Waziri
Asiye na Wizara Maalum wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Machano Othman
akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 10 nahodha wa timu
ya KMKM, Maulid Ibrahimu baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Grand Malt huko Zanzibar. (Na Mpiga
Picha Wetu
Wachezaji wa timu ya KMKM
wakiwa katika picha ya pamoja na kombe lao wakishangilia ubingwa wa soka wa Ligi Kuu ya Soka ya Grandmalt huko Zanzibar.
Timu ya KMKM wakiwa pamoja na kocha wao Ally Bushiri wakishangilia ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka ya Grand Malt huko Zanzibar.
Na Mwandishi Wetu,
Zanzibar
MABINGWA wapya wa
Ligi Kuu ya Grand Malt, KMKM imesema itahakikisha inafanya kweli katika
mashindano mbalimbali ili kudhihirisha umma kuwa, kinywaji hicho hakikukosea
kuidhamini ligi hiyo.
Akizungumza wakati
wa hafla ya kukabidhi washindi zawadfi iliyofanyika kwenye hoteli ya Zanzibar
Ocean View, Afisa Michezo wa KMKM, Ramadhan Hassan ‘Mabio’ alisema hilo
watalifanya pamoja na pia kuilinda heshima ya timu.
“Timu yetu ni moja
kati ya zile kongwe hapa Tanzania, hivyo napenda kuahidi kwamba tutafanya kila
iwezalo ili kuwafanya wadhamini wetu wajisikie furaha kwa kushinda kwa mechi
tutakazocheza.
“Kwa muda mrefu
soka la Zanzibar lilikuwa limeyumba kutokana na kukosa mdhamini, ila kwa sasa
tunapenda kuwashukuru Grand Malt kwa kudhamini Ligi Kuu ya Zanziobar,” alisema.
Maneno hayo
yaliungwa mkono na wadau mbalimbali wa soka visiwani hapa, ambao walisema
udhamini wa Grand Malt umesaidia kwa kiasi kikubwa kuinua soka la Zanzibar.
Naye kocha wa
KMKM, Ally Bushiri alisema kwa sasa anahakikisha anaiandaa timu kwa ajili ya
mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Tunashukuru kwa
kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Grand Malt na sasa tunachofanya ni kutazama mbele
zaidi,” alisema.
Ligi Kuu ya
Zabnzibar kwa sasa inadhaminiwa na kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt,
ambao wameidhamini kwa misimu mitatu.
No comments :
Post a Comment