hivyo, furaha yao ilizimwa dakika moja baadaye kufuatia bao lililofungwa na Yusuph Soka baada ya kuwatoka mabeki wa Toto na bao la nne lilifungwa pia na Soka.
Mbwana Samatta aliipatia Lyon bao la tano na dakika ya 74 na dakika ya 83, Samata alifunga bao la sita.
Mara baada ya mechi hiyo kumalizika, Kocha Mkuu wa Toto African, Mbwana Makatta, alisema tangu aanze kuifundisha timu hiyo, hajawahi kupata kipigo kama hicho.
Makatta alikiri kuzidiwa na African Lyon na kwamba yote hayo yamesababishwa na baadhi ya wachezaji kuwa na matatizo na uongozi na wengine walipata kadi nyekundu.

ZAIN LUGALO FIDDLE YA FANA

Mcheza gofu, Profeser Kamzora akijiandaa kupiga mpira wakati wa mashindano ya gofu ya Zain Lugalo Fiddle yaliyofanyika Ijumaa katika uwanja wa TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam . Mashindano hayo yalidhaminiwa na Zain Tanzania .Mchezaji gofu Gidion Sayore (kulia) akipokea zawadi ya kikombe cha kuhifadhi maji Moto kutoka Zain ( Mag) kutoka kwa Samon Sayore baada ya kuibuka mshindi wa pili kwa wazee katika mashindano ya gofu ya Zain Lugalo Fiddle yaliyofanyika katika uwanja wa gofu wa TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam .Mchezaji gofu kutoka Morogoro Mama Chilipachi (kulia) akipokea zawadi ya seti ya vyombo vya kunywea chai kutoka kwa Samon Sayore baada ya kuibuka mshindi wa jumla katika mashindano hayo ya gofu ya Zain Lugalo Fiddle yaliyofanyika katika uwanja wa gofu wa TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam .Mchezaji gofu Sara Denisi (kulia) akipokea zawadi ya kikombe cha kuhifadhi maji ya Moto kutoku Zain ( Mag) kutoka kwa Samon Sayore baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwa wasichana katika mashindano ya gofu ya Zain Lugalo Fiddle yaliyofanyika katika uwanja wa gofu wa TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam. Mcheza gofu, Sophia Mathias akiingiza mpira katika shimo wakati wa mashindano ya gofu ya Zain Lugalo Fiddle yaliyofanyika Ijumaa katika uwanja wa TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam .Mashindano hayo yalidhaminiwa na Zain Tanzania .Mchezaji wa gofu, Hatibu Senkoro akiingiza mpira katika shimo wakati wa mashindano ya gofu ya Zain Lugalo Fiddle yaliyofanyika Ijumaa katika uwanja wa TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam . Mashindano hayo yalidhaminiwa na Zain Tanzania .Mchezaji gofu, Amina Hamisi akijiandaa kutumbukiza mpira katika shimo wakati wa mashindano ya gofu ya Zain Lugalo Fiddle yaliyofanyika Ijumaa katika uwanja wa TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam . Mashindano hayo yalidhaminiwa na Zain Tanzania .

Friday, September 25, 2009

TBF WAANDAA TAMASHA LA KIHISTORIA

Jaji mkuu Agostino Ramadhani (kushoto) ambaye ni mlezi wa mpira wa kikapu Tanzania BFT akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la kuchangisha fedha zitakazojenga viwanja sita vya mchezo huo nchini.
Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania Limeandaa tamasha la kihistoria litakalojulikana kama BASKETBALL CHARITY DAY litakaloanza tarehe 17 oktoba,2009 na kuhitimishwa tarehe 24 Oktoba,2009, likiwa na madhumuni ya kuchangia maendeleo ya mpira wa Kikapu Nchini.
Amesema wanatazamia kuwa Mgeni wa heshima ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa jamuhur ya Muungano wa Tanzania, ambaye alikuwa Mlezi wa Shirikisho wa shirikisho, atakuwa mgeni rasmi na atajumuika katika kilele cha tamasha hilo.
Katika kufanikisha hilo, siku ya kilele kutakuwa na kadi maalum za aina nne, kadi za dhahabu, ya fedha, ya shaba na za kuchangisha kwa makundi.
Kiwango cha chini cha kuchangia kadi ya dhahabu ni Tsh 500,000/= ambapo kwa kadi ya fedha ni Tsh 300,000 kwa wale watakaochangia chini ya Tsh 300,000/= watapewa kadi ya shaba .
Wale wa kadi ya dhahabu watapata fursa ya kucheza au kushangilia timu ya wachezaji wa zamani.
wale wa kadi ya fedha watakuwa upande wa timu itakayoshindana na timu ya wakongwe.

TIMU YA TAIFA YA NETBALL YAJIFUA

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Netbol Wanawake, Naima Boll (kulia) akijiandaa kudaka mpira uku mchezaji wa timu ya taifa wanaume Benjamini Majiga, akijiandaa kuudaka wakati wa mchezo wao wa kujipima nguvu uliofanyika katika viwanja vya sigara chan'gombe ambao timu ya wanawake ilishinda 25 kwa 24.(Picha na Rajabu Mhamila)Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Netball ya Tanzania, Kate Capenter akiwapa somo wachezaji.Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Netbol wanawake wakiwa mazoezini wakati wa kuchagua wachezaji kumi na mbili watakawowakilisha katika mashindano hayo yanayotarajia kufanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.(Picha na Rajabu Mhamila)

KISININI KUFUATA NYAYO ZA TYSON

Bondia Christopher Kisinini wa uzito wa juu (Heavyweight) akiwa na meneja wake aliyeketi kulia toka Odyssey International LTD Spiros Hussein Palasli.
Bondia Kisinini ambaye amerejea toka Afrika kusini alipokuwa amejichimbia kwa kupata mafunzo ya mchezo huo wa masumbwi, ametamba sasa anataka kuzichapa na Awadhi Tamimu au AShrafu Suleimani.

MISS TANZANIA WAZURU VODACOM

Janet Masanja wa Vodacom akizungumza na warembo wakati walipotembelea ofisini kwake na kupata maelezo mmbali mbali juu ya huduma kwa wateja.Waandishi wa habari waandamizi wa TBC1 Angela Msangi(kulia)Khadija Kalili(Tanzania Daima) wakiwa na Miss Tanzania 2008 Nasri Kareem wakati warembo walipotembelea Vodashop mtaa wa Samora Avenue.

BAMBO NA MTANGA WAJIRUSHA NA OMO

Wasanii wa Maigizo Bambo na Mtanga wakionyesha umili wao wa kucheza ndombolo katika promosheni ya sabuni OMO inyajulikana kama “nyumba kwa nyumba na omo”iliyofanyika Kibaha katika Mkoa Mpwani.Wasanii wa Maigizo Bambo na Mtanga wakimvalisha kofia mshindi wa promosheni sabuni OMO inyajulikana kama “nyumba kwa nyumba na omo” Josephine Samson Mkazi wa kibaha kwa Yusufu katika Mkoa wa Pwani.

Thursday, September 24, 2009

WAREMBO WA MISS TANZANIA 2009 WAPEWA SOMO LA UTALII

Ofisa Utalii wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ernest Mwamaja (kushoto) akizungumza na warembo wanaowania taji la miss Tanzania 2009, wakati wa semina iliyoandaliwa na wizara hiyo Dar es salaam.(Picha na Rajabu Mhamila)
Baadhi ya warembo wanaowania taji la Vodacom miss Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa wakati wa semina ya warembo hawo iliyofanywa na Wizara ya maliasili na Utalii Dar es Salaam.(Picha na Rajabu Mhamila)

GOFU YA ZAIN LUGALO FIDDLE KURINDIMA IJUMAA

Wachezaji gofu kutoka klabu mbalimbali jijini Dar es Salaam Ijumaa wanatarajiwa kuchuana katika mashindano ya kila wiki ya Zain/Lugalo Fiddle kwenye Uwanja wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)Lugalo.
Mashindano hayo ya kila wiki, yanatarajiwa kuanza mchana, na baadaye jioni kutatolewa zawadi kwa washindi ikiwa ni pamoja na simu selula zinazotolewa na wadhamini wa mashindano hayo, kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania.
Meneja mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania, Beatrice Singano ambaye amesema jijini Dar es Salaam kuwa Zain inaona fahari ya kudhamini mashindano hayo ya kila wiki ya gofu katika klabu ya Lugalo, ili kusaidia kuinua kiwango cha mchezo huo nchini. “Zain inaona fahari kudhamini mashindano hayo ambayo yanawakutanisha wachezaji gofu wa rika zote kwa ajili ya michezo na burudani , na tunatumaini udhamini wetu utasaidia kuinua kiwango cha mchezo huo nchini ,” alisema Singano.
“Tunaamini udhamini wetu si kwamba utaongeza tu chachu ya ushindani na kujenga afya za wachezaji , lakini pia utasaidia kuendeleza na kuinua michezo ya Tanzania kwa ujumla, haswa mchezo wa gofu".
Nahodha wa klabu ya gofu ya Lugalo, Koplo Priscus Nyoni ameishukulu Zain kwa kudhamini mashindano hayo ya kila wiki, na kubainisha lengo la mashindano hayo ya kila wiki ni kukuza na kuendeleza mchezo wa gofu kwa kila rika na kila wiki uwanja unakuwa wazi kwa kila mtu.
“Naishukulu kampuni ya zain kwakutambua umuhimu wa mchezo huu wa gofu pia na wakaribisha wachezaji wote wakaribie kwa kuwa mchezo huu ni wa rika zote pia si wamatajiri pekee ni wa watu wote yani watoto wakubwa na wazee wanaweza kucheza mchezo huu karibuni sana”. Alisema Nyoni

Wednesday, September 23, 2009

MISS UTALII SASA WAPATA UDHAMINI

Baadhi ya warembo wanaowania taji la Miss Utalii Temeke wakiwa katika pozi wakati wa utangazaji wa wadhamini wa shindano hilo Dar es salaam.(Picha na Rajabu Mhamnila)

Tuesday, September 22, 2009

TFF - BAADA YA WASEMAJI, SASA NI ZAMU YA MAKATIBU KUNOLEWA

Shirikisho la kandanda hapa nchini TFF, limeandaa semina ya siku 2 kwa Makatibu wakuu 12 wa vilabu vinavyoshiriki Ligi kuu Tanzania Bara ya Vodacom itakayofanyika katika ofisi za Shirikisho hilo kuanzia Septemba 24 hadi 25 mwaka huu.
Akizungumza na kipindi hiki Afisa Habari wa TFF Frolian Loimamu Kaijage amesema lengo la kufanya hivyo ni kuwapiga msasa kuhusiana na masuala mbalimbali ikiwa sambamba na kufahamu majukumu yao ya kazi.
Kaijage ameongeza kuwa semina hiyo itaongozwa na Mkufunzi ambae pia ni Mjumbe wa Fifa Henry Tandau.
Wakati huo huo, Kaijage amewataka wadau na wapenzi wa mpira wa miguu wawe na subira kuhusiana na lawama wanazopelekewa Waamuzi kutokana na uchezeshaji mbovu unaotokea katika mzunguko mzima wa ligi kuu.

JITIHADA NA KUJITUMA KAZINI HULETA MAFANIKIO

The Managing Director of Zain Tanzania, Khaled Muhtadi (left) presents a Certificate Award to Customer Care Supervisor, Belinda Kivuyo (right) in recognition for her excellent performance during the third quarter of 2009. The event was organised by Zain to award employees with exemplary performance.

ZAIN TANZANIA WAFANYA KWELI IDDI

MAMBO YA VIDOLE JUU HAYO, KATIKA BONANZA LA ZAIN KATIKA IDDISHEREHE IPATE WENYEWE BWANA!!! WATU WEEEEEWEEEEWakazi wa Jijini wakicheza mduara kutoka kwa kundi la In Africa Band katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Kigamboni siku ya Jumatatu jioni katika bonanza maalum lililozaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ikiwa ni katika kusherehekea Siku Kuu ya Idi.Msanii wa In Africa Band, Bob Ludala akiwapa burudani wakazi wa Jijini katika bonanza la Idi lilofanyika katika ufukwe wa Bahari ya Hindi Kigaboni Jumatatu jioni katika bonanza maalum lilidhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ikiwa ni katika kusherehekea Siku Kuu ya Idi.Msanii wa In Africa Band Nurdin Athumani akiwapa burudani wakazi wa jijini katika bonanza la iddi lilofanyika katika ufukwe wa bahari (Sunireses) kigaboni jana bonanza ilo lilizaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania.Naamini mpango wa TFF kuanzisha soka la ufukweni kwa staili hii tutafanikiwaWakazi wa Jijini Dar es Salaam wakicheza mpira ufukweni mwa Bahari ya Hindi maeneo ya Kigamboni siku ya Jumatatu jioni ikiwa ni sehemu ya shamra shamra zaSikukuu ya Idi. Tamasha hilo lilidhaminiwa na Zain Tanzania kwa wakazi wa jijin la Dar es Salaam .

Monday, September 21, 2009

VIWANJA MBALI MBALI VYA IDDI MAMBO YALIKUWA HIVI

MAMBO YA JAHAZI
Mwimbaji wa kundi la Jahazi Morden Taarabu akiwajibika wakati wa onesho lao lililofanyika katika ukumbi wa Travertain hotel magomeni Dar es salaam kusherehekea sikukuu ya iddi.(Rajabu Mhamila)Wanamuziki wa kundi la Extra bongo wakiwajibika wakati wa onesho lao lililofanyika ukumbi wa mango gardeni Dar es salaam kulia ni Ridhiwani Mushi,Adamu Hasani na Sara Kideki.(Picha na Rajabu Mhamila)
Wanamuziki wa kundi la Exrta Bongo wakitumbuiza jana wakati wa sherehe za sikukuu ya iddi zilizofanyika Dar es salaam katika ukumbi wa Mango Garden.9Picha na Rajabu Mhamila)Wanamuziki wa kundi la Vijana Ochersta wakiwajibika wakati wa onesho lao lililofanyika Dar es Salaam katika ukumbi wa Vijana kinondoni kushoto ni Maulidi Makia na Shomari Ally.(Picha na Rajabu Mhamila)Waimbaji wapya wa Msondo music bandi wakiwajibika wakati wa onesho la bendi hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Amana Ilala Dar es Salaam wakati wa Iddi Mosi kushoto ni Rashidi Mwezingo na Eddo Sanga.(Picha na Rajabu Mhamila)Wanamuziki wa bendi ya Msondo music bandi wakiwajibika katika onesho lao wakati wa sikukuu ya iddy Dar es salaam walipokuwa wanapiga katika ukumbi wa amana Ilala kushoto ni Uluka Uvuluge na Ibrahimu Kandaya.(Picha na Rajabu Mhamila)