mwamuzi wa soka wa kimataifa Gwaza Mapunda katutoka
TFF imepokea kwa masikitiko kifo cha mwamuzi mstaafu wa kimataifa, Kanali mstaafu Gwaza Mapunda kilichotokea leo alfajiri katika Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam.
Mapunda alikuwa mjumbe wa Kamati ya Waaamuzi na baadaye Kamati ya Mashindano ya TFF kati ya mwaka 2005 – 2008 na pia alikuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Chama cha waamuzi FRAT.
Gwaza Mapunda alianza kujihusisha na masuala ya uamuzi mwaka 1974 na aalkuwa mwamuzi wa kimataifa anayetambuliwa na FIFA kati ya mwaka 1980 hadi mwaka 1984.
TFF itashiriki kikamilifu katika msiba huu ulioifika jamii ya mpira.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Gwaza Mapunda mahali pema peponi Amina
Fredrick Mwakalaebela
KATIBU MKUU
KAMISHNA BADRU AENDELEA KUIMARISHA UHUSIANO NA JAMII INAYOISHI NDANI YA
HIFADHI YA NGORONGORO
-
Mwandishi wetu Endulen Ngorongoro.
Tarehe 20 Desemba, 2025
Uhusiano kati ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na jamii inayoishi
ndani ya eneo la h...
17 hours ago
No comments :
Post a Comment