Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, May 8, 2013

SIMBA YAIFUNGA MGAMBO SHOOTING 1-0, YAJIHAKIKISHIA NAFASI YA TATU











SIMBA SC imeifunga Mgambo Shooting FC ya Tanga bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Uwanja wa Taifa leo.
Bao hilo lilifungwa na kiungo mshambuliaji wa pembeni, Haroun  Chanongo dakika ya nane, ambaye alitoka na mpira katikati ya Uwanja na kuanza kuwapangua mabeki wa Mgambo kabla ya kumchambua kipa Godson Mmassa.
Baada ya bao hilo, Simba SC waliongeza kasi ya mashambulizi langoni mwa Mgambo na Amri Kiemba alikaribia kufunga mara mbili wakati Nassor Masoud ‘Chollo’ na Ramadhani Singano ‘Messi’ kila mmoja alikaribia kufunga mara moja.
Kipindi cha pili, Mgambo JKT walipambana kutoruhusu mabao zaidi, ingawa Simba SC iliendelea kutawala mchezo huo kwa pasi maridadi na soka ya kuvutia.
Katika mchezo huo, kipa Juma Kaseja aliokoa hatari mbili tu kipindi cha kwanza moja alipopangua shuti la juu kabla ya kudaka na kipindi cha pili alipodaka shuti la chini, pembeni.
Ushindi huo, unaifanya Simba SC itimize pointi 45, sasa ikizidiwa pointi tatu na Azam FC inayoshika nafasi ya pili, ambayo Jumapili itamenyana na Mgambo kwenye Uwanja wake wa Azam Complex, Chamazi. 
Mchezo huo, ulichezeshwa na mwamuzi Andrew Shamba, aliyesaidiwa na Abdallah Rashid na Abdallah Mkomwa wote wa Pwani, huku mezani akiwepo Israel Nkongo.
Katika mchezo wa leo, kocha Mfaransa Patrick Liewig aliwapumzisha wachezaji kadhaa tegemeo, Mrisho Ngassa, Shomary Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu na Mussa Mudde kuelekea mchezo dhidi ya Yanga Mei 18.  
Kikosi cha Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’/Omary Salum, Haruna Shamte, Miraj Adam, Hassan Khatib, Jonas Mkude, Edward Christopher, William Lucian ‘Gallas’/Rashid Ismail, Amri Kiemba, Ramadhani Singano ‘Messi’/Salim Kinje na Haroun Chanongo.
JKT Mgambo; Godson Mmasa, Salum Mlima, Ramadhani Kambwili, Bashiru Chanacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Chande Magoja/Mussa Gunda, Peter Mwalyanzi, Issa Kandulu, Fully Maganga na Nassor Gumbo.

No comments :

Post a Comment