Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, December 31, 2011

WACHEZAJI WATIMU YA TAIFA YA NDONDI WAILOTEULIWA KUSHIRIKI KINYANGA"NYIRO CHA KUTAFUTA NAMBA YA KUSHIRIKI OLIMPIKI 2012

Kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila Super D akiwa na vifaa vya mchezo huo
Moja ya kambi za mazoezi ya mchezo wa ngumi
KOcha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila Super D akiwa na vifaa vya mchezo huo


Vijana chipukizi wakijifua katika kambi ya mazoezi ya ngumi
Kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila Super D akiwa na vifaa vya ngumi

Kocha Kondo nassoro akimwelekeza bondia chipukizi Zainabu Mhamila (Ikota) huku nyuma akielekezwa jinsi ya kutembea na kocha Habibu Kinyogoli wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala Dar es SalaamMAJINA YA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA NGUMI WALIOTEULIWA KWA AJIL YA MAANDALIZI YA MASHINDANO YA KUFUZU KWENDA KUWAKILISHA TAIFA KATIKA MASHINDANO YA OLMPIKI LONDON UINGEREZA Julai 2012.


KUTOKA NGOME BOXING TIMU:
1. .SELEMAN KIDUNDA.
2. PETER STANLEY
3. .MORIS MHINA
4. 3.KILLER MOHAMED
5. .ABDALAH KASSIM
6. SUNDAY ELIAS
7. DENIS MARTINE
8. ABDALAH KITENGE
9. HUSSEIN MNIMBO
10. HARUNA SWANGA
11. SAID PUME
12. HASHIM SAIMON
13. RAJABU MADINDA
14. ABDALAH SHABANI
15. ABDU RASHID
16. FRANK NICOLOUS
KUTOKA MMJKT BOXING TIMU:

1. EMILLIAN PATRICK

2. MAXIMILIAN PATRICK
3. ISSA ABDALAH KOBA
4. HAMDAN ISSA
5. SAID HOFU
6. KASSIM HUSSEN
7. BONIFACE MLINGWA
8. DOGO MUSSA
9. GRORGE COSTANTINO
10. JOHN CHRISTIAN
11. VICTOR NJAITI
12. ISMAIL ISACK
13. ELIAS MKOMO
14. WAMBURA AMIRI
KUTOKA MAGEREZA BOXING TIMU:
1. UNDULE LANG"SON

2. NURU IBRAHIM
3. SELEMAN BAMTULA
4. MICHAEL PASCHAL
5. SHABAN ALLY
6. MUSIN KIMWAGA
7. OSWARD CHAULA
8. ANTON IDOA
9. LUSAJO MWAIPOPO
10. MOHAMED CHIBUMBUI
KUTOKA SIFA BOXING TIMU
1. IDDI PIALALI

2. ANCE JOHN
3. SHABAN MAFIGA
4. DOTO SHOKA
KUTOKA POLISI BOXING TIMU
1. YAHAYA MALIKI
KUTOKA URAFIKI BOXING TIMU:
1. FADHIR HASSAN

KUTOKA TEMEKE BOXING TIMU:
1. EDWARD ASAJILE

2. ABDALAH MFAUME
KUTOKA NYAMBELE BOXING TIMU (DODOMA)
1. ANTONY NYAMBELE

KUTOKA MTONI BOXING TIMU
1. CHUKI MOHAMED

NB: MAZOEZI KWA WACHEZAJI 51 WALIOTEULIWA YATAANZA MARA TU BAADA YA KURIPOTI BFT NA KUPANGIWA KITUO CHA KUFANYIA MAZOEZI KATI YA VITUO TULIVYOANISHA VYA UWANJA WA NDANI WA TAIFA,MAGEREZA UKONGA, MGULANI JKT,NGOME,NA URAFIKI.
MWISHONI MWA Januari 2012 KUTAFANYIKA MASHINDANO MAALUM YA MCHUJO KWA HAO WACHEZAJI WALIOTEULIWA ILI KUPATA WACHEZAJI 20.

15-22/2/2012 TIMU HII ITASHIRIKI MASHINDANO YA TAIFA YATAKAYOSHIRIKISHA MIKOA YOTE YA TANZANIA BARA KWA LENGO LA KUSHIRIKISHA MIKOA YOTE ILI TUPATE WAWAKILISHI WA SURA YA KITAIFA.

BAADA YA MCHAKATO HUO NA KURIDHIKA NA WACHEZAJI WALIOFIKIA VIWANGO WATAINGIA KAMBINI KWA AJILI YA MAZOEZI KABAMBE YA MWISHO IKIWA PAMOJA NA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MAJARIBIO YA KIMATAIFA KABLA YA KWENDA CASABLANCA MOROCCO KATIKA MASHINDANO YA KUFUZU KWENDA KATIKA MASHINDANO YA OLIMPIKI.MASHINDANO YA KUFUZU MOROCCO YATAFANYIA KUANZIA TAREHE 27/4-6/5/2012.NA KATIKA MASHINDANO TUNATEGEMEA KUPELEKA WACHEZAJI 10 WA UZITO WA KUANZIA FLY WEIGHT HADI SUPER HEAVY WEIGHT


MAKORE MASHAGA

KATIBU MKUU(BFT)

Mob: +255 713 588818

Email: mashagam@yahoo.com

WADAU WAOMBWA KUISAIDIA TWIGA STARSTimu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) inaendelea na mazoezi jijini Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu Charles Boniface Mkwasa kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Namibia baadaye mwezi ujao.
Mechi hiyo ya kwanza itachezwa ugenini Januari 14 mwakani jijini Windhoek. Timu hiyo ambayo sasa inafanya mazoezi kwa wachezaji kutokea majumbani (off camp) inatarajia kuingia kambini Januari Mosi mwakani.
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linahitaji zaidi ya sh. milioni 50 ikiwa ni gharama za safari, kambi na posho kwa wachezaji na benchi la ufundi kwa ajili ya mechi hiyo moja tu. Mechi ya marudiano itachezwa Januari 29 mwakani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

KIPRE AIONGOZA AZAM KUIUA JKT RUVU CHAMAZI

Kiungo Michael Bolou Kipre wa Azam FC ameiongoza timu yake kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo jioni kwenye uwanja wa Azam Chamazi.

Azam FC imepata ushindi huo wa pili mfulilizo katika mechi zake za maandalizi ya ligi kuu na michuano ya Kombe la Mapinduzi, Azam waliifunga Yanga 2-0 kwenye mchezo wake wa kwanza wa kirafiki,

Kipre alikuwa wa kwanza kufungua kalamu hiyo ya magoli katika dakika ya 26 na dakika sita baadaye Khamis Mcha aliifungia klabu hiyo goli la pili na kupeleka timu mapumziko Azam wakiwa mbele kwa 2-0.

Katika mchezo huo uliozikutanishi timu zote zinazocheza ligi kuu ya Vodacom, JKT Ruvu walicheza katika kiwango kizuri na kufanya mchezo kuwa wa kiushindani japo walikuwa nyuma kwa idadi hiyo ya magoli.

Kiungo JKT ruvu kilikuwa chini ya mchezaji Mohamed Banka akishirikiana na wachezaji wengine wa timu hiyo huku Azam FC kulikuwa na Abdi Kassim, Mcha, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ na Kipre walioweza kuichezesha timu hiyo katika kipindi chote cha kwanza.

Kipindi cha pili timu zote ziliongeza kasi na kufanya mabadiliko Azam FC walitoka golikipa Mwadini Ally, Agrey Moris, Waziri Salum, Abdulhalim Humud, Abdi, Kipre na Gaudence Mwaikimba wakaingia golikipa chipukizi Aishi Mfula aliyechukua vyema nafasi hiyo katika dakika ya 72, Luckson Kakolaki, Samir Haji, Abdulghan Gulam, Himid Mao, Zahor Pazi na John Bocco.

Mabadiliko hayo yaliongeza nguvu kwa Azam na kupelekea dakika ya 78 Mcha kupachika goli la tatu baada ya kipa wa JKT Ruvu Amani Simba kupangua shuti la Bocco na mpira huo kumkuta mcha aliyeupeleka wavuni na kumaliza mchezo kwa Azam kupata ushindi huo wa 3-0.

Kocha msaidizi wa Azam, Kali Ongalah amesema ushindi wa mchezo huo ni maandalizi mazuri kwa ajili ya mechi zijazo.

“Tumeshinda huu mchezo wa pili, hatujaruhusu hata goli moja hivyo upande wa ulinzi inaonyesha tupo vizuri na tukiendelea hivi tutafikia malengo yetu” alisema Kali.

Azam FC itaondoka Dar es Salaam siku ya Jumapili kuelekea Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Mapinduzi, watacheza mechi ya kwanza siku ya Jumatatu dhidi ya Kikwajuni FC mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Amaan.

Ufunguzi wa Msikiti Donge MuwandaRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALHaj Dk Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya kuufungua Msikiti wa Masjid AL Haramayn Donge Muwanda Wilaya ya Kaskazini B Unguja jana,(kushoto) Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ali Juma Shamuhuna.
Picha na Ramadhan Othman IKULU.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALHaj Dk Ali Mohamed Shein,akikata utepe kama ishara ya kuufungua Msikiti wa Masjid AL Haramayn Donge Muwanda Wilaya ya Kaskazini B Unguja jana,(kushoto) Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ali Juma Shamuhuna.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALHaj Dk Ali Mohamed Shein,akitoa nasaha zake kwa waumini wa Dini ya Kiislamu wakati wa ufunguzi wa Msikiti wa Masjid AL- Haramayn Donge Muwanda, Wilaya ya Kaskazini B Unguja jana.
Baadhi ya wananchi na viongozi waliohudhurika katika sherehe za ufunguzi wa Msikiti Masjid Al- Haramayn Donge Muwanda uliofunguliwa jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ALHaj Dk Ali Mohamed Shein,Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Friday, December 30, 2011

WADHAMINI WAANZA KUJITOSA KUDHAMINI 'TABORA LIVINGSTONE MARATHON'
Meneja Maendeleo ya Biashara wa Auric Air, Deepesh Gupta (kushoto) akikabidhi msaada wa fulana kwa Mratibu wa mashindano ya mbio za Tabora Livingstone Marathon, Ramadhani Makula jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Uratibu wa mbio hizo, Tullo Chambo.


*************************************************


Na Mwandishi Wetu, jijini


KAMPUNI ya Ndege ya Auric Air ya jijini Dar es Salaam imejitosa kusapoti mashindano ya Mbio ya Tabora Livingstone Marathon yanayotarajiwa kufanyika mjini Tabora Machi mwakani.
Mbio hizo za kwanza katika historia ya Mkoa wa Tabora, zitakuwa za Nusu Marathon Kilomita 21 na zile za kujifurahisha za Kilomita 5.
Akikabidhi msaada wa fulana kwa Mratibu wa mbio hizo, Ramadhani Makula jijini Dar es Salaam jana, Meneja Maendeleo ya Biashara wa Auric Air, Deepesh Gupta, alisema, wamesukumwa kutoa msaada hyo ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu nne chini ya Rais Jakaya Kikwete katika kuendeleza na kuhamasisha michezo hapa nchini.
Gupta alisema, kwa kuzingatia malengo na madhumuni yam bio hizo, wameona japo watoe msaada huo mdogo wa fulana zitakazotumiwa na waratibu na wasimamizi wa mbio hizo ili kusaidia kufanikisha tukio hilo muhimu.
Akipokea msaada huo, Mratibu wa Tabora Livingstone Marathon, Makula, aliishukuru kampuni hiyo na kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuwaunga mkono katika kufanikisha mbio hizo za kihistoria.
Makula alisema, hafla ya uzinduzi rasmi wa mbio hizo ambao utawashirikisha wadau na wafadhili mbalimbali utafanyika jijini Dar es Salaam Januari 10.
Aliwataka vijana wenye vipaji mbalimbali wa Mkoa wa Tabora na maeneo ya jirani kujiandaa na mbio hizo, huku akitoa pongezi kwa ushirikiano unaotolewa na Chama cha Riadha Mkoa wa Tabora

TTCL YAGAWA MISADA MBALIMBALI LEO
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Bw. Said Amir Said (kushoto) na Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw. Amin Mbaga (kushoto) wakimkabidhi sehemu ya msaada walioutoa kwa Mkurugenzi wa Kijiji cha SOS kinacholea watoto yatima, Dkt. Alex Lengeju Dare es salaam jana kwa ajili ya sikukuu ya mwaka mpya
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Bw. Said Amir Said (katikati) na Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Bw. Amin Mbaga (kulia) wakimkabidhi sehemu ya msaada walioutoa kwa Mratibu wa Maafa Manispaa ya Ilala Bw. Mwasabite Elioth kwa ajili ya watu waliokubwa na mafuriko

PICHA ZA MWANZO KABISA 2012 HIZI HAPA


RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAMIA YA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA TBC MAREHEMU HALIMA MCHUKA LEO.


Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa TBC Bw Clement Mshana wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mtangazaji Halim Mchuka leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kabla ya kwwenda kuzikwa makaburi ya Msasani baada ya Sala ya Ijumaa. (Picha na Ikulu)


Rais Dk. Jakaya Kikwete pamona na baadhi ya ndugu na watoto wa marehemu wakiuombea dua mwili wa marehemu Halima Mchuka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo jijini Dar es salaam. (Picha na Aron Msigwa -Maelezo)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akitoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) marehemu Halima Mchuka aliyefariki tarehe 29 Desemba mwaka huu jijini Dar es salaam. Mwili wa marehemu umezikwa leo katika makaburi ya Msasani jijini Dar es salaam. (Picha na Aron Msigwa -Maelezo)

TASWA KUFANYA MAREKEBISHO YA KATIBAKAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ilikutana hivi karibuni pamoja na mambo mengine ilikubaliana kufanya marekebisho madogo ya Katiba ya chama hicho ili iendane na wakati wa sasa.
Kutokana na hali hiyo Kamati ya Utendaji inemteua mwanamichezo maarufu ambaye pia ni mwanasheria na wakala wa wachezaji wa soka Damas Ndumbaro kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Marekebisho ya Katiba ya TASWA.
Wajumbe wengine kwenye kamati hiyo ni George John ambaye ni Katibu Mkuu Msaidizi wa TASWA,Alfred Lucas ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA na Amir Mhando ambaye ni Katibu Mkuu wa TASWA na atakuwa Katibu wa kamati hiyo na Mwani Nyangasa ambaye ni mwanachama.Kamati hiyo itasimamia mchakato wa marekebisho hayo, kisha utaitishwa Mkutano Mkuu Maalum wa wanachama wote kwa ajili ya kupitia rasimu hiyo na ni imani ya Kamati ya Utendaji kuwa marekebisho hayo ya Katiba hayatachukua muda mrefu, ili mkutano Mkuu wa TASWA ufanyike kabla ya kumalizika robo ya kwanza ya mwaka 2012.

TIGO YASHEREKEA SIKUKUKUU YA CHRISTMAS NA WAKAZI WA MWANZA KATIKA VIWANJA VYA FURAHISHAMwanamuziki wa kundi la Top Top Connection Madee akitumbuiza umati katika tamasha maalum la Tigo la kusherehekea sikukukuu za Christmas mjini Mwanza katika viwanja vya Furahisha

WASANII WA AIRTEL BONGO 50 NA PAMOJA NA WAFANYAKAZI WA AIRTEL WATOA POLE NA MSANII WAATHIRIKA WA MAFURIKO DAR ES SALAAMMeneja Mawasiliano wa kampuni ya simuya Airtel ,Jackson Mmbando akizungumza kuhusiana na utoaji wa msaada uliotolewa na kampuni hiyo kwa kushirikiana pamoja na umoja wa wasanii wa Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Lugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni, Wasanii hao pamoja na Airtel wametoa msaada huo leo vikiwemo vifaa vya nyumbani zikiwemo nguo na vyakula vyote vinathamani ya Shilingi milioni 10/-, pichani kati ni Meneja Masoko wa Airtel, Rahma Mwapachu.


Msaani wa filamu/muziki ajulikanae kwa jina kisanii Shilole akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel pamoja na umoja wa wasanii wa Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Lugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni, Wasanii hao pamoja na Airtel wametoa msaada huo leo vikiwemo vifaa vya nyumbani zikiwemo nguo na vyakula vyote vinathamani ya Shilingi milioni 10/-


Wasanii wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Flava’ wa Kundi la Wanaume Halisi wakiongozwa na mkali Juma Nature na wakikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel pamoja na umoja wa wasanii wa Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Lugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko jijini Dar es salaam waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni, Wasanii hao pamoja na Airtel wametoa msaada huo leo vikiwemo vifaa vya nyumbani zikiwemo nguo na vyakula vyote vinathamani ya Shilingi milioni 10/-


Meneja Masoko wa Airtel, Rahma Mwapaju akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel pamoja na umoja wa wasanii wa Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Lugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni, Wasanii hao pamoja na Airtel wametoa msaada huo leo vikiwemo vifaa vya nyumbani zikiwemo nguo na vyakula vyote vinathamani ya Shilingi milioni 10/-


Ofisa Rasilimalii Watu wa Airtel, Doris Kibasa aliyeongozana na wafanyakazi wengine wa Airtel na wasanii muziki wa Bongo Flava akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel pamoja na umoja wa wasanii wa Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Lugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni, Wasanii hao pamoja na Airtel wametoa msaada huo leo vikiwemo vifaa vya nyumbani zikiwemo nguo na vyakula vyote vinathamani ya Shilingi milioni 10/-


Msanii mkongwe nchini katika muziki wa Bongo Flava Jafarai akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel pamoja na umoja wa wasanii wa Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Lugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni, Wasanii hao pamoja na Airtel wametoa msaada huo leo vikiwemo vifaa vya nyumbani zikiwemo nguo na vyakula vyote vinathamani ya Shilingi milioni 10/-


Ofisa Rasilimalii Watu wa Airtel, Doris Kibasa aliyeongozana na wafanyakazi wengine wa Airtel na wasanii muziki wa Bongo Flava akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel pamoja na umoja wa wasanii wa Bongo 50 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Lugimbana maalum kwa waathirika wa mafuriko waliokusanyika katika kituo cha Hananasifu kilichopo Kinondoni, Wasanii hao pamoja na Airtel wametoa msaada huo leo vikiwemo vifaa vya nyumbani zikiwemo nguo na vyakula vyote vinathamani ya Shilingi milioni 10/-Thursday, December 29, 2011

SUPER D BOXING COACH KUENDELEA KUWANOA VIJANA ZAIDI 2012
Super D Boxing Coach kushoto akiwa katika moja ya GYM


super D Boxing Coach

Super D Boxing Coach Akiwa na Talik Balozi wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala

mazoezi ni Afya akisisitiza Super D Boxing Coach
Super D Boxing Coach akiwa na mwanae Ikota anaefuata nyayo za masumbwi
Na Mwandishi WetuALIYEKUWA bondia wa ngumi za kulipwa Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye pia ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti Ilala amesema anajivunia mafanikio makubwa aliyoyapata katika mchezo wa ngumi katika kipindi cha mwaka 2011.Akizungumza na waandishi wa habari Super D ambaye pia ni mpiga picha wa Magazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na jarida la Maisha alisema moja ya mafanikio ni kuwaandaa vijana chipukizi wengi na kuwafikisha katika kiwango kizuri cha kuvuna matuna ya mchezo huo.Alisema pamoja na hilo pia ameweza kushirikiana vema na wadau wa ngumi pamoja na mapromota mbalimbali wanaoandaa mapambano makubwa kwa kutoa mchango wake wa vifaa vya ngumi ili kufanikisha mapambano mbalimbali yaliyofanyika katika kipindi cha mwaka huu.Katika hatua nyingine Super D amekua akitoa mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria mbalimbali kwa njia ya DVD zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khanny, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.Alisema mipango yake kwa mwaka 2012 ni kuhakikisha anaendelea kuwainua mabondia wengine chipkizi akiwemo bondia Shomari Mirundi na Ibrahimu Class ambao amewataja ni mabondia wazuri wanaohitaji kuendelezwa vipaji vyao.Alisema bondia Ubwa Salum ambaye alimtwanga Mustapha Doto,kwa pointi 60-57 alishinda ambapo pambano hilo lilikuwa moja ya mapambano ya utangulizi ya pambano kubwa la Rashidi Matumla na Maneno Osward lililofanyika DEsemba 25 mwaka huu.
Superd Boxing Coach

Wednesday, December 28, 2011

NETIBOLI HIYO ZANZIBAR KUSHIRIKI KOMBE LA MAPINDUZI

TTimu ya netiboli inayounda kikosi cha timu ya Taifa inaondoka kesho kuelekea visiwani ZANZIBAR kushiriki mashindano ya kombe la Mapinduzi ambapo kikosi hicho kitakuwa chini ya kocha MARY PROTAS na kocha kutoka TANZANIA VISIWANI.

Baadhi ya timu zilizoambwa kushiriki mashindano hayo ni ZAMBIA, BOTSWANA, MALAWI, NAMIBIA ,KENYA na UGANDA.

Mjumbe wa kamati ya utendaji wa CHANETA MWAJUMA KISENGO amesema timu hiyo itafanya vizuri kwani ndiyo timu iliyoshiriki mashindano ya ALL AFRICANS GAME nchini MSUMBIJI.

Hamad rashid agoma kuhojiwa na kamati ya mahadil cuf

Raymond Kaminyoge na Aziza Masoud


HALI bado tete ndani ya Chama Cha Wananchi (CUF) baada ya Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, kugoma kuhojiwa na Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho kuhusu tuhuma za kuvunja katiba. Mbunge huyo aliibua tuhuma nzito kwamba amekamata waraka wa siri wa viongozi wawili waandamizi wa chama hicho, waliokuwa wakipanga njama za kumfukuza.

Hamad aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa ana sababu tano za kugomea kikao hicho, ambazo ni pamoja na waraka huo wa siri aliodai ulitoka kwa mmoja wa viongozi hao kwenda kwa mwenzake. Waraka huo ambao Hamad alidai kuunasa unasomeka, “Tuwe waangalifu tusiingie katika mtego” na uliandikwa Desemba 14 2011 na kutumwa kwa barua pepe.

“ …anataka nifukuzwe kwenye chama, baadhi walioteua na walioteuliwa katika Kamati ya Nidhamu na Maadili wamekwishanituhumu hadharani na kunitia hatiani hivyo kikao hiki hakitatenda haki,” alisema Hamad.

Alitaja sababu nyingine ya kukataa kuhojiwa kuwa ni kutoelezwa tuhuma zake hasa vifungu vya Katiba alivyodaiwa kuvikiuka. “ Ni vema nikaelezwa ni vifungu vipi vya katiba hiyo nilivyokwenda navyo kinyume,” alisema Hamad. Alifafanua kwamba, alitaka apewe hadidu za rejea za kikao kilichounda Kamati ya Nidhamu na Maadili kwa sababu kikatiba, hakuna chombo kama hicho.

“Katiba ya CUF haina chombo kama hicho, kamati hii imeundwa na nani nikipewa hadidu za rejea za kikao kilichounda kamati hiyo zitanisaidia katika kumbukumbu,” alisema Hamad Rashid. Alisema alitaka pia apewe nakala ya uteuzi wa wajumbe walioteuliwa katika kamati hiyo.

Mbunge huyo pia alisema amegomea kikao hicho hadi atakapopewa kanuni zitakazotumika katika kuendesha shughuli nzima ya kujibu tuhuma hizo na kupewa katiba iliyotumika ambayo ameivunja. “Nataka kupewa vitu hivyo ili niweze kuweka kumbukumbu sahihi kwa kila hatua inayochukuliwa na chama,” alisema mbunge huyo wa CUF.

Akizungumzia kamati hiyo, mbunge huyo alisema kati ya wajumbe wanane, watano hana imani nao kwa sababu wamekuwa wakimtuhumu hadharani. “Hawa wajumbe sina imani nao uamuzi wao hautakuwa wa haki,” alisema Hamad. Juzi Hamad Rashid na wenzake 13 waliitwa na Kamati na Nidhamu ili kujibu tuhuma za kuvunja Katiba ya chama hicho. Hatua hiyo imekuja baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya Katibu Mkuu na Mbunge huyo kutuhumiana hadharani.

Waraka wa Siri


Hamad alisema hawezi kuhudhuria kikao hicho kwa kuwa tayari amebaini njama za kushughulikiwa zilizosukwa na vigogo wawili wa chama hicho dhidi yake.“ Nimeshauriana na Makamu na tumeona kuna haja ya jamaa yako (Rashid) na genge lake kuitwa katika Kamati ya Nidhamu na Maadili kuhojiwa,” inasema sehemu ya waraka huo ambao aliusambaza kwa vyombo vya habari.

Waraka huo uliongeza, “ushahidi wa kutosha umekusanywa dhidi yake na wasaidizi wake wakuu na muono wetu ni kuwa tumfukuze uanachama.” Waraka huo ulisisitiza, “Wanachama walio wengi wanatudadisi kwa nini hatuchukui hatua, akishajulikana kuwa si mwanachama atakuwa hana mashiko muache aende CCM au Chadema.” Alipoulizwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Nidhamu wa CUF, Abdul Kambaya alisema taarifa za Rashid kukataa kuhojiwa na Kamati zitapelekwa katika Kamati ya Utendaji.

“ Ni kweli Hamad amegoma kuhojiwa kuhusu tuhuma zinazomkabili, lakini tunachofanya ni kupeleka taarifa kwa kamati ya Utendaji itakayofanya maamuzi,”alisema Kambaya na kubainisha kuwa kamati hiyo inaendelea kuwahoji wanachama wengine wanaotuhumiwa kuvunja katiba ya chama hicho.

Hivi karibuni Hamad Rashid alijikuta kwenye mgogoro na baadhi ya viongozi wa makao makuu ya chama hicho, baada ya kutangaza dhamira hiyo yake ya kugombea nafasi ya katiba mkuu mwaka 2014. Kuanzia hapo akajikuta ameingia kwenye mgogoro na chama hicho kiasi cha kunusurika kushambuliwa na watu wasiojulikana wakati akigawa misaada katika matawi ya chama hicho, kata ya Manzese. Mvutano huo ulisababisha vurugu katika tawi la Chechnya ambako wanachama wanaomuunga mkono walipambana na walinzi wa Blue Guard na kusababisha umwagaji damu.www.mwananchi.co.tz

Rais Dk. Shein ashiriki katika mazishi ya marehemu Kanali Nassor Waziri Mageta

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) pamoja na Viongozi wengine wakiusalia mwili wa Marehemu Kanal Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia,katika msikiti masjid Twariq Bububu nje wa mji wa Zanzibar, aliyefariki jana na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.


Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya Magharibi Unguja wakilibeba jeneza la Marehemu Kanal Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia,aliyefariki jana na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.


Askari wa Vikosi vya SMZ,wakilibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Kanal Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia,aliyezikwa jana katika kijiji cha mkanyageni Wilaya ya Magharibi mkoa wa mjini magharibi Unguja.


Askari wa Vikosi vya SMZ wakiondoa Nguo alizozitumia marehemu Kanali Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia, aliyefariki jana na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,( katikati) pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika maziko ya Marehemu Kanal Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia, aliyefariki jana na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,akitia udongo katika kaburi la Marehemu Kanal Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia,aliyefariki leo na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.


Askari wa Vikosi vya SMZ wakitoa salamu ya hesha katika kaburi la marehemu Kanali Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia, aliyefariki jana na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja. Picha na Ramadhan Othman IKULU