''Tunaipongeza timu ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani kwa kutwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani baada ya majuzi (Aprili 6 mwaka huu) kuifunga Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.
Ushindi
kwa timu hiyo ni fahari kwa Tanzania, lakini kubwa ni kwa kituo cha
Mwanza ambacho ndicho kinachoiendesha pamoja na wadhamini na wafadhili
walioiwezesha kushiriki fainali hizo kwa mara ya pili mfululizo.
Vilevile
ushindi huo unatoa changamoto kubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kuwa
watoto wa mitaani ni sehemu tu ya vipaji vilivyotapaa nchini, hivyo
iliyopo ni kuvisaka na kuvibaini vipaji hivyo kwa ajili ya ustawi wa
mchezo huo nchini.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tutaendelea kushirikiana na kituo
hicho cha Mwanza, na vingine vyote ambavyo vinajishughulisha na mchezo
huu, lengo likiwa ni kuundeleza na hata kutoa ajira kwa vijana hapo
baadaye kupitia mpira wa miguu.
Timu
hiyo imerejea nchini leo ambapo imetua
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 9 na nusu jioni kwa
ndege ya Emirates''
No comments :
Post a Comment