Tigo yatoa ofa ya nyongeza ya 50% muda wa maongezi kusherekea miaka 50 ya Uhuru
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
9 Desemba, 2011, Dar es Salaam. Tigo, moja ya makampuni ya simu za mkononi yanayoongoza kwa kutoa huduma bora, inasherehekea miaka 50 ya uhuru kwa kutoa ofa ya muda wa maongezi kwa nyongeza ya 50%, kupiga simu Tigo kwenda Tigo kwa wale wateja wote watakaonunua muda wa maongezi kupitia huduma ya Tigo Pesa na Tigo Rusha kati ya Desemba 8 na 11, 2011.
“Promosheni hii ni sehemu ya kampeni yetu ya nyongeza ya muda wa maongezi ambayo ilianza Nov. 25, 2011,” Alisema David Mugittu ambaye ni Mratibu wa Mawasiliano wa Tigo,” Tumeongeza nyongeza ya 50% wiki hii kwa ajili ya kuungana na watanzania wengine kusherehekea miaka 50 ya Uhuru,” Alisema.
Ili kupata muda huu wa nyongeza, mtumiaji atahitaji kuongeza muda wa maongezi kupitia Tigo Pesa na Tigo Rusha. Baada ya kuongeza muda wa maongezi mteja atapata ujumbe wa kumfahamisha kiasi cha nyongeza alichoongezewa, halikadahalika mteja anaweza kupiga *102# ili kuangalia salio. Ofa hii itadumu kwa muda wa siku mbili tu.
Mwisho
Kuhusu Tigo:
Tigo ni mtandao wa simu za mkononi ya kwanza Tanzania, ilianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania wenye ubunifu ya hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemu ya Millicom International Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.
Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambao,ni Gharama nafuu, Uwepo na Upatikanaji .Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa yetu 26 ,Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa taarifa zaidi tembelea: http://www.facebook.com/TigoTanzania
Imetolewa na:
Alice Maro • PR-Tigo
• Simu 255 715 554501 • a.maro@trinitypromotions.co.tz
No comments :
Post a Comment