Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amewataka wafanyabiashara ndogo ndogo (machinga ) mjini Iringa kuendelea kufanya kazi katika eneo la Mashine tatu bila kufanya vurugu zozote kwa wale wanaozuia kufanya hivyo.
Akizungumzia suala la Machinga kuendelea kunyanyasika mbunge Msigwa amesema kuwa tayari suala hilo ameanza kulipigania bungeni kwa waziri mwenye dhamana hivyo kamwe machinga Iringa wasikubali kunyanyasika .
Aidha mbunge huyo amemtaka katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Bw Kinana kutosubiri muda wa siku 21 alizozitoa kumfikisha mahakamani kuwa yupo tayari kwenda mahakamani hata kesho.
Mbunge Msigwa amesema kuwa katika ukweli kama hata kuwa tayari kumwogopa mtu na kuwa siku zote atasimama katika ukweli katika kupigania maslahi ya Taifa hili.
Mbunge Msigwa amesema kuwa hatua ya katibu mkuu wa CCM kukimbilia katika vyombo vya habari kutishia kumfikisha mahakamani bila yeye mhusika kupelekewa taarifa ni sawa na kumwogopa na hivyo suala la Kinana kwenda Mahakamani si sawa na kumtishia nyau mtu mzima.
Kwani alisema kuwa Chadema ina mawakili waliojitosheleza na kuwa hawatanyamaza kusema ukweli kwa kuogopa vitisho vyovyote .
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini akiwahutubia umati mkubwa wa wananchi wa jimbo hilo jioni hii katika eneo la stendi kuu ya mabasi ya mikoani
Umati mkubwa wa wananchi wakimsikiliza mbunge wao wa jimbo la Iringa mjini
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji ,Msigwa akiwahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini
No comments :
Post a Comment