Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi akizungumza na shangazi wa mtoto
aliyeibiwa pembeni ni baadhi ya waandishi wa habari walioshuhudia
makabidhiano hayo
BAADA ya Jeshi la Polisi mkoani Mbeya
kumtia nguvuni Askari wake anayetuhumiwa kuiba mtoto wilayani Kyela,Mtoto
huyo akabidhiwa kwa wazazi wake huku wakiendelea na uchunguzi zaidi.
Makabidhiano hayo yamefanyika
katika Hospitali ya Wazazi Meta alikokuwa akipatiwa matibabu mtoto
huyo katika chumba cha Joto na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi.
Akipokea Mtoto wake Mama mzazi Mboka
Mwakikagile(20) amelishukuru Jeshi la polisi na wananchi wema kwa kufanikisha kupatikana
kwa mtoto wake Goodluck Salehe aliyeibwa na Askari wa Jeshi la Polisi WP
5367 Prisca Kilwai April 6, mwaka huu huko Kasumulu wilayani Kyela.
Aidha mwanamke huyo amemshukuru zaidi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi pamoja na Askari wengine
waliofanikisha mtoto wake kupatikana akiwa hai.
Baadhi ya ndugu waliofurika katika
Hospitali ya Meta kushuhudia makabidhiano hayo wamesema hawaamini kile
kilichotokea baada ya kuwa katika hofu takribani siku kumi na moja baada ya
kuibwa katika zahanati ya Njisi iliyopo Kasumulu Kyela.
Aidha ndugu hao wamelipongeza Jeshi la
Polisi kwa kufanikisha kupatikana mtoto na wasamaria wote walioshirikiana nao
katika maombi hata kufanikisha upatikanaji wa mtoto huyo akiwa salama salimini.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mbeya, Ahmed Msangi,akizungumza baada ya kukabidhi mtoto huyo aliwasihi
wazazi kuwa makini na utunzaji wa watoto ili kuepuka vitendo kama hivyo
kujirudia.
Ameongeza kuwa Jeshi la polisi bado
linafanya upelelezi na kukusanya ushahidi zaidi ili waweze kuwafikisha
mahakamani watumiwa kujibu mashtaka wanayokabiliana nayo.
Amesema Mtoto huyo alipatikana Aprili
17, mwaka huu akiwa na Askari huyo majira ya saa nne asubuhi na kuongeza
kuwa mpaka sasa sababu za kuiba mtoto huyo hazijafahamika na atafikishwa
mahakamani wakati wowote baada ya kuhukumiwa kijeshi.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments :
Post a Comment