Meneja
Masoko wa TBL, Fimbo Butallah, akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mashindao ya Castle
Lager Perfect 6 yaliyofanyika kwenye ufukwe wa Mbalamwezi jijini.
Kushoto ni Meneja wa Bia ya Castle Kabula Nshimo.
Meneja
wa Bia ya Castle Kabula Nshimo, akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi huo, uliofanyika jana kwenye ufukwe
wa Mbalamwezi, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja masoko wa TBL,
Fimbo Butallah.
************************************
Na Sufianimafoto Reporter, Dar
Timu
ya Soka ya Puyo chini ya Nahodha wake Majuto Omary jana jioni iliibuka
kidedea katika mashindao ya Castle Lager Perfect 6 yaliyofanyika kwenye
ufukwe wa Mbalamwezi jijini.
Mashindano
hayo ambayo yalijumuisha timu sita za waandishi wa habari za Michezo
yamezinduliwa juzi ambapo timu hiyo ya Puyo ambayo ilikuwa na wachezaji
wengi wazee, imetinga moja kwa moja kwenye fainali za Taifa
zitakazofanyika mwishoni mwa mwezi Julai.
Puyo
ilinyakua zawadi ya Kombe na Medali kutoka kwa wadhamini wa mashindano
ya hayo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Castle
baada ya kuzisambaratisha timu za Xavi, Mess, Neymer na Masherano.
Awali
akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Castle Kabula Nshimo
alisema mashindano hayo yatashirika wachezaji wa baa mbali mbali ambao
wanatumia kinywaji cha Castle na kwamba yataanza kwa ngazi ya baa, Kanda
hadi Taifa ambapo timu sita zitapatikana na kuungana na ile ya Taswa
ambapo zitacheza fainali na timu itakayoibuka kidedea katika shindano
hilo la Perfect Six watapata fursa ya kutembelea uwanja wa Camp Nou na
kujionea timu ya FC Barcelona ikicheza katika ziara ambayo itagharamiwa
na Castle.
"Shindano
hili litadumu kwa miezi mitano, litafanyika nchi nzima, ambapo timu
mbali mbali katika Kanda saba zitasajiliwa na kucheza katika hatua ya
mtoano kenye maeneo mbali mbali ambayo yatachaguliwa na kutangazwa
mapema.
"Kila
kanda itatoa timu moja na kufanya kuwa jumla ya timu saba ambazo
zitawakilisha kanda hizo huku timu ya nane ikiwa ni Puyo ambayo inaundwa
na waandishi wa habari, timu hizo zitachuana kwa mtoano kwenye robo
fainali, nusu fainali na hatimaye fainali.
Naye
Meneja masoko wa TBL, Fimbo Butallah akifafanua zaidi alisema "Sio kwa
wachezaji tu kutakuwa pia na droo maalum kwa wanywaji wa Castle na
wateja wawili nao watapata fursa ya kwenda Hispania kujionea Barcelona
inavyocheza na pia kila wiki kuna zawadi ya Sh100,000 itatolewa kwa
washindi sita.
Hata
hivyo Fimbo alionya kuwa shindano hilo la Perfect Six halitawahusisha
wachezaji wa zamani ambao wameshachezea timu mbali mbali za Ligi Kuu, na
kwamba litahusisha wale tu ambao hawajawahi kucheza mpira kabisa katika
ngazi yoyote inayotambulika na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
No comments :
Post a Comment