Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, April 30, 2014

STEPS SOLAR YAZINDULIWA KIGAMBONI


Mkurugenzi wa Steps Solar Dilesh Solanki kushoto pamoja na wasanii wa filamu ambao ni mabalozi wa Steps Solar ,Salma Jabu 'Nisha' na Amri Athumani 'Mzee Majuto' wakiomkabidhi zawadi ya solar kwa ajili ya kutumia nyumbani Mbunge wa jimbo la Kigamboni, DR, Faustine Ndugulile wakati wa tafrija ya uzindudhi wa bidhaa hizo zilizofanyika mji mwema kigamboni Dar es salaam Picha na www.burudan.blogspot.com
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Steps Solar Jairaj wa pili kulia akimuonesha Mbunge wa jimbo la Kigamboni, DR, Faustine Ndugulile wakati wa tafrija ya uzindudhi wa bidhaa hizo zilizofanyika mji mwema kigamboni Dar es salaam katikati ni
Mkurugenzi wa Steps Solar Dilesh Solanki 
Picha na www.burudan.blogspot.com
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Steps Solar Jairaj  kulia akimuonesha Mbunge wa jimbo la Kigamboni, DR, Faustine Ndugulile pasi jinsi ilivyopata moto wakati wa tafrija ya uzindudhi wa bidhaa hizo zilizofanyika mji mwema kigamboni Dar es salaam katikati ni
Mkurugenzi wa Steps Solar Dilesh Solanki  na Ofisa wa kampuni hiyo Moses Mwanyilu
Picha na www.burudan.blogspot.com
Ofisa wa kampuni ya Steps Solar Moses Mwanyilu akimwelekeza
Mbunge wa jimbo la Kigamboni, DR, Faustine Ndugulile wa pili kushoto jinsi wa umeme unavyopatikana kupitia mashine ndogo ya kuifadhia umeme wa jua kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Steps Solar Jairaj
katikati ni
Mkurugenzi wa Steps Solar Dilesh Solanki na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya temeke Sikunjema Shabani

Picha na www.burudan.blogspot.com

Tuesday, April 29, 2014

Muumin & Double M Sound kujitambulisha Kigoma


Muumin
BAADA ya kukonga nyoyo za mashabiki wa mikoa ya Shinyanga na Kagera wakati wa sikukuu ya Pasaka, bendi iliyorejeshwa upya ya Double M Sound mwezi ujao inatarajiwa kwenda kujitambulisha kwa wakazi wa Kigoma.
Mkurugenzi wa bendi hiyo, Prince Mwinjuma Muumini aliiambia MICHARAZO kuwa, wanatarajia kwenda kuitambulisha bendi yao katika miji ya Kibondo na Kasulu iliyopo mkoani Kigoma.
Muumin alisema onyesho la kwanza mkoani humo watalifanya Mei 9 mjini Kibondo kabla ya siku inayofuata watahamia Kasulu kabla ya kurejea maskani kwao Kahama-Shinyanga kwa ajili ya kufanya mazoezi za uzinduzi rasmi.
"Tunashukuru tumerejea salama kutoka kwenye maonyesho yetu wakati wa sikukuu ya Pasaka kwa kutambulisha bendi eneo la Kakola, Ushirombo, Ruzewe, Ngara na Katoro. Kwa sasa tupo kambini mjini Kahama kujiandaa na ziara ya mkoani Kigoma mapema mwezi ujao," alisema Muumin.
Muumin aliongeza kuwa uongozi wao unajipanga kufanya uzinduzi na onyesho la kwanza kuitambulisha na kuizindua Double M Sound mjini Kahama mwishoni mwa mwezi ujao.
"Pamoja na watu kujua Double M Sound ipo Kahama, lakini hawajawahi kuiona hadharani kwa sababu tunapanga kuizindua rasmi mwishoni mwa Mei na kisha ndipo tuanze kuifanya maonyesho mjini hapa," alisema Muumin.
Double M Sound iliyowahi kutamba na nyimbo mbalimbali ilisambaratika mara baada ya uzinduzi wa albamu yao ya Titanic mwaka 2004 na Muumin ameamua kuifufua upya na kujichimbia Kahama kama maskani yake kwa sasa.

Kamanda Kova afunguka vifo vya watoto Bwawa la Kuogolea Dar


Picha haihusiani na habari, ila watoto wakifurahia kuoga kwenye bwawa la kuogolea kama wanavyuoonekana
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum  Suleiman Kova amefafanua juu ya taarifa ya vifo vya watoto watatu
waliofariki wakati wakiongolea kwenye bwawa la hoteli.
Kamanda Kova alisema April 27  kulitokea vifo vya watoto 3 ambao walikua na birthday party nyumbani lakini baada ya kukamilika kwa taratibu za party ya nyumbani waliamua kuimalizia party hiyo hotel ya Landmark,walipofika walienda kuogelea kwenye swimming pool ya watoto lakini baadae watoto hao walitoka kwenye pool ile ya watoto wakaingia kwenye pool ya wakubwa na kwa bahati mbaya waliingia sehemu yenye kina kirefu.
Watoto wenzao walipoona wenzao wanazama walianza kuwavuta kuwatoa nje lakini hali zao tayari zilikua mbaya, mmoja wapo hali yake ilikua kidogo afadhari lakini kwa bahati mbaya nayeye alifia hospital wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Masana na kufanya Idadi ya watoto waliofariki kuwa 3 majina yao ni Janet Zacharia, Eva na Ndimbuni.
Kamanda Kova amesema; "’Kusema kweli sio mara ya kwanza kutokea, mara nyingi vifo vya watoto vinatokana na uangalifu au uzembe kutoka kwa wale wanaotakiwa kuwaangalia hao watoto wao, hizi hotel zote zenye swimming pool lile eneo la kuogelewa basi wasiruhusiwe watoto wadogo kuogelea au kuwe na mtu ambaye anajua kuogelea au kuokoa ambaye yupo pale’
‘Unajua watoto wana tabia ya kuigana mmoja akiingia akiogelea pengine anafahamu kidogo wengine wote wanafata mkumbo wanaona wanaweza,sisi kama jeshi la Polisi tumeamua hili kosa la uzembe kusababaisha kifo kisheria mtu anaweza kushtakiwa kwa kuzembea kwa kutochukua tahadhari mpaka watoto kama wale ambao hawana hatia uwezo wao mdogo wa kufikiri au kuijiokoa’
‘Tunafatilia kwa umakini lakini jukumu la kufatilia maisha ya watoto ni la wazazi mia kwa mia wasipofanya hivi wakiwa hawapo makini matokeo yake ni haya watoto 3 wamefariki,tunaendelea na uchunguzi na baadae tutatoa taarifa kamili’.

DVD MPYA ZA MASUMBWI KUTOKA SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION




 DVD HII YA MASUMBWI IKIMUHUSISHA IBRAHUMU CLASS .KING CLASS MAWE.  MAPAMBANO MAKALI YA NGUMI ZOTE KALI LIPO KWENYE DVD MOJA SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania


DVD MPYA ZA MASUMBWI ZIKIMSHILIKISHA BONDIA IBRAHIMU CLASS KING CLASS MAWE
MPAMBANO WA MASUMBWI AMBAO UMEACHA HISTORIA KATIKA MCHEZO WA NGUMI DUNIANI

IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE SASA ATAKA KUWANIA UBINGWA




Ibrahimu Class King Class Mawe birth place Iringa, Tanzania won 10,
birthdate 1990-10-10 (age 23)
division light welterweight
Ibrahimu Class King Class Mawe birth place Iringa, Tanzania won 10,
birthdate 1990-10-10 (age 23)
division light welterweight
Ibrahimu Class King Class Mawe birth place Iringa, Tanzania won 10,
birthdate 1990-10-10 (age 23)
division light welterweight





EAST AFRICA MELODY KUWASHA MOTO MEI MOSI TRAVENTINE MAGOMENI MEI MOSI


Na Mwandishi wetu

BENDI ya taaarabu ya East African Melody  itatoa burudani katika ukumbi wa traventine Dar es salaam kwa ajili ya kusherekea siku kuu ya wafanyakazi Duniani Mei mosi

akizungumza onesho hilo muhandaaji wake Abbass Chezntemba 'Abbas  Chez' Cash Money' amethibitisha kufanyika onesho hilo ambali litakuwa la kihistoria jijini 

ambapo wasanii mbalimbali wamealikwa kushiriki kutoa burudani siku hiyoambayo imepewa jina la Usiku wa habiti za sauti za dhahabu ambapo watasindikizwa na ngwiji wa mziki wa dansi nchini

king kiki mzee sugu na kitambaa cheupe na Pr, Muhamed Issa  Matona,Rukia Ramadhani,Sabaha Muchacho, Hadija Yusuph ,Shakila Said, Ustadh Muhamed

na wasanii wengine wengi
kingilio kitakuwa ni  shilingi 7000 na 10,000 kwa watu watakaokaa V.I.P pia kutakuwa na zawadi kumi tofauti kwa ajili ya sikukuu hiyo itakayotolewa na Cash Money siku hiyo katika ukumbi wa traventine kwa watakaofika kuangalia onesho hilo

MSONDO WATOA BURUDANI KWA WAFANYAKAZI


Mwimbaji wa bend ya msondo ngoma Shaban Dede akiimba wakati wa maonesho ya mahadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam

Waimbaji wa bendi ya Msondo ngoma wakitoa burudani wakati wa siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam
Wapuliza hara wa bendi ya msondo ngoma wakiwajibika wakati wa mahadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini kutoka kushoto ni Shabani Lendi, Hamisi Mnyupe na Roman Mn'gande

WLADIMIR KLITSCHKO AMTWANGA LEAPAI KAMA GUNIA NA KUTETEA MATAJI YAKE



BONDIA Wladimir Klitschko ameendeleza ubabe wake katika ndondi za uzito wa juu baada ya usiku wa kuamkia leo kumchapa kwa Knockout (KO) ya raundi ya tano, Alex Leapai katika pambano la kutetea mataji yake. 
Klitschko, alitumia mikono yake mirefu kumchapa kama 'mwanawe' mpinzani huyo wa Samoa mzaliwa wa Australia, ambaye raundi ya tano alisalimu amri katika pambano lililofanyika mjini Oberhausen, Ujerumani Magharibi. 
Leapai alikwenda chini baada ya kuchanganyiwa makonde ya mikono yote, kushoto naa kulia mfululizo. 
Aliinuka kujaribu kutaka kuendelea, lakini kwa nia nzuri, Klitschko raia wa Ukraine akajisogeza mbali zikiwa zimesalia sekunde 58 raundi hiyo kumalizika.
Pokea hiyo: Konde la Klitschko likichapa kidevu cha Leapai jana katika pambano la ubingwa wa dunia uzito wa juu mjini Oberhausen, Ujerumani Magharibi.
Down you go: Klitschko watches as Leapai falls to the canvas
Chini: Klitschko akimuangalia mpinzani wake, Leapai anavyopambana na sakafu
Conveyor belt of success: Wladimir Klitschko celebrates victory over Australia's Alex Leapai after the WBA, IBF, WBO and IBO title bout
Mataji kibao: Wladimir Klitschko akisherehekea ushindi wake dhidi ya Alex Leapai ambao umemfanya atetee mataji yake ya WBA, IBF, WBO na IBO

PSPF WASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA USALAMA NA AFYA DUNIANI,KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA DAR


Ofisa muendeshaji wa Mfukowa pesheni wa mashirika ya umma PSPF, Bw, Hadji Jamadary kushoto akimwelekeza kujaza fomu Shabani Maganga wakati wa mahadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam

Afisa muendeshaji wa mfuko wa pesheni wa mashirika ya uma PSPF Bw, Lule Kasembwe kushoto akitoa maelekezo kwa wazee waliojitokeza
Ofisa muendeshaji wa PSPF Hadji Jamadary kushoto akiwapatia mahelezo ya jinsi ya kujiunga na PSPF wakati wa mahadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam

Saturday, April 26, 2014

TAIFA STARS YALA KICHAPO CHA 3-0 KUTOKA KWA BURUNDI KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MUUNGANO


FT: TAIFA STARS 0: 3 BURUNDI

Dakika 45` za kipindi cha pili zimeshakatika na kuongezwa dakika 3.
Dakika ya 38 kipindi cha pili, stars wanapata kona na kukosa bao la wazi baada ya kazi nzuri ya Msuva na Omary Nyenje kushindwa kugusa mpira kuutumbukiza wavuni.
Dakika ya 35` kipindi cha pili, Stars wapo nyuma kwa mabao 3-0
Dakika ya 30` kipindi cha pili Burundi wanaongoza kwa mabao 3-0.
Dakika ya 25` kipindi cha pili, Taifa stars wapo nyuma kwa mabao 3-0 dhidi ya Burundi.
Dakika ya 19` kipindi cha pili, Taifa Stars inashindwa kumudu kabisa kasi ya Burundi, lakini Kocha Salum Mayanga amefanya mabadiliko yanayoonekana kuwapa uhai Stars.
Burundi wanaandika bao la tatu kupitia kwa Yusuf Ndikumana.
Amis Tambwe anaifungia Burundi bao la pili kwa shuti kali la chini chini lililomshinda kipa Deo Munish.
Dakika ya 9` kipindi cha pili kona inachongwa kueleka lango la Stars, lakini mabeki wanaokoa.
Didier Kavumbagu anadhihirisha kuwa kasi yake ya kufunga ni ileile.
Wachezaji wa Taifa stars hawana kasi kama wanavyocheza katika klabu zao. Sijui tatizo ni nini hapo uwanja wa Taifa.
Jonas Mkude, Harun Chanongo na Himid Mao wamenyanyuliwa na kuanza kupasha moto misuli.
Dakika ya 4` kipindi cha pili, Burundi bado wanaoongoza kwa bao 1-0.
Almanusura Burundi waandike bao la pili, lakini mpira unaokolewa na Dida na kuwa kona inayoondoshwa na Agrey Moris.
Mpira umeshanza hapa uwanja wa Taifa
Kipindi cha pili kinatarajia kuanza hivi punde, naona waamuzi na wachezaji wa akiba wakiingia uwanjani.
HT: TAIFA STARS 0: 1 BURUNDI
Dakika ya 45` kipindi cha kwanza, Didier Kavumbagu anaifungia Burundi bao la kuongoza.
DDakika ya 40` kipindi cha kwanza bao bila kwa bila.
Mpira umesimama hapa uwanja wa Taifa, kipa wa Stars, Deo Munish akiwa chini akigangwagangwa.
Dakika 31` za kipindi cha kwanza zimeshakatika, hakuna bao kwa timu zote.
Mohamed Seif anaikosesha bao Taifa stars kufuatia krosi ya Saimon Msuva.
Stars wanafanya shambulizi kali, lakini shuti alilopiga Saimon Msuva linakuwa mboga kwa kipa wa Burundi.
Dakika ya 16` kipindi cha kwanza hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Dakika ya 8` kipindi cha kwanza Burundi wanapata kona,lakini Ramadhan Singano `Messi` anaokoa. 
 Mpira umeshaanza uwanja wa Taifa

TAIFA STRS 0 VS 3  BURUNDI

BONDIA THOMAS MASHALI APATA AJARI




Bondia Thomasi Mashali akionesha majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali hivi karibuni picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
JERAHA LINALO ONEKANA MKONONI
Bondia Thomasi Mashali akionesha majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali hivi karibuni picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
THOMAS MASHALI
Bondia Thomas Mashali wa tatu kushoto akiwa na baadhi tya ndugu na jamaa akiuguza majeraha ya vidonda baada ya kupatas ajari hivi karibuni picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Thomasi Mashali akionesha majeraha aliyoyapata baada ya kupata ajali hivi karibuni picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu
BONDIA Thomasi Mashali amepata ajari ya gari mara baada ya kuangukia mtaloni akiwa anaendesga gari aina ya vitz lenye namba za usajili T 777 BMW ajari hiyo iliyotokea maeneo ya kimara baruti siku ya april 20

wakati akitokea manzese kwenda nyumani kwake kimara mwisho akielezea tykio zima la ajari hiyo Mashali 'Alisema nilikuwa naendesha mwenyewe nikakutana na tuta nikaruka tuta nilivyomaliza tu tuta kumbe mbele yangu kulikuwa kumefungwa kutokana na matengenezo ya barabara ya morogoro  ile nataka kukwepa uzioambapo nilipo kwepea nika ingia mtaloni moja kwa moja

katika gari hiyo tulikuwa wawili na mdogo wangu George Maluma ambaye ajaumia chochote katika ajari hiyo

akizungumzia mchezo wake unao mkabili ambao ulikuwa ufanyike siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba kwa ajili ya kumkabili Kalama Nyilawila, mashali alisema kuwa kwa sasa sifanyi mazoezi kwa kuwa nauguza majeraha yangu ya kuchubuka na kutoka kwa ngozi katika mkono wangu wa kulia na ubavuni mwangu

namwambia Kalama kuwa kafala laker limegonga mwamba hivyo akae tayali kwa kipigo cha mbwa mwizi kama nilivyo mfanya mwenzie Mada Maugo

kwani na yeye alikuwa anachonga sana lakini mwisho wa siku nikachukuwa ubingwa kupitia kwake yeye mana mpambano huu nilikuwa nausubili kwa hamu kubwa sana leo kesho

mbali na majeraha haya napenda kuwashukuru baadha ya watu walionisaidia  katika tukio zima la mimi kupata ajari na kunisaidia kutoa gari bondeni mpaka sasa ipo katika mikono salama ingawa imearibikwa kwa sababu ya kubondeka

mbali na hivyo nashukuru  promota Ally Mwazoa kwa kuwa na moyo wa huruma na kuhamua kusogeza mbele mpambano huo mpaka siku utakapotangazwa tena pia naomba watanzania waniombee duwa kwani naenderea vizuri kutibu majeraha yangu

JUKWAA LA KATIBA WATANGAZA KUSULUHISHA MGOGORO WA BUNGE MAALUM LA KATIBA




Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Jukwaa la Katiba jijini Dar es Salaam katika kutoa tamko rasmi za tathimini ya Jukwaa la Katiba Tanzania kuhusu Katiba Mpya, Tulipotoka, Tulipo na Tuendako. Pembeni ni Msimamizi wa Mradi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya (NGO Network for Dodoma) Bw. Edward Mbogo (kushoto) na Mjumbe wa Jukwaa la Katiba toka Pemba Bw. Omari Omari.



Waandishi wa Habari wakifuatilia.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.


Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) limejitolea kuratibu maridhiano miongoni mwa makundi ya kisiasa asasi za kiraia, asasi za wananchi na taasisi zote za muhimu zilizoguswa na migogoro inayoendelea katika Bunge maalum la katiba Tanzania.


Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Jukwaa la Katiba jijini Dar es Salam, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Deus Kibamba juu ya tathimini walizozifanya katika bunge hilo wameamua kujitolea kufanya maridhiano hayo kwa kuwashirikisha viongozi maarufu Afrika Mashariki akiwemo mheshimiwa jaji mkuu mstaafu wa Tanzania, Barnabas Samatta ambaye atakuwa mkuu.


wa jopo hilo la usuluhisho na ndugu Patrice Lumumba kutoka nchini Kenya ambaye atakuwa msaidizi.
Aidha jukwaa hilo limeonyesha masikitiko yake kwa kile alichookiita ni uvunjifu wa kanuni mara baada ya wabunge zaidi ya mia mbili kutoka nje lakini wabunge waliobakia kuendelea kurekebisha kanuni za bunge hilo jambo ambalo wamesema kuwa haikustaili kwani wana uwezo wa kujitungia sheria.

Kibamba amesema kuwa kutokana na mwenendo wa bunge hilo hadi hapa lilipofikia wabunge hao hawana nia ya dhati ya kulipatia taifa katiba mpya huku akitolea mfano kuwa katiba mpya ilipangwa kuwekwa saini na Rais siku ya tarehe 26 mwezi huu yani leo lakini hadi sasa hata majadiliano ya sura mbili hayajamalizika, na kuwahakikishia watanzania kuwa hakuna katiba mpya itakayopatikana kwa mwaka huu.
Hata hivyo mwenyekiti huyo amewataka wajumbe wote na asasi zote zilizopo nje ya muendelezo wa bunge hilo maalumu la katiba kuwa tayari kwa maridhiano kwa mtu au taasisi yoyote atakayekuwa tayari kutatua migogoro yao ili kuwezesha upatikanaji wa katiba kwa taifa letu.

SALAM ZA HERI YA MIAKA 50 YA MUUNGANO KUTOKA NGOMA AFRICA BAND



Bend maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "NGOMA AFRICA BAND" aka FFU Ughaibuni,yenye makao yake kule nchini Ujerumani,inaungana na watanzania wote nyumbani na ughaibuni katika kusherehekea "MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANZANIA",Ngoma Africa band inatoa salam za heri na shangwe kwa watanzania wote popote duniani.

ZIDUMU FIKRA ZA WAASISI WA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR = TANZANIA

                                UDUMU UMOJA WA KITAIFA

                                UDUMU MUUNGANO WETU

                                  MUNGU IBARIKI TANZANIA

Tafadhali pata burudani ya muziki at www.ngoma-africa.com

HAPPY UNION DAY



SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO ZAFANA JIJINI DAR ES SALAAM



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Jeshi la wananchi kwenye sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
 Kikosi cha Makomandoo kikipita kwa mwendo wa aina yake wakati wa sherehe za miaka 50 ya Muungano.

 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano ambazo zimefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
 Kikosi cha Makomandoo kikitoa salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.
 Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana bila kutumia nyenzo hapa wakivunja matofali kwa kutumia kichwa na mikono.
 Baadhi ya silaha zakijeshi zikipitishwa mbele ya umati kuonyesha uwezo mkubwa wa jeshi letu.
 Kikosi cha Wanamaji 
 Ndege za kivita zikilinda Ndege ya Rais katika maonyesho ya Ndege yaliofanyika kwenye Kilele cha  Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano.
 Askari wa kikosi cha Mwamvuli akishuka kutoka futi 4500 kwenye uwanja wa Uhuru kwenye kilele cha miaka 50.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pongezi mmoja wa wanajeshi wa kikosi cha mwamvuli .
 Maandamano ya Pikipiki.
 Matembezi maalum ya kusheherekea miaka 50 ya Muungano .
Njiwa wakirushwa juu kama ishara ya miaka 50 ya Muungano ambapo watu waliorusha njiwa hao nao wametimiza miaka 50.