Waandaji
wa mbio hizo maarufu nchini wamesema jijini hapa leo kuwa kwa sasa mbuzi
watakaoshiriki mbio hizo wako kwenye kambi za mazoezi huku zawadi kemkem za
kuvutia zikiwa zimeandaliwa kwa mwaka huu.
“Tunachokihitaji
kwa sasa ni uwepo wa mashabiki watakaohudhuria tukio hilo la kufurahisha na
hivyo kutusaidia kufikia lengo tulilojiwekea la kusanya shilingi bilioni moja kwa
ajili ya taasisi mbalimbali za kujitolea nchini,” Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi, Mama Karen Stanley alisema.
“Siku
hiyo tumeandaa sehemu mahsusi kwa ajili ya aina mbalimbali ya vyakula vya
kuvutia kutoka sehemu maarufu zinazohusika na mapishi jijini Dar kama Rose
Garden, Arca di Noe, Black Tomato na Q Bar.
“Pia
tutakuwa na eneo lililokarabatiwa kwa ajili ya michezo ya watoto
litakalowafanya watoto watakaofika kufurahi na kuikumbuka siku hiyo. Lipo eneo
jingine jipya kwa watoto wadogo zaidi huku eneo jingine lililotayarishwa na Neverland
Playgroup and entertainment kwa ajili ya watoto wakubwa zaidi litakalokuwa na
michezo kama sarakasi, ngoma, kucheza muziki na wachekeshaji kutoka asasi ya Kigamboni Community Centre.”
Tukio
hilo ka kifamilia la kila mwaka litafanyika Juni Mosi mwaka huu kwenye eneo la Green,
mtaa wa Kenyatta kuanzia saa sita mchana hadi saa 11.30
jioni. Gharama za tiketi ni Sh 5,000 kwa watu wote na zitauzwa getini.
Mbio
hizo za mbuzi za hisani zinafanyika kwa mara ya 13 mwaka huu. Tangu
yalipoanzishwa mwaka 2001, tayari zaidi ya shilingi milioni 660 zimekwisha
kusanywa kwa ajili ya mashirika na taasisi mbalimbali za kujitolea nchini.
Mwaka
jana tukio hilo liliweka rekodi kwa kukusanya shilingi milioni 115 kwa kwa
ajili ya mashirika 15, huku wahudhuriaji wakifika 4,200 na kulipa kiingilio
getini.
Mama
Stanley alisema: “Mwaka huu tunatarajia kufanya makubwa zaidi. Tunafuraha ya
kuwa na wadhamini wengi muhimu sana, ambao ndio uti wa mgongo wa tukio lenyewe.
Bila wao hakika tusingekuwa hapa. Kwa namna ya pekee yunatoa shukrani kwa
wadhamini wa mbio hizo Southern Sun, Coca-Cola, Tanzanian Breweries Limited,
Mantra Tanzania, Erolink, FNB na Symbion.
“Lakini
ukweli ni kwamba bila ujio wa watu wa kawaida, mashabiki kutoka sehemu mbalimbali
za Dar, wenyeji na wageni, kushuhudia mbio hizo za aina yake kusingekuwa na
maana yoyote. Kwa hiyo karibuni nyote, msiisahau siku hiyo ya ajabu kabisa!”
Miongoni
mwa zawadi kubwa kwa mwaka huu ni tiketi ya kwenda Ulaya na kurudi
itakayotolewa na SWISS, safari ya kwenda kwenye mbuga ya wanyama ya Selous na
kifurushi cha kupata mtandao wa Intaneti kwa mwaka mzima kutoka UhuruOne kikiambatana
na vifaa na uunganishaji.
Dhana
ya mwaka huu, ‘Viumbe wa Baharini na Mabaharia’,
inaweza kuvutia wengi wanaopenda kuingia kwenye mashindano ya mavazi ya kuvutia
huku kukiwa na zawadi nono kwa kundi litakalovaa vyema. Kutakuwa pia na
shindano la mavazi maalumu kwa watoto na zawadi kwao.
Mama
Stanley alisema: “Ukija umevaa kwa mtindo wa nguva au baharia, au hata ukiwa
kawaida tu utafurahia mambo tuliyokuandalia mwaka huu.”
Kwa habari zaidi tembelea tofutti yetu; www.goatraces.com
No comments :
Post a Comment