Maofisa
wa kuzuia bidhaa zisizo na hati miliki nchini China wamekamata makombe
feki ya kombe la dunia zaidi ya 1,000 katika ghala ya kampuni moja
kubwa ya utengenezaji na usafirishaji wa bidhaa
NDOTO ya mashabiki wa timu ya Taifa ya England `Simba watatu` ni kunyanyua kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Lakini
suala hili limechukua sura mpya na shukurani za dhati
ziwaendee viongozi wa desturi wa China waliofanikisha kukamata mzigo
feki.
Nchi
ya China imekamata makombe feki ya kombe la dunia zaidi ya elfu moja (
1,000) katika ghala ya kampuni moja kubwa ya usafirishaji nchini humo.
Makombe
hayo feki 1, 020 ya kombe la dunia yamekamatwa katika mji wa Yiwu,
jimbo la Zhejiang, ambalo ni moja ya miji mikubwa ya usafirishaji wa
bidhaa duniani.
Makombe hayo feki kwa asilimia kubwa yanafanana na makombe halisi ya FIFA na yalikuwa tayari kusafirishwa kwenda nchini Libya.
Mkurugenzi
wa desturi wa China mwenye mamlaka ya kuzuia nyara zisizohalali
alianzisha kampeni mwezi huu wa nne ili kukamata bidhaa zote feki
zilizotengenezwa kuelekea kombe la dunia bila kuwa na hati miliki.
Kombe
la dunia nchini Brazil linatarajia kuwa na biashara kubwa, na China
wameshakamati dili hili na viwanda vyake vimetengeneza bidhaa nyingi za
kombe hilo, lakini kuna wajanja wachache wanaotaka kujinufaisha bila ya
hati miliki.
Nahodha
wa England Steven Gerrard ana matumaini ya kubeba kombe halisi mwaka
huu nchini Brazil ambapo wapo kundi moja na mataifa ya Italia, Costa
Rica na Uruguay.Source DJ Sek B
No comments :
Post a Comment