Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, May 31, 2013

NEY WA MITEGO: NDOA ZINASHUSHA KIWANGO CHA MSANIINa Elizabeth John

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Emmanuel Elibriki ‘Ney wa Mitego’ amesema asilimia kubwa ya wasanii ambao wanashuka kimuziki ni wale ambao wanakua wameingia katika maswala ya ndoa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ney alisema wasanii wengi wa bongo wanakurupuka katika hilo na ikitokea ambaye amejipanga ni wachache sana na hapa bongo hajaona.

“Wasanii wengi wa bongo tunakurupuka na hatujipangi katika mambo ya familia zetu na ndio maan aikitokea msanii anaoa basi ujue lazima atashuka kimuziki,” alisema Ney.

Katika hatua nyingine, mkali huyo alimpongeza msanii mwenzake, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ kwa kuwa na mpango wa kuoa hivi karibuni.

“Diamond ni mdogo wangu, nampa hongera kwa kutaka kuingia katika maisha ya ndoa hilo sio swala dogo namuombea afanikishe mipango hiyo,” alisema.

Diamond ametangaza kwamba anatarajia kufunga ndoa miezi miwili ijayo na kusema kwamba anaamini kwa kufanyahivyo utakua ni hatua moja wapo ya kuzidi kufanikiwa kimaisha.

Waziri mkuu Mizengo Pinda akiwa emina ya siku Mbili 

 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimfafanulia jambo  Mkuu wa Wilaya ya Bunda Ajelina Mabula nje ya ukumbi wa Loyal Village Dodoma walipoku wakitoka Kwenye Semina ya wakuu wa mikoa, Wilaya na Wabunge kuhusu Mfumo mpya wa utoaji wa Ruzuku ya Mbolea ya mazao kwa wakulima, iliyoandaliwa na Wizara ya kilimo na Chakula.
Waziri mkuu Mizengo Pinda akitoka kufunga Semina ya siku Mbili iliyofanyika Dodoma jana iliyowahusisha Wabunge, Wakuu wa Mkoa na Wilaya wa Nchi Nzima Kuhusu Utaratibu mpya wa Utoaji wa Ruzuku ya mbolea ya mazao kwa Wakulima katikati ni Waziri wa Kilimo na Chakula Christopher Chiza Naibu Waziri wa wizara hiyo Adamu Malima na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Anjelina Mabula
Washiriki wa Semina ya Utaratibu Mpya wa utoaji wa Ruzuku ya Mbolea Kwa wakulima iliyofanyika mjini Dodoma kwa siku mbili

PICHA NA JOHN BANDA 

Big Brother Africa: Washiriki watano waingia danger zone, wawili kutoka Jumapili hii

Baada ya saa 24 kupita toka mchezo uanze big brother alitoa tangazo la washiriki watano walioingia katika hatari ya kuiaga Big Brother “The Chase” Jumapili hii (June 2).

Majina ya washiriki walio katika hatari ya kutoka ni matano lakini watakaofungasha mizigo yao Jumapili hii ni wawili kati yao.

Upande wa Rubies House walio katika list hiyo ni hawa:


Selly wa Ghana

Natasha kutoka Malawi.
Upande wa Diamond House panga la eviction limemdondokea Betty wa Ethiopia baada ya mkuu wa nyumba hiyo Fezza kumuokoa mshiriki wa Ghana Elikem ambaye ndio aliyekuwa amechaguliwa na Big Brother.

Betty wa Ethiopia
Moja ya mamlaka aliyonayo mkuu wa nyumba ni pamoja na kumuokoa mshiriki anayekuwa amechaguliwa kutoka, kwa kumpendekeza mshiriki mwingine kwa niaba yake.

Washiriki wengine waliongia katika hatari ya kutoka weekend hii ni muwakilishi wa Kenya Huddah Manroe, pamoja na Denzel kutoka Uganda.


Huddah Manroe

Denzel

SUMITOMO CORPORATION FOR KINYEREZI POWER GENERATION The Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Finance Dr. Servacius Likwelile and Sumitomo Corporation Senior Official signs a Memorandum of Understanding(MOU) for Kinyerezi 240 MW combined cycle power project at SUMITOMO Corporation Headquarters in Tokyo this morning. Witnessing the signing ceremony is President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and SUMITOMO Corporation President and CEO Mr.Kuniharu Nakamura.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete receives bouquet of  flowers shortly after he arrived at SUMITOMO Corporation Headquarters in Tokyo Japan for talks with senior corporation officials .Looking on is SUMITOMO Corporation President and CEO Mr.Kuniharu Nakamura. Photo by Freddy Maro

NSSF MEDIA ALL STARS Vs WABUNGE LIVE ON STAR TV Kocha wa timu ya NSSF Media All Stars, Sanifu Lazaro akipimwa afya na Dk. Frida Francis kutoka Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo kabla ya kuanza kwa safari ya kwenda Dodo kupambana na timu ya Wabunge siku ya Jumamosi Juni Mosi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Pambano hilo litaoneshwa Live kupitia Star Tv.
 Dk. Margreth Mtaki kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo akimpima afya mshambuliaji wa timu ya soka ya NSSF Media Kombaini, Maulid Kitenge kabla ya safari ya kwenda Dodoma kupambana na timu ya Wabunge. 
 Mchezaji wa timu ya Netiboli ya NSSF Media Kombani, Somoe Ng'tu akipimwa afya.

TASWIRA ZA MSIBA WA MSANII ALBERT MANGWEA HUKO MBEZI BEACH NYUMBANI KWA BABA MDOGO WAKE


MAOMBOLEZO ya msiba wa aliyekuwa mwanamuziki wa kizazi kipya, marehemu Albert Mangwea, yameanza nyumbanmi kwa baba yake mdogo, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambako jana jioni ndugu, jamaa na majirani walikutwa wakiwa katika matayarisho ya kuupokea mwili wa marehemu.

Floyd Mayweather Jr KUPANDA ULINGONI September 14 NA Saul “Canelo” Alvarez


Floyd Mayweather Jr. (44-0, 26 KO’s) VS Saul “Canelo” Alvarez (42-0-1, 30 KO’s) step foot inside the ring on September 14th at the MGM Grand in Las Vegas, Nevada

Wednesday, May 29, 2013

KASEBA APANIA KUMKALISHA MMALAWINa Elizabeth John


BONDIA wa ngumi za mateke ‘Kick Boxer’ Japhet Kaseba amesema amejipanga kuweka rekodi nzuri katika tasnia hiyo kwa kumchapa Mmalawi, Rasco Chimwanza katika pambano lao la kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati linalotarajiwa kuchezwa Juni 8, mwaka huu.Akizngumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Kaseba alisema anajua kama bondia huyo ni nyota katika tasnia hiyo, lakini kutokana na maandalizi aliyoyapata atahakikisha anaweka heshima katika ngumi za mateke.
“Namshukuru mungu nina afya nzuri hadi sasa na naendelea na mazoezi kwajili ya pambano hilo naomba Watanzania wajitokeze kwa wingi katika ukumbi huo wa DDC Magomeni,” alisema Kaseba.
Naye Katibu Mkuu wa Oganizasheni ya ngumi ya za kulipwa Tanzania (TPBO), Ibrahim Kamwe alisema maandalizi ya pambano hilo yamekamilika, na tayari wamemtumia nauli Mmalawi huyo na kwamba anategemea kuingia nchini Juni 5.
Alisema TPBO imemtengenezea mazingira mazuri ya ushindani, Kaseba na kwamba wanategemea atafanya vizuri katika pambano hilo kutokana na maandalizi ambayo anaendelea kufanya.

 Nae kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake kukiwa na clips za mabondia  wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali

CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika masumbwi

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata DVD hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo

Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia
 
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila ,Japhert Kaseba,Rashidi Matumla, Hassani Matumla,Thomas Mashali Dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis  Miyeyusho,Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe. 
 
 mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

MTOTO RAMLA ADAM ASHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWAMTOTO RAMLA ADAM
MTOTO RAMLA ADAM kushoto akilishana keke na Zainabu Mhamila 'Ikota' wakati wa siku yake ya kuzaliwa kwake iliyofanyika nyumban kwao Buguruni ramla alitimiza miaka sita katika siku yake hiyo
Mtoto Ramla Adam kulia akiwa katika picha ya pamoja na mama yake mzazi na Zainabu Mhamila 'Ikota'

BEN PAUL KUWASINDIKIZA MISS UN-COLLEGE TEMEKE
 Florence Josephat, mratibu Redd's Miss Uni-college. Kulia ni mmoja wa waratibu Francisca Mansilo.


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Bernard Paul ‘Ben Paul’, anatarajiwa kuwasindikiza warembo wa kinyang’anyiro cha Redd’s Miss Uni-college Temeke kitakachofanyika kesho katika ukumbi wa Club Bilicanas, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, mratibu wa shindano hilo, Florence Josephat, alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na kwamba kilichobaki ni shoo yenyewe ambayo alitamba itakuwa katika ubora wa hali ya juu.
Alisema kuwa jumla ya warembo 13 wanatarajia kupanda jukwaani siku hiyo, ikiwa ni baada ya kunolewa vilivyo kwa takribani wiki tatu na kwamba wameiva kuwapagawisha watakaofika kushuhudia uhondo huo.
“Maandalizi yote yamekamilika hivyo tunawaomba wapenzi wa burudani na urembo kwa ujumla kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwani kipenzi cha warembo, Ben Paul, atatoa burudani ya hali ya juu itakayoambatana na shoo kutoka kwa warembo wetu kutoka vyuo vitano vilivyopo Temeke,” alisema.
Alivitaja baadhi ya vyuo hivyo kuwa ni Chuo Kikuu cha Uganda, TIA, Chuo cha Bandari, DUCE na Chuo cha Utalii, huku akitamba kuwa kutokana na ubora wa warembo walionao, wana imani mwaka huu Redd’s Miss Tanzania atatoka katika kitongoji chao hicho.
Florence ambaye alikuwa mshiriki wa fainali za Miss Tanzania 2008, aliwataka wapenzi wa urembo na burudani, hasa wanafunzi wa sekondari na vyuo, kujitokeza kwa wingi siku ya shoo yao ili kujionea warembo bomba, huku wakipata burudani ya aina yake.
Alitaja kiingilio cha shoo yao kuwa ni Sh 10,000 na kwamba mbali ya kinywaji cha Redd’s ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo, wadhamini wengine ni Shome Decoration & Catering, djfetty.blogspot.com na Lamada Hotel.

MISS SINZA/ MISS TANZANIA 2012-2013 BRIGIT ALFRED AWAFUNDA WAREMBO WA REDD'S MISS SINZA 2013
 Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (kulia) akizungumza na Warembo wanaotarajia kuwania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea katika Kambi yao ya mazoezi jana katika Ukumbi wa Meeda Sinza na kuwafunda kuhusu mashindano hayo kuelekea shindano hilo linalotarajia kufanyika Juni 7 mwaka huu kwenye Ukumbi huo. Katika shindano hilo Viingilio vitakuwa ni Sh. 20,000 kwa VIP na viti vya kawaida ni Sh. 10,000. Shindano hilo limedhaminiwa na Mtandao wa www.sufianimafoto.com, kinywaji cha Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Clouds Media Group, CXC Africa, Saluti5 na Fredito Entertainment.
 Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (katikati) akipozi na warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea kwenye Kambi yao ya mazoezi katika Ukumbi wa Meeda Sinza.
Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (katikati) akipozi na warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea kwenye Kambi yao ya mazoezi katika Ukumbi wa Meeda Sinza. Picha zote na www.sufianimafoto.com

SUPER NYAMWELA AKAMILISHANYIMBO YAKE MPYA YA DUVELLEE DUVELLEE LA POP BONGO
MNENGUAJI Mahiri wa muziki wa dansi nchini, anayeshambulia na bendi ya Extra Bongo, Super Nyamwela, amekamilisha Song lake jipya linalokwenda kwa jina la Dullee Duvellee, linalopigwa katika mtindo wa Bongo Pop.

Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.com, Nyamwela, amesema kuwa Wimbo huo aliourekodia katika Studio za C91, zilizopo Kinondoni, amemshirikisha Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Muki kutoka katika Kundi la Makomandoo lililo chini ya THT.

Aidha alisema kuwa Msanii huyo aliyemshiriki ni yule anayetamba na Song lake kali ya Staili ya Kibega, ambao kwa pamoja katika wimbo huo wemefanya kazi ya kueleweka na inayomvutia kila mmoja atakayepata bahati ya kuusikiliza wimbo huo.

''Hivi sasa najipanga kuzindua staili yangu mpya ya Bongo Pop, inayokwenda na 'Swaga za Duvellee Duvellee' ambyo kwa maana halisi ya kiswahili cha Kitaa ni Shwari Shwari, na tayari wimbo huu nimeshausambaza katika Vituo mbalimbali vya Redio nchini na baadhi wameshaanza kuutendea haki kwa kuupiga na kuwapa raha wasikilizaji''. alisema Nyamwela

Pia Nyamwela amesema kuwa yupa katika maandalizi ya kurekodi Video ya Wimbo huo mwishoni mwa wiki hii katika Studio mpya za THT.http://www.sufianimafoto.com/

MASHINDANO YA CHESS KUTIMUA VUMBI JUNI 14-6
 Mkurugenzi wa Spicenet Tanzania, Viney Choundary akizungumza  na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mashindano ya wazi ya kimataifa yajulikanayo kama ‘Spicenet Tanzania Open Chess Championship 2013’ yanayotarajiwa kutimua vumbi juni 14-16 katika  ukumbi wa Meru uliopo katika jengo la Golden Jubilee Tower mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam. Kulia ni Emmanuel Mwaisumbe na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha mchezo wa Chess, Joe Anea.
Emmanuel Mwaisumbe akifafanua jambo.

Na Elizabeth John
CHAMA cha Mchezo wa Chess nchini, kimeandaa mashindano ya wazi ya kimataifa yajulikanayo kama ‘Spicenet Tanzania Open Chess Championship 2013’ ambayo yanatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 14 hadi 16 katika ukumbi wa Meru uliopo katika jengo la Golden Jubilee Tower mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam
Katika kunogesha mashindano hayo ambayo yataweka rekodi Afrika Mashariki, yatashirikishwa na bingwa ambaye alikua ni mchezaji namba tatu duniani mwaka 1990, Nigel Short.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Chess, Joe Anea alisema mashindano hayo yatahusisha wachezaji kutoka Tanzania, Zambia, Uganda na Kenya na kwamba yanatarajiwa kuhudhulia na jumla ya wachezaji 80, huku wachezaji 50 wakitoka Tanzania na 30 kutoka nchi za jirani.
Alisema kuwa mshindi wa kwanza atajinyakulia sh. 1,000,000, sh.500,000 kwa mshindi wa pili, sh. 300,000 kwa mshindi wa tatu, sh. 100,000 kwa mshindi wa nne na tano.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni ya Spicenet, ambayo ndio wadhamini wa mchezo huo, Vinay Choudary alisema wameamua kuungabnisha nguvu na chama cha Chess kuufufua mchezo huo Tanzania katika jitihada za kuhakikisha nchi yetu inang’ara katika medani ya michezo katika mashindano ya kimataifa.
“Nia yetu ni kukisaidia chama hiki kuhakikisha mchezo huo unatangazwa na hatimaye kutambulishwa kwa watu wengi kupitia shule, taasisi, vyuo vikuu na njia nyingine,” alisema.
Naye Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Benson Chacha aliupongeza uongozi wa Chess pamoja na wadhamini wake kwa kuamua kuurudisha mchezo huo ambao ulisajiliwa na BMT mwaka 1984.
“Sisi kama Baraza tutausaidia mchezo huu kupata vitambulisho mbalimbali vya kushiriki mashindano ya mchezo huu, pia tunaomba wadau wajitokeze kudhamini kwa lengo la kukuza michezo nchini,” alisema.

Monday, May 27, 2013

KING CLASS MAWE KUPAMBANA NA BAUNSA JUNI 16 PANANDI PANANDI ILALAKING CLASS MAWE
BAADA ya kumsambalatisha Amosi Mwamakula kwa point  bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' anakabiliwa na kibarua kizito kwa kupanda ulingoni na bondia  Patrick Anthony Kavako 'Baunsa' wa Morogoro  mpambano wa raundi 8 utakaofanyika katika ukumbi wa Panandi panandi Ilala Bungoni Juni 16 akizungumzia mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa mpambano huo ni wa kukata na shoka ambao si wa kukosa kwani kila mmoja amejitahalisha kivyake hivyo wasubili tu siku ya mpambano huo
Patrick  Kavako'Baunsa'
Unajua morogoro na Dar es salaam ni mahasimu katika michezo yote ukiangalia na sasa wamekutanishwa vijana katika masumbwi hivyo kila mmoja anaitaji ushindi ili ajiongezee rekodi yake kwani 'King Class Mawe' ato kubali kupigwa na Kavako ato kubali kabisa kupoteza mpambano wake kiraisi kwani na yeye anaitaji ajulikane katika ulimwengu wa masumbwi na kuiperekea sifa morogoro kama ilivyo kwa mabondia wengine wanao tamba mkoani hapo 
Mpambano huo ulioratibiwa na Kinyogoli Fondition kwa kushlikiana na PST itakuwa chachu kwa vijana kuendelea kuupenda na kuucheza mchezo huo unaopendwa na wengi nchini
mbali ya mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka bondia Abuu Mtambwe ataoneshana umwamba na Kassim Gamboo na Bondia mkongwe kabisa Yohana Robart atamenyana na Mussa Sunga
 
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini,Rajabu Mhamila ‘Super D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake kukiwa na clips za mabondia  wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali

CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika masumbwi

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata DVD hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo

Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia
 
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila ,Japhert Kaseba,Rashidi Matumla, Hassani Matumla,Thomas Mashali Dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis  Miyeyusho,Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe. 
 
 mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

Zantel yazindua Epiq Open Mic
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond na Ney wa Mitego wakitumbuiza jukwaani kwenye uzinduzi wa tamasha la  Epiq Open  Mic 
=======  ======  ========
Katika kuelekea msimu wa sita wa shindano la kuimba la Epiq Bongo Star  Search, kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imezindua Epiq Open  Mic ikiwa ni nafasi nyingine kwa vijana wenye vipaji vya muziki kuonyesha  vipaji vyao kabla usaili wa Epiq Bongo Star Serach haujaanza.

Epiq  Open  Mic  inatarajiwa  kuwapa  nafasi  vijana  kujifunza  misingi  ya  muziki kutoka kwa mmoja wa watayarishaji wa muziki maarufu zaidi nchini,  Marco Chali. Marco  Chali  ambaye  pia  ni  mtunzi  na  mwimbaji,  ametayarisha  nyimbo  nyngi ambazo zimeshinda tuzo ndani na nje ya nchi za wasanii kama Ms. 

Trinity  kutokea  Jamaica,  A.Y  wa  Tanzania,  Prezzo  wa  Kenya,  J  Martins  kutoka Nigeria na wengine wengi. Tamasha  hilo  la  Epiq  Open  Mic,  ambalo  ni  la  bure  litazinduliwa  rasmi  kwenye  viwanja  vya  Mwembe  Yanga  Temeke  tarehe  26  ya  mwezi  huu  ikisindikizwa  na  wakali  kibao  wa  Bongo  flavor  kama  Diamond  Platnumz,  Madee, Godzila, Ney wa Mitego, Mabeste na Mrap.

Akizungumza  wakati  wa  kuzindua  matamasha  hayo,  Afsa  Biashara  Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema kampuni ya Zantel inaaminini katika  kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao. ‘Muziki ni ajira kwa vijana wengi, na kuamini hilo ndio maana kampuni ya  Zantel  imeamua  kuwafikia  vijana  wote  wenye  vipaji  na  kuwapa  nafasi  ya  kuonekana’ alisema Khan.

Baada  ya  uzinduzi  wa  tamasha  la  Epiq  Open  Mic  Mwembe  Yanga  tamasha  hilo  litaendelea  kila  jumamosi  kwenye  makao  makuu  ya  Zantel  likiwapa nafasi vijana kujisajili na kurekod sauti zao.  Vijana watakaorekodi sauti zao watapigiwa simu na timu ya watayarishaji  wa muziki chini ya Marco Chali pamoja na wanamuziki ili kuwapa ushauri   wa namna ya kuboresha muziki wao zaidi. 

‘Zantel imejipanga kutumia fursa hii kuwahamasisha vijana kushiriki katika  kukuza  vipaji  vyao,  kuongeza  uelewa  wa  mambo  ya  muziki  pamoja  na  kuchangamkia fursa zilizopo katika muziki’ alisisitiza Khan. Epiq  Open  Mic  pia  inatarajia  kuwapa  fursa  ya  kurekodi  baadhi  ya  vijana  watakaokua na vipaji.

GARI LAGONGA TRENI DAR MKE ALIYEKUWA AKINDESHA YUPO TAABANI MUME WAKE AFA PAPO HAPOWakazi wa Dar es Salaam wakingalia eneo ajali hiyo ilipotokea majira ya asubuhi leo.
 
Treni likiendelea na huduma zake likipita jirani na eneo lilipogongana na gari dogo aina Honda CRV jirani na Moshi Bar Dar es Salaam asubuhi leo. Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni mume wa dereva wa gari hilo alifariki papo kwa hapo. Mwanafunzi wa shule aliyejulikana kwa jina la Grace Samsoni alipata michubuko  wakati wa ajali hiyo alitibiwa na kuruhusiwa katika hospitali ya Amana.
 
Baadhi ya wakazi wa eneo la Moshi Bar karibu na Mombasa nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam wakiangalia kioo cha gari aina ya Honda CRV eneo ajali ilipotokea. 

Agnes Msoka aliyekuwa akiendesha gari lililogonga treni na kusababisha kifo akisubiri kufanyiwa upasuaji hospitalini.
 
Dereva wa gari liligonga Treni akiwa amelazwa ICU kwa matibabu.

Gari iliyogonga treni likiwa limeegeshwa Kituo cha Polisi Kikuu cha TAZARA Dar es Salaam.

Huyo ndo marehemu aliyefariki katika ajali hiyo.

HAMADUU MWALIMU ALIVYO MWONESHA UBABE COSMAS KIBUGABondia Cosmas Kibuga kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hamaduu Mwalim wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki mwalimu alishinda kwa pointi  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Cosmas Kibuga kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hamaduu Mwalim wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki mwalimu alishinda kwa pointi  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Cosmas Kibuga akimsubili kwa hamu hamaduu mwalim baada ya kudondoka chini wakati wa mchezo wao jana
Bondia Hamaduu Mwalimu kushoto akioneshana umairi wa kurushiana makonde na Cosmas Kibuga wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana Mwalimu alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mpambano wa utangulizi kwa ajili ya kusafisha uwanja