Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, December 13, 2011




BONDIA AMIR KHAN KUMSHITAKI REFARII WA MPAMBANO ALIOPOTEZA





Khan apokwa pauni mil. 20

WASHINTON, Marekani

AMIR Khan amepokwa ubingwa mataji mawili na pauni milioni 20, baada ya kupoteza pambano lake kiutata dhidi ya bondia wa Marekani, Lamont Peterson katika mechi iliyochezwa Washington DC.

Wakuu wa ngumi sasa wanachunguza kitendo cha refa Joe Cooper, aliyemnyang'anya pointi mbili Khan kwa madai alisukuma kitu kilichochangia kupoteza mechi katika sekunde 10 za mwisho.

Kitendo hicho kilimfanya bondia huyo wa Uingereza, Kahn kupokwa mikanda yake ya light-welter ya WBA na IBF kwa Peterson, ambaye alitangazwa mshindi kwa tofauti ya pointi moja.
Khan mwenye miaka 25, atarudiana na Peterson Machi 31 mwakani lakini mpiganaji huyo wa Bolton, atapata pauni 600,000 badala ya pauni milioni 20 kwa kuingia katika uzani wa welterweight katika pambano na Floyd Mayweather Jnr.
Khan alishakusanya pauni milioni 15, wakati alipofahamika katika taasisi inayosimamia Ngumi Uingereza, baada ya kutwaa medali ya fedha 2004 katika michezo ya Olimpiki ya Athens.
mwaka huu alipigana na Paul McCloskey, Zab Judah na kuwashinda lakini Jumamosi alipoteza pambano kwa Peterson na kupata kiasi cha pauni milioni 5.
Khan alimlaumu mwamuzi kwa kumpoka pointi mbili katika sekunde za mwisho, wakati yeye akipigana ugenini.
"Sote tunajua kuwa ni nani alishinda katika mechi ile, ingawa baadhi ya wasimamizi walisema ilikuwa ni maamuzi ya utata. Lakini niko tayari kutwangana na Peterson wakati wowote mahali popote, hata kama kesho."
Peterson alisema hawezi kuogopa kwenda kupigana naye Uingereza, lakini hadi mkataba uwe mzuri kama kila kitu kitakuwa sawa.

"Sina mashaka ya kurudiana baada ya kunitia kovu katika ubingwa kwanini nisimpe nafasi ili kulipa kisasi?"

Khan alisema: "Pambano lingine pangine linaweza kufanyika
Las Vegas au kama Peterson, atajiamini acha tufanye England."

Alisema hawezi kuhama katika uzito huo, hadi kwanza amalizane na Peterson katika mechi ya marudiano."

Kituo cha televisheni cha HBO ambacho kina mkataba na Khan, kinataka mechi hiyo kuchezwa Marekani na kutoa tarehe ya pambano hilo na alisema: "Bado ninaamini ninaweza kuwa mpiganaji namba moja duniani.

Awali alisaini mkataba wa mapambano matatu na Sky Sports, mwezi uliopita kwa kiasi cha pauni milioni moja, mkataba huo bado uko licha ya kupoteza pambano.

No comments :

Post a Comment