Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu fainali za mashindano ya Mitumbwi ya Balimi Extra Lager yanayofanyika kesho jumapili Decemba 18, Mwaloni Jijini Mwanza.Kulia ni Meneja mauzo na usambazaji wa Kanda, Malaki Staki.
Meneja mauzo na usambazaji wa Kanda , Malaki Staki akizungumza na waandishi wa habari kuhusu fainali za mashindano ya Mitumbwi ya Balimi Extra Lager yanayofanyika kesho jumapili Decemba18, Mwaloni Jijini Mwanza.Katikati ni Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa na Meneja matukio wa Kanda, Erick Mwayela.
FAINALI ZA MASHINDANO YA MITUMBWI YA BALIMI EXTRA LAGER 2011 KUWAKA MOTO JUMAPILI.
Mwanza; Desemba 16, 2011: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager leo imetangaza kukamilika kwa fainali za Mashindano ya mitumbwi ya Balimi Extra Lager 2011, ambazo zitafanyika siku ya Jumapili tarehe 18 desemba 2011 katika Mwalo wa Kirumba jijini Mwanza.
Fainali hizi zinazotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kufuatia maandalizi ya kutosha toka kwa timu shiriki zitakutanisha timu zaidi ya 12 za akina Baba na timu zaidi ya 8 kwa upande wa kina Mama, toka katika Mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Visiwa vya Ukerewe.
Akithibitisha kukamilika kwa fainali hizo, meneja wa Bia ya Balimi Bi. Edith Bebwa alisema “Balimi Extra Lager imekamilisha maandalizi yote ya Fainali hizi, na timu zitaanza kuingia jijini Mwanza siku ya Jumamosim tayari kabisa kwa mpambano huu mkali utakaofanyika Jumapili katika Mwalo wa Kirumba hapa Mwanza. Gharama zote za usafiri na malazi kwa timu zote zitalipwa na Balimi Extra Lager, hivyo kazi ya washindani ni kupambana kupata vitita vinono vya zawadi tulivyowaandalia”
Akizitajazawadihizo Bi. Edith alisema; kamatulivyotangazahapoawali, mwakahuutumeongezazawadikwawashindiilikuongezachachuyaushindaninapiakutoahamasakwawashirikiwengizaidisikuzijazo. Katikangazihiiyafainaliwashindiwatapatazawadikamaifuatavyo;
FainaliKuu | ||
Wanaume | Wanawake | |
Mshindiwa kwanza | 2,600,000 | 2,200,000 |
MshindiwaPili | 2,200,000 | 1,600,000 |
MshindiwaTatu | 1,600,000 | 850,000 |
MashindiwaNne | 850,000 | 600,000 |
5 hadi 10 - Kilatimu | 400,000 | 200,000 |
No comments :
Post a Comment