Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kuwahutubia wananchi waliohudhuria mkesha wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck sadick, akizungumza jukwaani kutoa salam za sherehe hizo kwa wananchi.
Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Vijana wakishangia burudani iliyokuwa ikitolewa jukwaani na makundi mbalimbali ya sanaa, wakati wa sherehe hizo.
Wasanii wa Kundi la Safi wakiwapagawisha wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Wanamuziki wa Bendi ya Msondo Ngoma, wakiimba jukwaani ikiwa ni sehemu ya kutoa burudani maalum ya kusherehekea sherehi hizo.
Rapa na mwimbaji wa Bendi ya TOT Plus, Jua Kali, akighani rap zake jukwaani wakati wa mkesha wa sherehe hizo.
Wanenguaji wa Bendi ya Msondo Ngoma, wakishambulia jukwaa wakati wa mkesha wa sherehe hizo.
Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha JKT Mgulani, wakishambulia jukwaa kwa kucheza ngoma ya Bugobogobo ya Kabila la Wasukuma, wakati wa sherehe hizo.
Mbunge, John Shibuda, akipagawishwa na ngoma ya Kisukuma ya Bugobogobo, iliyokuwa ikipigwa na wasanii wa kundi la JKT Mgulani.
Wasanii wa Kundi la Taarab la Culture kutoka Zanzibar, wakitoa burudani jukwani.
No comments :
Post a Comment