Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, May 8, 2013

WADAU WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MWANZA (MPC) WAJITOKEZA KUCHANGIA UNUNUZI WA MASHINE YA KUCHAPISHA MAJARIDA




Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani Mwanza (MPC) Deus Bugailwa akitamka ahadi za watu mbalimbali na mashirika ambayo hayakufanikiwa kufika katika Harambee hatua ya Mwanza ya kuchangisha fedha ili kununua mashine ya kisasa ya kuchapisha magazeti mbele yake ni Rais wa UTPC Keneth Simbaya. Harambee hiyo ilifanyika katika ukumbi wa JB Belmont Mwanza.

Meneja wa Kanda wa Benki ya NMB Straton Chilongola (wa pili kulia) akiwa na Meneja Mawasiliano wa benki hiyo Bi. Josephine Kulwa wakikabidhi hundi ya shilingi milioni mbili kwa Rais wa UTPC Keneth Mbaya, katika kuchangia harambee ya ununuzi wa mashine ya kisasa ya kuchapisha magazeti. Kushoto kabisa ni Mwenyekiti wa MPC Deus Bugailwa.  

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani Mhe. Stanslaus Mabula alitoa kauli ya ofisi yake kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja kwenye harambee ya ununuzi wa mashine ya kisasa ya kuchapisha magazeti, iliyofanyika Hotel JB Belmount Mwanza.

Ni mkono wa shukurani kutoka kwa mwenyekiti wa MPC Bw. Deus Bugahilwa kwa Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula. Hata hivyo meya huyo hakukaa sana kwenye harambee hiyo kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine ya kijamii, hivyo aliomba radhi na kuondoka. 

Ilikuwa ni zamu ya Brother kutoka Mwananchi Communication Fredrick Katulanda.

Na hapa ilikuwa ni zamu ya mdau kutoka New Habari Cooperation Grace Chilongola.

Brother Jimmy Luhende hakulichukulia suala hili mzaa alikuja na mpunga wa kutosha wa kitu 'cash'.

Mwanasheria wa Kampuni ya vyombo vya usafiri majini Marine service hakuwaangusha wanahabari.

Naye katibu wa MPC alihusika changizoni.

Meza ya Mwandishi wa habari wa ITV Mwanza Mabere Makubi ilipendeza sana.

CEO wa Gsengo blog Mr. Albert G. Sengo akiwasilisha mchango wake katika harambee ya kuchangisha fedha ili kununua mashine ya kisasa ya kuchapisha magazeti.

No comments :

Post a Comment