KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ilikutana hivi karibuni pamoja na mambo mengine ilikubaliana kufanya marekebisho madogo ya Katiba ya chama hicho ili iendane na wakati wa sasa.
Kutokana na hali hiyo Kamati ya Utendaji inemteua mwanamichezo maarufu ambaye pia ni mwanasheria na wakala wa wachezaji wa soka Damas Ndumbaro kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Marekebisho ya Katiba ya TASWA.
Wajumbe wengine kwenye kamati hiyo ni George John ambaye ni Katibu Mkuu Msaidizi wa TASWA,Alfred Lucas ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA na Amir Mhando ambaye ni Katibu Mkuu wa TASWA na atakuwa Katibu wa kamati hiyo na Mwani Nyangasa ambaye ni mwanachama.
Kamati hiyo itasimamia mchakato wa marekebisho hayo, kisha utaitishwa Mkutano Mkuu Maalum wa wanachama wote kwa ajili ya kupitia rasimu hiyo na ni imani ya Kamati ya Utendaji kuwa marekebisho hayo ya Katiba hayatachukua muda mrefu, ili mkutano Mkuu wa TASWA ufanyike kabla ya kumalizika robo ya kwanza ya mwaka 2012.
No comments :
Post a Comment