Meneja
Mauzo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wa Mkoa wa Morogoro, Jemes
Gomile(kushoto) akimkabidhi Vifaa vya michezo,Nahodha wa timu ya Chuo
cha SUA, Calvin Mjema wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo kwa
Vyo shiriki vya mashindano ya mchezo wa Pool kwa Vyuo vya Elimu ya juu
Mkoani Morogoro.Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Pool Mkoa wa
Morogoro, Patrick Lugang’ha.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
KAIMU Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,
John Laswai anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya mchezo wa Pool 'Safari Lager Higher Learning Pool Competition 2013'. kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya
mkoa wa Morogoro yatakayofanyika Mei 11.
Akizungumza na waandishi wa habari
jana wakati wa kukabidhi
sare za kuchezea pamoja na fedha kwa ajili nauli na maadalizi kwa vyuo
vitakavyoshiriki, mwenyekiti wa chama cha mchezo huo mkoani hapa (MOPA),
Patrick Lugeng'ha alisema kuwa mashindano hayo yatakayoshirikisha vyuo vikuu
vinne yatafanyikia kwenye ukumbi wa Vijana.
Lugeng'ha alisema kuwa mashindano hayo
yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari
Lager yatafunguliwa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa na yatafungwa na
Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro,Lydia Mbiaji.
Aliongeza kwa kuvitaja vyuo
vitakavyoshiriki mashindano hayo kuwa ni chuo cha SUA, Mzumbe, Ardhi na chuo
cha uandishaji wa habari ( MSJ).
Lugeng'ha alisema kuwa mashindano hayo
yatachezwa kwa mtindo wa chuo kwa chuo na mchezaji mmoja mmoja wanaume na
wanawake.
Alisema bingwa kwa upande wa chuo licha ya
kujinyakulia fedha taslim Sh.500,000 pia itakuwa imekata tiketi ya kuuwakilisha
mkoa huo katika fainali za taifa zitakazofanyika kuanzia Juni mosi mwaka huu
jijini Dar es Salaam, mshindi wa pili atazawadiwa Sh.300,000, mshindi wa tatu
Sh.200,000 na mshindi wa nne Sh.100,000.
Aidha alisema kuwa bingwa kwa upande wa
mchezaji mmoja mmoja (wanaume) atajinyakulia Sh.150,000 na tiketi ya kushiriki
fainali za taifa, mshindi wa pili Sh.100,000, ambapo bingwa kwa upande wa
wanawake atazawadiwa Sh.100,000 na tiketi ya kushiriki fainali za taifa huku
mshindi wa pili akiondoka na Sh.50,000.
No comments :
Post a Comment