Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akionyeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Mussa Iombe, sehemu ya
Daraja la Mpiji linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam, lililokatika
kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini, wakati Makamu alipofanya
ziara hiyo ya kujionea maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo leo Aprili 13, 2014.
Sehemu ya daraja hilo, linavyoonekana baada ya kuongezeka upana kwa kulika
kutoka mita 25 na sasa kufikia mita 75,
ambapo tayari Malori yameanza kumwaga vifusi vya mawe ili kuziba eneo hilo na
kuweza kuunganisha njia hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa
maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Mussa Ibrahim Iombe, wakati
alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika
kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.Katikati ni Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Mecky Sadick.
Malori
yakimwaga vifusi vya Mawe kwenye daraja hilo.
Malori
yakimwaga vifusi vya Mawe kwenye daraja hilo.
Nguzo
za umeme zikiwa zimeinama baada ya kuzidiwa nguvu na maji hayo yaliyobomoa
daraja.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhitimisha ziara yake hiyo, katika
eneo la Daraja la Mpiji, linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam, leo Aprili
13, 2014.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na baadhi ya viongozi kuelekea eneo la tukio kukagua maendeleo ya
ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na Mvua kubwa zinazoendelea
kunyesha nchini.
Nguzo
za umeme zikiwa zimeinama baada ya kuzidiwa nguvu na maji hayo yaliyobomoa
daraja.
Malori
yakimwaga vifusi vya Mawe kwenye daraja hilo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiondoka eneo la tukio Daraja la Mpiji baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo lililokatika kutokana na mvua kubwa
zinazoendelea kunyesha nchini.
No comments :
Post a Comment