Mmoja wa wachezaji wa Friends Rangers (mwenye mpira) akichakarika uwanjani kabla timu yao haijafuzu ligi ya mabingwa wa mkoa (RCL) ambapo pia imepeta hadiu raundi ya pili |
Na Boniface Wambura
Wakati
Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inaanza kutimua vumbi keshokutwa (Mei
12 mwaka huu), timu mbili zinakwenda moja kwa moja raundi inayofuata
baada ya mabingwa wa Pwani, Kiluvya United kuondolewa na mkoa wa Manyara
kutowasilisha bingwa wake.
Kamati
ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
iliyokutana leo (Mei 10 mwaka huu) imeiondoa Kiluvya United baada ya
kubaini kuwa timu hiyo haikushiriki ligi ya mkoa wala wilaya msimu
uliopita, hivyo kutokuwa na sifa ya kucheza Ligi ya Mkoa msimu huu.
Hivyo
Friends Rangers ya Dar es Salaam iliyokuwa icheze na Kiluvya United na
Mpwapwa Stars ya Dodoma iliyokuwa iwakabili mabingwa wa Manyara
zinakwenda moja kwa moja raundi ya pili.
Timu
nyingine iliyokwenda moja kwa moja raundi ya pili itakayochezwa kati ya
Mei 25 na 25 mwaka huu na mechi za marudiano ni kati ya Juni 1 na 2
mwaka huu baada ya kupita kwenye upangaji ratiba ni mabingwa wa
Shinyanga, Stand United FC.
Kamati
hiyo iliyokutana chini ya uenyekiti wa Blassy Kiondo pia imeagiza
viongozi wa mikoa ya Manyara na Pwani waandikiwe barua za onyo kwa
kushindwa kuwasilisha majina ya mabingwa wao.
Vilevile
imesisitiza viwanja vitakavyotumika kwa mechi za RCL ni vya makao makuu
ya mikoa tu, isipokuwa kwa Uwanja wa CCM Mkamba ulioko Ifakara,
Morogoro ambao ulishakaguliwa na TFF, hivyo kutumika kwa michuano ya
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu. Pia usajili unaotumika katika RCL
ni ule ule wa ligi ya mkoa.
Mechi
za Mei 12 mwaka huu zitakuwa kati ya Kariakoo ya Lindi dhidi ya Coast
United ya Mtwara (Uwanja wa Ilulu), Techfort ya Morogoro vs African
Sports ya Tanga (Uwanja wa CCM Mkamba), Machava FC ya Moshi vs Flamingo
SC ya Arusha (Uwanja wa Ushirika), Simiyu United ya Simiyu vs Magic
Pressure ya Singida (Uwanja wa Simiyu) na Polisi Jamii Bunda ya Mara vs
UDC ya Mwanza (Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume).
Polisi
SC ya Geita vs Biharamulo FC ya Kagera (Uwanja wa Geita), Saigon FC ya
Kigoma vs Milambo FC ya Tabora (Uwanja wa Lake Tanganyika), Katavi
Warriors ya Katavi vs Rukwa United ya Rukwa (Uwanja wa Katavi), Njombe
Mji ya Njombe vs Mbinga United ya Ruvuma (Uwanja wa Sabasaba) na Kimondo
SC ya Mbeya dhidi ya 841 KJ FC ya Iringa (Uwanja wa Sokoine, Mbeya).
Mechi
kati ya Red Coast na Abajalo itachezwa Mei 13 mwaka huu Uwanja wa Azam
ulioko Chamazi, Dar es Salaam. Mei 12 mwaka huu uwanja huo utatumika kwa
mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Azam na Mgambo Shooting.
ZA LEO LEO
No comments :
Post a Comment